Njia rahisi ya kuleta 'sense' kwa Wamalawi: Tanzania itangaze kuanza utafiti wa mafuta Ziwa Nyasa!

Nadhani watu wanazungumzia kupeleka wanajeshi kule kwa urahisi sana. Hupeleki wanajeshi kwenye mpaka wa nchi nyingine bila kuwa tayari kupigana vita. Kuna vitendo ambavyo kisheria vikifanyika vinachukuliwa kuwa ni "act of war". Tanzania haipaswi kupeleka wanajeshi wake karibu na mpaka na Malawi bila kuwa tayari kwenda vitani. Swali, Watanzania mko tayari kwa vita siyo kwenda kujionesha tu. Nani kawaambia ati mkipeleka wanajeshi basi wamalawi watanywea? Na wenyewe si wana jeshi?

Unafikiri kuwa na wingi wa jeshi na silaha ndio kushinda vita? Lakini kubwa zaidi ni kuwa viongozi wetu tayari hawana ile cloud ya kuwa viongozi wa wakati wa vita. Kama kwenye amani wametutawala hivi wakati wa vita itakuwaje? Njia pekee ya kuleta hiyo heshima ni sisi kutangaza tunaanza utafiti wetu wa mafuta kwenye nusu yetu tukiheshimu mipaka yetu na hatutagusa nusu ya Malawi. Malawi watakuwa wametupiwa mpira!

Kama wao wanaamini ziwa zima ni lao basi wao ndio wafanye hatua ya kwanza vita.... hapo ndio JWTZ linapoenda kulinda mpaka wetu!

Mzee Mwanakijiji, nina kubaliana na wewe hapo kwenye utayari wa watawala wetu na wananchi kama tunaweza kufanya/kuingia vitani kwa sasa? ila hapo kwenye red labda kama unataka kuwatega Wamalawi kama watakubaliana na sisi kuwa mpaka wa Tanzania na Malawi upo katikati ya Ziwa - iwapo tutaamua kufanya utafiti wa mafuta!

Kama ni Tz itaamua kuingia katika mtego huo basi itakuwa ni tofauti na wao wanavyodai na kujua kuwa mpaka wa nchi hizi mbili upo ufukweni kwetu, ikimaanisha kuwa (maji ni ya Malawi na ufukwe ni wetu), kwa maana ingine ni kuwa wamalawi wanaamini na wanajua kabisa kuwa kama Mtanzania utaamua kuoga au kuvua samaki achilia mbali kufungua nguo kwa kutumia maji ya ziwa inakubidi kuwaomba ruhusa, angalia hii source "http://www.nyasatimes.com/malawi/2012/08/01/cold-war-over-lake-malawi-continues-ghost-of-kamuzu-nyerere-revisit-malawi/".

Wakati fulani nilikuwa Mbambay 2004-2008: nilipata faragha na mzee mmoja mstaafu serikali wa huko, katika kufahamu habari za mpaka akaniuma sikio " akasema kwa kusema ukweli haya maji ni ya Malawi, hata Mwl.Nyerere anafahamu hilo, ila kilichofanyika ni mwl. alimchukia Kamuzu baada ya huyo Kamuzu kutambua utawala wa makaburu na wareno wa msumbiji, kwa hio alimuona ni kikwazo, na pia bada huyo alikuwa anasema sehemu za Mbambay, mbiga na sehemu za kuvuka mto Ruvuma ni sehemu ya Malawi, hivyo Mwl. alikuwa anamtafutia sababu za kumwodoa jamaa". Na ndio maana sie Tanzania ramani zetu zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa wakati jamaa zetu mpaka upo kabla ya mbambabay - ufukweni mwa ziwa.

Tuzidi kujadiri - kama mtu ana reference zaidi anaweza weka hapa kwa ufahamu zaidi..
 
