Saalah (Silent Ocean): Anavyotakatisha na kutorosha pesa nchini, Uhujumu Uchumi, Kuteka na Kutesa watu, anavyolindwa na viongozi

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
810
2,851
Utangulizi wa kunukuu maelezo ya Muhanga aliyetusaidia kujua undani wa hizi operations za kampuni ya Silent Ocean Nchini, zikiongozwa na CEO wake, Saalah Mohammed, mdogo wake na GSM.

Hapo nikapokea simu kutoka kwa Salah (C.E.O) au Simba wa Bahari akinitaka ndani ya wiki moja niwe nimetimiza hela za transifer kinyume na hapo basi ndipo nitakapo uona ubaya wake.

Kwakweli kibinaadamu pale nilichanganyikiwa sikua na akili ya kufanya maamuzi sahihi ndipo nilipo waita baadhi ya ndugu na jamaa nyumbani Kariakoo Kipata nikawaeleza hali halisi ijapo kuwa wote hawa walikua wananidai pesa za mizigo China na kawaida fedha hua ina mchakato wake mpaka inalipwa China.

Boss Saalah akawa ananitaka tena ofsini kwake mara hii nilienda na ndugu mmoja anaitwa Nundu Nevin kwasababu niliingiwa na woga na hofu kubwa sana kimaisha. Ndipo boss Salah akaniambia nihakikishe nalipa hela zake zote ndio utakua usalama wa maisha yangu kinyume na hapo basi nitaujua uhalisia wake na upande wake wa pili wa shilingi ambao sijawahi kuona katika maisha yangu. Kwa kitisho hicho hofu kubwa ilitanda moyoni sikuweza kuwa na maamuzi makini.

Kwa hali hiyo ilinibidi kukubaliana na uamuzi wake wa mimi kukabidhi kwake mali zote za dukani, za store, pesa taslimu na mizigo yote ambayo ilikua njiani kutoka China katika kampuni yake pia ilichukuliwa.

Pia aliniambia nilete pesa zote za bank ambazo tuliomba mkopo mimi na Ndugu yangu ………………….. mwenye no ya simu …………… ambae pia aliweka dhamana ya nyumba yake ya Dodoma kwaajili ya mkopo wa kiasi cha sh 90,000,000, ambapo pesa hizi zote nilizepeleka ofisini kwake. Chumba changu ambacho nilikuwa nafanyia biashara kikauzwa kwa sh 80,000,000 cash kwa ndugu mmoja anaitwa CHAULA pesa hizi zote zikaenda kwa boss Salah.

Ndugu Salah boss wa kampuni ya SILENT OCEAN baada ya kutaifisha mali, pesa na thamani zote nilizokuwa nazo alihaidi kwa kinywa chake, Kwamba tutapiga hesabu na pesa zinazozidi atanirudishia, lakini mpaka leo toka june 14 /2022 hakuna jambo lolote lililofanyika kila ninapoenda ofisini kwake naambiwa hayupo na muda mwingine yuko bize na vikao, mara ya mwisho niliambiwa na secretary wake Sabrina kwamba atanipa appointment ya kukutana nae lakini nikimuuliza anasema boss hajanipa jibu.

Kwakweli nimetumia muda na nguvu nyingi sana kufanyakazi za kampuni ya boss Saalah nimekuwa mwaminifu na barozi mzuri kwa wafanya biashara wa soko la kariakoo kinacho niumiza pamoja na yote yaliyotokea hakujali mazuri yangu ambayo nimeyafanya na hata kile kidogo nilichokuwa nacho nimepoteza kwa nguvu na hatua ambazo boss Salah alitumia kutaifisha mali zote nilizokuwa nazo hakuthamini utu wala ubinadamu ukilinganisha na uhusiano ambao tayari ulishajengeka kati yetu.


“ELIUD GASPA”. Mwisho wa kunukuu maelezo yake.


MTIRIRIKO WA MATUKIO, NA MATENDO ULIVYOKUWA NA MAMBO MACHAFU YANAYOFANYWA NA SILENT OCEAN YAKISIMAMIWA NA CEO WAKE, SAALAH.

Huyu kijana anayeitwa Eliud Gaspar Mbwillo (Muhanga wa kutojua), kwa kabila ni Mkinga alikuwa ni mmoja wa vijana wanaofanya kazi ambayo wao wanajua ni kazi ya marketing ya wafanyabiashara kusafirisha mzigo kutoka China kuleta Tanzania kupitia kampuni ya Silent Ocean.

Kama tunavyojua kuwa wafanyabiashara wengi Kariakoo kwa sasa ni wakinga, hivyo walikuwa wanamtuma kijana huyu kuchukua pesa na kuzipeleka Silent Ocean kwa ajili ya kulipia mizigo Viwandani huko China.

Salaah alikuwa anaangalia wanaoleta pesa na akaona huyo kijana ni top performer, yaani siku amefeli sana basi kaleta milioni mia nne (400,000,000/-). Baada ya Salaah kuona hivyo ikabidi amuagize mfanyakazi wake ampigie waje waonane.

Ndipo wakaonana na akampongeza kwa kazi na kumpa majukumu yafuatayo;

  • Ahakikishe Wafanyabiashara wote wa kabila la wakinga ambao walikuwa wanafanya nao biashara na wakakosana wanarudi na kutumia Silent Ocean.
  • Atamfungulia nae biashara ya nguo, aache biashara yake ya Uwakala wa Pesa wa Mabenki na mitandao ya simu.
  • Akamwambia aweke juhudi na muda mwingi katika kazi za marketing za Silent Ocean.
  • Akamuagizia mzigo wa nguo na kumkopesha wenye thamani ya dola 235,000/-.

NB: Hawa vijana wanafanya kazi wanayoijua ni kutafuta masoko kwa ajili ya wateja wanaosafirisha mizigo, lakini hawajui kwa undani nini kinatokea, kama ifuatavyo;
  • Wanakusanya pesa na kuzipeleka Silent Ocean na zinafanyiwa exchange
  • Wafanyabiashara hao wanapouza bidhaa zao hawapeleki pesa katika Taasisi za fedha, bali wakikusanya pesa wanazipeleka Silent Ocean.
  • Wakizipeleka kama ni Tanzania Shilingi na wanataka kulipia mzigo basi Silent Ocean wanampa rate ya kuchenji toka Tshs hadi Yuan ya China, hivyo la kwanza anafanya biashara haramu ya kubadilisha pesa (black market ya bureau de change), maana hana kibali cha kazi hiyo toka Benki Kuu.
  • Kama ni USD pia anawapa exchange rate ya Chinese Yuan na wanabadili ile pesa kuwa ya China. Kotekote anafanya biashara ya kubadili pesa.
  • Akishafanya exchange ya hiyo pesa anatoa maagizo kwa ofisi yake ya China inafanya malipo kwa kiwanda husika kwa kiwango kilicho kwenye invoice ya mteja huyo. Hivyo hapo mfanyabiashara wa kariakoo anakuwa anafanya transfer ya pesa kutoka kwenye uchumi wetu bila kufuata taratibu na sheria za fedha kama zinavyotolewa na benki kuu.
  • Kumbuka wanachukua hadi pesa haswa USD toka kwa wafanyabiashara wa DRC, Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia n.k. hizi mara nyingi zinakuwa kwenye USD.
  • Wanatumia njia haramu kusafirisha dola toka Tanzania kwenda nje ya Tanzania, kumbuka mwaka 2017 zilikamatwa USD 750,000/- pesa za Salaah, ambazo Mzee mmoja ustaadhi alikuwa amebeba kwenye begi anaenda nazo China zikakamatwa, na enzi hizo kama unavyojua hizo pesa zilitaifishwa na Serikali.
Kwa hiyo kiufupi Silent Ocean/Salaah wao ni taasisi ya pesa, inakusanya pesa, inabadili pesa bila kibali, inatorosha pesa za kigeni kutoka Tanzania kwenda kwenye matawi yake nje ya Tanzania bila kufuata sheria zilizowekwa.

Katika kufanya hivyo, unakuta wafanyabiashara wengi wa kariakoo hawaweki pesa benki, hawana transaction history sababu njia wanazotumia kufanya transfer ni haramu. Na hapa nitoe angalizo kwa watu wa TRA na bandari, wanapomtolea mtu mzigo aambatanishe na slip ya pesa alizolipa toka benki zetu, au kama anasema alienda na cash basi aonyeshe kibali cha Benki Kuu Cha kumruhusu kutoka Nchini na kiwango hicho kikubwa cha pesa. Sasa wewe unapokea mzigo kama maiti, unajuaje huenda zimenunuliwa na pesa za ugaidi zije kusafishwa? Hata vitu hivi vidogo kwenye mafunzo yenu au uzoefu wa kazi hamuoni?

Ndio maana ni rahisi kukuta Kariakoo kuna mfanyabiashara amenunua ghorofa la bilioni 10 kariakoo lakini kodi kwa mwaka analipa shilingi milioni tatu, na watu wa TRA wamelala usingizi wa pono au basi ni asali imewalevya.

Hivyo wanachokifanya Silent Ocean, kwanza ni uhujumu Uchumi, pili kinawafanya wafanyabiashara wengi wawakimbilie, na mwisho wa siku wanakuwa na competitive advantage dhidi ya kampuni zingine zinavyofanya kazi za usafirishaji, na mwisho wa siku ili nao waweze kusurvive nao wameanza mtindo huo.

Hivyo hatua zisipochukuliwa basi pesa nyingi za kigeni zitakuwa zinachukuliwa kila siku nchini kwa njia hizo na ili kuzipata itabidi kila siku serikali iwe inakopa ili kufidia upungufu wa fedha za kigeni.


ELIUD ALIVYOPATA HASARA
Baada ya Eliud kupewa mkopo wa nguo za biashara ni kama kichaa kilimuingia, wakawa karibu sana na Salaah, hana appointment kumuona boss, hata usiku was aa 9 anampigia simu na boss anapokea, yaani wakawa maswahiba sana.

Sasa unajua sisi waswahili ukishakuwa karibu na boss akawa na motisha sana kufanya kazi, biashara yake muda mwingi akawa anaisimamia kijana wake wa kazi anaitwa Pius.

Akafikia level simu moja wa Salaah kuwa lipa China pesa kwa mtu Fulani nitaleta inalipwa na baadae anakusanya ile pesa ana anapeleka. Na watu wengi hasa jamii ya wakinga na wengine walikuwa wanamuamini, hivyo alikuwa anapewa pesa nyingi kupeleka na zilikuwa zinafika bila shida.

Baada ya muda akang’amua kuwa pesa aliyonayo na ambayo inadaiwa Silent Ocean kuna upungufu, maana alikuwa hana mhasibu (jambo ambalo anakiri ni makossa yake maana mara nyingi Salaah alimshauri awe na mhasibu aliyesomea), kwa hiyo pesa za biashara zake na anazokusanya za Silent Ocean zote zilikuwa zinawekwa kapu moja.

Ndipo akaomba kumuona Salaah na akamueleza anaona kuna upotevu wa pesa, akaomba amsaidie ili aweze kutrace na kujua hizo pesa zimepoteaje, ndipo Salaah akamgeuka na kumwambia yeye anachotaka ni pesa zake na asipolipa zote ndani ya wiki moja maisha yake yatakuwa hatarini maana yeye anaujua upande wake mmoja na ule mwingine haujui na sasa ndio muda umefika wa kuujua.

