Nadhani watu wanazungumzia kupeleka wanajeshi kule kwa urahisi sana. Hupeleki wanajeshi kwenye mpaka wa nchi nyingine bila kuwa tayari kupigana vita. Kuna vitendo ambavyo kisheria vikifanyika vinachukuliwa kuwa ni "act of war". Tanzania haipaswi kupeleka wanajeshi wake karibu na mpaka na Malawi bila kuwa tayari kwenda vitani. Swali, Watanzania mko tayari kwa vita siyo kwenda kujionesha tu. Nani kawaambia ati mkipeleka wanajeshi basi wamalawi watanywea? Na wenyewe si wana jeshi?
Unafikiri kuwa na wingi wa jeshi na silaha ndio kushinda vita? Lakini kubwa zaidi ni kuwa viongozi wetu tayari hawana ile cloud ya kuwa viongozi wa wakati wa vita. Kama kwenye amani wametutawala hivi wakati wa vita itakuwaje? Njia pekee ya kuleta hiyo heshima ni sisi kutangaza tunaanza utafiti wetu wa mafuta kwenye nusu yetu tukiheshimu mipaka yetu na hatutagusa nusu ya Malawi. Malawi watakuwa wametupiwa mpira!
Kama wao wanaamini ziwa zima ni lao basi wao ndio wafanye hatua ya kwanza vita.... hapo ndio JWTZ linapoenda kulinda mpaka wetu!
Mzee Mwanakijiji, nina kubaliana na wewe hapo kwenye utayari wa watawala wetu na wananchi kama tunaweza kufanya/kuingia vitani kwa sasa? ila hapo kwenye red labda kama unataka kuwatega Wamalawi kama watakubaliana na sisi kuwa mpaka wa Tanzania na Malawi upo katikati ya Ziwa - iwapo tutaamua kufanya utafiti wa mafuta!
Kama ni Tz itaamua kuingia katika mtego huo basi itakuwa ni tofauti na wao wanavyodai na kujua kuwa mpaka wa nchi hizi mbili upo ufukweni kwetu, ikimaanisha kuwa (maji ni ya Malawi na ufukwe ni wetu), kwa maana ingine ni kuwa wamalawi wanaamini na wanajua kabisa kuwa kama Mtanzania utaamua kuoga au kuvua samaki achilia mbali kufungua nguo kwa kutumia maji ya ziwa inakubidi kuwaomba ruhusa, angalia hii source "http://www.nyasatimes.com/malawi/2012/08/01/cold-war-over-lake-malawi-continues-ghost-of-kamuzu-nyerere-revisit-malawi/".
Wakati fulani nilikuwa Mbambay 2004-2008: nilipata faragha na mzee mmoja mstaafu serikali wa huko, katika kufahamu habari za mpaka akaniuma sikio " akasema kwa kusema ukweli haya maji ni ya Malawi, hata Mwl.Nyerere anafahamu hilo, ila kilichofanyika ni mwl. alimchukia Kamuzu baada ya huyo Kamuzu kutambua utawala wa makaburu na wareno wa msumbiji, kwa hio alimuona ni kikwazo, na pia bada huyo alikuwa anasema sehemu za Mbambay, mbiga na sehemu za kuvuka mto Ruvuma ni sehemu ya Malawi, hivyo Mwl. alikuwa anamtafutia sababu za kumwodoa jamaa". Na ndio maana sie Tanzania ramani zetu zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa wakati jamaa zetu mpaka upo kabla ya mbambabay - ufukweni mwa ziwa.
Tuzidi kujadiri - kama mtu ana reference zaidi anaweza weka hapa kwa ufahamu zaidi..