Wamalawi wamejua dhahiri kuwa Tanzania haina uongozi na haina amiri jeshi mkuu. Wako tayari kucheza makidamakida yao mpakani wakijua hawataguswa. Jamani Tanzania hatuna Amiri Jeshi Mkuu! Tuna Mr. Dhaifu na Spika dhaifu na waziri mkuu dhaifu ndiyo maana wanatuchokonoa machoni!
 
Nakumbuka kuna kampuni imepewa kibali cha kufanya utafiti kwa upande wa Tz!
Tena kuna post humu JF inataja mpaka iyo kampuni ngoja niisake iyo thread
Personally kama tungelikuwa na viongozi ambao wazalendo faster jamaa washasalim amri
 
Unacho sema ni kweli mkuu, yaani tunashindwa na Uganda ilivyo deal na Kenya kuhusu kisiwa ndani ya ziwa Victoria; Uganda aikulaza damu kwa kusubuli mambo ya majadiliano i.e KUBEMBELEZANA - mambo ya diplomacy yalichukua a back seat. Kinacho nishangaza mimi ni kuona nchi yetu anasuhasua katika suala hili la hatari, hivi kuna haja gani ya malawi kununua patrol boats zaidi ya kumi na nne, a very powerful RADAR - nasikia na airforce na washauri wa Kiyaudi pamoja na mazabazabina (Wingereza) sina shaka Waigereza hawa hawa ndio wanawapa kichwa Wamalawi, wala siwezi kushangaa kama awajapewa vitalu vya kuchimba visima vya mafuta na GAS katika ziwa hilo.

Kwa mawazo yangu Serikali yetu inapaswa kuwafahamisha Wamalawi kwamba wakiendelea na jeuri yao basi TANZANIA hiko tayali kwa lolote tunasema hilo wakati tuna mobilise drilling rigs kwenda ziwa Nyasa tuone watafanya NINI.

Mkuu haya ya wabunge kusema eti wanajeshi wetu watumike kulinda nguzo za umeme wenye msongo mkubwa wakisingizia kwamba wafisadi wamejipanga kuzifanyia hujuma pamoja na mabwawa ya hydro Electric - tahadhali hii naona ni ya uzushi tu wanajaribu kutisha Serikali ya JK ili aogope kuwachukulia hatua wahujumu uchumi, JK awezi kutishwa na NYAU bwana.

Ndugu yangu hapo kwenye red:,chondechode kwa viongozi hawa itakula kwetu, kwa taarifa yako - hata wao (viongozi wetu)wanafahamu kabisa kuwa mpaka wetu na Malawi haupo katikati ya maji ila upo ufukweni, yaani ukigusa maji tu basi ujue umegusa Malawi, kwa maana hiyo hao wanyasa na wamatengo wanapofua au kuoga achilia mbali kuvua samaki katika ziwa Nyasa wajue kabisa wanatakiwa kuomba ruhusa upande wa pili (Malawi) ili wapewe kibali. Hivyo hizo kelele wanazopiga mjengoni ni kujikakamua tu ili hali wakijua kuwa muda wowote Malawi wanaweza leta invoice ya sisi kutumia maji yao bila kibali, kama unabisha muulize hata kapteni Komba mbuge wao (mbinga Magharibi) anajua fully story, kwa issue hii ya Ziwa Nyasa hata tukiwa wazalendo kiasi gani hatuiwezi labda tuombe Nyerere afufuke.
 
Mkuu hivi Nyerere alihusika kweli katika uhamishaji wa mipaka? Mbona nilipo kuwa nasoma shule ya msingi tulikuwa tunachora Ramani ya Tanzania kwa kuweka mipaka katikati ya ziwa NYASA. Hata ukiangalia ramani ya Google Map utaona mpaka wa Tanzania na Malawi umewekewa a dotted line (zinazo fanana na mipaka ya kutenganisha mikoa nchini Tanzania) lakini wa Msumbiji na Malawi ambao huko katikati ya Ziwa umechorwa kwa solid line! Hii ina maana gani?

