Tutafakari pamoja: Kwa nini Dubai wanalazimisha mfumo wa mikataba unaojumuisha IGA na HGA wakati miradi yote itatekelezwa nchini Tanzania?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1697990304560.png

Mchoro wenye kuonyesha: Mtindo wa Mikataba ya Kimataifa Unaotumiwa na Dubai (The Dubai BIT Model) wenye sura ya piramidi la mikataba ifuatayo: (1) Inter-Governmental Agreement (IGA), ambacho ni kitako cha piramidi; (2) Host Governmental Agreement(HGA) ; (3) Project-level Lease Agreement (PLA); na (4) Project-level Concession Agreement (PCA), ambacho ni kilele ha piramidi."

I. USULI


Ukuu wa nafsi iliyo kitovu cha mamlaka ya kimaamuzi na kiutendaji yasiyo paswa kuhojiwa na mtu yeyote baki, kama ilivyo kwa mtu binafsi akiwa nyumbani kwake, mfalme akiwa katika himaya yake, mkutano kuu wa azaki, mkutano mkuu wa wanahisa katika kampuni, kikao ha bunge la nchi, kikao cha majaji wa mahakama ya rufaa ya nchi, na kikao cha Baraza la Mmawaziri wa dola kama vile Kenya na Uganda, unaitwa "sovereignty" kwa Kiingereza.

Kwa neno moja jipya tunaweza kuseme "usoverini," baada ya kutohoa neno hilo la Kizungu. Hivyo, neno "usoverini" linarejea dhana ya kisheria, kisiasa na kifalsafa inayotaja haki ya uhuru wa nafsi husika kufanya maamuzi bila hofu ya kuulizwa na mtu yeyote baki, haki hiyo ikiwa inaambatana na haki ya kuwapuuza watu wote baki watakaojaribu kuhoji maamuzi hayo.

Katika mataifa yanayoongozwa kwa mujibu wa kanuni za jamhuri ya kidemokrasia, ukuu wa nafsi iliyo kitovu cha mamlaka ya kimaamuzi na kiutendaji, yaani "popular sovereignty," uko mikononi mwa watu wengi.

Katika mfumo huu, mamlaka hayo yanaweza kutumika kupitia demokrasia ya moja kwa moja au demokrasia ya uwakilishi kupitia vyombo kama vile Baraza la Maendeleo la Kata, Baraza la Madiwani, Bunge la Nchi, na Baraza la Mawaziri katika nchi.

Katika Afrika, kuanzia miaka ya 1880 ukuu wa nafsi inayoitwa "dola" au "himaya" umekuwa unamomonyolewa na wageni kutoka Ulaya na Asia kwa kutumia mikataba ya kimataifa, yaani "treaties."

Ukoloni wa kiporaji (extrative colonialism) chini ya Wazungu kutoka Bara la Ulaya na ukoloni wa kilowezi (settler colonialism) chini ya Waarabu kutoka Bara la Asia ulimomonyoa ukuu wa himaya na dola za Afrika ya kale.

Kadhalika, biashara ya utumwa iliyoratibiwa na Waarabu kutoka Bara la Asia ilimomonyoa ukuu wa nafsi ya binadamu mmoja mmoka kwa kuwageuza Wabantu kuwa bidhaa katika masoko ya watumwa.

Na katika siku za karibuni, mkataba wa kimataifa uliotumika kumomonyoa ukuu wa dola inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni Mkataba wa Pande Mbili Kati ya Tanzania na Dubai kwa ajili ya wawekeaji kutoka Dubai kwenye Bandari za Tanzania Bara.

Ni mkataba unaohalalisha "ukoloni wa kikampuni," yaani "corporate colonialism," unaotukuza "ukoloni wa wawekezaji wa kigeni," yaani "foreign invester colonialism," dhidi ya ukuu wa dola ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hivyo, tasnifu hii inachunguza "Changamoto ya Ukoloni wa Wawekeaji wa Kigeni Unaotokana na Kuinuliwa kwa Ukuu wa Makampuni Dhidi ya Ukuu wa Taifa Chini ya Kizazi cha Tano cha Mikataba ya Uwekezaji wa Kimataifa."

Ni utafiti kwa ajili ya kujibu swali lifuatalo: "Watanzania Tunapaswa Kuchukua Hatua Gani Baada ya Mkataba wa Pande Mbili Kati ya Tanzania na Dubai Kuruhusu Ubinafsishaji wa Rejareja wa Bandari za Tanzania kwa Kiwango Kinahotishia Usalama wa taifa Letu?" Taarifa kamili inafuata hapa chini.

II. UTANGULIZI

1. Chimbuko la tasnifu hii


Makubaliano ya Pande Mbili Kati ya Tanzania na Dubai Kuhusu Ubinafsishaji wa Rejareja wa Bandari za Tanzania, kama ulivyosainiwa na serikali tarehe 25 Oktoba 2022 na kuidhinishwa na Bunge tarehe 10 Juni 2023, unazo sifa zote za mkataba. Hivyo, awali ya yote yafaa tuanzie kwenye fasili ya dhana ya "mkataba" itakayozingatiwa kwenye andiko hili.

Tunapendekeza kwamba, neno "mkataba" ni alama inayomaanisha makubaliano baina ya pande mbili ambayo yana sifa tano muhimu. Sifa hizo ni kama ifuatavyo:
  • Ridhaa ya wahusika wawili wenye uwezo wa kutoa ridhio huru kuhusu jambo mojawapo,
  • Tamko kuhusu haki na majukumu ya kila upande,
  • Uwepo wa madai ya haki kutoka kila upande, ambapo haki ya upande mmoja ni sababu ya wajibu wa upande mwingine, na kinyume chake,
  • Tamko la adhabu kama matokeo ya ukiukwaji wa haki na utelekezaji wa majukumu yaliyotajwa kwenye mapatano, na
  • Uwepo wa mamlaka huru iliyo na jukumu la kutafsiri mapatano, kutamka adhabu, na kusimamia utekelezaji wa adhabu zilizotajwa katika mapatano, mamlaka hiyo ikiwa yenye kuongozwa na ukweli kwamba, haki na majukumu vimetajwa ndani ya mapatano husika kwa kutumia maneno yanayoashiria "upaswa" na "ulazima."
Mkataba kati ya watendaji wa kimataifa, kama vile mataifa, mashirika ya kimataifa (IOs), na makapuni ya kimataifa (MNCs), unaitwa “mkataba wa kimataifa.”

Kwa kuizngatia maana hii, mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai sio habari mpya kwetu, kwani kwa karne nyingi, mikataba ya kimataifa imetuika kudhibiti mahusiano kati ya nchi na nchi, na nchi yetu ikiwemo.

Kwa mfano, Hollis (2020) anasimulia kisa cha Kibiblia cha mkataba wa kimataifa uliosainiwa kati ya Yoshua na Wagibeoni, mkataba uliosaiiwa yapata karne ya 7 KK.

Kulingana na masimulizi ya Hollis (2020), Mungu wa Kiebrania alikuwa amewaelekeza Waisraeli wawateketeze majirani wote waliokuwa wakiishi katika nchi ya ahadi ya Kanaani na ‘wasibakize kitu chochote chenye pumuzi ya uhai’ (Kumbukumbu la Torati 20:10–18 ).

Lakini Mungu aliwaruhusu kutowadhuru wageni kutoka nchi za mbali. Na wakai wa Gibeoni waliokuwa wanakaa Kanaani walijua kwamba wangeangamizwa. Kwa hiyo, walituma ujumbe kwa kiongozi wa Waisraeli, Joshua, huku wakijigeuza wawe kama wajumbe kutoka nchi za mbali.

Joshua alianguka kwenye mtego wa udanganyifu wao na kufanya mapatano ya amani na Gibeoni. Hatimaye viongozi wa Israeli waliidhinisha mapatano hayo kwa kiapo cha kidini (Yoshua 9:3–21).

Vile vile, mchakato wa wakoloni wa wazungu kuiteka na kuitawala Afrika ulifanikishwa na mikataba ya kimataifa. Mieke van der Linden (2017: 294-300), ametuandalia "orodha ya mikataba ya kimataifa husika kulingana na mpangilio wa tarehe zake."

Ameorodhesha mikataba 128 iliyofungwa katika Afrika wakati huo. Mikataba hii ya kimataifa ilitiwa saini na kuwa leseni ya "Kumegwa kwa Ardhi ya Afrika" tangu mwaka 1870 hadi 1914.

Kulingana na ingizo la Wikipedia linaloongelea "Mikataba ya Kimataifa ya Tanzania," tangu uhuru hadi sasa, Tanzania imeidhinisha angalau mikataba ya kimataifa 166.

Lakini pia, kuna mikataba ya uwekezaji baina ya nchi mbili kuhusu uchimbaji madini ambayo ilitiwa saini wakati wa utawala wa Rais Mkapa.

Kuna mikataba ya uwekezaji kati ya nchi mbili kuhusu uchimbaji wa mafuta na gesi asilia iliyotiwa saini wakati wa utawala wa Rais Kikwete.

Na kuna mkataba wa hivi karibuni kati ya Tanzania na Dubai kuhusu ubinafsishaji wa sehemu ya majukumu ya bandari za bahari na maziwa nchini Tanzania, ambao ulitiwa saini wakati wa utawala wa Rais Samia tarehe 25 Oktoba 2022.

Mkataba huu kati ya Tanzania na Dubai umeleta mabishano makubwa nchini Tanzania kutokana na utata uliomo kwenye muundo na maudhui yake. Tutaeleza kwa kifupi utata huu.

Tangu mwaka 1947 mikataba ya uwekezaji wa kimataifa (Bilateral Investment Treaty--BIT) ilikuwa unaratibiwa chini ya mwongozo wa viwango vya biashara duniani, yaani General Agreements on Tarrifs and Trade (GATT).

Utaratibu mpya ukaibuka mwaka 1959, pale Mkataba wa kwanza wa uwekezaji wa kimataifa uliposainiwa kati ya Ujerumani na Pakistani, kwa kutumia mfumo tofauti na mwongozo wa GATT. Bila shaka ni kutokana na udhaifu uliokuwemo kwenye mwongozo wa GATT.

Baada ya hapo mataifa mengine mengi yakafuata barabara ya Ujerumani na Pakistani. Lakini, kila taifa likiwa linabuni muundo wake wa mkabata wa uwekezaji wa kimataifa.

Mwaka 1995 dosari za GATT ziliondolewa na kazi zake kurithiwa na shirika la biashara duniani (WTO), ambapo mwongozo wa GATT ulifanywa kuwa sehemu ya WTO.

Hadi leo, kumetokea mabadiliko makubwa kwenye muundo na maudhui ya mikataba ya aina hiyo (Zhan, Weber na Karl 2011).

Yaani, katika miongo sita iliyopita, maendeleo ya biashara ya uwekezaji wa kimataifa, yamesababiisha mvuvumko katika mfumo wa sheria zinazoratibu "Uhamisho wa Mitaji ya Kimataifa," yaani "Foreign Direct Investments (FDI)."

Mvuvumko huu umetokana na mahitaji ya kuimarisha mfumo wa sheria za kulinda wawekezaji wa kigeni na kuhami maslahi ya nchi ambazo ni wenyeji wa wawekezaji (Alvarez and Sauvant 2011).

Wawekezaji wa kigeni wanaonekana kutokuwa na imani na uimara, uwazi na utabirifu wa mifumo ya sheria za uwekezaji katika mataifa ya ulimwengu wa tatu.

Hofu yao kuu ni kutokana na wanasiasa walioko katika uliwengu huu kufanya maammuzi ya kisera yatakayohatarisha uwekezaji.

Kati ya mambo mengine, hofu yao inatokana na uwezekano wa kutaifishwa kwa mali za makampuni ya kigeni chini ya itikadi ya ujamaa na ukomunisti. Hofu nyingine ni mabadiliko ya sheria za kodi zitakazoweza kupunguza faida wanayoitafuta kupitia uwekezaji.

Hivyo, zimekuwepo hatua za makusudi zinazofanywa na serikali za ulimwengu wa kwanza kwa kubadilisha kanuni za kimataifa kuhusu namna ya kulinda uwekezaji wa kigeni katika nchi za ulimwengu wa tatu.

Kuna awamu kuu tano za mabadiliko hayo. Awamu ya kwanza ni mikataba ya kimataifa kuhusiana na urafiki, biashara na usafirishaji wa kimataifa (friendship, commerce and navigation treaties). Mkataba wa kwanza wa aina hii ulisainiwa mwaka 1778 kati ya Amerika na Ufransa. Na utarataibu huu ulikomma mwaka 1947.

Awamu ya pili ilitokana na kuanzishwa kwa mfumo wa GATT mwaka 1947 kwa ajili ya kupunguza vikwazo ya kibiashara duniani.

Awamu ya tatu ilitokana na kuanzishwa kwa mfumo wa WTO uliurithi mfumo wa GATT mwaka 1995, ukiambatana na maboresho kadhaa.

Awamu ya nne ni kushamiri kwa mikataba huria ya uwekezaji wa kimataifa (Bilateral Investent Agreeents--BITs), hasa kwa zile nchi ambazo hazikuridhika na mwongowo wa WTO.

Na awamu ya tano ya mageuzi katika mikataba ya uwekezaji wa kimataifa imetokea tangu mwaka 1999, katika usanifu na ujenzi wa bomba la mafuta linaloanzia Bahari ya Kaspiani hadi Bahari ya Mediteraniani. Bomba hili lInaitwa Bomba la "Baku-Tbilisi-Ceyhan," yaani "BTC Pipeline."

Mradi huu wa BTC unaunganisha nchi tatu za Azerbaijan, Georgia na Uturuki. Kwa sababu hii mradi huu uliibua mfumo mpya unaojumuisha mikataba mitatu iliyobebana, yaani: Intergovernmental Agreement (IGA) kati ya Uturuki, Azerbaijan, na Georgia.

Mkataba huu, uliosaniwa mwaka 1999 ulikuwa na viambatanisho vitatu vya “Host Government Agreement (HGA),” “The Turnkey Agreement (TKA),” na “The Government Guarantee Agreeent (GGA).”

Nchini Azerbaijan, Georgia na Uturuki mkataba wa IGA na viabatanisho vyake uliwasilishwa bungeni na kuridhiwa na mabunge husika, mwaka 2000. Ujenzi wa boba la BTC ulianza Aprili 2003 na kukailika 2005.

Lakini, mabadiliko haya yamekuwa yakifanywa na watu walioko kwenye kambi tofauti, kila kambi ikifikiri kivyake, pasipo usimamizi wa pamoja, kiasi kwamba, leo tunayo maelfu ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa inayopishana kimuundo na kimaudhui.

Jambo hili linaleta changamoto kwa wawekezaji wa kimmataifa na kwa nchi wenyeji wao pale wanapokutana ili kujadili kwa ajili ya kusaini mikataba mipya ya aina hii. Hakuna mwongozo wa pamoja duniani kote.

Utata huu umeongezeka baada ya serikali ya Dubai kuleta mfumo mpya kabisa nchini Tanzania, ikitaka ndio utumike kama msingi wa uwekezaji wake katika bandari zetu.

Dubai wameleta mfumo wenye ngazi nne za mikataba iliyobebana, yaani mkataba wa PIGA, mkataba wa IGA, mkataba wa HGA na mkataba wa mradi mmoja moja, yaani "Project contracts."

Nchini Tanzania, mkataba wa IGA umewasilishwa bungeni pasipo kiambatanisho cha mkataba wa HGA, na hivyo kuzalisha maswali mengi yasiyo na majibu.

Tatizo kubwa ni kwamba, kulingana na maudhui ya IGA, mfumo huu unakweza ukuu wa kampuni ya uwekezaji (corporate sovereignty) dhidi ya ukuu wa nchi ambayo ni mwenyeji wa wawekezaji (state sovereignty). Ni mfumo unaotishia usalama nchi kwa kiwango kisichoruhusu ukimya.

Hivyo, tasnifu hii inachunguza changamoto zinazoambatana na mvuvumko huu, kwa kuzingatia maudhui ya Mkataba kati ya Tanzania na Dubai Kuhusiana na ujenzi, uboreshaji, usimamizi na uendeshaji wa Bandari za Tanzania.

2. Mikataba ya uwekezaji wa kimataifa ni kama mtego wa panya

Awali ya yote, yafaa ieleweke kwamba, miradi ya uwekezaji inayotegemea uhamishi wa mitaji ya kigeni, hutokea pale mtu binafsi au kampuni kutoka katika nchi moja, inayoitwa "nchi inayotoa mitaji ya uwekezaji" (home state), husajili hisa zote au sehemu ya hisa kwenye kampuni iliyosajiliwa kwenye nchi nyingine, inayoitwa "nchi inayopokea mitaji ya uwekezaji" (host state).

Kwa upande mmoja, lengo la nchi inayotoa mitaji ya uwekezaji huwa ni kupata maliasili kama vile madini, nguvu kazi nafuu, na masoko mapya. Na kwa upande mwingine, lengo la nchi inayopokea mitaji ya uwekezaji huwa ni kuongeza kipato kwa njia ya kodi, uhamisho wa tekinolojia, na kuzalisha ajira.

Kwa kawaida "nchi inayotoa mitaji ya uwekezaji" na "nchi inayopokea mitaji ya uwekezaji" hufunga mikataba ya kimataifa (treaties), yenye kuonyesha haki na majukumu ya kila upande.

Mikataba hiyo hutaja majukumu yanayominya uhuru wa kila upande kwa sehemu fulani. Kwa kuwa hii ni mikataba kati ya nchi na nchi, hii maana yake ni kwamba majukumu hayo yanafinya "ukuu wa nchi" husika, yaani "state sovereignty," kwa maana ya kupunguza uhuru wa nchi husika katika kutunga sheria, kutafsiri sheria na kutekeleza sheria zake.

Miaka 22 iliyopita, Profesa wa Mahusiano ya KImataifa, Robert Owen Keohane, wa huko Marekani, aliongelea hatari hii kupitia maneno yafuatayo;

"I have asked how we can overcome the governance dilemma on a global scale. That is, how can we gain benefits from institutions without becoming their victims? How can we help design institutions for a partially globalized world that performs valuable functions while respecting democratic values? And how can we foster beliefs that maintain benign institutions? ... Our objective should be to help our students, colleagues, and the broader public understand both the necessity for governance in a partially globalized world and the principles that would make such governance legitimate ... If global institutions are designed well, they will promote human welfare. But if we bungle the job, the results could be disastrous." (Keohane 2001:11-12).

