Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete: Leadership Styles and A Lesson to Learn!

Nimeshindwa kuweka jedwali zuri.

Uzalendo: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete
Ufisadi: Kikwete, Mkapa, Mwinyi, nyerere
Udictator: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete
Ubepari: Mkapa, Mwinyi, Kikwete, Nyerere
Utajiri: Mkapa, Mwinyi, Kikwete, Nyerere
Ufalsafa: Nyerere, Mkapa, mwinyi, Kikwete
Matumizi: Kikwete, Mwinyi, Mkapa, Nyerere
Vita na Ubabe: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete

Kwakweli hawa ni binaadamu wa kawaida, na wana mazuri na mapungufu.:whoo:
 
kura za marais wabovu JMK atazibeba zote, the worst ever sasa hivi hata ukimuuliza ratiba ywa mwezi huu hajui anajiendea Mungu atunusuru tungeshakufa jamani hili tumepewa kanyaboya full

Mmechagua wenyewe jamani. asilimia arobaini ya asilimia ishirini ya wapiga kura wote mlisema ndiyo. ni kweli? hahahahahaha! ushindi mnono
 
wewe unafikiri yule mtu aling'atuka kwa kupenda? kuruhusu haki za binadamu kulimpunguzia maamuzi
 
nimeshindwa kuweka jedwali zuri.

Uzalendo: Nyerere, mkapa, mwinyi, kikwete
ufisadi: Kikwete, mkapa, mwinyi, nyerere
udictator: Nyerere, mkapa, mwinyi, kikwete
ubepari: Mkapa, mwinyi, kikwete, nyerere
utajiri: Mkapa, mwinyi, kikwete, nyerere
ufalsafa: Nyerere, mkapa, mwinyi, kikwete
matumizi: Kikwete, mwinyi, mkapa, nyerere
vita na ubabe: Nyerere, mkapa, mwinyi, kikwete

kwakweli hawa ni binaadamu wa kawaida, na wana mazuri na mapungufu.:whoo:
hii imekwenda shulee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
BENJAMINI WILLIUM MKAPA ANAONGOZA
WA PILI NI JULIUS KAMBARAGE NYERERE
WA TATU NI ALLY HASSAN MWINYI

NA WA MWISHO TENA MWISHO KABISA NA NINAAMINI HAKUTA TOKEA KIONGOZI KAMA HUYU DAIMA JAKAYA MRISHO KIKWETE,HUYU MMMMMMMMHmmmm;;
 
itnojec, i first thought that way, kabla JK hajamaliza miaka mitano i realized how wrong i was, to me JK is the worst of them all, very weak, can't make solid decisions, can't stand for his weak decisions, can't lead by example, can't bring people together, not even in his party, he has got no agenda, ask him what you want to achieve in the next one year and you will get hundreds of answers...yaani Mungu atusaidie tu

Kwenye mdahalo kipindi kile cha uchaguzi, alishindwa kujibu swali "....unawaachia watz regacy gani, ambayo wakukumbuke nayo"
Akasema wanaikumbuke kama niliwatoa hapa na kuwapeleka pale...
Jamani JK ni maandazi kabisa huyu jamaa, atlesat Ben alikuwa anatupeleka shimoni kwa misingi ya kuua "kujitegemea kwa taifa" lakini huyu hata hajui anatupeleka wapi.
 
Kwenye kampeni last election aliulizwa swali kwenye ule mdahalo wa kizushi.'Mh.Umezunguka tanzania nzima kwenye kampeni,Je unaiöaje tanzania?'Alijibu hivi'Ee si..sij..ui kuiona kwa mtazamo upi lakini mi naonaTUTASHINDA!'
 
Jambo moja liko wazi ambalo laweza kumfanya Kikwete awe rais ovyo zaidi. Akilitekeza nitaona kaanza kubadilika kuwa bora. Majuzi aliagiza tena hadharani ukuta wa mabati yaliyozungushiwa pale Jangwani yaondolewe. Yasipoondolewa mtajaza wenyewe tuna rais wa aina gani.
 