MATESO MAKALI KWA PIUS, MFANYAKAZI WA ELIUD

Nakumbuka alimpigia simu mtu ambaye kwa maelezo ya Salaah ni mtu wa TISS, huyo mwamba alitutisha sana kwa maneno yake, hii ilinifanya mimi na vijana wangu wawili kuathirika sana kisaikolojia, japo baadae ilithibitika kijana wangu mmoja Pius alihusika kuniibia.

Tulipewa muda wa kufikiria mpaka kesho yake twende na pesa, kama hakuna pesa basi kikosi kingine kipo ambacho kimeandaliwa kitatupa mateso makali kiasi kwamba tutakuwa vilema maisha yetu yote. “Eliud” mwisho wa kunukuu.


Kesho yake ilipofika Eliud na Pius walikwenda ofisini kwa Saalah kama walivyoagizwa. Kweli walikuta kuna kikosi kama walivyopewa taarifa jana yake, wakamhoji Pius aeleze pesa zilipo nae akakana kuwa hajui pesa zimepoteaje katika biashara.

Ndipo Saalah akamuwekea Pius bastora kichwani na kumwambia aseme pesa zilipo la sivyo anaweza kumuua na hakuna ambacho yeye atafanywa hapa Tanzania kwa sasa.

Ndipo Saalah akaruhusu vijana wake waanze kumtesa Pius, kwa muda wa masaa kadhaa walimtesa na kumpiga sana, kilikuwa kichapo kikali huku wamemvua nguo na wanamvuta sehemu za siri na kubinya masikio yake na praizi ili aseme pesa ziko wapi. Kijana akapata majeraha mwilini kwake, na mateso haya yanafanyika ofisini kwa Salaah na yeye ndio msimamizi wa hicho kikosi na yuko hapo.

Mateso yalipozidi Pius akawasihi wasiendelee kumtesa na atasema ukweli wote kwani ni kweli yeye ndio alikuwa anaiba pesa kwa sababu muda mwingi boss wake Eliud alikuwa busy kufanya marketing ya Silent Ocean, hivyo pesa nyingi ambazo anauza wakati Eliud hayupo alikuwa haziweki benki, pia kuna mzigo alikuwa anauiba toka stooni bila Eliud kujua kwa sababu alimuamini sana.

Akakiri kuwa pesa alizomwibia Eliud alizifanyia matumizi yafuatayo;
  • Alimsaidia baba yake mdogo kufungua kampuni ya Bima Posta.
  • Alimsaidia baba yake mdogo kujenga nyumba kubwa na ya kisasa.
  • Alianzisha Pharmacy Tegeta.
  • Yeye na baba yake mdogo walikuwa na mradi wa kusambaza madawati Dodoma.
  • Kuna pesa hadi muda huo anateswa walikuwa wameagiza gari aina ya Vogue.
  • Alinunua viwanja viwili.
  • Fedha zingine alikuwa anachezea Kamari.
  • Pesa zingine alikuwa anatumia kwa matumizi yake ya kawaida.
Baada ya mateso ya siku nzima kwa Pius jioni wakaruhusiwa kuondoka katika ofisi za Silent Ocean, huku Eliud akiambiwa na Salaah kuwa anataka pesa zake yeye atajuana na mfanyakazi wake, alichomsaidia ni kumtesa ili ajue pesa zilipo, jukumu la kupata pesa toka kwa Pius na Baba yake mdogo azifanye mwenyewe.


PIUS AFUNGUA KESI YA KUTEKWA NA KUTESWA KITUO CHA POLISI MSIMBAZI
Baba yake mdogo na Pius alikuwa Smart, baada ya mwanae kutoka goligota kwenye mateso ya Salaah kwenye ofisi za Silent Ocean – Lumumba, mkabala na Makao Makuu madogo ya Chama Cha Mapinduzi walienda kituo cha Polisi kufungua kesi kwa madai ya kutekwa na kuteswa na kujeruhiwa.

NB: Kiwanja ambacho zipo ofisi za Silent Ocean kilikuwa cha CCM, na waliuziwa na Mzee Yusuph Makamba akiwa katibu Mkuu wa CCM, imagine such a location.

Watuhumiwa katika hiyo kesi ya kuteka na kujeruhi walikuwa wafuatao;
  • Eliud
  • Salaah
  • Waliomtesa, ambao Salaah ndio alitakiwa awalete maana Pius hawajui kwa majina.

Salaah na Eliud walipokea wito wa kuitwa kituo cha Polisi Msimbazi, walikwenda na yafuatayo yakajiri.

  • Salaah alikana kuhusika kumteka na kumtesa Pius.
  • Alikana madai ya kumuwekea Pius bastola kichwani kwa madai kuwa yeye hamiliki bastola ma muda wote anavaa kanzu, hivyo sio rahisi yeye kutembea na bastola.
Baada ya majadiliano Mkuu wa kituo, Polisi Msimbazi aliwaambia yafuatayo;

  • Akashauri wazungumze na wayamalize mambo hayo nje ya vyombo vya dola kwa sababu yeye hawezi mfungulia mashitaka Salaah.
  • Kuwa tayari kishapigiwa simu na wakubwa zake asiendelee na kufungua shitaka hilo wala asijaribu kumpeleka Saalah mahakamani.
  • Na Afande huyo akamwambia Pius, naye ana familia hawezi haribu kazi yake.
Basi malalamiko yake yakawa yamekufa kifo cha mende na yakawa yameishia hapo.


ELIUD AMFUNGULIA KESI YA WIZI PIUS, KANDA MAALUM (CENTRAL POLISI)
Baada ya kesi ya Msimbazi kufutwa, na baada ya Eliud kujua aliyehusika na upotevu wa pesa ni Pius akaenda kumfungulia mashitaka kituo cha Polisi Central ili kuweza kupata pesa hizo amlipe Salaah. Maana kumbuka Saalah alimueleza yeye amemsaidia kujua aliyeiba kwa kumtesa, suala ya anazipataje toka kwake afanye mwenyewe na amletee hizo pesa maana muda wa wiki aliompa unayoyoma.

Baada ya kufungua kesi, Polisi wakamuita Pius ambaye aliambatana na Baba yake mdogo. Pale kituoni Pius akakiri baadhi ya mambo na akakana mengine. Akasema ni kweli aliiba pesa kiasi cha 22,500,000/- na ameenda nacho ili amrejeshee Eliud.

Akasema kuwa vingine alivyotaja siku anapewa mateso na Saalah na vijana wake sio vya kweli bali alisema ili kuokoa nafsi yake maana wale jamaa walimtesa sana huku wamemvua nguo na huku wanamvuta sehemu zake za siri, na akasema hana hakika kama anaweza simamisha tena.

Afande aliyekuwa anasimamia shitaka hilo akamshauri Eliud ni bora tu achukue kiasi hicho cha pesa aachane na hiyo kesi kwani akitaka kuendelea nayo itabidi Saalah naye awe sehemu ya kesi kuwa alimtesa Pius hadi akakiri kuiba pesa tofauti ana alizoiba kweli. Ikamlazimu Eliud achukue hicho kiasi maana Afande alimsisitiza hawezi kuendelea zaidi na hiyo kesi.


JINSI SALAAH ALIVYOTAIFISHA MALI ZA ELIUD
Baada ya wiki kuisha Salaah akamwambia achague yeye achukue mali zake zote au aagize vijana wake wamshughulikie. Na akamwambia wewe kubali kusalenda mali zako zote kisha tukae chini tupige hesabu, nichukue pesa zangu na zinazosalia nitakurejeshea.

Kwa kuwa kijana huyo alikuwa mhanga, na ameona jinsi mfanyakazi wake alivyoteswa basi akawa hana chaguo zaidi ya kukubali, maana alikuwa anajua mali alizonazo zinatosha kulipa deni na hasara ya Salaah na angebaki na kiasi cha kuendekeza biashara zake na kulipa watu wengine wanaomdai.