Mimi suala hili alijanigia akili! Swali - nani kabadirisha mipaka hii na lini? Suala la mipaka kati ya Hondurus na Venezuela lilisuruhisha kwa njia gani?
 
Kuna time nilifanyakazi huko kusini ziwani Nyasa, kuna mzee mmoja very famous huko (ni former senior government staff),aliniuma sikio kuwa "maji ni ya Malawi" ila tunatake advantage tu kwa Banda alikuwa muoga wakati huo 1960s-70s, maana kumbuka wakati huo tulikuwa tunapambana na ukombozi kusini mwa Afrika na nchi zote za kusini mwa Afrika zilikuwa kwenye allied ya "nchi za mstari wa mbeli" kwa ajili za kuzipa tafu "msumbiji - wareno/RENAMO, Zimbabwe - Ian Smith, S/Africa&Namibia - makaburu, Angola - Savimbi" ili ziwe huru na tulivu, kwa maana hio Zambia, Botswana, Malawi na Tanzania ndio zilikuwa huru na tulivu - ila Malawi kwa upande wake haikuwa mstari wa mbele na kinyume chake chini ya Kamuzu Banda ikawa na uhusiano wa kikaribu sana na Wareno kwa upande wa msumbiji na kwa Makaburu, kwa hio kwa Nyerere banda na Malawi yake ilikuwa ni obstacle kwa ajili ya ukombozi wa kusini na pia Banda alidai sehemu ya Kyela ni sehemu ya Malawi, in that case Nyerere akaamua kupiga mkwara na kupanga kumtoa noma Banda na hapo Nyerere akaamua na kudclere that mpaka ni katikati ya ziwa (according to Berlin conference na international Law),ila kulingana na soo za WWI wingereza kuchukua Tz ziwa likarudi Malawi.

au unaweza kucheki hizi source kwa msaada zaidi
1.
"http://www.nyasatimes.com/malawi/2012/08/03/malawi-says-lake-row-with-tanzania-to-be-resolved-amicably/"
2. "http://www.africareview.com/News/Malawi+vows+to+continue+oil+exploration+on+disputed+lake/-/979180/1468214/-/90tmymz/-/index.html"
3."http://www.trademarksa.org/news/tanzania-malawi-row-over-lake-nyasa-again"
4. "http://www.nyasatimes.com/malawi/2012/08/01/cold-war-over-lake-malawi-continues-ghost-of-kamuzu-nyerere-revisit-malawi/"

kwa source hizo naweza kukubaliana na yule mzee kuwa sie (Tz) ni wavamizi wa Malawi, na kwa jinsi viongozi wetu wanavyopenda sifa wasingekaa kimya na kuongea bungeni tu wakati meli za Malawi zinafanya business sehemu yetu, mbona huko ziwa Tanganyika kila wakati boat za DRC zinalipuliwa kila kukicha? au kama una jamaa yako yupo JWTZ muulize ni ziwa lipi kuna boat zetu za doria? atakuambia ni ziwa Tanganyika, Victoria bahari ya Hindi na hakuna kwingine... Membe ni vuvuzela tu, hapo wanaomba Nyerere afufuke ili awape ushauri ni nini cha kufanya, hivi kama eneo ni lako kweli unahitaji mazungumzo na mtu mwingine juu ya namna ya kutumia eneo lako?
 
Wakuu,
Pamoja na mjadala huu kuwa na hoja zilizo nzuri kwa maslahi ya taifa letu, upo uwezekano mkubwa kwamba, maadam mchokozi na watu wake nao wanajua Kiswahili, pengine wako hapa (JF) nasi wakifuatilia kila kinachoandikwa kwa sababu zao za kiintelijensia.
Hivyo tunapoendelea kujadili, si vibaya kutahadhari tusijikute tumemweleza adui kila udhaifu tulionao. Badala yake, tunaweze kujikita katika kuanika kile anachoendelea kufanya katika eneo letu na kile anachokusudia kufanya baadaye.
Wazee wa kule kanda ya ziwa Nyanza wana msemo; Zamani chui alikuwa hajui kukamata shingo la mawindo yake, alijifunza baada ya kusikia mawindo ya kinong'ona kwamba; ‘tunachomoka maana anakamata mikia, siku akikamata shingoni, tumekwisha'
 
