bht
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 10,336
- 1,862
Hii ni ya utu, akili na mwili...lol... Hii afya inaitwa afya ya Utu!! ..Lol! tofauti na ile ya mwili.... Ni afya muhimu !
Ntarudi nikawsome kama mli conclude UTU ni nini!
Hii ni ya utu, akili na mwili...lol... Hii afya inaitwa afya ya Utu!! ..Lol! tofauti na ile ya mwili.... Ni afya muhimu !
... Afya ya namna hii (afya ya Utu)... tafiti zinaonesha inaogeza CD4 ... kuliko mboga mboga na matunda...Lol ..sio utani mkuu ni kweli chukulia na Mwenzio ..very close ..in day to day ..life ...lakini full of vinyongo, chuki, hasira..na hisia hasi nyingine... lazima ikate CD4... yaani Msamaha wa dhati ni dawa...ya Asili ..au? lol ...wala sio jambo la kujishauri ..Just do it!!
Hata urafiki ni mahusiano...na naongelea mahusiano ya aina yote...kimapenzi..kirafiki..kindugu n.k
Swali...kumsamehe mtu kunahusiana vipi na utayari wako kurudia mahusiano yenu ya mwanzo???
Ni kweli hasira, vinyongo na visasi vinadororesha afya aisee...
Lakini bado na sisitiza 'kusamehe ni mchakato'...angalau kwa baadhi ya watu na kukingana na kosa na mahusiano ya wahusika
Boss mimi na wewe tupo kwenye ukurasa mmoja...ila naona tunatofautiana na MJ hapo chini.
Aiseee...
Kwahiyo mami unataka kuniambia kwamba kwa mtazamo wako mtu akikwambia amekusamehe ili uhusiano mliokua nao unakoma/hautorudi kama mwanzo anakua hajakusamehe???Kwanini unadhani kusamehe bila kurudi mlipokua sio kusamehe kweli?
mbu hakuna makosa ambayo'hayasameheki'
kitendo cha kutokusamehe ni 'kujiumiza mwenyewe'
ndo maana mimi na LIZZY tunasema una let go...
yaani unahakikisha hilo 'kosa' halikuumizi tena wala
husikii 'maumivu' wala 'kuwakasirikia' waliokuudhi....
unaweza hata kuzungumza nao tu..
inasaidia 'kiafya' ku let go....
yaani unafunga ukurasa.....
Hapo kwenye red ndo pagumu Mbu.
Kuna vitu havisahauliki labda kwa amnesia kwasababu vinakua vimeaffect maisha yako kwa kiasi fulani /wakati mwingine kwa kiasi kikubwa. Sasa kama hiyo effect/impact ni negative mtu utasahauje iwapo kila unapoamka kinakukudolea macho??No one should require you to do such thing...samehe kisha endeleza maisha yako vile uonavyo inakuafaa wewe FULL STOP.
... Ni kutokuwa na hata tone moja la hisia hasi za chuki, hasira, kinyongo, shaka nk kwa muhusika!!
MBU 'spouse' wako ndo utegemee makosa makubwa zaidi..
why?
kwa sababu mmekutana ukubwani na kila mtu ana malezi yake
mimi nafikiri makosa makubwa ni ya ndugu wa damu ambao mmekuwa pamoja..
na ambao wanajua kabisa 'walilokufanyia' linauma kiasi gani..
lakini kwenye 'mapenzi' kuna visasi na kukomoana sometimes
usiposamehe unakuwa'umemfanya ashinde' kwa sababu
pengine aliazimia kukufanyia jambo 'la kukuumiza' milele..
na wewe kweli 'umekubali' kuumizwa milele...
Ni kweli kabisa Lizzy, kusamehe kuna leta hisia nzuri sana kwenye moyo wako na ofcoz Bosi kuwa ni 'afya'.
ukisamehe unajisikia mwepesi na 'comfortable' sana hata ukiwa na wale waliokutenda.
Usiposamehe unaumia sana.
Lakini tukumbuke pia kwamba kusamehe ni process jamani!
nafikiri point yangu ni sio 'kutegemea the worst'
bali kutokuwa 'suprised' yakitokea
Umenikumbusha ile unasema "Ahaaa fulani bana namuamini sana hawezi kunifanyia jambo lolote baya"
The Boss hii nimeipenda ingawa ningeomba unifafanulie zaidi kwani katika hii post yako tuko ukurasa mmoja BUT kulet it go unakokuzungumzia wewe na mimi ni tofauti! Nahisi kuwa wewe unazungumzia kulet it go but usirudie uhusiano mlokuwa nao mwanzo ambayo kwangu mimi bado huja-let it go but umehold it freely!
Ni nini maana halisi ya kusamehe??
Je ukimsamehe mtu unalazimika kuwa karibu yake tena?? Kurudiana kimapenzi kama ndivyo mlivyokua mwanzo?? Kuongea mara kwa mara kama ndivyo mlivyokua mwanzo? Kutembeleana mara kwa mara kama ndivyo mlivyofanya mwanzo??
Nauliza kwasababu mara nyingi nimeona/sikia watu wakisema ''mi nilidhani umenisamehe/umemsamehe'' pale wanapotaka mambo yarudi kama mwanzo/au hata yawe zaidi na kuambiwa kwamba haiwezekani. Ina maana ukimsamehe mtu moja kwa moja unategemewa/una jukumu la kumchukulia/treat kama vile hilo kosa alilofanya halikuwahi kutokea?
