Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,221
Kuwaza kwako rafiki yangu ni kufupi sana. You run into conclusions. Kufikia conclusion kwamba Nyerere alikuwa na tamaa ya madaraka kwa kuwa alimwachia Kawawa uwaziri Mkuu badala ya kina Kambona kama ungekuwa mwanafunzi wangu wa political science ningekupa 8% ya upendeleo.
Je unasahau Nyerere, japo ya kuwa raisi kwa mika 23, alikuwa raisi mojawapo wa kwanza Africa kuachia madaraka kwa hiari? Na kumbuka alitaka kuachia mapema, lakini akasema basi ngoja angalau nisaidie kurekebisha makali ya vita ya Kagera. Angalia kwamba kina Museveni waliokuja baada ya Nyerere wamekuwa maraisi muda mrufu zaidi ya Nyerere!
Angalia kina Puttin wamerudi tena kwenye uraisi!
Nyerere alikjua nini kifanyike baada ya uhuru ili kuwafaidisha watanzania wote, vijijini na mijini, ki-elimu, afya na umasikini. akawa na mtazamo wa kisiasa wenye kupambana na haya mambo matatu; ujinga (elimu kwa wote), maradhi (huduma ya afya kwa wote) na umasikini (umiliki wa umma wa uchumi).
Kina Kambona walikuwa na mtazamo tofauti, walitaka tufuate sera za kibepali (capitalism). Nyerere akawa ana argue kwamba capitalism itazua tabaka la watanzania masikini sana na wachache matajiri sana - watwana na mabwana. Akasema mkiwinda mnyama kijijini, ni vema mwanakijiji apewe mgawo sawa, hata kama hakuhusika moja kwa moja kuwinda kwa kuwa alikuwa na kazi nyingine kijijini. (Kenyatta alisema hapana, waindaji wanapaswa kupata maini, na kama hukuwapo uambulie kitakachobaki baada ya wawindaji kuchukua sehemu nzuri nzuri!)
Sasa niambie, ungekuwa wewe ndio Nyerere, katika mazingira hayo, ungewaachia nchi kina Kambona ambao ukijua wazi mna mitazamo tofauti katika uongozi wa nchi? Nyerere alichofanya ni tamaa ya madaraka au rational thinking?
Unafikiri nini kingetokea iwapo angewaachia kina Kambona? Angefanya hivyo nadhani leo hii tungekuwa na historia inayosema Nyerere ailikufa kifungoni mwaka 1961, na wengi wetu lecture halls za UDSM tungekuwa tunazisikia redioni tu. Huenda baba yako hata darasa la saba asingefika!
Asante sana kwa kumueleza vizuri.