Hasa anachokilalamikia Keohane (2001) ni kanuni ya mtego wa panya, yaani "mousetrap strategy," ambayo hutumika wakati wa kusanifu na kusaini mikataba ya kiataifa.

Mtego huu unazo hatua tatu. Kwanza, unaandaliwa mkataba wenye kubeba kifungu kiachosema kuwa wahusika pekee wenye mamlaka ya kuuvunja ni wakuu wa nchi badala ya mahakama au Bunge.

Pili, mkataba unabeba kifungu kinachosema kwamba mmaudhui yake yanaweza kuhaririwa kwa ridhaa ya wakuu wa nchi husika.

Na tatu, vifungu hivi vinaandikwa kwa kutumia misammiati yenye maana tata (equivocation), kiasi kwamba, dhamira ovu ya kutokuwa tayari kuhariri wala kuvunja mkataba husika inakuwa imejificha. Mkataba ukishasainiwa tu, mtego unanasa "panya" pasipo uwezekano wa kuchomoka.

Ujanja mwingine unaotumika kufanikiwa mkakati huu unafafanuliwa vema na Profesa wa Falsafa, Desmond Connell(1926–2017), katika "Ripoti ya Tume ya Uchunguzi ya Murphy," katika Jimbo la Dublin huko Uingereza, pale anaposema maneno yafuatayo:

“Well, the general teaching about mental reservation is that you are not permitted to tell a lie. On the other hand ... you can use an ambiguous expression realising that the person who you are talking to will accept an untrue version of whatever it may be ― permitting that to happen ― not willing that it happened, that would be lying. It really is a matter of trying to deal with extraordinarily difficult matters that may arise in social relations where people may ask questions that you simply cannot answer. Everybody knows that this kind of thing is liable to happen. So mental reservation is, in a sense, a way of answering without lying.” (Murphy Investigation Report 2012, Article 58.20)

Usahihi na upotofu wa maneno haya unategemea fasili ya maneno "kusema uwongo," yaani "lying" au "to tell a lie."

Ama “Kusema uwongo ni kitendo cha kuupindisha ukweli kwa lengo la kumpotosha mtu baki" au “Kusema uwongo ni kitendo cha kuupindisha ukweli kwa lengo la kumpotosha mtu baki mmwenye haki ya kuujua ukweli."

Kama tukichukua fasili ya pili kama fasili iliyo sahihi, basi, ubaya wa maneno ya Desmond Connell, yaliyonukuliwa hapo juu, unaonekana bayana.

Mfumo wenye ngazi nne za kimkataba unakuwa na misamiati tata kuanzia ngazi ya kwanza hadi ngazi ya tatu.

Ni mkakati wa kufanya ulaghai kwa kumweka msomaji wa mkataba kwenye kilele cha mlima unaoteleza (slippery slope), kiasi cha kumfanya mtu kuserereka na kuanguka kwenye mtaro wa uwongo.

Hivyo, kunahitajika umakini mkubwa wakati wa kuandaa na kusaini "mikataba ya kimataifa kwa ajili ya uwekezaji" ili mikataba hiyo isije ikawa milango ya kukaribisha wakoloni mamboleo kupitia mgongo wa uwekezaji wa kiuchumi.

Yaani, maneno ya wanazuoni hawa yanatukumbusha jukumu letu la kuchunguza, kwa lengo la kuhariri, makubaliano ya Kiserikali kati ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari za Tanzania.

3. Muundo na maudhui ya mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai

Makubaliano haya yaliyosainiwa mnamo 25 Oktoba 2022, na baadaye, tarehe 10 Juni 2023 yaliidhinishwa na BUnge, na hivyo kuwa mojawapo ya sheria za Kimataifa zinazozibana sheria zote za Tanzania, kwa kuwa zinakuwa na nguvu dhidi ya sheria baki pale mgongano kati ya sheria hizi mbili unapotokea.

Kwa ajili ya kuweka mgawanyo wa haki na majukuu kati ya serikali mwmenyeji ya Tanzania, wawekeaji kutoka Dubai, na serikali ya kigeni ya Dubai inayotuma mwekeaji, makubaliano haya yanaongozwa na mfumo wa mikataba wenye ngazi kuu nne.
  1. Ngazi ya kwanza ni mkataba wa IGA (Inter-governental Agreement), yaani mkataba kati ya serikali ya Tanzania ambayo ni mwenyeji wa wawekeaji wa kigeni na serikali ya kigeni iliyotuma wawekeaji.
  2. Ngazi ya pili ni mkataba wa HGA (Host Government Agreement), yaani kataba katia ya serikali ya Tanzania ambayo ni mwenyeji na kampuni ya uwekezaji kutoka ugenini.
  3. Ngazi ya tatu ni mikataba ya mradi mmoja mmoja (Project ALevel Lease Agreement), ambayo husainiwa hatua kwa hatua kadiri mahitaji yanapojitokeza. Mchoro hapo juu unaonyesha mwingiliano wa mikataba hii.
  4. Na Ngazi ya nne ni Project Level Concession Agreements, ambayo pia husainiwa hatua kwa hatua kadiri mahitaji yanapojitokeza. Mchoro hapo juu unaonyesha mwingiliano wa mikataba hii.
Mchoro ufuatao unaonyesha uhusiani kati ya aina hizi nne:

1697994093504.png

Mchoro: Ngazi nne za "The Dubai BIT Model" inayojumuisha: P Inter-Governmental Agreement (IGA); Host Governmental Agreement(HGA) ;na Project-level Lease Agreement (PLA), na Project-Level Concession Agreement (PCA)."

4. Kiini cha tatizo katika mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai

Mara nyingi, mfumo huu uliotajwa hapo juu umekuwa ukitumika kwenye miradi ya gesi na nishati ya mafuta inayosafirishwa kwa kuvuka mipaka ya nchi mbili au tatu.

Mfano mmoja ni mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima ya Uganda hadi Tanga ya Tanzania, yaani mradi wa bomba na Hoima-Tanga (EACOP) lenye urefu wa kilommeta 1,443. Tazama mchoro hapa chini.

1690828784973.png


Na mfano mwingine ni mradi wa bomba la mafuta kutoka Bahari ya Kaspiani hadi Bahari ya mediteraniani, linalovuka nchi tatu za Azerbaijani, Armenia na Uturuki, yaani Baku–Tbilisi–Ceyhan (BTC) pipeline lenye urefu wa kilometa 1,768. Tazama mchoro hapa chini pia.

1690828734151.png


Lakini pia, tunafahau kuwa hapa nchini, kuna wawekezaji wa kimataifa ambao wanatumia mfumo wa mikataba wenye gazi mbili za mwisho, kati ya ngazi tatu zilizotajwa hapo juu.

Mfano ni Kampuni ya Helios ya Uingereza inayojenga minara Afrika mashariki na kati na hatimaye kuikodisha kwa makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano kwenye maeneo haya.

Lakini, sasa uwekezaji wa Dubai nchini Tanzania unahusisha nchi mbili pekee, lakini bado tumelazimika kusaini mkataba wa uwekezaji kati ya serikali Tanzania na serikali Dubai, wakati miradi yote inatekelezwa nchini Tanzania.

Hata hivyo, kuna matatizo makubwa zaidi ya hilo. Tatizo moja linaanzia kwenye kifungu kinachoongelea "kulinda uimara wa mkataba," yaani "contract stabilization clause."

Kwa mujibu wa kifungu hiki, uimara wa mkataba unapaswa kulindwa kwa kipindi chote cha mkataba kwa kuhakikisha kwamba hakuna sheria zitakazotungwa na Bunge wala kanuni zikazotungwa na serikali kwa ajili ya kubadilisha matarajio ya wekezaji yaliyotajwa kwenye mkataba.

Paul Comeaux and Stephan Kinsella (1994:24), wanasema yafuatayo kuhusu uhalisia wa kifungu cha aina hii:

"A stabilization clause states that the law in force in the state at a given date-typically, the time the concession takes effect-is the law that will apply to supplement the terms of the contract, regardless of future legislation, decrees, or regulations issued by the government. Its purpose is to 'preclude the application to an agreement of any subsequent legislative (statutory) or administrative (regulatory) act issued by the government ... that modifies the legal situation of the investor.' In other words, by agreeing to a stabilization clause, a state alienates its right to unilaterally change the regime and rights relied upon by, and promised to, the investor. [Therefore, such clauses do not preclude a state from enacting new legislation, but rather prevent it from enforcing new regulations against a specific contractual party.]"

Hivyo, vifungu hivi vinazifunga mikono na miguu serikali na bunge, na kuikweza kampuni ya uwekezaji juu yake. Ukuu wa serikali na ukuu wa Bunge unaegwa kwa ajili ya kuanzisha ukuu wa kampuni ya uwekezaji wa kigeni.

Ubaya huu ulipata kuelezwa vema na mtaalam mzoefu katika masuala ya mahusiano ya kimataifa, Jean-Louis Pierre Tauran(2003), aliposema maneno yafuatayo:

"It is true that through [HGAs] with the public authorities, [foreign investors] can assure the guarantee of certain of their rights. But the fact remains that these agreements are subject to local law and therefore will always be fragile, insofar as they are dependent upon the hazards posed by the political regimes or parliamentary majorities of the future...[But IGA] shields them from any arbitrariness of succeeding [democratic control by the] governments [by putting these agreements under international law, from which it follows that IGA is always and everywhere intended as a democracy freezing and sovereignty eroding strategy where home state sovereignty is squeezed to give way to foreign corporate sovereignty]."

