Huduma zenu ni hafifu, hamuwajali wateja wenu!! Wateja ni wengi wahudumu wachache na wengi wao hawajitumi wanafanya kazi kusubiri muda tu, jaribuni kuwaelimisha kuwa wateja wanapokuja bank huwa wanaacha shughuli nyingine Ili wajali muda WA wateja
 
Hivi inachukua muda gani mpaka kuifungia account isiyotumika?

kwa crdb ukienda tawi ulilofungulia account inategwmea na foleni.km foleni hakuna ukifika kwa cashier ni 1minutes unaifufua.kwa NMB tujuzeni mlioexperience
 
hongereni NMB kwa kuboresha huduma ya mikopo, mimi leo nimerudisha fomu yangu ya mikopo asubuhi kufika mida ya mchana naangalia salio nakuta tayari NMB wameishaniwekea mkopo wangu niliouomba.

Hongereni sana NMB.
 
hongereni NMB kwa kuboresha huduma ya mikopo,mimi leo nimerudisha fomu yangu ya mikopo asubuhi kufika mida ya mchana naangalia salio nakuta tayari NMB wameishaniwekea mkopo wangu niliouomba.Hongereni sana NMB.

Mi nina mwezi wa pili huu sijapata mkopo hawa jamaa siwaelewagi kabisa sijui wananijua kama mgumu kulipa
 
Hongereni kwa kuboresha huduma zenu, naombeni mwachunguzeni maafisa mikopo hasa branch ya kigoma na kasulu kwani ukitaka upate mkopo haraka lazima utoe rushwa, pili naomba mnijuze riba yenu ya mkopo kwa mwaka ni %ngapi, na hii bima ya mkopo ikoje?
 
Hamna maana mnamkopesha mtu milioni 6 mnamubana kwa miezi 6 kwa biashara gani hapa Tanzania ambayo INA rundo la kodi lukuki pia maafisa mikopo wenu wanapenda rushwa.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 
mi huwa s

iwaelewi kira wakati munabadilisha waraka wa mikopo mwaka huu mulisema kurenew mkopo baada ya miezi sita sasa kufika mwezi wa kumi mumebadirisha kurenew mpaka miezi kumi babadiriko yasifanyike zaidi ya mara moja kwa mwaka
 
Kitendo cha ATM kutotoa noti za elfu tano ni wizi mkubwa.

Nikirudia kukopa Nmb nitakuwa na matatizo kichwani.
 
Kwa yeyote mwenye access na mamlaka zinazohusika na kusimamia mazingira na afya makazini, ninaomba asaidie kufikisha taarifa hii. Ni miezi mitatu sasa tangu Viyoyozi (Air Conditioners) katika tawi hili (NMB Ifakara Branch) viharibike na hakuna hatua za makusudi zimefanyika kurekebisha hali hii. Ukiingia ndani ya tawi hili kuna hewa nzito na joto la ajabu ambalo linatokana na msongamano wa wateja pamoja na wafanyakazi. Watu wanavuja jasho na harufu zisizovumilika. Pamoja na hali hiyo, bado mlango wa mbele ambao ungefunguliwa kunusuru na kusaidia hewa kuingia, umekua ukifungwa.

Wateja wamekua wakipiga kelele lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Hili limekua ni eneo hatarishi kwa afya za wateja pamoja na wafanyakazi wa bank hii. Katika tawi zima, ni ofisi ya Manager wa tawi pekee yenye kiyoyozi na hii imechangia kwa yeye kutochukua hatua zozote kurekebisha hali hii. Endapo ikitokea mtu mwenye magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya hewa, ni dhahiri hali itakua mbaya sana.

Naomba mamlaka ziweze kuchukua hatua ili kunusuru afya za watu wanaoingia pale.

Wakuu naomba wenye access muweze kufikisha ujumbe huu mahali panapohusika

Asante
 
NMB Kipindi cha mwisho wa mwaka mmeonyesha kutokuwa makini na experience tuliyopata tawi la TUKUYU NMB imetusikitisha sana.

Hakukuwa na huduma za kuridhisha kabisa za ATM na hakukuwa na maelezo ya sababu ya hali hiyo. Watu wakawa wanahisi tuu, labda MTANDAO, labda FEDHA HAKUNA na kadhalika.
USHAURI;

Kama mitandao inasumbua ni vema kutangaza kuwa kuwa huduma zitakuwa zinapatikana kuanzia muda fulani hadi muda fulani...maana kwa kutokuwa na uhakika watu walisubiri kwa masaa mengi tu na hatimaye huduma isipatikane.
 
NMB Please improve your services....kuweni strategic! Nyakati za peak periods k.v. mwisho wa mwezi (waajiriwa wanapokuja kwa wingi kuchukua mishahara), ama nyakati za sikukuu, (na hata masaa fulani kila siku) haipendezi kuona Cashiers wawili tu kwenye booth wakihudumia rundo la watu! Zanzibar ni mfano mzuri wa changamoto hii.
 
Kwa mtu mwenye mshahara wa laki saba na nusu na take home ni laki tano na nusu anaweza kopa maximum sh ngapi kwa marejesho ya Mwaka mmoja, Miaka miwili miaka mitatu na miaka mitano?
 
Ongezeni mashine za ATM hata kwenye maeneo ya mikusanyiko si lazima mpk eneo la benki..km vile stendi,sokoni nk.
 
Yaaan sina ham na benk nko mt uluguru moro lisaa la tano hv kweli maendeleo yatakuja kwa namna hii hata unipe pesa hii benk sifunguiii ac sema tu hz huduma za serikali ndo zinatulazimisha kuja la svyoo majengo yao ningekuwa nayaona kwa nje
 
Mmeanzisha kitengo maalum cha kufuatilia na kujibu maswali yote yanayotupwa hapa jukwaani lakini? Maana Msije mkaanza kujutia kujiunga humu naona maswali ni mengi sana hapa!
 
Hii thread kuna mtu wa NMB huwa anaipitia na kujibu maswali yanayoulizwa ?
 
Back
Top Bottom