Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

zakumi,
Mkuu uchumi ni somo langu na naweza kabisa kutoka nje ya somo na kuelezea hali halisi.. Kuficha mali inaweza kabisa kupandisha bei na kuzua inflation ktk nchi hata kama uzalishaji na supply ni sawa na demand. Ulanguzi unaweza kuathiri principal zote za uchumi na kile wewe unachotumia ni uchumi kulingana na kitabu wakati mimi nakupa upana wa matukio ya hali halisi iliyotokea...
Then again nitakuuliza kitu kingine pamoja na kwamba hujajibu la kwanza. Iweje serikali iweke vita ya Uhujumu Uchumi ikiwa hakuna magendo isipokuwa ni uhaba wa uzalishaji!.. I mean Nyerere na kina Sokoine walikuwa na ujinga gani ku target wafanya biashara na viongozi wanaohujumu uchumi wakati wakijua uwezo wa viwanda vyenyewe ku supply kulingana na demand ni mdogo..Mhujumu huyo ni nani na wapi anaingia kiuchumi?
 
zakumi,
Mkuu bado nitakataa hoja yako kwa sababu nimefanya biashara hiyo... Tanzania tulikuwa tukisafirisha mazao zambia kwa kificho sana na haikuruhusiwa hata kidogo. Tulikuwa na njia za maporini pale Tunduma wakija mabebaji kuchukua mali usiku wa manane. Wenye mali walipita border kama kawaida huku mali imeshapakiwa ktk mabus tayari kwenda Lusaka..
Mimi hapa nimewahi kupeleka Zambia hiriki toka Tukuyu ambako ndio tulikokuwa tukizifuata kwa wakulima. Kwa mara ya kwanza nimekula Ugali na Maparachich ktk kusaka hirikii..
Hata siku moja hatukuwa na shida ya hiriki lakini ilikuwa hairuhusiwi kusafirisha unless una kibali ambacho process yake tu unaweza kukata tamaa..
Pia Ujamaa ulitulemaza tukashindwa kuelewa biashara kwa mapana ya soko na na bei kupanda. Price control ilikuwa moja ya sababu kubwa sana ya walanguzi kutafuta soko nje. haiwezekani wala haiwezi kuingia akilini unaposema vitu hivi kuuzwa nje wakati kuna uhaba na soko lipo Tanzania. Kama kulikuwa na Uhaba inawezekana vipi tukasafirisha mali ambayo kwa uhaba wake ingekuwa na soko nchini?..Umejaribu kufikiria hilo. Then itakuwaje tuseme viwanda vilishindwa kuzalisha ikiwa tuliweza kupata mali za kusafirisha nje!
Yaani mtu asafirishe mazao yake kwenda Zambia wakati kuna soko (uhaba) nchini!..haiwezekani isipokuwa kwa sababu nje ya somo hilo na nimesema kwamba price control nchini na bei kubwa zilizotolewa nje ziliwafanya walanguzi kutojali mahitaji ya ndani..
Na nashndwa kuelewa mnaposema uhaba hapa nchini kamam kweli ilikuwa vile kwa nini mlipeleka mahindi Zambia msirudi na mchele ama ngano badala yake ilikuwa nguo na sabuni za kuogea..!

Mkandara:

Sasa naelewa matatizo yako yapo wapi. Kumbuka kabla kitu hakijamfikia mlaji. Ni lazima kizalishwe na lazima vilevile kisambazwe.

Hivyo basi uzalishaji unaweza kuwa mzuri lakini kama usambazaji ni mbovu, bado uhaba wa bidhaa utatokea.

Na vilevile uzalishaji ukiwa mbaya na usambazaji kuwa mzuri, bado uhaba wa bidhaa utatokea.

Walaji wa kitanzania walikuwa wanaangalia vitu vilivyopo madukani na sio nani kazalisha au nani kasambaza.

Unachoeleza wewe ni uzalishaji wa bidhaa. Lakini usambazaji ulikuwa complicated. Na mifano yako ya jinsi ya walanguzi mlivyo haribu nchi ulisahau kitu kimoja. Walanguzi walikuwa flexible ku-operate. Mlanguzi anaweza kukodi gari kwenda kuchukua matairi Arusha. Lakini RTC ilikuwa haifanyi kazi kwa namna hiyo. Matairi, dagaa, mchele kusafirishwa pamoja na bado dreva atataka kuchelewa kufika kituoni.

Mkandara nimebeba mabox kwenye distribution centers, bidhaa zilizouzwa wakati wa Xmass zilikuwa kwenye maghala toka September na labda waChina walitengeneza vitu hivyo January 2008 (Supply Chain).
 
Zakumi,
kwa kuongezea tu hapa leo mafuta ktk gas pump zote mjini inasemekana yamekwisha. Lakinikuna uvumi mkubwa kwamba mafuta hayakwisha isipokuwa wafanyabiashara ambao walinunua mafuta hayo ghali mwanzo wa week wameyaficha wakisubiri bei kupanda baada kesho. wanacheza patapotea ama kamali ya kibashara na demand ya mafuta ipo palepale.. Huku Ulaya unaweza kabisa kuona foleni ya magari kununua mafuta kwa sababu tu bei yake ni nafuu kuliko gas station nyingine lakini haina maana supply ya kutosha haipo. Kuna factors nyingi sana zinazoweza kuleta picha tofauti na jinsi vitabu vinavyo tafsiri supply na demand. Hujuma za uchumi ni crime na siku zote crime ni nje ya taratibu na principal za uchumi, ndio maana zinapigwa vita.
 
Zakumi,
kwa kuongezea tu hapa leo mafuta ktk gas pump zote mjini inasemekana yamekwisha. Lakinikuna uvumi mkubwa kwamba mafuta hayakwisha isipokuwa wafanyabiashara ambao walinunua mafuta hayo ghali mwanzo wa week wameyaficha wakisubiri bei kupanda baada kesho. wanacheza patapotea ama kamali ya kibashara na demand ya mafuta ipo palepale.. Huku Ulaya unaweza kabisa kuona foleni ya magari kununua mafuta kwa sababu tu bei yake ni nafuu kuliko gas station nyingine lakini haina maana supply ya kutosha haipo. Kuna factorsa nyingi sana zinazoweza kuleta picha tofauti na jinsi vitabu vinavyotafsiri supply na demand. Hujuma za uchumi ni crime na siku zote crime ni nje ya taratibu na principal za uchumi, ndio maana zinapigwa vita.

Mkandara:

Sasa naelewa matatizo yako yapo wapi. Kumbuka kabla kitu hakijamfikia mlaji. Ni lazima kizalishwe na lazima vilevile kisambazwe.

Hivyo basi uzalishaji unaweza kuwa mzuri lakini kama usambazaji ni mbovu, bado uhaba wa bidhaa utatokea.

Na vilevile uzalishaji ukiwa mbaya na usambazaji kuwa mzuri, bado uhaba wa bidhaa utatokea.

Walaji wa kitanzania walikuwa wanaangalia vitu vilivyopo madukani na sio nani kazalisha au nani kasambaza.

Unachoeleza wewe ni uzalishaji wa bidhaa. Lakini usambazaji ulikuwa complicated. Na mifano yako ya jinsi ya walanguzi mlivyo haribu nchi ulisahau kitu kimoja. Walanguzi walikuwa flexible ku-operate. Mlanguzi anaweza kukodi gari kwenda kuchukua matairi Arusha. Lakini RTC ilikuwa haifanyi kazi kwa namna hiyo. Matairi, dagaa, mchele kusafirishwa pamoja na bado dreva atataka kuchelewa kufika kituoni.

Mkandara nimebeba mabox kwenye distribution centers, bidhaa zilizouzwa wakati wa Xmass zilikuwa kwenye maghala toka September na labda waChina walitengeneza vitu hivyo January 2008 (Supply Chain).
 
zakumi,
Mkuu wangu wee unachukulia makosa ya kiuandishi kujenga hoja babuuu!. Tumezungumzia RTC hivi kweli hawa walikuwa wazalishaji mkuu wangu!. Sigara zilizokuwa zikisafirishwa Uganda unafikiria zilikuwa ktk swala la kusambazwa au hujuma! walioneemeka na Ulanguzi walikuwa viongozi wa mashirika ya Umma na sio viwandani hivyo sioni point ya kusingizia viwanda. waliohujumu uchumi ni ktk usambazaji na nilichokataa kwa Jokakuu ni kusema viwanda vilikuwa havina uwezo wa kuzalisha.
Na iweje kati ya hoja zenu ilikuwa viwanda vilishindwa kuzalisha kisha nikijibu mnabadilisha kuwa usambazaji!.. Kote huko nime cover isipokuwa nyie ndio hamtaki kukubali.
 
zakumi,
Mkuu uchumi ni somo langu na naweza kabisa kutoka nje ya somo na kuelezea hali halisi.. Kuficha mali inaweza kabisa kupandisha bei na kuzua inflation ktk nchi hata kama uzalishaji na supply ni sawa na demand. Ulanguzi unaweza kuathiri principal zote za uchumi na kile wewe unachotumia ni uchumi kulingana na kitabu wakati mimi nakupa upana wa matukio ya hali halisi iliyotokea...
Then again nitakuuliza kitu kingine pamoja na kwamba hujajibu la kwanza. Iweje serikali iweke vita ya Uhujumu Uchumi ikiwa hakuna magendo isipokuwa ni uhaba wa uzalishaji!.. I mean Nyerere na kina Sokoine walikuwa na ujinga gani ku target wafanya biashara na viongozi wanaohujumu uchumi wakati wakijua uwezo wa viwanda vyenyewe ku supply kulingana na demand ni mdogo..Mhujumu huyo ni nani na wapi anaingia kiuchumi?

Katika zoezi hili Nyerere na Sokoine walitumia vichwa vya panzi tu. Mwanasiasa anaweza kutaka kuwa na moral obligations ambazo haziwezi kufikiwa na jamii.

Masuala ya vita dhidi ya wahujumu uchumi ni sawa na prohibiton of alcohol in USA 1920-33. Kulikuwa hakuna sababu zozote za kiuchumi bali Moral Obligations.
 
Zakumi,
Kwa hiyo unachojaribu kusema hapa ni kitu gani!.. maanake unakubali kulikuwepo na uhaba wa vitu kutokana na sababu ambazo wewe mwenyewe unazijua.. Ni sababu zipi hutaki kusema. Nimesema vizuri sana kwamba uwezo wa viwanda kuzalisha ulikuwepo isipokuwa Uhaba wa mali nchini ulikuwa wa kujitakia... Ulanguzi wa mali zetu kupelekwa nchi za nje jirani ndio sababu moja kubwa sana. TRC na vyombo vyote vya usambazaji walikuwa wakiuza mali hizo kwa walanguzi wakikatiwa chao..price control ndani na Ujamaa vilichangia sana kuzidisha tamaa ya pato kubwa nje.
Bila shaka mali haiwezi kufika madukani ikiwa sehemu kubwa imepelekwa nje na nimesema wazi stock nzima hawa jamaa waliuza pengine asilimia 20 na iliyobakia wanaipitisha mlango wa nyuma kwenda nje.
Mdipo serikali ikaanza vita ya wahujumu Uchumi lakini kwa bahati mbaya Nyerere hakuweza kuimaliza kutokana na sababu nje ya wahujumu wenyewe. Ujamaa kama mfumo wa siasa ulikuwa unakufa, sisi wenyewe baada ya Ujamaa kufa tulishindwa kuziba pengo la Uhujumu uchumi ambalo Nyerere aliendelea kusisitiza tuzibe ufa kabla hatujajenga nyumba. Badala yake hao viongozi wa mashirika ndio wamepewa Uwaziri na Azimio la Zanzibar limewapa nguvu zaidi ya kuendeleza yale waliyoyaanza toka wakati wa mwalimu. sasa hivi tunajenga nyumba mkuu fedha zinnzoibiwa nchini ni mara mbili ya bajeti ya serikali kwa mwaka na kuna matajiri wa cash Tanzania kuliko nchi zilizoendelea...
na bado wananchi wake wanazidi kukataa kuona kwamba nchi imepelekwa kubaya!.. dhumuni la Rev. Kishoka ni kutafuta dawa ya maafa haya na kama tutayafumbia macho basi hata nyumba yenyewe itatushinda kujenga..

Nadhani nimefahamika zaidi na nakutakieni sikukuu njema!
 
zakumi,
Mkuu wangu wee unachukulia makosa ya kiuandishi kujenga hoja babuuu!. Tumezungumzia RTC hivi kweli hawa walikuwa wazalishaji mkuu wangu!. Sigara zilizokuwa zikisafirishwa Uganda unafikiria zilikuwa ktk swala la kusambazwa au hujuma! walioneemeka na Ulanguzi walikuwa viongozi wa mashirika ya Umma na sio viwandani hivyo sioni point ya kusingizia viwanda. waliohujumu uchumi ni ktk usambazaji na nilichokataa kwa Jokakuu ni kusema viwanda vilikuwa havina uwezo wa kuzalisha.
Na iweje kati ya hoja zenu ilikuwa viwanda vilishindwa kuzalisha kisha nikijibu mnabadilisha kuwa usambazaji!.. Kote huko nime cover isipokuwa nyie ndio hamtaki kukubali.

Point ninayokupa mimi ni kuwa mlanguzi alikuwa efficient kusambaza vitu kuliko mashirika ya umma. Hivyo unapotoa mfano wako wa kutafuta Hiriki na kula ugali wa maparachichi, kumbuka shirika la kiserikani haliwezi kufanya hivyo.

Kumbuka vilevile hivyo viwanda vilikuwa vinategemea mashirika ya usafirisha kama vile TRC, Moretco, n.k. Kama mashirika haya yalishindwa kupeleka vitu kwa mlaji on time ni ukweli kuwa yalishindwa kupeleka malighafi viwandani. Hivyo kucheleshwa kwa malighafi kulisababisha uzalishaji kupungua pia.

