Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?
 
Kweli jamani hakuna mtu ajuae dawa? Haya bana! mama muuza niletee safari baridiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Natalipa kesho iikhi
 
Mkuu umepata hiyo dawa. Nilipo hapa kuna mtalaam anatoa hii dawa ambayo ukiinusa tu utapa kichefu chefu cha ajabu kila unapohisi harufu ya pombe yoyote. Kichefuchefu hiki kinapelekea kutapika kusikokwisha mpaka kuachia ngazi. Wengi wameshaachia ngazi na hawakurudia tena pombe. Tuwasiliane.
 
Kaka kuachia ngazi mbona ni matisho. Yaani nitapike mpaka niachie ngazi? Noooooooooo hapana. Mi nataka niache pombe tu sio niachie ngazi.
 
Sisi kule kwetu pombe ambayo inapatikana kwa wingi inaitwa ulanzi. Sasa tukiona mtu ni munywaji sana, kiasi cha kwamba amepitiliza, huwa tunamwekea konokono mbichi kwenye huo ulanzi halafu unamwachia lita nzima anywe peke yake. Iwapo haangalii, anaweza ama kumtafuna huyo konokono au akapitiliza tumboni. Akipitiliza tumboni ni bahati yake, lakini akimtafuna basi hatakaa anywe ulanzi tena, manake akiuona tu atakuwa anasikia kichefuchefu. Sasa kwenye mbege sijui tunaweza kuweka nini?
 
Bana sinywagi mbege bana. Mi nakunywa safari ka 18, ndovu sijui ngapi maana huwa nakunywaga tuuuu, sitaki serengeti maana ina kama kaharufu fulani hv, Valuer kama 3 ama nne hivi, Konyagi zile kubwa kama 4 hv sasa nitaachaje?
 
Kaka, kuacha pombe is a mind game. Ukitaka kuacha pombe, kama we ni mnywaji bia, hata kama huwa unakunywa kreti tatu unatakiwa uache bia moja tu! Utakua umefanikiwa.

Jizuie usinywe ile bia ya kwanza. Basi.
 
sikumbukagi nimeanza saa ngapi ila huwa nakuta nina bia mezani! mateso jamani nisaidieni!
 
Wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?

kaka kuacha pombe ni rahisi sana, wala usitumie dawa yoyote, Dawa acha kwenda bar au Grossary yoyote. Mimi mwenyewe nilikuwa nakunywa sana na nikaapa kwa mchumba wangu ambaye sasa ni mke wangu kuwa mimi sitaacha pombe, katika maisha yangu. lakini nilishaacha na dawa ni kutokwenda bar sasa huu ni mwaka wa saba. Ingawa siku zile za mwanzo mwanzo nilikuwa siku moja moja napata moja baridi.

kwa sasa nilishaacha kabisa. wala usitumie dawa yoyote we usiende bar.
 
  • Thanks
Reactions: B40
Bana sinywagi mbege bana. Mi nakunywa safari ka 18, ndovu sijui ngapi maana huwa nakunywaga tuuuu, sitaki serengeti maana ina kama kaharufu fulani hv, Valuer kama 3 ama nne hivi, Konyagi zile kubwa kama 4 hv sasa nitaachaje?

Pole mkuu, lakini inawezekana kabisa kupanga mikakati ya kuacha. Mojawapo ikiwa ni pamoja na kuahirisha kwenda bar siku moja moja au kuanza kupunguza kiasi cha bia unazokunywa. Najua ni vigumu, kama huna kazi nyingine ya kukuweka busy kiasi cha kushindwa kwenda kunywa. Mimi kwa mfano kuna wakati ambapo huwa nina kazi ofisini hadi saa nne usiku na siku ya pili natakiwa kuingia saa moja. Kwa hiyo nikitoka hapo ni nyumbani, huwa sina ubavu wa kupita popote. So kama unaweza kutafuta kitu cha kukulia muda wako zaidi inaweza ikasaidia angalau kupunguza.
 
kaka kuacha pombe ni rahisi sana, wala usitumie dawa yoyote, Dawa acha kwenda bar au Grossary yoyote. Mimi mwenyewe nilikuwa nakunywa sana na nikaapa kwa mchumba wangu ambaye sasa ni mke wangu kuwa mimi sitaacha pombe, katika maisha yangu. lakini nilishaacha na dawa ni kutokwenda bar sasa huu ni mwaka wa saba. Ingawa siku zile za mwanzo mwanzo nilikuwa siku moja moja napata moja baridi.

kwa sasa nilishaacha kabisa. wala usitumie dawa yoyote we usiende bar.
Hata asipoenda bar anaweza kuagiza akawa ananywea nyumbani au hata ofisini. Kuacha pombe ni kazi ngumu sana!!!
 
wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?

warning
 
Attachments

  • POME.jpg
    POME.jpg
    51.5 KB · Views: 213
Where there is a will there is a way

but the will should be a will power
 
Back
Top Bottom