Ndipo Salaah akafanya yafuatayo:
  • Aliamuamuru Eliud akachukue pesa zote zilizo benki na ampelekee pale Silent Ocean, akatii.
  • Saalah aliuza fremu ya Eliud ya biashara kwa shilingi milioni 80.
  • Alichukua mzigo wote uliokuwa stoo na dukani kwa Eliud.
  • Alitaifisha mizigo yote iliyokuwa inatoka China ya Eliud na ya baadhi ya wateja waliompa pesa ambayo ilikuwa inasafirishwa na Silent Ocean, na kuwataka hao watu wamdai Eliud pesa zao.
Wakati tunaongea nae kituoni baada ya kujaribu kumshitaki Salaah kwa kutaifisha mali zake na kukataa kupiga nae hesabu alisema kuwa kama kweli Salaah angetimiza ahadi yake kuwa anachukua mali zote kisha wapige hesabu atoe pesa zake na kumrejeshea zake ambazo kwa hesabu alizonazo yeye sio chini ya milioni 250, ambazo zingemsaidia kurudi kwenye biashara na kulipa madeni ya watu.


MAJUMUISHO YANGU:
  • Mimi ni askari na nayajua haya sababu niko Kanda Maalum.
  • Watu wanaofanya uonevu na kulindwa haswa wenye pesa dhidi ya watu ni makubwa sana na wanatetewa na kulindwa na wakubwa zetu, sisi unajua kazi zetu ni kupokea order.
  • Saalah anasema yeye ni untouchable, kwa serikali ya sasa hakuna mtu anayeweza kumfanya lolote maana hata Rais yuko upande wao.
  • TRA na bandari nimewapa tip muhimu kama mtaweza mzifanyie kazi au muweke katika mpango kazi.
  • Uchumi wetu hauwezi kukua kama tutawaruhusu watu wanatorosha pesa kiholela kama anavyofanya Salaah na watu wengine.
  • Tume ya Haki Jinai ianzie hapa, mtu anatekwa, anateswa, anajeruhiwa, anadhurumiwa na akienda kwenye vyombo vya Dola hapati haki sababu waonevu wanatamba kulindwa hadi na aliyeunda Tume ya Haki Jinai.
  • Kama kweli Tume ya Haki Jinai ina malengo ya kutatua changamoto hizi tunategemea kuona taarifa hizi au za kufanana na hizi maana hata Mahamakani ukienda na watu hawa hupati haki.
  • Tunaamini Tume ya Haki Jinai haijaundwa ili kuhalalisha watu wote wahujumu Uchumi kurejeshewa mali zao kinyemela.
  • Nimeandika haya nikijua huyo Saalah anaweza kuwadhuru hao vijana Pius na Eliud kwa kutoa siri hizi maana hadi sasa wanaishi kwa hofu.
  • Ikiwa mmoja wa vijana hawa watapata shida tayari mchawi anajulikana.
  • Mwisho nitoe wito kwa mtu yeyote, anayeweza mfunga huyu paka kengele basi afanye hivyo, maana sitaki kuamini kuwa Rais wetu, na Mama yetu anabariki huu ufedhuri, bali mbeleko wanayopewa wanaitumia vibaya, ni sawa na kumtukanisha Rais wetu.
  • Kariakoo hivi sasa kila mtu anamuogopa Saalah na wanajua hivi sasa anaweza kuwafanya lolote.
  • Sisi watu weusi tunatakwa kujitafakari sana, maana sisi ndio tunaotumika kuwaonea na kuwaumiza ndugu zetu dhidi ya hawa watu wengine.

