Hadi leo sielewi shida ni nini, mimi binafsi siwezi na sidhani kama nitakuja kuweza kufanya ngono na mwanamke asiye wangu!

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Salamu nishamuachiaga ndugu yangu GENTAMYCINE na ndugu zake wa Butiama & Nyamuswa kina Cognizant

Wakuu mimi binafsi huwa sijielewi nina matatizo gani!,yawezekana nikawa dhaifu kwa baadhi ya watu hapa JF lakini pengine yawezekana ndivyo nilivyo!

Tangu nimekuwa mtu mzima huwa sitamani mwanamke tofauti na mwanamke wangu anayenivulia chupi!

Sometimes huwa nikiwaga na washikaji zangu viwanja (Sehemu za starehe) wakati wenzangu baada ya kulewa wakitamani kila mwanamke mimi kwangu mambo huwa tofauti!,Kwanza huwa nikilewa sitakagi kabisa mambo ya wanawake wa kwenye ma-bar!, hadi jamaa wananiitaga kuwa nina misimamo!

Kiukweli mimi huwa nikinywa pombe huwa sitaki kufanya ngono/mapenzi na mwanamke ambaye sijamzoea au ambaye si mwanamke wangu!!

Huwa nikisafiri kuelekea mikoani kwenye shughuli zangu naweza kukaa hata mwaka bila kufanya ngono kwasababu huwa nina kinyaa mno kufanya ngono na mwanamke tofauti na niliyemzoea,kiukweli huwa naonekana kituko lakini hivyo ndivyo nilivyo!

Huwa sitamani ovyo wanawake barabarani hata akiwa mzuri vipi,kiukweli hadi huwa najishangaa nikoje lakini uenda hivyo ndivyo nilivyo,na nadhani hali hii pia imepelekea kusevu pesa ya kutosha kwasababu kama tujuavyo wanawake wengi ni wanyonyaji kama kupe!

Huwa nikiwa na mwanamke nikiyemzoea naenjoy sana na huwa namfaidi sana na huwa nikiwa peke yangu sitamanigi kabisa mwanamke mwingine tofauti na niliyemzoea!, Mwanzo nilidhani uenda likawa limbwata lakini huwa nikikosana na mwanamke wangu niliyemzoea tukaachana huwa inanichukua muda mrefu hadi tena kuja kutafuta mwanamke nitakayempenda na kuzoeana naye kisha tukaanzisha mahusiano!.

Huwa nawashangaa sana washikaji zangu ambao kila Bar tutakayoenda ni lazima watoke na wanawake,kiukweli kwangu huwa tofauti na huwa nina kinyaa sana na wanawake ambao huwa hatujazoeana!.

Nimewahi kujaribu kuwa kama washikaji zangu lakini nikashindwa kwasababu naonaga kama mwanamke ambaye sijamzoea ni mchafu kuliko kawaida!

Wakuu nyie mnawezaje kuwa na michepuko kila kona?
 
Back
Top Bottom