Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta ? Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe ?Siri?)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Sijajua kama limeshajibiwa hili ila kwa vile customer care ni kumhudumia mteja individually naomba mjibu tu hata kama ninauliza mara ya 111100.
Je mna mpango wa huduma za pesa kwa mtandao? hii namaanisha kuwa kuwe na app kwenye simu za adroid na iOS ambayo mtu akiwa na data tu anaweza kuhamisha pesa, kuona statement ama kuangalia balance bila makato ya kijinga kabisa kama ya sasa. Sijui mnakuaje bank za Tz, eti huduma ya bank mpk niwe na vocha kwenye simu alafu *150*66#, hapo bado bank na nyie mnakata (eti gharama za kuangalia salio) huu ni wizi wa wazi wazi. Sasa kama natumia wi-fi au sipo Tanzania siwezi ona salio/statement/transfer monies.
Wenzetu walishapiga hatua hizo zamani sana, mpaka ukipoteza kadi unapewa nyingine free na haraka.
Je mna huo mpango ama lazima tuwafaidishe wenye mitandao ya simu na nyie?
rant rant rant rant