Huu ni mkakati huu wa "kufisha ganzi mifumo ya kidemokrasia na kumomonyoa ukuu wa nchi. Ubaya huu ulielezwa vema na mtaalam mzoefu katika masuala ya mahusiano ya kimataifa, Jean-Louis Pierre Tauran(2003), aliposema mmaneno yafuatayo:

"It is true that through [HGAs] with the public authorities, [foreign investors] can assure the guarantee of certain of their rights. But the fact remains that these agreements are subject to local law and therefore will always be fragile, insofar as they are dependent upon the hazards posed by the political regimes or parliamentary majorities of the future...[But IGA] shields them from any arbitrariness of succeeding [democratic control by the] governments [by putting these agreements under international law, from which it follows that IGA is always and everywhere intended as a democracy freezing and sovereignty eroding strategy where home state sovereignty is squeezed to give way to foreign corporate sovereignty]."

Ni kupitia ufafanuzi huu, maneno kwamba "ukuu wa nchi yetu umeuzwa kwa wageni" yanapata, sio tafsiri ya kitamathari, bali tafsiri sisisi.

Lakini sio hivyo tu. Pia kuna vifungu vinavyomega ukuu wa mahakama, hasa katika suala la kuvunja mkataba. Kuna kifungu kinasea kwaba, mktaba hauwezi kuvunjwa na mahakama yoyote kama wakuu wa nchi husika hawajaridhia uvunjwe.

Hapa ndipo wawekezaji wa kimataifa kutoka Magharibi na Mashariki walipoyafikisha mataifa ya ulimwengu wa tatu.

5. Maswali yanayaohitaji kupatiwa ajwabu ya kitafiti

Hivyo, utata huo hapo juu unammaanisha kwamba kuna haja ya tutafakari pamoja kuhusu swali kuu la utafiti lifuatalo:

"Changamoto ya Ukoloni wa Wawekeaji wa Kigeni Unaotokana na Kuinuliwa kwa Ukuu wa Makampuni Dhidi ya Ukuu wa Taifa Chini ya Kizazi cha Tano cha Mikataba ya Uwekezaji wa Kimataifa: Watanzania tunapswa Kuhukua Hatua Gani Baada ya Mkataba Kati ya Tanzania na Dubai Kuruhusu Ubinafsishaji wa Rejareja wa Bandari za Tanzania kwa Kiasi KInahotishia Usalaa wa Taifa Letu?"

Yaani, katika Kiingereza swali hili linasomeka hivi:

"A Challenge of Foreign Investors Colonialism as Manifested by the Elevation of Corporate Sovereignty Above State Sovereignty Under the Fifth Generation of International Investment Agreements: Where should Tanzania Go After the BIT Between Tanzania and Dubai has Facilitated Partial Privatization of Tanzania Ports in a Way that Threats Our National Security?"

Majibu ya utafiti huu yataelekezwa kwa Baraza la Usalama la Kitaifa nchini Tanzania. Tunafahamu kuwa, Baraza hili linajumuisha wajummbe wafuatao: (1) Marais wote wastafu na aliye madarakani bara na visiwani; (2) Makamu wa rais wote wastafu na walio kazini bara na visiwani; (3) Mawaziri wakuu wote waliostafu na aliye kazini; (4) Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama walio stafu na walio madarakani; (5) Maspika wote waliostafu na walio madarakani; (6) Majaji wakuu wote waliostafu na aliye madarakani; na (7) Makatibu wakuu viongozi waliostafu na walio marakani.

Kwa ajili ya kujibu swali hilo hapo juu, na kukidhi mahitaji ya hadhira tajwa, tunaona kwamba yafaa kuyajibu maswali yafuatayo:
  1. Hivi chimbuko la mfumo huu wa kimikataba wenye ngazi nne ni kitu gani?
  2. Ni hoja gani zinatuika kuhalalisha mfumo huu wa kimikataba wenye ngazi nne kwa ajili ya kulinda haki za wawekezaji?
  3. Ni hoja gani zinatumika kuukataa mfumo huu wa kimikataba wenye ngazi nne wenye kuminya haki za dola mwenyeji katika kusimamia uchumi wa ndani?
  4. Tunaweza kutummia mbinu gani ili kutengeneza uwiano mwafaka kati ya ukuu wa haki na majukumu ya wawekezaji na ukuu wa haki na majukumu ya dola katika kuratibu mambo ya ndani ya nchi?
  5. Na je, Tanzania ifanye nini ili kukwepa mabaya ya mfumo huu wa kimikataba wenye ngazi tatu na kufadika na mazuri yake?
Maswali haya yalipaswa kuwa yanajibiwa majukwaani ambako sasa hivi wanasiasa na wanaharakati wanajadili makubaliano ya Tanzania-Dubai. Hayajajibiwa.

Hivyo, kuna pengo la kimaarifa linalopaswa kuzibwa kitafiti. Hivyo, hapa chini, nawakaribisha kuleta michango ya mawazo ambayo yatatumika kujaza nafasi zilizoachwa wazi hapa chini.

Lakini, kabla ya kufanya hvyo yafaa tukubaliane kuhusu nadharia itakayotuogoza kwa kufanya upekuzi wa fasihi za kinadharia na fasihi za mjaraba, yaani "theoretical and emperical literature reviews".

6. Umuhimu wa utafiti huu

Mwaka 1967, yaani miaka saba baada ya kupata uhuru wa mwaka 1961, Tanzania ilitangaza "siasa ya ujamaa na kujitegeema."

Kanuni hii ni msingi wa kifalsafa na kisosiolojia kwa ajili ya kuratibu maisha ya kila siku katika nchi kwa kuhakikisha kwamba, kila mtu, kila azaki, kila kampuni, na kila idara ya serikali, inaitambua nafasi yake na kujifaragua inayotaka pasipo kuingilia himaya ya jirani.

Kwa Kiingereza, "siasa ya ujamaa na kujitegeema" inaitwa "the priniple of subsidiarity." Kanuni hii iliingizwa kwenye Katiba ya Tanzania mmwaka 1977.

Sehemu ya Kwanza ya Sura ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inahusu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Muungano, Vyama vyaSiasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Na chini yake, kuna ibara ya 9 inayotamka kwamba "lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano" kwa "kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa [na kibepari] kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano."

Pamoja na uwepo wa tafsiri tofauti, tafsiri zote za "siasa ya ujamaa na kujitegemea" zinakubaliana kwamba ni kanuni inayopinga unyonyaji unaotokana na uholela wa mfumo wa kibepari na kukataa ukatili unaotokana na mabavu ya mfumo wa kijamaa.

Ni kanuni ya kupatanisha maslahi binafsi na maslahi ya pamoja katika Taifa kwa kuhakikisha kwamba maslahi binafsi yanapatikana kupitia uratibu wa maslahi ya pamoja. Na kazi pekee ya serikali ni kuratibu upatikanaji wa maslahi ya pamoja.

Sheria ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi, namba 18/2010 (sura ya 103), imetoa tafsiri ya kisheria ya "siasa ya ujamaa na kujitegemea," kupitia kanuni zake za Toleo la Serikali Na 37/2020.

Katika kanuni hizi, Ibara ya 2 inasema yafuatayo, kuhusu tafsiri ya kisheria ya "siasa ya ujamaa na kujitegemea,":

“[Public-private] 'partnership model' means any form of engagement of the private party by the public party to which may include among others the form of: (a) service and management contracts; (b) design, build, operate and transfer; (c) design, build, operate and maintain; (d) build, operate and transfer; (e) design, build and operate; (f) design, build, finance, operate and maintain; (g) build, own, operate and transfer; (h) build, lease and transfer; (i) build, transfer and operate; (j) operation and maintenance;(k) operation, maintenance and management; and (l) lease, develop and operate.(k) operation, maintenance and management; and (l) lease, develop and operate."

Mitindo yote 12 ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi inaheshimu jukumu la serikali katika kuratibu (the duty to regulate) maisha ya makundi yote yaliyomo ndani ya nchi, wakiwemo wawekezaji wa kigeni.

Katika kutekeleza jukumu hili, Kanuni ya Ujamaa na Kujitegemea inaweza, na inapaswa, kutumika katika kuratibu ushirikiano na mshikamano ndani ya taifa na katika Jumuiya ya Kimataifa, kwa kuweka msingi wa kuendelea kuboresha sera, mikataba na itifaki mbali mbali zilizowekwa na wadau mbalimbali.

Serikali, Bunge na Mahakama ni vyombo vyenye nafasi kubwa katika mchakato huu. Lakini, Mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai unazipora madaraka taasisi hizi nyeti.

Kwanza, hauna ukomo wa muda na wala ukomo wa idadi ya miradi. Pili, unatishia ukuu wa Bunge katika kutunga sheria. Tatu, unatishia ukuu wa mahakama kwa kuziondolea mamlaka ya kuubatilisha.

Nne, unatishia ukuu wa serikali kwa kuiweka chini ya serikali ya Dubai. Na tano, unatishia ukamilifu wa mipaka ya himaya ya Tanzania, kwa kutishia kuwaondolea baadhi ya raia haki ya kumiliki ardhi.

Ni mkataba ambao unafungua milango ya ukoloni wa walowezi wa Kigeni katika Pwani ya Bahari ya Hindi na kwenye maziwa yote yaliyoko nchini Tanzania Bara.

