Ajabu Na Kweli Hawajibu Hoja
Invisible Tufanyie Utaratibu Hawa Watu Kama Nmb, Vodacom, Star Time

Wawe Wanajibu Hoja Sasa Kuna Watu Tunatamani Kusoma Majibu Ili Nasi Tuone Uzuri Na Ubaya Wao Kabla Ya Kujiunga Huko
 
Wahusika NMB nilikuwa KARIAKOO siku ya juzi muda ya saa 6 mchana.. nikajaribu Kutoa pesa kwenye Account yangu kiasi cha Tshs 250, 000.. kiukweli pesa sikupata na salio likawa limekwisha.. nikaenda Kutoa riport wakanipa form nijaze.. ila mpaka sasa pesa yangu haijarudi jaman.. tatizo nini?
 
NMB,changamoto ambayo mom nmkumbana nazo,kupotea hela hasa ukihamisha kwenda mpesa, folen kili ukienda bank,makato makubwa sana ktk mikopo,huduma za kirasimu,kufanya kaz kwa mazoea
 
Usumbufu ukiwa na chaque yaani ukiwa na chaque yako watumishi wenu wanasumbua sana kwa lengo la kujenga mazingira ya rushwa
 
Hivi nyie benki ya makwabela inawachukua muda gani kumpa mtu ATM card
 
Hongereni kwa kazi nzuri lakini kuna tatizo limenipata leo tarehe 9/9/2015,saa 9:55 jioni hii tawi la NMB,MBALIZI ROAD,MBEYA nimetoa pesa Tshs,400,000.mashine imehesabu lakini haijatoa pesa nimeingia ndani kuomba msahada na wamenipa form niijaze na wakanitaka copy ya ATM card yangu sasa nimetoka nje kutoa copy narudi baada ya dk6,nikamkuta mlinzi akaniambia muda umeisha huku nimeshika form mkononi nimeshindwa kurudisha hii form na pesa zinahitajika hospitali kesho asubuhi sasa nashindwa chakufanya msahada wenu wadau.
 
Kwann nmb hawapo serious na wepesi ktk kuhudumia wateja?kwann mkopo uchukue wiki mbili tatu au zaid kutolewa?_its much boring doing business with nmb
 
Mimi niuliza kwa nini mnakata processing fee pindi mtu anapokopa pesa toka Bank? Mfano mimi juzi nimeenda kukopa milioni tano na nusu mpaka sasa sijaipata lakini tayari nimeshaoneshwa makato yangu ikiwemo hiyo ada na insurance jumla nitakatwa kiasi cha shilingi 294000 (laki mbili na tisini na nne elf) sasa najiuliza huu utaratibu mbona siulewi mbona kwenye taasisi zingine tofauti na bank hakuna hizo ada wala insurance
 
Huduma kuhamisha pesa kwenda m-pesa imewashinda ondoeni tu inatutesa sana maana unahamisha pesa leo unapata pesa kesho.
 
Card zenu tu ndo tatizo. Zinapigwa sana bao na hata ukitipoti hakuna msaada wa kuzuia na fidia.
Jee hamna bima za kukinga majanga ya cyber crime?

Bunafsi sijaibiwa lakini nimeshuhudia wa karibu yangu mara tatu card zao zikiliwa na hata aliporipoti baada ya siku tatu iliibiwa tena na alishauriwa kubadili password haikusaidia.

Angalau mngefanya kulipa fidia. Na pia angalieni ku arrange insurance cover inayo toa kinga ya kutosha.
Mteja kupoteza hela ambazo zipo Bank ni jambo linauma sana
 
Hivi ukihamisha pesa yako kutoka account yako ya NMB na kwenda account yako ya M-mpesa na muamala ukakamilika na ukakatwa pesa za kukamilisha muamala huo na NMB lakini mwisho wa siku pesa ifanikiwe kuingia kwenye Account yako ya M-Mpesa wakati tayari pesa umeisha katwa ya kuhamishia!kisha baaadaye wao NMB wanakuomba radhi kwa kushindwa kuihamisha ile pesa .

Swali je ile pesa uliyokatwa kwa ajili ya kuhamisha ile pesa nitaipataje?
 
Hakuna huduma mbaya ya kiwango cha chini kabisa yaani zero kama ilivyo NMB mobile. NMB mobile ni tatizo na mimi nitashaangaa kuendelea kuona matangazo yenu ya kutushawishi kutumia huduma hii.

Na huduma hii ni mbaya zaidi yaani iko chini ya zero kwa maana ya negative kwenye link ya kutuma pesa kwenda M~pesa. Just imagine unahamisha pesa kwa mahitaji ya haraka alafu inakaa zaidi ya masaa 24 haijaingia M~pesa. Sasa mtu unajiuliza kuna uhalali wa kuwepo huduma kama hii?.

NMB mobile ni kati ya huduma zinazo izalilisha nchi hii ni kati ya huduma zinazo onyesha teknolojia yetu bado ni primitive. Kwa ushauri wangu uondoeni huduma hii, ina create frustrations na inafanya tuichukie NMB.
 
Yaaani sijuii nisemajee ninyii nmb huduma mbaya kama nini yaani hasa hizi tarehee za mishwo wa mweziii ndio kuna kuwa na matatizo ya atm zenu kuishiwa helaa kama vip mtagutee mobal car zenye atm ili kukidhii huduma kwa watumiajii kipindi cha mwishooo wa mweziii mana tuna sumbuka asaana
 
Mnazingua tu! Huduma zenu bado mbovu!

Mtu anatoa hela kwenye ATM hela yenyewe haitoki na kwenye akaunti yake tayari imeshakatwa na msg kwenye simu tayari imeshaingia kuwa umetoa hela.

Sometime mtu anajua salio lake lakini hela yake inakatwa bila sababu, akiomba bank statement anazungushwa na hata akipewa anakuta kuwa alituma hela kwa mtu wakati hakufanya hiyo huduma.
WIZI MTUPU!!
 
Mnazingua tu! Huduma zenu bado mbovu!
Mtu anatoa hela kwenye ATM hela yenyewe haitoki na kwenye akaunti yake tayari imeshakatwa na msg kwenye simu tayari imeshaingia kuwa umetoa hela.
Sometime mtu anajua salio lake lakini hela yake inakatwa bila sababu, akiomba bank statement anazungushwa na hata akipewa anakuta kuwa alituma hela kwa mtu wakati hakufanya hiyo huduma.
WIZI MTUPU!!

Hama hiyo Bank, amia Bank nyingine karibu Barclays Bank...!
 
Back
Top Bottom