Binafsi naamini kwamba kumsamehe mtu ni kile kitendo cha kuachilia (letting go) kile kilichotokea. Kumruhusu awe na amani..na kufungua ukurasa mpya ambao unaweza ukachagua awepo ndani yake au asiwepo na sio kukifuta kabisa alichofanya na kulazimika kurudi mlipokua mwanzo bila mhusika (mkosewaji) kutaka/penda kufanya hivyo. Yani inawezekana kumsamehe rafiki mwizi bila kumkaribisha tena nyumbani kwako...kumsamehe mke/mume/mpenzi cheater bila kurudiana nae tena..kumsamehe ndugu/rafiki mmbea bila kumshirikisha mambo yako tena. I don't know...inawezekana kwa kufanya hivyo mtu anakua hajasamehe ila ndivyo nnavyoamini na kufanya pia...hata mimi siwezi lazimisha/taka/tegemea mtu niliyemkosea na akanisamehe kurudisha mahusiano yetu ya mwanzo kwasababu tu ameniambia ''NIMEKUSAMEHE''. Ntategemea anipotezee/awe karibu na mimi kwasababu anapenda/taka kufanya hivyo na sio kama jukumu linalofuatana na msamaha wake.
We unaonaje...?
...mwj1, ndio kusema kwako wewe kuna nafasi kubwa ya 'baby come back' sababu msamaha wako hauna masharti, au nimekusoma vibaya?
Little X aksante- kutokumbuka ya nyuma.... Je unapokatisha mahusiano baada ya kusamehe ni kweli kuwa hutoyakumbuka yakotokezea hadi ukakatisha mapenzi yenu?Kusamehe inamaanisha kutokumbuka ya nyuma.
Loading...
Kwahiyo hata kama ni mwizi unajifanya kama vile sio mwizi kisa umemsamehe???
Aiwezekani kwako kumsamehe mwizi hata kama ujui kama atendelea na tabia hiyo? Kusamehe akugarantee mtu kuacha tabia yake!
...mwj1, ndio kusema kwako wewe kuna nafasi kubwa ya 'baby come back' sababu msamaha wako hauna masharti, au nimekusoma vibaya?
Kwahiyo hata kama ni mwizi unajifanya kama vile sio mwizi kisa umemsamehe???
Aiwezekani kwako kumsamehe mwizi hata kama ujui kama atendelea na tabia hiyo? Kusamehe akugarantee mtu kuacha tabia yake!
Mie kwa maoni yangu kama mko kwenye mapenzi na mwenzio akakukosea na kosa lake lilimfanya yule aliyekosewa awe tayari kuvunja uhusiano wa kimapenzi kati yao basi anapokuomba samahani na kuomba muendelee na penzi lenu inapendeza zaidi kama utamtamkia kwamba umemsamehe na kumpa nafasi nyingine ya kuendelea na penzi lenu. Sioni kama ni sawa kumtakia mkosaji kwamba nimekusamehe kosa lako na wakati huo huo unashikilia uamuzi wako wa kwamba penzi lenu limefikia tamati, kusema kweli mkosaji katka hali kama hii haamini kabisa kwamba samahani yake ilipokolewa na hivyo ataendelea kuwa na donge lake kwa muda mrefu ujao na huku akiamini kabisa kwamba samahani aliyoiomba haikukubaliwa.
The Boss hii nimeipenda ingawa ningeomba unifafanulie zaidi kwani katika hii post yako tuko ukurasa mmoja BUT kulet it go unakokuzungumzia wewe na mimi ni tofauti! Nahisi kuwa wewe unazungumzia kulet it go but usirudie uhusiano mlokuwa nao mwanzo ambayo kwangu mimi bado huja-let it go but umehold it freely!
Lizzy mpenz sijui kwa nini nimeijenga imani juu ya Msamaha wa kusahau na kurudi kama mwanzo! Huwezi nambia nimekusamehe halafu haturudiani kuwa pamoja!!! Kwangu ni umekubali YAISHE kuwa huna kinyongo na mimi lakini unayakumbuka niliyokukosea....Mbu kama sijakwambia YAMEKWISHA, you are still in my heart baby.
Mbu calm down......jamani jamani jamani.....!
kaka mimi bado sijakuelewa bana.
unamaanisha kwa wale wanaoachana hawajasameheana?
aisee mimi mwenzenu ndio nilipokwama hapa, nioneeni huruma!!!
yaani msamaha maana yake nirudiane na mwenzangu, otherwise sijamsamehe?
hebu nifafanulie bana, maana nipo kwenye exact situation...natakiwa nisamehe na kumrudia
SIWEZI AISEE!
Mwanajamiione hebu nionee huruma bana,.....
huo msamnaha wa masharti bana.... kumsamehe mtu haina maana kurudiana bana....plssssss!
au nakuelewa vibaya?.....kiukweli nimechanganyikiwa na hizi post zenu wanajamiiforums....
mke/mume baada ya abusive relationship (psychological/physical or both) kamtelekeza mume/mke zaidi ya mwaka mmoja...kila mtu akaendelea na maisha yake...kwakuwa upande ulodhulumiwa umeamua kudai/kutoa talaka kipatikane cheti cha RITA, mtuhumiwa anaomba msamaha ati mrudiane... na asiporudiana nae bado hajamsamehe? hapana...
...mbu nipo kwenye situation hii. Potelea mbali kama msamaha wangu hautaeleweka, kurudiana nae sitaki!