Nadhani watu wanazungumzia kupeleka wanajeshi kule kwa urahisi sana. Hupeleki wanajeshi kwenye mpaka wa nchi nyingine bila kuwa tayari kupigana vita. Kuna vitendo ambavyo kisheria vikifanyika vinachukuliwa kuwa ni "act of war". Tanzania haipaswi kupeleka wanajeshi wake karibu na mpaka na Malawi bila kuwa tayari kwenda vitani. Swali, Watanzania mko tayari kwa vita siyo kwenda kujionesha tu. Nani kawaambia ati mkipeleka wanajeshi basi wamalawi watanywea? Na wenyewe si wana jeshi?

Unafikiri kuwa na wingi wa jeshi na silaha ndio kushinda vita? Lakini kubwa zaidi ni kuwa viongozi wetu tayari hawana ile cloud ya kuwa viongozi wa wakati wa vita. Kama kwenye amani wametutawala hivi wakati wa vita itakuwaje? Njia pekee ya kuleta hiyo heshima ni sisi kutangaza tunaanza utafiti wetu wa mafuta kwenye nusu yetu tukiheshimu mipaka yetu na hatutagusa nusu ya Malawi. Malawi watakuwa wametupiwa mpira!

Kama wao wanaamini ziwa zima ni lao basi wao ndio wafanye hatua ya kwanza vita.... hapo ndio JWTZ linapoenda kulinda mpaka wetu!

Mkuu kwenye situation "hostile" kama hiyo,huwezi kupeleka hao watafiti bila kuwahakikishia ulinzi wao.Wamalawi tayari wanawalinda watafiti wa "upande wao" ambao wako all the way hadi upande wa "Tanganyika/Tanzania" .Kama tayari wanafanya utafiti upande wa Tanzania,na sisi tukafanye utafiti upande wao?Na hata tukifanya upande wetu tayari wako hapo...
 
Kuna time nilifanyakazi huko kusini ziwani Nyasa, kuna mzee mmoja very famous huko (ni former senior government staff),aliniuma sikio kuwa "maji ni ya Malawi" ila tunatake advantage tu kwa Banda alikuwa muoga wakati huo 1960s-70s, maana kumbuka wakati huo tulikuwa tunapambana na ukombozi kusini mwa Afrika na nchi zote za kusini mwa Afrika zilikuwa kwenye allied ya "nchi za mstari wa mbeli" kwa ajili za kuzipa tafu "msumbiji - wareno/RENAMO, Zimbabwe - Ian Smith, S/Africa&Namibia - makaburu, Angola - Savimbi" ili ziwe huru na tulivu, kwa maana hio Zambia, Botswana, Malawi na Tanzania ndio zilikuwa huru na tulivu - ila Malawi kwa upande wake haikuwa mstari wa mbele na kinyume chake chini ya Kamuzu Banda ikawa na uhusiano wa kikaribu sana na Wareno kwa upande wa msumbiji na kwa Makaburu, kwa hio kwa Nyerere banda na Malawi yake ilikuwa ni obstacle kwa ajili ya ukombozi wa kusini na pia Banda alidai sehemu ya Kyela ni sehemu ya Malawi, in that case Nyerere akaamua kupiga mkwara na kupanga kumtoa noma Banda na hapo Nyerere akaamua na kudclere that mpaka ni katikati ya ziwa (according to Berlin conference na international Law),ila kulingana na soo za WWI wingereza kuchukua Tz ziwa likarudi Malawi.