Kila Rais ana mazuri na mabaya yake. Tukingilisha kati ya hawa watu wanne waliokaa pale magogoni who will go to the history as the worst president ever? ...why?


Pamoja na mapungufu ya hapa na pale kwangu mimi la msingi ni hili; kwamba, Mwl. Nyerere aliachia ngazi tukiwa WATANZANIA, Mwinyi ametuacha tukiwa WATANZANIA, Mkapa naye ametuacha tukiwa WATANZANIA. Kikwete sina shaka atatuacha waislam, wakristo, ccm-mtandao, ccm itakadi, ccm-watazamaji, ccm-A, ccm-B, wakwere, wasukuma, wachaga, wamasai, wanyakyusa, wanzanzibari, wanzanzibara n.k. Kwa maana nyingine atatuacha vipande-vipande sio tu ndani ya CCM bali hata ndani ya vyama vya upinzani (kapindikiza mamluki kama Shitambala) na jamii yote kwa ujumla, VIPANDE VIPANDE!

Imechukuwa takriban miaka 50 kuunganisha watu wa kabila, dini na tabaka mbalimbali kuwa kitu kimoja lakini kwa kasi ya ajabu na mbinu za kushangaza amevunjilia mbali umoja huo. Na ungeniuliza ni lini alianza, ningesema ni siku ile Watanzania tulipoamka na kukuta taarifa kila kona zinatuambia kuwa Salim Ahmed Salim ni mwarabu, hisbu n.k. Cha ajabu hakuna kiongozi wa juu aliyejitokeza kwa kipindi hicho kukemea tabia hiyo ya kibaguzi si Kingunge, wala Malecela, wala hao wanaojiita UVCCM. wote kimya! hapo wengi wetu tulijua safari ya siasa za maji taka zimeanza na matokeo yake tunayaona. Sasa hivi wanatafunana wenyewe kwa wenyewe. Haponi mtu. Atatuacha vipande vipande. Unforgivable!
 
Nadhani sio Fair kumjumuisha Nyerere katika Kundi hili, Japokua alikuwa na mapungufu yake lakini nadhani yeye yupo kundi lingine. lakini mimi nadhani Mkapa he was worse president maana aliiongoza Nchi kama ya kwake.
 
Kila Rais ana mazuri na mabaya yake. Tukingilisha kati ya hawa watu wanne waliokaa pale magogoni who will go to the history as the worst president ever? ...why?

Dikteta NYERERE... Ndio iliyeweka misingi ya umasikini Tanganyika na Zanzibar.
 
itnojec, i first thought that way, kabla JK hajamaliza miaka mitano i realized how wrong i was, to me JK is the worst of them all, very weak, can't make solid decisions, can't stand for his weak decisions, can't lead by example, can't bring people together, not even in his party, he has got no agenda, ask him what you want to achieve in the next one year and you will get hundreds of answers...yaani Mungu atusaidie tu

Correct,udhaifu mkubwa ni kutoweza kufanya maamuzi magumu na yenye manufaa
 
Nadhani kikwete anaonewa sana.yapo mapungufu yake bt na haki yake apewe.kama ni ufisadi hakuna raisi alokuwa fisadi kama mkapa.alichukua kila kitu kikawa mali yake nanyi mkanyamaza kimya.mkapa kasababisha kwa mara ya kwanza nchi kutoa wakimbizi.naomba niambiwe kwa data ni upi udini wa kikwete?sio tukurupuke kusema mambo yasiyo na mashiko.nyerere kawaweka watu ndani kizuizini bila makosa wala kufunguliwa kesi.huo si ubabe?au hamjawahi kusikia habari hz?toweni uamuzi wa haki sio kuongozwa na hisia.
 
Nduguyangu

Nahisi kumekuwa na campaign siku za karibuni za kutaka kumpaka matope Mwl Nyerere. Hata Rais Kikwete amenukuliwa na vyombo vya habari kwenye moja ya hotuba zake hivi karibuni akisema kuwa Mwl aliondoka madarakani ili nchi ikiwa maskini. Nadhani tuwe waungwana. Mwl. mwenyewe aliwahi kukiri kuwa katika uongozi wake kuna mema na mazuri na ni juu wale wanaochukuwa dhamana ya kuongoza Taifa kuuendeleza yale mazuri na kuacha yote yaliyo mabaya. Narudia - endeleza mazuri, acha yale yote mabaya. Sasa ndugu yangu unayetaka kutupa historia ya maisha ya watanzania chini ya uongozi wa Mwl Nyerere naomba nikukumbushe machache yafuatoyo:

1. Viongozi wengi wa juu akiwemo Kikwete mwenyewe walisoma bure kwa vihela vya korosho, pareto, pamba, kahawa n.k. - bure kabisa.
2. Mwl Nyerere anaweza kabisa akawa hajaacha Balance sheet ya Taifa ikiwa nzito kwa maana hakuacha hela nyingi kule Hazina lakini ikumbukwe kuwa Mwl. Nyerere hakuacha MASHIMO. Natural resources za nchi hii ameziacha nzima.
3. Mwl. Nyerere wakati anaondoka literacy rate ilikuwa zaidi ya 90% , uliza sasa iko vipi - aibu!
4. Mutex, Mwatex, Kilitex, Machine tools, Tanganyika packers etc - wapi?
5. Ranchi za taifa zi wapi. Pamoja za speech nyingi kuhusu MIKAKATI ya kufufua ranchi leo hii ni ngapi ziko hai?
6. Mara ya mwisho ATC kuvuka bara la bara la Afrika ilikuwa 1999 - kuchukuwa mwili wa marehemu Mwl. Nyerere London. Sasa hivi inaitwa ATCL kuna ndege ngapi na zinaenda wapi? Shirika la Reli nalo?
7. Mbuga za taifa- shamba la bibi
9. Ni wapi na ni lini ulimsikia Mwl Nyerere anajadiliana na wahujumu uchumi?
10. Ni lini na wapi mtoto wa Mwl alitumia polisi escort kuwahi shughuli zake? au Mama Maria kupanda ndege kumpigia debe mume wake?

Mwisho hakuna dhambi kubwa kama kumsema vibaya marehemu. Hayuko hapa kujitetea! Tabia mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Wote ni wabaya sema labda kuna ambaye kawzidi wengine na nafikiri jibu lipo wazi kabisa kila mtu anajua hata yeye mwenyewe anajijua
 
Nimeshindwa kuweka jedwali zuri.

Uzalendo: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete
Ufisadi: Kikwete, Mkapa, Mwinyi, nyerere
Udictator: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete
Ubepari: Mkapa, Mwinyi, Kikwete, Nyerere
Utajiri: Mkapa, Mwinyi, Kikwete, Nyerere
Ufalsafa: Nyerere, Mkapa, mwinyi, Kikwete
Matumizi: Kikwete, Mwinyi, Mkapa, Nyerere
Vita na Ubabe: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete

Kwakweli hawa ni binaadamu wa kawaida, na wana mazuri na mapungufu.:whoo:
kaka nimeipenda... imetulia
 
Utajibiwa na watoto waliozaliwa juzijuzi kisha utegemee walinganishe maraisi waliotuongoza miaka 50 iliyopita? Kumbuka somo la historia mashuleni lilifutwa!
 
acha ushabiki, ebu eleza mabovu ya JK

Amekumbatia mafisadi,ametengeneza serikali ya undugu na ubest,ameongeza tabaka la masikini na matajiri kuwa kubwa,uozo unafanyika ndani ya serikali yake,akiulizwa anasema hajui na anashangaa.upo hapo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom