Mwanamutapa
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 513
- 489
Kwa mujibu wa taarifa za utendaji wa serikali ya CCM. imaonyesha raisi kikwete amefanikiwa sana kuliko maraisi wote waliopita. natoa mifano michache tu hapa kuthibitisha hoja yangu. 1. Wanafunzi wa shule za sekondari kutoka 524.325 mwaka 2005 hadi kufikia wanafunzi 1.884.272 mwaka huu haya ni mafanikio makubwa sana. Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka 40.719 mwaka 2005 mpaka 166.484 mwaka huu haya nimafanikio makubu sana katka elimu. yapo mambo mengi sana ya mafanikio yaliyo fanywa na kikwete haya hayaonwi na dk slaa nampongeza mbowe kuuona ukweli huu.chazo gazeti la uhuru toleo la leo.
Nikiwa nakubaliana kuwa Kikwete kaongeza nafasi za wanafunzi wengi vyuo vikuu kuliko wakati wowote ule katika Tanzania ukweli ni kwamba kwa idadi ya wanafunzi waliokuwa wanaingia vyuo vikuu 2005 bado ilikidhi mahitaji ya graduate katika uchumi wa Tanzania kwa sasa wahitimu ni wengi na hawana pa kwenda pamoja na degree zao na isitoshe hao graduate hawana quality ya elimu wengi wao wakienda kutafuta kazi waajiri wanajiuliza hawa kweli walimaliza degree kwa lugha nyingine tunazalisha quantity badala ya quality.
Jambo la maana katika nchi na kubwa kuliko vyote iwapo tayari kuna idadi ya wasomi hata wengi wa kawaida ni ajira na mfumuko wa bei kwa Jk alivyoingia mwaka 2005 na kwa idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu tuliokuwa nao Tanzania jambo muhimu ilikuwa ni utengenezaji wa nafasi za kazi na sio kuanzisha vyuo vikuuu vingi ambayo wanafunzi wakihitimu hawana ajira kwa sababu mtu anaweza kuishi bila degree lakini hawezi kuishi bila kazi. Na siku hizi nafasi za watu wa diploma zimejazwa na watu wenye degree matokeo yake tumeharibu mfumo wa elimu nafasi ya technician inafanywa na mhandisi maana vyuo vya tech vimelazimishwa kuwa vyuo vikuu na cha kushangaza huyo mhandisi sio mzuri kama yule technician wa zamani pamoja na kuwa mhandisi ana degree
Marekani na nchi za ulaya sio kila anayemaliza high school lazima aende chuo kikuu bali wana mifumo ya elimu kuwa mwingine anaweza kwenda kupata degree mathalani ya biashara na mwingine akaenda kupata diploma mathalani ya unesi lakini mwenye diploma ya unesi analipwa mshahara zaidi ya yule mwenye degree ya biashara kwa lugha nyingine kuwa na maisha mazuri sio kuwa na degree inatokana na taaluma na mahitaji yake kwa wenzetu kitu cha muhimu ni ajira, kudhibiti mfumuko wa bei na huduma bora za afya. Kwa kuangalia indicators za uchumi yaani ajira, mfumuko wa bei, pato la mmoja mmoja na social services kama wenzetu wa ulaya Mkapa was much better kuliko Kikwete maana Kikwete ni msanii kabakiza kutaja idadi ya vyuo vikuu na urefu wa barabara mambo ambayo watu wanaweza kusihi bila kuwa nayo na kuacha vitu muhimu kama ajira, mifumuko ya bei na huduma za afya ambazo zimedhoofika.