kwa source hizo naweza kukubaliana na yule mzee kuwa sie (Tz) ni wavamizi wa Malawi, na kwa jinsi viongozi wetu wanavyopenda sifa wasingekaa kimya na kuongea bungeni tu wakati meli za Malawi zinafanya business sehemu yetu, mbona huko ziwa Tanganyika kila wakati boat za DRC zinalipuliwa kila kukicha? au kama una jamaa yako yupo JWTZ muulize ni ziwa lipi kuna boat zetu za doria? atakuambia ni ziwa Tanganyika, Victoria bahari ya Hindi na hakuna kwingine... Membe ni vuvuzela tu, hapo wanaomba Nyerere afufuke ili awape ushauri ni nini cha kufanya, hivi kama eneo ni lako kweli unahitaji mazungumzo na mtu mwingine juu ya namna ya kutumia eneo lako?

Mkuu nakushukuru sana kwa ufafanuzi wa kina; ndio nina ndugu yangu ni Kanali jeshini - Mambo yenyewe kam ndio haya naona Wamalawi wamekwisha tuzidi KETE na actually wanafanya uhungwana kutuachia tufanye tutakavyo kwenye ziwa
lao save uchimbaji wa MAFUTA.
 
Ndugu yangu hapo kwenye red:,chondechode kwa viongozi hawa itakula kwetu, kwa taarifa yako - hata wao (viongozi wetu)wanafahamu kabisa kuwa mpaka wetu na Malawi haupo katikati ya maji ila upo ufukweni, yaani ukigusa maji tu basi ujue umegusa Malawi, kwa maana hiyo hao wanyasa na wamatengo wanapofua au kuoga achilia mbali kuvua samaki katika ziwa Nyasa wajue kabisa wanatakiwa kuomba ruhusa upande wa pili (Malawi) ili wapewe kibali. Hivyo hizo kelele wanazopiga mjengoni ni kujikakamua tu ili hali wakijua kuwa muda wowote Malawi wanaweza leta invoice ya sisi kutumia maji yao bila kibali, kama unabisha muulize hata kapteni Komba mbuge wao (mbinga Magharibi) anajua fully story, kwa issue hii ya Ziwa Nyasa hata tukiwa wazalendo kiasi gani hatuiwezi labda tuombe Nyerere afufuke.

Mkuu hapo umenifumbua MACHO, ni kweli tujitia ujuwaji inaweza kula KWETU tukajikuta tunadhalillika kimataifa.
 
mkuu kwenye situation "hostile" kama hiyo,huwezi kuepeleka hao watafiti bila kuwahakikishia ulinzi,wao tayari wanawalinda wa "upande wao" ambao wako upande all the way hadi upande wa "tanganyika/tanzania" kama tayari wanafanya utafiti uapnde wa tanzania,na sisi tukafanye utafiti upande wao?

good direct to the point..watu wanaleta siasa hapa wakati tumeshaingiliwa ndani ya mpaka wetu..,eti tuanzishe na sie utafiti si utoto huo...wengine wameanza kusema eti mwalimu alichukua zanzibar na malawi ndio alikosea...ujinga mtupu tunashindwa kulinda mipaka yetu tunaanza kusingizia marehemu...nashindwa kuamini kama tunautaifa tena naona tujiandae kutawaliwa na yeyote kwa mwendo huu
 
Mkuu nakushukuru sana kwa ufafanuzi wa kina; ndio nina ndugu yangu ni Kanali jeshini - Mambo yenyewe kam ndio haya naona Wamalawi wamekwisha tuzidi KETE na actually wanafanya uhungwana kutuachia tufanye tutakavyo kwenye ziwa
lao save uchimbaji wa MAFUTA.