Hivyo, ni lazima kutumia ushahidi wa kitafiti ili kulinda na kuhami ukuu wa dola ya Tanzania, haki za Watanzania, wajukuu zao na wajukuu wa wajukuu zao.

7. Yaliyomo kwenye andiko hili

Kwa ujumla, andiko zima limegawanywa katika sehemu zifuatazo;

I. Usuli​
II. Utangulizi​
1. Chimbuko la andiko hili​
2. Mikataba ya uwekezaji wa kimataifa ni kama mtego wa panya​
3. Muundo na maudhui ya mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai​
4. Kiini cha tatizo katika mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai​
5. Maswali yanayaohitaji kupatiwa ajwabu ya kitafiti​
6. Umuhimu wa utafiti huu​
III. Methodolojia ya utafiti iliyotumika​
1. Utaratibu na hatua za utafiti​
2. Misingi ya kimetafizikia inayobeba utafiti huu​
3. Mtiririko wa kimantiki wa utafiti huu​
4. Mkakati wa utafiti huu​
5. Upeo wa majira ya utafiti huu​
6. Utengenezaji wa sampuli ya utafiti huu​
7. Mbinu za kukusanya taarifa za kitafiti​
IV. Upekuzi wa fasihi za kinadharia na kimjaraba​
1. Upekuzi wa fasihi zenye ushahidi wa kinadharia​
2. Upekuzi wa fasihi zenye ushahidi mwa kimjaraba​
3. Usanifu wa mfumo wa dhana na nadharia elekezi​
V. Uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti​
VI. Udadisi wa matokeo ya utafiti​
1. Udadisi wa matokeo ya utafiti kuhusu hoja ya utetezi​
2. Udadisi wa matokeo ya utafiti kuhusu hoja ya ukinzani​
3. Udadisi wa matokeo ya utafiti kuhusu hoja ya usuluhishi​
VII. Muhtasari, hitimisho, na mapendekezo​
VIII. Marejeo​

III. METHODOLOJIA YA UTAFITI ILIYOTUMIKA

1. Utaratibu na hatua za utafiti


Huu ni utafiti wa kupekua nyaraka za karatasi na kidijitali zilizoko mezani kwa mtafiti. Umefanyika kwa msaada wa kanuni ya kubainisha pengo la maarifa, kukusanya taarifa stahiki, kuzitathmini taarifa hizo, na hatiaye kuliziba pengo hilo. Yaani "information gap analysis and evaluation methodology." Methodolojia hii inazo hatua zifuatazo:
  1. Kubainisha swali kuu la utafiti
  2. Kubainisha maswali madogo ya utafiti
  3. Kubainisha maswali ya utafiti ambayo tayari majibu yake yanafahamika.
  4. Kubainisha maswali ambayo mmajibu yake hayafahamiki.
  5. Kubainisha vyanzo vya taarifa vinavyohusiana na maswali ambayo majibu yake hayafahamiki. Hapa kuna taarifa za karatasini, mdomoni na taarifa za kidijitali. Yaanu printed, human and digital intelligence.
  6. Kupekua fasihi andishi zilizokusanywa na kujibu maswali yasiyo na majibu
  7. Kuchakata matokeo ya utafiti kwa kuandika taarifa ya mwisho.
  8. Kuhariri na kuchapisha taarifa ya utafiti.
2. Kanuni za kimetafizikia zinazobeba utafiti huu (Philosophical foundations of the study)

Utafiti huu umefanyika kwa kuzingatia kanuni ya kifalsafa isemayo kwamba hapa duniani kuna ukweli wa aina mbili.

Mosi, kuna ukweli unaopatikana nje ya kichwa cha mtafiti, ambaye anaweza akaugundua na kutuletea taarifa sahihi, au akashindwa kuugundua na kutuletea taarifa potofu.

Hapa kuna vitu vitatu, yaani mawazo, maneno na ukweli, vinavyounda pembetatu ya kisemantiki (semantic triangle).

Yaani, kanuni ya pembetatu ya kisemantiki ni kanuni ya kifalsafa isemayo kwamba, kuna ukweli ambao hautengenezwi na akili ya binadamu.

Badala yake, akili ya binadamu inaugundua ukweli huo, na hata ukweli huo usipogunduliwa na binadau yeyote unaendelea kuwepo pasipo kujulikana kwa yeyote (positivistic reality). Mfano ni ukweli kwamba kuna Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania.

Kinyume cha ukweli unaotajwa kwenye pembetatu ya kisemantiki ni ukweli unaotengenezwa na akili ya binadamu, na sio vinginevyo.

Huu ni ukweli unaotengenezwa na kikundi cha watu kwa njia ya makubaliano ya kura za kidemokrasia. (constructivistic reality)

Mifano hapa ni kanuni za mpira wa miguu au kanuni zinazohusu muundo wa mikataba ya uwekezaji wa kimataifa.

Yaani, miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa inayotumika Amerika, India, Udachi, Dubai, Ujeruamani, na katika mataifa baki ya dunia ya kwanza na dunia ya pili, ni tofauti kwa sababu imebuniwa na watu tofauti.

Huu ni ukweli ambao unaweza kubadilishwa na watu hao hao kupitia maammuzi mapya.

Hivyo, sisi kama watafiti kuhusu miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa tunaongozwa na kanuni ya "positivism" na serikali za magharibi zinapokuwa zinatengeneza miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa zinaongozwa na kanuni ya "constructivism."

Ni muhimu kuelewa tofauti hii kwa ajili ya kujipanga sawa sawa katika siku za usoni, maana nasi katika ulimwengu wa tatu tunayo haki ya kusanifu au kuhakiki miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa.

3. Mtiririko wa kimantiki wa utafiti (Logical sequence of the study)

Utafiti huu ulianzia kwenye nadharia ya msingi yenye kuongoza mahusiano ya kimmataifa kati ya nchi na nchi, nchi na makampuni, nchi na azaki.

Kisha uchunguzi wa hatua kwa hatua wa miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa ulifanyika kwa nchi zilizoteuliwa. Hatimaye ufananisho na hitiisho vilifanyika.

Kwa hiyo, huu ni utafiti ulioanzia kwenye ushahidi mwingi na kufanya udadavuzi kuelekea kwenye hitimisho linalobeba ushahidi dogo, yaani "deductive reasoning."

Yaani, huu sio utafiti ulioanzia kwenye ushahidi mchache na kufanya udadavuzi kuelekea kwenye hitimisho linalobeba ushahidi mwingi, yaani "inductive reasoning."

4. Mkakati wa utafiti (Research strategy)

Mkakati wa kesi sambamba za kitafiti, yaani "multiple case study strategy," ulitumika ili kutoa mwanya wa kufananisha na kutofautisha miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa katika nchi kadhaa.

5. Upeo wa majira ya utafiti (Time horizon)

Kwa ajili ya kupata mwanga zaidi, utafiti huu ulichunguza mabadiliko kwenye miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa tangu mwaka 1947 iliponzishwa GATT hadi sasa.

6. Utengenezaji wa sampuli ya utafiti (sampling design)

Kusudi kupata mwanga halisi kuhusu miundo ya mikataba ya uwekezaji wa kimataifa nchi zenye mikataba mingi zilihusika, hasa nchi ya Udachi, mmarekani, Ujerumani, India, UAE, na Dubai.

7. Mbinu za kukusanya taarifa (Data collection methods)

Taarifa za utafiti zilikusanywa kwa kujaza dodoso lenye maswali ya utafiti, na kisha kuyajibu maswali hayo kwa kupekua fasihi andishi, kuchabua taarifa za kidijitali (hotuba), na vyanzo baki

IV. UPEKUZI WA FASIHI ZA KINADHARIA NA FASIHI ZA KIMJARABA

1. Upekuzi wa fasihi zenye ushahidi wa kinadharia (theoretical literature review)


...........................
.........................

2. Upekuzi wa fasihi zenye ushahidi wa kimjaraba (empirical literature review)

....................
....................

3. Mfumo wa dhana na nadharia zilizo msingi wa utafiti (conceptual and theoretical framework)


Mapitio ya fasihi andishi hapo juu yanabainisha jambo moja la wazi. Utafiti huu unachunguza mikataba ya kimataifa kuhusu uwekezaji katika nchi husika, ambao unazalisha uhusiano kati ya serikali za nchi na wawekezaji wa kigeni kutoka nchi za ng'ambo.

Mikataba hii inaongelea uhusiano kati ya nchi mwenyeji, nchi mgeni na makampuni ya kigeni. Makampuni ya kigeni yanafanya kazi na makapuni ya kigeni na mapkampuni ya kienyeji pia. Kunapotokea mgogoro wa kimikataba, migogoro hiyo inatatuliwa ama katika mahakama za usuluhishi za kimataifa, au kwenye mahakama za ndani.

Tunaona kuwa, miradi inayotekelezwa na makampuni ya kigeni ni ile ambayo ingetekelezwa na serikali, lakini serikali za nchi husika hazina uwezo, ama wa kifedha, kitekinolojia au kiustadi.

Pia, tunaona kuwa, mikataba ya uwekezaji wa kimmataifa inasema kuwa migogoro ya uwekezaji inayoweza kutatuliwa ndani ya nchi itatuliwa na mahakama za ndani.

Kadhalika, tunaona kwamba migogoro ya uwekezaji isiyoweza kutatuliwa ndani ya mahakaa za nchi mwenyeji itatuliwe na mahakama za kimataifa.

Tena, tunaona kwamba, serikali za nchi wenyeji zinabinafsisha kwa sekta binafsi za nje yale majukumu ya kiuchumi ambayo haziwezi kuyatekeleza. Lakini, zinabakiza majukumu ya kiuchumi na kiserikali yaliyo ndani ya uwezo wake.

Kutokana na haya yote, tafsiri yetu ni kwamba, nadhari unayoongoza mmahusiano haya ya kimataifa ni kanuni ya kifalsafa, kisiasa na kijamii, iitwayo "kanuni ya ujamaa na kujitegemea," yaani, "the principle of subsidiarity."

Hapo awali tumeona kuwa, ibara ya 9 ya Katiba ya Tanzania (1977) inatamka kwamba "lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano" kutokana na kufuata "siasa ya Ujamaa na Kujitegemea."

Pia tumeona kuwa Sheria Namba 18/2010 na Kanuni zako Toleo Namba 37/2020 ni tafsiri rasmi ya siasa hii.

Sasa tunataka kuifafanua kwa ukamilifu kanuni hii kusudi kuweka msingi thabiti wa kinadharia kwa ajili ya utafiti huu.

Kwa mujibu wa "kanuni ya ujamaa na kujitegemea," katika kila nchi mahusiano baina ya serikali na watu binafsi, familia, azaki, taasisi za kidini, na makapuni, yanapaswa kuratibiwa kwa kuzingatia mambo mawili makubwa.

Kwanza, kanuni ya ujamaa na kujitegemea inaweka kikomo cha kuingilia kati kwa mamlaka ya juu dhidi ya mtu au jumuiya iliyo katika nafasi ya kujiendesha yenyewe.

Na pili, kanuni ya ujamaa na kujitegemea inaeleza wajibu kwa mamlaka hiyo ya juu kuchukua hatua za uingiliaji kati kwa faida ya mtu au kundi hilo katika ngai ya chini ili kuhakikisha kwamba ngaiz hiyo inapewa njia ya kufikia malengo yake (Ken Endo 1994).

Kwa hiyo, kanuni ya ujamaa na kujitegemea inayo tafsiri hasi na tafsiri chanya, zinaofanya kazi pamoja, kama pande mbili za shilingi.Tunaweza kufafanua tofauti kati yatafsiri hasi na tafsiri chanya kwa njia zifuatazo.

Kwa upande mmoja, tafsiri hasi ya kanuni ya ujamaa na kujitegemea inaweka kizuizi cha uwezo wa jumuiya ya juu kuhusiana na mtendaji wa chini.

Hasa, tafsiri hasi ya kanuni ya ujamaa na kujitegemea ina maana kwamba: (1) jumuiya ya juu haiwezi kuingilia kati ikiwa halaiki ya chini inaweza kutimiza malengo yake kwa njia ya kuridhisha; au kwamba (2) jumuiya ya juu haipaswi kuingilia kati ikiwa halaiki ya chini pekee inaweza kutimiza malengo yake kwa njia ya kuridhisha; au (3) jumuiya ya juu hailazimiki kuingilia kati ikiwa haijakabidhiwa jukumu la kufanya hivyo.

Hivyo, kwa mujibu wa tafsiri hasi ya kanuni ya ujamaa na kujitegemea, katika ngazi ya jumuiya ya kitaifa, sio serikali au juuiya nyingine yoyote ya ngazi za juu, iliyo kati ya Ikulu na kaya, yenye haki ya kusimmamia rasilimali, au kuchukua ubunifu na wajibu wa watu binafsi na jumuiya zilizo kwenye ngazi za kati, ikiwa jumuiya hizo zinajiweza.

Na katika ngazi ya jumuiya ya kimataifa, sio serikali ya nchi baki au makampuni ya kimataifa, yaliyo kati ya Ikulu na umoja wa mataifa, yenye haki ya kusimamia rasilimali, au kutekeleza wajibu wa serikali yoyote ya nchi na mashirika ya kisekta yaliyo chini yake, iki jumuiya hizi zinajiweza.

Kwa upande wa pili, tafsiri chanya ya kanuni ya ujamaa na kujitegemea inaondoa katazo la uingiliaji kati na kuongelea uwezekano na hata ulazima wa uingiliaji kati kutoka kwa jumuiya ya juu.

Hasa, tafsiri chanya ya kanuni ya ujamaa na kujitegemea ina maana kwamba: (1) jumuiya ya juu inaweza kuingilia kati ikiwa halaiki ya chini haiwezi kutimiza malengo yake kwa kuridhisha; au kwamba (2) jumuiya ya juu inapaswa kuingilia kati ikiwa halaiki ya chini haiwezi kutimiza malengo yake kwa njia ya kuridhisha; au kwamba (3) jumuiya ya juu inalazimika kuingilia kati kama ikipewa jukumu la kufanya hivyo.

Katika nchi inayoongozwa na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia, Kanuni ya ujamaa na kujitegemea ni nyenzo muhimu sana katika kuweka mipaka kati ya serikali, mtu binafsi, familia, asasi za kiraia, taasisi za kidini, na makampuni yanayotekelea kazi zake sokoni, ili kuhakikisha kwamba, hakuna hata kundi moja kati ya makundi haya ya jamii linalovuka mipaka ya hiaya yake na kuingia kwenye himaya ya jirani yake bila sababu halali.

Kila mtu na kila kundi la kijamii lililotajwa ni mtendaji mwenye uhuru kamili unaokomea kwenye mipaka ya himaya yake.

Kwa maneno mengine, kanuni ya ujamaa na kujitegemea inasisitiza kwamba maamuzi katika jamii yanahitajika kuchukuliwa katika ngazi ya chini kabisa, karibu na wananchi wanaolijua vizuri tatizo na wenye uwezo wa kulitatua.

Kama wananchi wanaolijua vizuri tatizo hawana uwezo, basi ngazi ya kwanza, iliyo juu kidogo, ifanye uingiliaji kwa kutoa msaada unaotakiwa, na kisha kujiondoa.

Ndio kusema kwamba, matatizo ya kijamii yanapaswa kutatuliwa vyema katika ngazi ambako yanatokea kwa kushirikiana na watu wa ngazi hiyo. Na ikiwa utatuzi huo hauwezekani, msaada utolewe na ngazi ya juu kidogo yenye uwezo wa kufanya utatuzi.

Yaani, shughuli yoyote ambayo inaweza kufanywa kwa ufanisi katika ngazi fulani ya kijamii na chombo cha maauzi kilichogatuliwa inapaswa kutekelewa na chombo hicho katika ngazi hiyo, na sio katika ngazi nyingine.

Kanuni hii maana yake ni kwamba, ni kitendo cha uonevu kuchukua kutoka kwa watu binafsi yale majukumu wanayoweza kukamilisha kwa juhudi na ubunifu wao wenyewe na kuyaweka mikononi mwa jumuiya kubwa zaidi.

Kanuni hii inamaanisha kwamba, vivyo hivyo ni dhuluma na uvunjifu wa utaratibu wa haki kuyaweka majukumu yanayoweza kutekelewa na watu binafsi au jumuiya za chini mikononi mwa jumuiya kubwa zaidi.

Na Kanuni hii inamaanisha kwamba, kila shughuli ya kijamii inapaswa kwa asili yake kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa wanajamii, na kamwe wasitelekezwe wala kunyonywa.

Kwa ujumla, kanuni ya ujamaa na kujitegemea inatokana na ukweli kwamba kila mtu ni kiumbe ambaye ni kitovu cha vitu vitatu vikuu.

Mosi, kuna akili ya kufanya tafakari juu ya ukweli na uwongo, malengo mema na malengo mabaya, mbinu haramu na mbinu halali.

Pili, kuna uwezo wa kufanya maamuzi huru ya kuchagua baadhi ya mbinu na malengo na kubagua mbinu na malengo baki.

Na tatu, hatimaye, kuna uwezo wa mhusika kutekeleza maamuzi yanayotokana na uchaguzi wake kwa kufanya matendo huru ya kimwili.

Kwa mujibu wa kanuni hii, aina nyingine zote za jamii, kuanzia kwenye familia, kupitia kwenye azaki, makampuni, serikali za mitaa, serikali kuu hadi na jumuiya za kimataifa, ni vyombo ambavyo ni maslahi ya pamoja vinavyoundnwa ili vitumike kama mbinu za kufanikisha ustawi binafsi wa mtu mmoja mmoja.

Kwa hiyo, kanuni hii inayo matumizi katika ngazi ya jumuiya ya kimataifa pia. Yaani, kama ambavyo, katika kila nchi mahusiano baina ya serikali na watu binafsi, familia, azaki na makapuni, yanaongozwa na kanuni ya ujamaa na kujitegemea, hali kadhalika, kanuni ya ujamaa na kujitegemea inapaswa kutumika katika kuratibu mahusiano baina ya serikali ya nchi moja na serikali ya nchi baki, serikali ya nchi na wawekezaji, duniani kote.

Kwa hiyo, kuanzia kijijini, kupitia katani, wilayani, mkoani, ikulu, kwenye serikali za kikanda, hadi huko umoja wa mataifa, kusudi haki itawale katika maeneo yote, ya maisha binafsi na ya umma, ya maisha ya kiuchumi na ya kijamii, ya maisha ya kisiasa na ya kisheria, basi, haki inahitaji kutegemezwa na kanuni ya ujamaa na kujitegemea.

Hivyo, hitimisho la kimantiki ni kwamba, ubinafsishaji wa rasilimali na taasisi za ndani unapaswa kuilenga sekta binafsi ya ndani ya nchi, kabla ya kuilenga sekta binafsi kutoka nje ya nchi, isipokuwa kama sekya binafsi ya ndani haiwezi hata baada ya kuwezeshwa.

Aidha, hitimisho la kimantiki ni kwamba, serikali ya nchi inapaswa kujizuia kubinafsisha, kwa jumuiya ya kimataifa, huduma za kiuchumi na kiutawala zilizo ndani ya uwezo wake, au ndani ya uwezo wa jumuiya ya kitaifa.

V. UCHAMBUZI NA UWASILISHAJI WA MATOKEO YA UTAFITI
(Analysis and Presentation of study findings)


...........................
..........................

VI. UDADISI WA MATOKEO YA UTAFITI
(Discussion of study findings)

1. Udadisi wa matokeo ya utafiti kuhusu hoja ya utetezi

............................
...........................

2. Udadisi wa matokeo ya utafiti kuhusu hoja ya ukinzani

........................
.....................

3. Udadisi wa matokeo ya utafiti kuhusu hoja ya usuluhishi

..........................
.......................

VII. MUHTASARI, HITIMISHO, NA MAPENDEKEZO
(Summary conclusion and recommmendations)


..............................
.............................


VIII. MAREJEO
  1. Alfred Charles(2014), "The new scramble for Africa’s resources: implications for its development," Africanus, 44.2:114.
  2. Anthony Angie(2004), Imperialism, Sovereignty and the Making of International Law (Cambridge: CUP)
  3. Antony Anghie (2004), Imperialism, Sovereignty and the Making of International Law (Cambridge: CUP)
  4. Barbara Gayling-Westphal (2015), Intergovernmental Agreements and Host Government Agreements on Oil and Gas Pipeline: A Comparison (Brussels, Belgium: Energy Charter Secretariat).
  5. Q. Biyyaa (2009), The environmental cost of the EuroArab scramble for Africa. Sourced at: http://farmlandgrab.org/2799.
  6. Charles Riziki Majinge (2012), "Emergence of New States in Africa and Territorial Dispute Resolution: The Role of the International Court of Justice," Melbourne Journal of International Law, 13.1:463-503.
  7. Charlotte SieberGasser (2021), “Flexibility in International Economic Law versus Pacta Sunt Servanda: Maintaining Legitimacy Over Time,” Published in C. SieberGasser and A. Ghibellini (2021) (eds), Democracy and Globalization: Legal and Political Analysis on the Eve of the 4th Industrial Revolution.
  8. Dakas C.J. Dakas (2018), “Interrogating Colonialism: Bakassi, the Colonial Question and the Imperative of Exorcising the Ghost of Eurocentric International Law,” In: Chile EboeOsuji and Engobo Emeseh (Eds.), Nigerian Yearbook of International Law 2017, Volume 2017: 113-141.
  9. Daniel C. Turack (1984), "A Review of ‘International law and the new states of Africa: A study of the international legal problems of state succession in the newly independent states of Eastern Africa,' a Book by Yilma Makonnen (1983)," Maryland Journal of International Law, 8.2:303-305.
  10. Department of Justice and Equality(2009), Report by Commission of Investigation into Catholic Archdiocese of Dublin (Murphy Report), See Article 58.20.
  11. Duncan B. Hollis(2020), (Editor), The Oxford Guide to Treaties, 2nd Edition(OUP)
  12. Gardner David (2014), “The Colonial Nature of International Law”, EInternational Relations . Sourced at: http://www.eir.info/2010/06/08/thecolonialnatureofinternationallaw/
  13. Guy Leopold Kamga Wafo(1998), Political Risk and Foreign Direct Investment (University of Konstanz: Dissertation)
  14. Haendel Dan (1979), Foreign Investments and the Management of Political Risk, Westview special studies in international Economics and Business.
  15. Honoré Le Leuch(2017), "International oil and gas pipelines: Legal, tax, and tariff issues," In: Philip Daniel, Michael Keen, Artur Świstak, Victor Thuronyi (2017), (Eds.), International Taxation and the Extractive Industries: Resources without borders (New York: Routledge).
  16. James Thuo Gathii, “Evaluating the Dispute Settlement Mechanism of the African Continental Free trade Agreement”, Afronomicslaw Blog, April 10, 2019; Online: http://www.afronomicslaw.org/2019/0...ismoftheafricancontinentalfreetradeagreement/
  17. James Zhan, Jorg Weber, Joachim Karl (2011), "International Investment Rulemaking at the Beginning of the Twenty-First Century: Stocktaking and Options for the Way Forward," In: Jose E. Alvarez and Karl P. Sauvant (2011), Pages 193–210.
  18. Jean-Louis Pierre Tauran (2003), Hotuba ya Kustaafu Uwaziri wa Mambo ya Nje wa Vatican. Kwa miaka 13 Tauran alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya dola ya Vatican. Maneno hayo hapo juu aliyasema kupitia hotuba yake ya kustaafu, aliyoitoa mbele ya Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Ufaransa, tarehe 5 Novemba 2003.Ufafanuzi zaidi wa mawazo yake unapatikana hapa: "Vatican Foreign Ministers on concordats: Tauran (1990-2003) Justifies Vatican diplomacy."
  19. Jiang Zhifeng (2022), “Pacta Sunt Servanda and Empire: A Critical Examination of the Evolution, Invocation, and Application of an International Law Axiom,” Michigan Journal of International Law, 43.3:745-801.
  20. John H. Dunning and Sarianna Lundan (2008), “Institutions and the OLI Paradigm of the Multinational Enterprise,”Asia Pacific Journal of Management 25(4): 573-593.
  21. José Alvarez, Karl Sauvant, Kamil Ahmed and Gabriela Vizcaíno(2011), The Evolving International Investment Regime: Expectations, Realities, Options (NY:OYP).
  22. Jose Alvarez, Karl Sauvant, Kamil Ahmed, and Gabriela Vizcaino (2011) (eds), The Evolving International Investment Regime. Expectations, Realities, Options (Oxford: Oxford University Press).
  23. Jose E. Alvarez (2009), “Contemporary foreign investment law: An ‘empire of law’ or the ‘law of empire’?” Alabama Law Review 60: 943–75.
  24. Karl Sauvant and José Alvarez(2011), "International Investment Law in Transition," In:Jose Alvarez and Karl Sauvant, Kamil Ahmed and Gabriela Vizcaino (2011), eds., The Evolving International Investment Regime: Expectations, Realities, Options (New York: Oxford University Press), pp. xxxixlii.
  25. Ken Endo (1994), "The Principle of Subsidiarity: From Johannes Althusius to Jacques Delors," Hokkaido Law Review, 44.6:652-553.
  26. Kimenyi, MS and Lewis, Z. 2011. The BRICs and the new scramble for Africa. http://www.brookings.edu/~/media/research/files/reports/2011/1/africa economy agi/01_africa_economy_agi_ kimenyi_lewis.pdf (Accessed 7 March 2012).
  27. Mareike Oldemeinen (2010), “Is International Law Colonial?”, EInternational Relations. Sourced at: https://www.eir.info/pdf/3958.
  28. Matthew Craven (2005), “What Happened to Unequal Treaties? The Continuities of Informal Empire,” Nordic Journal of International Law, 74: 335–382.
  29. Mieke van der Linden (2017), The Acquisition of Africa, 18701914: The Nature of International Law (The Netherlands: Brill Nijihoff).
  30. MIGA (Multilateral Investment Guarantee Agency) (2009), World Investment and Political Risk 2009 (Washington DC: World Bank Group).
  31. MIGA (Multilateral Investment Guarantee Agency), (2011) World Investment and Political Risk 2011 (Washington DC: World Bank Group).
  32. OECD (2010), Evolution of International Investment Agreements in the MENA Region. Paper prepared in the context of the MENAOECD Working Group on Investment Policies and Promotion.
  33. Paul Comeaux and Stephan Kinsella (1994), "Reducing Political Risk in Developing Countries: Bilateral Investment Treaties, Stabilization Clauses, Bilateral Investment Treaties, Stabilization Clauses, and Miga & Opic Investment Insurance And Miga & Opic Investment Insurance," NYLS Journal of International and Comparative Law: 15.1, Article 2:1-48.
  34. Patricia Lindelwa Makoni (2015), "An Extensive Exploration of Theories of Foreign Direct Investment," Risk Governance and Control: Financial Markets and Institutions, 5.2:7783.
  35. Piyaphan Changwatchai (2010), The Determinants of FDI Inflows By Industry to Asean (The University of Utah: Department of Economics, PhD Dissertation).
  36. Rafael Leal-Arcas (2015), Energy Transit Activities: Collection Of Intergovernmental Agreements On Oil And Gas Transit Pipelines And Commentary (Brussels, Belgium: Energy Charter Secretariat).
  37. Robert Owen Keohane (2001), "Governance in a Partially Globalized World: Presidential Address, American Political Science Association, 2000," American Political Science Review 95:1.
  38. Roberto Echandi and Anna JoubinBret (2007), Bilateral Investment Treaties, 19952006: Trends in Investment Rulemaking (New York/Geneva: United Nations).
  39. UNCTAD (2009), World Investment Report 2009: Transnational Corporations, Agricultural Production and Development (Geneva: UNCTAD).
  40. Wenhua Shan, Sheng Zhang and Jinyuan Su (2020) (Eds), China and international dispute resolution in the context of the belt and road initiative (NY:CUP).
  41. World Bank(2019), Retention and Expansion of Foreign Direct Investment: Political Risks and Policy Responses (Washington, DC: World Bank Group).
  42. Yilma Makonnen (1983), International law and the new states of Africa: A study of the international legal problems of state succession in the newly independent states of Eastern Africa (Addis Ababa: Ethiopian National Agency for UNESCO).

Utafiti huu umeratibiwa na:

Mama Amon Desk
"Sumbawanga Town"

Sumbawanga.
31 Julai -15 Agosti 2023.
 

Attachments

  • 1691170723400.png
    1691170723400.png
    17.5 KB · Views: 24
  • 1691264884489.png
    1691264884489.png
    6.9 KB · Views: 29
1690826887153.png

Mchoro: Uhusiano kati ya Tanzania, Dubai, Kampuni zitakazotekeza miradi, na mikataba husika

I. Utangulizi


Tangu 25 Oktoba 2022, kuna makubaliano ya Kiserikali kati ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari za Tanzania yanayoongozwa na mfumo wa mikataba unaojumuisha mkataba wa IGA, mkataba wa HGA, mikataba ya wakandarasi, mikataba ya mikopo ya mabenki, na kadhalika, kama mchoro hapo juu unavyoonyesha.

Mara nyingi, mfumo huu hutumika kwenye miradi inayovuka mipaka ya nchi ambili au tatu. Mfano mmoja ni mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, yaani mradi wa bomba na Hoima-Tanga (EACOP) lenye urefu wa kilommeta 1,443.

View attachment 2704199

Na Mfano mwingine ni mradi wa bomba la mafuta kutoka Bahari ya Kaspiani hadi Bahari ya mediteraniani linalovuka nchi tatu, yaani Baku–Tbilisi–Ceyhan (BTC) pipeline lenye urefu wa kilometa 1,768.

View attachment 2704194

Hivyo, leo nashauri tutafakari pamoja kuhusu maswali yafuatayo:
  1. Hivi kwa nini Wawekezaji katika bandari kutoka Dubai wanalazimisha mfumo wa mikataba unaojumuisha mapatano ya IGA na makubaliano ya HGA wakati miradi yote itatekelezwa ndani ya ardhi ya Tanzania pekee?
  2. Faida na hasara za mfumo huu wa kimikataba ni zipi?
  3. Je, kwa nini Tanzania tumekubaliana na mfumo huu wa kimikataba?
  4. Na je, ni lazima Tanzania tukubaliane na mfumo huu wa kimikataba?
Karibuni kwa michango ya mawazo ambayo yatatumika kujaza nafasi zilizoachwa wazi hapa chini.

II. Matokeo ya utafiti kutokana na michango ya watu

...........................

III. Muhtasari, hitimisho, na mapendekezo

..............................


IV. Marejeo

...............................

Utafiti huu unratibiwa na:

Mama Amon Desk
"Sumbawanga Town"

Sumbawanga.
Epuka Matapeli..
 
Kuendesha nchi kwa Tz imekuwa kazi kuliko hata kuendesha mradi wa kupika vitumbua mjini. Ndio ujinga wetu ulipo
 
Nadhani ni kuupa nguvu mkataba. Yaani kuwakumbusha wadau wa mradi kuwa hapa nchi inaangalia kwa ukaribu, msije leta dharau kuwa mna deal na just a mere company. Pia kuwapa confidence wadau wa mradi- yaani ni kama vile bond za BOT, zinakuwa na guarantee, zero risks...
 
Unaifahamu IGA ni nini? Na HGA ni nini?


Hiyo yote siyo mikataba ya uendeshaji chochote.

IGA ni makubaliano ya kushirikiana au kufanya shughuli zipi kwenye nyanja zipi baina ya serikali husika.

HGA ni mkataba unaoonesha sheria na kanuni za nchi mwenyeji ambazo wageni wsnatakiwa wazifate wakiwepo katika kutimiza shighuli zao.

Nao sio mkataba wa uendeshaji chochote.

Hizo zote ni "guidelines" zap mikataba ya utendaji.
 
Unaifahamu IGA ni nini? Na HGA ni nini?


Hiyo yote siyo mikataba ya uendeshaji chochote.

IGA ni makubaliano ya kushirikiana au kufanya shughuli zipi kwenye nyanja zipi baina ya serikali husika.

HGA ni mkataba unaoonesha sheria na kanuni za nchi mwenyeji ambazo wageni wsnatakiwa wazifate wakiwepo katika kutimiza shighuli zao.

Nao sio mkataba wa uendeshaji chochote.

Hizo zote ni "guidelines" zap mikataba ya utendaji.

Political Risks, Bilateral investment treaties, Host Government Agreements, and Stabilization Clauses
1697923214878.png


Hello Faiza Foxy, no research no right to speak. Here are the facts about the terms you are fumbling about:

1. Political Risks to International Investors

Political Risks refers to risks faced by investors involved in cross-border transactions, including currency inconvertibility, expropriation, war and insurrection (such as a coup d’etat), terrorism, and actions of non-government activists, paramilitaries, or revolutionaries.

To protect themselves from these risks, foreign investors can take several actions including: Obtain political risk insurance, Negotiate a stabilization clause or economic equilibrium clause with the local government, and Structuring the transaction to take advantage of a bilateral investment treaty (BIT).

2. Bilateral investment treaty (BIT)

A Bilateral investment treaty (BIT), also known as an International Investment Agreement (IIA) is an agreement made between two countries containing reciprocal undertakings for the promotion and protection of private investments made by nationals of the signatories in each other's territories. These agreements establish the terms and conditions under which nationals of one country invest in the other, including their rights and protections.

BITs provide protection against illegal nationalization and expropriation of foreign assets and other actions by a signatory of the BIT that may undermine the ownership or economic interest of a national of the other signatory.

BITs are negotiated agreements between the signatory parties, their terms vary. However, they generally include the following rights and protections: National treatment, Most-favored-nation treatment, Fair and equitable treatment,
Compensation in the event of expropriation.

One of the main protections under a BIT is that it allows foreign investors to sue states directly by submitting claims for breach of the BIT to international arbitration tribunals rather than to local courts.

3. Host Government Agreement (HGA)

A Host Government Agreement (HGA) is an agreement between a foreign investor and a local or host government governing the rights and obligations of the foreign investor and the host government with respect to the development, construction, and operation of a project by the foreign investor in the host country.

Many HGAs include a stabilization clause designed to minimize the financial and political risks posed to foreign investors as a result of sudden changes in national law in the host country. An HGA is often required by foreign investors in host countries where foreign investors' rights are not otherwise protected by a bilateral investment treaty, where the latter is also known as an intergovernmental treaty (IGA).

4. Stabilization Clause

Stabilization Clause is a clause often included in a host government agreement (HGA) or other international investment agreement that addresses how changes in law following the execution of the HGA are to be treated and the extent to which these changes modify the rights and obligations of the foreign investors under the HGA. A stabilization clause is a means for foreign investors to mitigate or manage the political risks associated with their project.

5. Types of stabilization clauses

The most common types of stabilization clauses are: Freezing clauses, Economic equilibrium clauses, and Hybrid clauses.

Freezing clauses: These clauses fix or freeze for the term of the project the applicable domestic legislation or regulations affecting the project to those in effect as of the date of the HGA. Under these clauses, legislation adopted after the date of the HGA do not apply to the foreign investors or the project unless the investors agree.

Economic equilibrium clauses: Under these clauses, changes in law occurring after the execution of the HGA apply to the project and its foreign investors except that the host government must usually indemnify the investors from and against the costs of complying with the new laws.

For example, the host government may impose new emissions standards concerning a power plant, but the costs of modifying the plant's design or re-fitting the plant will be borne by the government.

These clauses are intended to preserve the economics of the project. The scope of the host government's indemnification obligation depends on the negotiating strength of the parties and the host government's need for the proposed investment.

Hybrid clauses: A combination of the freezing and economic equilibrium clauses. Under these clauses, foreign investors are not automatically exempted from the application of new laws. Rather, these clauses provide that the investors may be granted an exemption. Hybrid clauses may also require compensation for certain specified changes in law as opposed to all laws that may affect the project and its foreign investors.

Although stabilization clauses are beneficial to foreign investors and are perceived as helping host governments attract foreign investment, they can prevent host governments from taking the actions necessary to protect their citizens' rights and enforce national laws that apply elsewhere in the country.

Domestic investors generally do not like these clauses because foreign investors may receive better terms than they do. Stabilization clauses have also been criticized by international human rights organization Amnesty International as placing a price tag on human rights because they may exempt either explicitly (through the freezing clauses) or implicitly (through economic equilibrium clauses by making it expensive for the government) foreign investors and their projects from complying with human rights laws.

6. Questions to Faiza Foxy

Has the government of Tanzania or any Tanzanian investors invested anything in Dubai that requires protection under IGA?

If no, why do Dubai investors require an IGA with respect to ports privatization, instead of a singe HGA that works as a framework agreement to embrace various project contracts to be determined dynamically?
 
Back
Top Bottom