NB: Mnisamehe kwa kuandika kwa uchache na sio kwa details kama nilivyokusudia maana yako mengi sana kuandika juu ya misheni za huyu jamaa, niliahidi asipolipa ndani ya masaa 72 nitamlipua lakini lengo langu lilikuwa kumlipua tu maana hata muda huo haujafika na sijawasiliana na hao vijana. Pia nimewaza watu humu wamesema hawa jamaa wanatuma majini, nikaona bora nitupie leo hata yakininyonga usiku tayari sitawaacha ndugu zangu na hii Kiu.

Na kwa kuwa majini hayapendi pombe na kitimoto, usiku huu napiga KVANT kubwa na Kitimoto kilo 2, yakija yanakutana na kitu hayapendi.

Mwisho ndugu zangu watanzania, tujitafakari, nchini kwetu tunaonewa hadi na Saalah, this form four failure? Tunakwama wapi na tunapungukiwa na nini?


OVAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Kama mtu anaweza kufanya unyama huu wa Kutesa watu ofisini kwake,wizi na kudhulumu watu,uhujumu uchumi na Uchafu wote huu,Hivi tuna usalama wa taifa wanaojielewa kweli?Tuna polisi kweli?
IGP anapaswa kubaki kwenye nafaasi take kweli?

Mheshimiwa Raisi, kwakuwa juzi umesema huwa unapitia hapa Jamii Forums, chukua hatua juu ya hili.

Hili ni tukio moja tu, Je amefanya mangapi ambayo hatujui?
Ukipitia ule Uzi wa kwanza utaona jinsi watu walivyofunguka juu ya Uhuni wa huyu mtu,mpaka analawiti watu?

Tunaaubiri tuone hatua gani utachukua.

Mleta Mada Mungu akulinde.
 
Huenda mie ndio nikawa wa kwanza kusoma na kumaliza hii skendo.

Kama nchi yetu tumefikia hapa huenda usalama wa kesho yetu ukawa Mdogo hasa sir vijana tunaomini kwenye Biashara naomba mamlaka husika zitende haki kwenye hili.

Sababu mama Samia huwa anapita JF basi nimuombe alivalie njuga hili swala na Mambo Kama haya Kama yapo kweli na wanachi wanayashuhudia Basi huenda Taifa likaja kupata bomu ambalo litapeleka Taifa kwenye umaskini na kuingia kwenye fujo na nchi kuwa ngumu kutawalika sababu wahuni sharubu zao zishakuwa za chuma.

MAMA SAMIA NAOMBE UJE PM TUZUNGUMZE KWANIABA YA VIJANA WENZANGU WENGI KWA UCHACHE SANA.
 
Huenda mie ndio nikawa wa kwanza kusoma na kumaliza hii skendo.

Kama nchi yetu tumefikia hapa huenda usalama wa kesho yetu ukawa Mdogo hasa sir vijana tunaomini kwenye Biashara naomba mamlaka husika zitende haki kwenye hili.
Uko sahihi kaka. Haya ni machache sana kati ya mengi makubwa sana. Hata mbolea zinaingizwa na hawa Watanzania wenye asili ya Asia. Ukigusa kuleta mbolea kwa bei nafuu wanakuua.

Hivi sasa wanatamba kuwa wamepata mtelezo kwa Mama Samia.

Kwa kuwa anapitia humu tuone hatua anayoweza kuchukua.

Kama anawalinda aendelee kuwalinda.

Ni Tanzania pekee unalala masikini kesho unanunua nyumba Masaki na hakuna anayekuuliza umepata wapi hizo pesa.

Mifumo ikiwa mibovu uchumi hauwezi kukua.
 
Ashasema anapita humu
Na apitie na kuonyesha uamiri jeshi wake.

Sio kuunda Tume ya Haki jinai ili kuhalalisha wahujumu uchumi waliotaifishiwa mali zao walizokwiba serikalini warejeshewe. Wahujumu uchumi walichukuliwa hatua toka enzi za Mwalimu Nyerere.

Anyway hata wakituma majini sasa nitakufa kwa amani maana kamwe sitaishi milele.

Ukweli una gharama sana.
 
Back
Top Bottom