inawezekana kweli kabisa wanatufanyia uungwana ila kama tutaingiza timu...basi wale jamaa ninahisi ni wazalendo sana, tena wanawashangaa viongozi wao kwanini hawachukui hatua dhidi yetu - tena hii issue wao wanaichukulia kitaifa zaidi, yaani sisi kama tunataka kuwin hii issue labda tuunde kitu kama "mamlaka" ambayo itasimamia maendeleo ya eneo hili kwa faida ya nchi zote mbili na to take advantage ya kuhama kwa mpaka katika mto Songwe, kuna jamaa mmoja ambaye ni mwanajeshi wa(JWTZ)katika thesis yake hata yeye ni kama anakubaliana kuwa hii issue ni kama tunawatapeli ingawa kaiandika kidiplomasia sana, hebu soma comments za wamalawi hapa chini uone wanaichukuliaje hii issue

"Cant you see that the issue is not about the waters but the the oil? Tell me a country in Africa that has both peace and oil? Its the atsamundawa that are working behind the scenes. Open your eyes and look beyond the nose. Mayi anapweri anuwa mukuwadziwa bwinobwino koma?"

Like Thumb up 0
Reply
46
Geve Says: August 3rd, 2012 at 12:15 pm

"My people are destroyed for lack of knowledge. Because you have rejected knowledge, I will also reject you, that you may be no priest to me. Because you have forgotten your God's law, I will also forget your children (Hosea 4:6). Why fighting for the boundaries imposed by colonialists?? How told you that people living in the borders do not relate to each other by blood??"

Like Thumb up 0
Reply
45
2by2 Says: August 3rd, 2012 at 10:16 am

"zazibambo zodzola zimafuta zoyeretsa kuzinkhope ngati fanta n coke manja biiii nditimiyendo biiiiiiiiii.amalawi tidzaphunzira liti?chili chonse chili m'manja mwa ma foreigner WHY?ndimalo omwe kumagulitsidwa ndi amwenye,mabulundi,ma naigeria ngati kwao kuno.pomwe ife eni mtunda kulephera ndikuti ugule malo,lero mukufuna kubetsa nyanja chifukwa chokonda ndalama.mawa ndi mkuja akakuuzani kuti akulanda nyanja mudzadabwe?"

Like Thumb up 0
Reply
44
Ntaba Says: August 3rd, 2012 at 9:48 am

"Patriotic Tanzanian my foot. Why should people disguise themselves as patriotic tanzanian????You stupid dpp fool. Is there any connection between the international dispute between Malawi and TZ and your myopic thinking of bringing down JB's government??? Indeed there are people who do not wish this country well. You would be happy if your so called professor was still at the helm and continued torturing the innocent lives of Malawians???. We do not want the scarcity of fuel,sugar, bad governance to come back. All these were buried together with your fake professor. Mukagwere!!!!!!!!!!!!!!!!!"

Like Thumb up 0
Reply
43
Patriotic Tanzanian Says: August 3rd, 2012 at 6:56 am

"This time who is backing you up guys,The other time you were with Boers from South Africa.Shame on you betrayals,homosexuals this is why your land is cursed up to now you are suffering from extreme poverty and hunger,you are paying back the betrayal you did to your own brothers and sisters during African liberation struggle movement!If you don't want diplomatic way to solve this then military will solve this and we will see the consequences.We will fight until we bring down the leadership of your narrow minded Joyce Banda".

Like Thumb up 1
Reply
42
Friend of Malawians Says: August 3rd, 2012 at 4:29 am

"Thank you Tanzania for bringing together the people of Malawi! It seems that your language of intimidation is great for Malawian nationalism. Thanks ndugu you have brought Malawians together!!"

Like Thumb up 0
Reply
41
Friend Says: August 3rd, 2012 at 4:20 am

"Perhaps if our Tanzanian friends kept their noses out of the affairs and businesses of other countries they could better deal with their own domestic issues. Please consider handling corruption and graft in Tanzania first! We will talk with you as we continue to explore, no doubt you would do the same if you were in our position. Actually being the wa Swahili
that you are I am sure you could be exploring Lake Malawi as we speak!"

