Hebu turudi nyuma kidogo,"Mikingamo... Sasa vita vimetangazwa jama, wananchi wote tuwe imara, vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi"
Nini kulikuwa chimbuko la kuanzishwa kwa vita dhidi ya wahujumu uchumi, walanguzi na wafanya magendo?
Sheria ya Uhujumu Taifa ya mwaka 1984 bado iko hai, kwa nini haitumiki?
Naona wachangiaji wote wanasahau kwamba zoezi hili lilikuja baada ya lile jaribio la kuipindua serikali ya Nyerere.
Pamoja na matatizo yaliyotokana na vita ya Kagera, miaka ya '80 mwanzoni viwanda vyetu bado vilikuwa vina uwezowa kutosha kuzalisha mahitaji yetu ya ndani. Kilichotokea ni kwamba; kuna kikundi cha wafanya biashara ambao kwa makusudi walikuwa wanahodhi bidhaa (na wala hawakuwa wanauza) na kusababisha upungufu mkubwa sokoni. Mojawapo ya conspiracy theories wakati ule, ilikuwa mara tu baada ya mapinduzi, maduka yangefurika bidhaa ili kushawishi uungwaji mkono na wananchi.
Yaliyofuatia kwenye kamata-kamata ni matokeo ya utekelezaji mbovu wa watendaji ambapo hata walanguzi wa sigara na vibiriti walijikuta ndani ya lupango. Hata hivyo waliokuwa watu wazima wakati ule, mtakubaliana nami kwamba uungwaji mkono wa operesheni hiyo ulikuwa mkubwa sana miongoni mwa wananchi wa kawaida na ni sehemu ya umaarufu aliojipatia Sokoine wakati huo akiwa Waziri Mkuu.
Kwa mazingira ya sasa hivi, mwanasiasa yeyeto anaweza kupanda chati kwa kuwakusanya MAFISADI na kuwasweka ndani; hata kama wakishinda kesi baadaye, naamini wananchi wengi wataandamana kumuunga mkono! Mheshimiwa Masha upo hapo???