Mkuu yaani suala hili la Ziwa Nyasa ni kama michezo ya Mickey Mouse, buzz word hapa ni discrepancy, discrepancy even more discrepancies!! Waingereza walicho kuwa wanafanya hapa ni kuchezea lugha TU katika azma yao ya kuchanganya watu akili.
Kama kweli report na ramani zilizo tolewa na Serikali ya kikoloni ya Nyasaland kati ya mwaka 1920 - 30 ilionyesha mpaka huko katikati ya ZIWA, alafu cha ajabu Waingereza hao hao kati ya mwaka 1933-34 kwa upande wa Tanganyika walifanya kimaksudi kuonyesha kwenye maaadishi kwamba mpaka huko katikati ya ziwa lakini kwenye ramani wanaonyesha kwamba mpaka huko ufukweni mwa ziwa!! Hii maanake nini, walikuwa na ajenda gani ya SIRI?
Mkuu hivi Nyasaland ilikuwa ni koloni au Protectorate, sasa kama Waingereza walikuwa wanatawala Nyasaland na Tanganyika at the same time kwa nini walikuwa wanazungumzia suala hili with a folked tongue?
Mkuu hebu angalia statements hizi hapa chini zinavyo ji-contradict!
" I n his review of the legal evidence, Brownlie notices earlier discrepancies in the CARTOGRAPHY of the Lake, both before the I 9 I 4- I 8 war, and perhaps more significantly in the description and depiction of the boundary under the Mandate. Thus between 1924 and 1932 the British Annual Report on Tanganyika refers, although not always EXPLICITLY, to a CENTRE LINE as the Lake BOUNDARY. In 1933 and 1934 a DISCREPANCY appears between THE TEXT, which refers TO A CENTRE LINE, and the MAP which shows the EASTERN SHORE BOUNDARY!!!!.
Then from 1935 until 1938, as in the post-World War II reports to the Trusteeship Council, both TEXT and MAP refer to the eastern shore line. Official reports and maps produced in the Nyasaland Protectorate during the 1920 and 1930 also SHOW A MIDDLE LINE!!!!!!!. "
Waingereza bwana! Mtu unaweza kufikili suala zima walilichukulia kama watu wanao andikia URL ya wikipedia ambayo kila mtu yuko free kuongezea, kumodify au kupunguza maadishi.
Iwapo lina mkanganyiko hivi, basi inawezekana kabisa tunaweza gawana pasu kwa pasu, ila nitakuwa na amani kama jamaa zetu (serikali) itakuwa inakusanya reference kama hizi kwa ajili kuweka mambo sawa iwapo ubishi utaanza. Ila Jamaa zetu (serikali)nao hawaaminiki, wanaweza kuchukua hii issue kama deal na wakapewa cha juu na kuacha ziwa linakwenda, maana issue hii ina reference nyingi sana.
Inawezekana kabisa Waingereza walifanya hivyo kwa kuamini kuwa Tanganyika haitakuwa yao (wanayo kwa dhamana ya UN) na Malawi ni yao ya kudumu, ndio maana wakachakachua