Like Thumb up 0
Reply

Kama Tanzania inaamini nusu ya Ziwa Nyasa ni mali yake kwanini wanasubiri kuwabembeleza Wamalawi kuhusu suala la kusitisha utafiti wa mafuta ili kupisha majadiliano? HIvi tumekuwa wasahaulifu hivi kiasi kwamba hatujui suala hili nusura litulete katika vita na Kamuzu Banda?

Jambo rahisi ni Serikali kuanza utafiti wa mafuta na gesi kwenye "upande wetu" na kutoa kibali kwa makampuni ya kimataifa kufanya hivyo. Wamalawi watafanya nini?

Mzee MM mbona tayari Ngeleja alishafanyia kazi hoja yako toka Januari, inawezekana waMalawi wamechukia baada ya sisi kuanza utafiti wa mafuta kule Kyela.

Angalia hapa chini:
Today's occasion of signing three PSAs is an important milestone towards exploration of hydrocarbons in Tanzania and East Africa at large. The Petrobras PSA is for hydrocarbon exploration in Block-8 deep offshore Tanzania, the Heritage PSA is for exploration in the Kyela Basin (northern and onshore portion of Lake Nyasa) and the Motherland PSA is for exploration in the Malagarasi Basin North West part of the country.
Source:
SPEECH BY WILLIAM NGELEJA, MINISTER FOR ENERGY AND MINERALS DURING THE SIGNING CEREMONY OF PETROBRAS, HERITAGE AND MOTHERLAND PRODUCTION SHARING AGREEMENTS ON 24TH JANUARY, 2012 | Tanzania news - TheHabari - Blog Tanzania
 
Halloo na wasiwasi ktk hizi post kuna informer wa malawi,na wanajaribu kutuingizia ktk vichwa vyetu kushindwa,tuwe carefull tunapoisoma post maana hata nao wanakijua kiswazi.ALUTA CONTINUA MESSAGE FROM ROCK CITY
 
inawezekana kweli kabisa wanatufanyia uungwana ila kama tutaingiza timu...basi wale jamaa ninahisi ni wazalendo sana, tena wanawashangaa viongozi wao kwanini hawachukui hatua dhidi yetu - tena hii issue wao wanaichukulia kitaifa zaidi, yaani sisi kama tunataka kuwin hii issue labda tuunde kitu kama "mamlaka" ambayo itasimamia maendeleo ya eneo hili kwa faida ya nchi zote mbili na to take advantage ya kuhama kwa mpaka katika mto Songwe, kuna jamaa mmoja ambaye ni mwanajeshi wa(JWTZ)katika thesis yake hata yeye ni kama anakubaliana kuwa hii issue ni kama tunawatapeli ingawa kaiandika kidiplomasia sana, hebu soma comments za wamalawi hapa chini uone wanaichukuliaje hii issue.

Mkuu yaani suala hili la Ziwa Nyasa ni kama michezo ya Mickey Mouse, buzz word hapa ni discrepancy, discrepancy even more discrepancies!! Waingereza walicho kuwa wanafanya hapa ni kuchezea lugha TU katika azma yao ya kuchanganya watu akili.

Kama kweli report na ramani zilizo tolewa na Serikali ya kikoloni ya Nyasaland kati ya mwaka 1920 - 30 ilionyesha mpaka huko katikati ya ZIWA, alafu cha ajabu Waingereza hao hao kati ya mwaka 1933-34 kwa upande wa Tanganyika walifanya kimaksudi kuonyesha kwenye maaadishi kwamba mpaka huko katikati ya ziwa lakini kwenye ramani wanaonyesha kwamba mpaka huko ufukweni mwa ziwa!! Hii maanake nini, walikuwa na ajenda gani ya SIRI?

Mkuu hivi Nyasaland ilikuwa ni koloni au Protectorate, sasa kama Waingereza walikuwa wanatawala Nyasaland na Tanganyika at the same time kwa nini walikuwa wanazungumzia suala hili with a folked tongue?

Mkuu hebu angalia statements hizi hapa chini zinavyo ji-contradict!

" I n his review of the legal evidence, Brownlie notices earlier discrepancies in the CARTOGRAPHY of the Lake, both before the I 9 I 4- I 8 war, and perhaps more significantly in the description and depiction of the boundary under the Mandate. Thus between 1924 and 1932 the British Annual Report on Tanganyika refers, although not always EXPLICITLY, to a CENTRE LINE as the Lake BOUNDARY. In 1933 and 1934 a DISCREPANCY appears between THE TEXT, which refers TO A CENTRE LINE, and the MAP which shows the EASTERN SHORE BOUNDARY!!!!.

Then from
1935 until 1938, as in the post-World War II reports to the Trusteeship Council, both TEXT and MAP refer to the eastern shore line. Official reports and maps produced in the Nyasaland Protectorate during the 1920 and 1930 also SHOW A MIDDLE LINE!!!!!!!. "

Waingereza bwana! Mtu unaweza kufikili suala zima walilichukulia kama watu wanao andikia URL ya wikipedia ambayo kila mtu yuko free kuongezea, kumodify au kupunguza maadishi.
 
Mwanakijiji,

Kwani kama "tukiwaachia" ziwa lote kuna tabu gani? Manake kama ziwa ni maliasili, ni maliasili kiasi gani tumeziachia kwa "wawekezaji" na maisha yanaendelea?
 
Nadhani watu wanazungumzia kupeleka wanajeshi kule kwa urahisi sana. Hupeleki wanajeshi kwenye mpaka wa nchi nyingine bila kuwa tayari kupigana vita. Kuna vitendo ambavyo kisheria vikifanyika vinachukuliwa kuwa ni "act of war". Tanzania haipaswi kupeleka wanajeshi wake karibu na mpaka na Malawi bila kuwa tayari kwenda vitani. Swali, Watanzania mko tayari kwa vita siyo kwenda kujionesha tu. Nani kawaambia ati mkipeleka wanajeshi basi wamalawi watanywea? Na wenyewe si wana jeshi?

Unafikiri kuwa na wingi wa jeshi na silaha ndio kushinda vita? Lakini kubwa zaidi ni kuwa viongozi wetu tayari hawana ile cloud ya kuwa viongozi wa wakati wa vita. Kama kwenye amani wametutawala hivi wakati wa vita itakuwaje? Njia pekee ya kuleta hiyo heshima ni sisi kutangaza tunaanza utafiti wetu wa mafuta kwenye nusu yetu tukiheshimu mipaka yetu na hatutagusa nusu ya Malawi. Malawi watakuwa wametupiwa mpira!

Kama wao wanaamini ziwa zima ni lao basi wao ndio wafanye hatua ya kwanza vita.... hapo ndio JWTZ linapoenda kulinda mpaka wetu!

Tunasubiri nini wakati Wa-Malawi wamepeleka Jeshi lao right there!!.......utapelekaje wawekezaji wako wakati wa-Malawi wana jeshi lao pale...........Unajua ukondoo wetu huu unatuponza sana..........watu wanatuchezea chezea tu huko mipakani...............hivi umeshawahi kufika kule ziwani hivi karibuni?.......kweli hali yetu Kijeshi ni mbaya kiasi hiki!!.. kwamba tunashindwa kulinda mipaka yetu.....dah
 
Mwanakijiji,

Kwani kama "tukiwaachia" ziwa lote kuna tabu gani? Manake kama ziwa ni maliasili, ni maliasili kiasi gani tumeziachia kwa "wawekezaji" na maisha yanaendelea?
Hapa umechanganya vitu viwili, haki ya nchi na uzembe wa nchi.
Haki ya nchi ni pamoja na kulinda eneo lake. Hiyo haihusiani na uzembe wa kutumia rasilimali wa nchi yetu.

Huwezi kwenda kulala kwa jirani yako eti kwasababu baba mwenye nyumba ni mlevi!
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom