Nini dhumuni la Serikali kuanzisha tahasusi hii ya biashara ikiwa na somo la 'Islamic Knowledge'?

Serikali kupitia TAMISEMI imetangaza ongezeko la tahasusi mpya kadhaa ambazo vijana wetu watatakiwa kusoma, nimeona nyingi haziridhishi labda zimewekwa kimkakati...
Wala musihofu, Mungu akiwa upande wetu hawatuwezi, si munajua hawa jamaa wako nyuma kwa kilakitu? Hata wapandishwe watashuka tu.
 
Serikali kupitia TAMISEMI imetangaza ongezeko la tahasusi mpya kadhaa ambazo vijana wetu watatakiwa kusoma, nimeona nyingi haziridhishi labda zimewekwa kimkakati...

Labda hao watakuwa wanajifunza Islamic business and banking.
 
Hapa kuna jambo. Jambo hili halikubaliki na halitakubalika kamwe mpaka mwisho wa dunia.

Baada ya kufaulu kumdanganya Mama kwa kiwango cha kimataifa kwa ajili ya maslahi yao, sasa wameamua kummalizia kabisa.

Wizara ya Elimu kuanzisha Tahasusi ambayo ndani yake kuna somo la dini, ni kummalizia kabisa mama.

Nashauri, Tahasusi hii ifutwe mara moja ili kuepusha vurumai zisizo za lazima.
 
Mama anaupiga mwingi
 
Kwa akili hizi za viongozi wetu wanafunzi kupewa maarifa ya ujarasiliamali wa mambo ya e-commerce na fursa kama za ‘dropshipping’, fulfilment services, etc hadithi za 5th Industrial Revolution.

Watu wanafundisha watoto wao jinsi kuangalia fursa za 5th Industrial Revolution; sisi kama nchi hata vigezo vya kutimiza 1st Industrial Revolution bado.

Sasa kuna wataalamu wangapi hapo unahitaji kwenye gap from 1st-5th Industrial Revolution ambao wanahitajika. Sisi tunawaza dini.

Hayo masomo ya dini yangekuwa yanatolewa huko kwenye vyuo vya dini sawa, lakini kuingiza kwenye mainstream education ni ushamba. Vyuo vinaweza fundisha shahada za Islamic studies au Religious studies za dini nyingine (this is theology). Lakini kuweka combination za dini kwenye mainstream.

Watanzania ni muda wa ku-demand watu wenye uwezo kuongoza hii nchi CCM kazi imewashinda.
 
Dini ya kiislamu ina mfumo kamili wa kibiashara ulioelezwa vzuri xn kwenye Quran, utaskia tu benki za kiislamu ulishawahi kuskia benki za ukristo?
 
Hapa kuna jambo. Jambo hili halikubaliki na halitakubalika kamwe mpaka mwisho wa dunia...
Acheni ushamba hapo Uganda tu A level zote kuna combination mfano HED yaani History Economics na Divinity. Na hiyo divinity ni principle kabisa sio subsidiary. In fact ili udahiliwe masomo kama sheria basi unapaswa usome walau History, literature na Divinity!!!

Nashangaa hapa Tanzania imekua kitu cha ajabu sana, jamani safirini nchi za wenzenu.
 
Hii nchi sio ya kislamu na haitumii sheria za kislamu
Ukishasoma utaenda tumia wapi
Acha ujinga basi NYONYO.Kuna wanafunzi Waislam wamesoma vyuo vya kidini kama University of Arusha (UOA),chuo cha kiasbato.Pale wanafundisha baadhi ya masomo katika shahada zao ambayo ni ya kiimani na wanafunzi Waislam wanasoma na wanafaulu.Sasa wameenda wapi.Si wapo Tanzania hapahapa tena wanafanya kazi katika sekata mbalimbali na wemgine wanafanya kazi nje ya nchi.
 
mie nadhani ni muhimu sana ili tuwe na wachumi na wafanyibiashara wenye Imani thabiti, wanaomjua Mungu, wenye hofu ya Mungu, wa kweli, wa uaminifu, wasiopenda rushwa hongo na udanganyifu 🐒

inahitajika wachumi na wafanyibiashara walipakodi kwa hiari bila kuibia serikali n.k🐒

rejea machumi na mafanyabiashara yasio eleweka dini zao ndio hayo mafisadi na mavuruga uchumi 🐒
Naamini Watanzania wengi wamelelewa katika msingi ya kidini iwe uislamu,ukristu au uhindu lakini bado kuna ufisadi,hivyo kuweka somo la dini kwenye tahasusi sidhani kama itapunguza ufisadi.
 
Acheni ushamba hapo Uganda tu A level zote kuna combination mfano HED yaani History Economics na Divinity. Na hiyo divinity ni principle kabisa sio subsidiary. In fact ili udahiliwe masomo kama sheria basi unapaswa usome walau History, literature na Divinity!!!

Nashangaa hapa Tanzania imekua kitu cha ajabu sana, jamani safirini nchi za wenzenu.
Tanzania Kuna ushamba uliokithiri especially kwa baadhi ya watu wanaodhani kuwa wao ndiyo binaadam peke yao na wenye akili.Kuna wakati mtu anakataa kitu ambacho hana ujuzi nacho.Nakumbuka DP world.Watu walitoa mimacho na mapovu utafikiri wana kifafa.Vitisho kibao.Sasa hivi siwasikii tena.Hebu tembeleeni TPA -Dar.
 
Serikali kupitia TAMISEMI imetangaza ongezeko la tahasusi mpya kadhaa ambazo vijana wetu watatakiwa kusoma, nimeona nyingi haziridhishi labda zimewekwa kimkakati.

Moja ya tahasusi, si kwa ubaya, ila nadhani wengi tungependa kufahamu kuhusu hii combination mpya ya Biashara inayojumuisha masomo ya Economics, Business Studies na Islamic Knowledge. Hapo somo la Islamic Knowledge linahusika vipi na masuala ya biashara?

Ni bahati mbaya au makusudi. Huenda nimeachwa na mambo ya kisasa lakini kwangu bado haileti maana yoyote.

View attachment 2940349
Dhumuni lao haswa ni kutaka kuendeleza ujinga kwa wananchi wake.
 
Acheni ushamba hapo Uganda tu A level zote kuna combination mfano HED yaani History Economics na Divinity. Na hiyo divinity ni principle kabisa sio subsidiary. In fact ili udahiliwe masomo kama sheria basi unapaswa usome walau History, literature na Divinity!!!

Nashangaa hapa Tanzania imekua kitu cha ajabu sana, jamani safirini nchi za wenzenu.
Tanzania kuna bank ngapi za kiislamu zinazofuata sharia law au biashara unazojua wewe ambazo hazipo kutafuta maximum profit zitakazo waajiri hao watoto.

Unawafundisha watu biashara ya kiislamu kwenye nchi ambayo uchumi wake unaendeshwa kibepari halafu graduates wakienda kuomba kazi ata kwa Bakhresa anaesaka maximum profit unazani yupi atakuwa ana advantage kupata nafasi. Kati ya mwanafunzi wa sharia na aliepitia circular curriculum.

Huko baadae mtaanza kusema waislamu wanabaguliwa kwenye ajira Tanzania.

Wewe unajua bank hata moja au biashara inayofuata sharia law (faida ndogo) Tanzania au duniani. Huo ni mtego mnaingizwa watoto wenu wawe disadvantaged huko mbele. Nyie udini umewajaa mnashangilia tu, yaani ata akienda ulaya na degree yake kupata kazi iwe shida.
 
Back
Top Bottom