Chukua mfano wa kiwanda cha bia. Uzalishaji ulitegemea kurudi kwa chupa za bia pia.

Suala la kuwa uzalishaji ulikuwa mdogo bado lipo palepale.
 
Zakumi,
Duh mkuu wangu niseme lugha gani Kiingereza!..
Mimi kama mlanguzi sikuweza kusambaza mali kama inavyotakiwa kisheria. Hizo hiriki badala ya kuzipeleka ktk maduka yetu nimeziuza Zambia ambako kunalipa mara tatu ya bei ya Tanzania kisha niliweza kurudi na mali ambayo ingeweza kuuzika kirahisi Tanzania kwa faida mara mbili hata kama ilikuwa ya anasa.. Hivyo niliweza kuua ndege pande mbili zote kwa manuifaa yangu binafsi.. hapa mimi sikuwa mfanya biashara mlanguzi halali isipokuwa mhujumu wa uchumi wa nchi kwani hiriki ambayo ilitakiwa sana nchini ilikosekana madukani kwa sababu Mkandara kaipeleka Zambia. hapa utanipa sifa gani ya usambazaji!
 
Unaona sasa. Sio walanguzi wote walitoa vitu nje ya nchi. Wengi walinunua vitu Tanzania na kuviuza Tanzania.

Tatizo lako ume-tune ubongo wako kuwa uhujumu uchumi ulikuwa ni wa kutoa bidhaa nje ya nchi tu.

Mfano wako nimeutoa kuonyesha flexibility ya mtu binafsi anavyoweza kuwa mvumilivu hili kusambaza bidhaa kwa kutumia mbinu ambazo serikali haiwezi. Na mambo yote uliofanya yalikuwa perfect legal ni experimentation za viongozi wetu zilizofanya kuwa biashara ni dhambi.

Na kukujibu posti yako kuhusu sababu za upungufu wa vitu na ulanguzi. Demand ilikuwa kubwa kuliko supply. Kwa sababu za kiuzalishaji au kiusambazaji, bidhaa zilikuwa hazimfikii mlaji (period).

Hayo mambo ya kusema kuwa viwanda vyetu vilikuwa vinazalisha bidhaa bora zinazotakiwa nje do not make sense to me. Kama ni kweli basi kiuchumi ingetokea expansion ya viwanda hivyo.

Kwa sababu expansion haikutokea, phenomena yako inaweza kuwa sawa na hile ya prohibition of Alcohol iliyokea Marekani. Watu walikwenda Cuba au Canada kufuata Alcohol.
 
Zakumi,
Mkuu tunazungumzia vita ya Uhujumu Uchumi na sio walanguzi.. Na mlanguzi ambaye aliuza vitu ndani ya nchi hakuweza kuhujumu uchumi kulingana na hoja iliyotangulia, wala hakuwa target ya serikali kulingana na vita ile isipokuwa wale walioficha mali na kuzua uhaba wa mali.. sasa mimi nimekwenda one step further kuelezea kwa nini mali zetu zilifichwa na nini sababu ya uhaba wa mali nchini.

Labda mada hii umeichukulia katikati na swala kubwa kwako limekuwa walanguzi.. nadhani ni mimi niliyesema kuhusiana na walanguzi na nimewataja kwa nafasi yao kama middlemen na walihusika vipi ktk hujuma za Uchumi wetu, sikuwa na maana ya kuzungumzia Ulanguzi kwa ujumla wake.
Na kukujibu posti yako kuhusu sababu za upungufu wa vitu na ulanguzi. Demand ilikuwa kubwa kuliko supply. Kwa sababu za kiuzalishaji au kiusambazaji, bidhaa zilikuwa hazimfikii mlaji (period).
Sasa wapi mimi nimeelezea tofauti na hoja hiyo..Nilichoandika mimi sio tu principal ya demand na supply isipokuwa factors ambazo zinaweza kuathiri demand na supply..maadam inategemea tu the point of intersection between demand na supply..
Je, unafahamu kwamba price control inapokuwa chini ya market equilibrium, demand ya kitu hicho kupanda kuliko suppply na kuzua shortage..Je, unakubali kwamba meaning it's not necessary kulaumu viwanda kama Jokakuu alivyozungumza kuwa uzalishaji ndio ulisababisha supply kuto tosheleza.
 
Zakumi,
Mkuu tunazungumzia vita ya Uhujumu Uchumi na sio walanguzi.. Na mlanguzi ambaye aliuza vitu ndani ya nchi hakuweza kuhujumu uchumi kulingana na hoja iliyotangulia, wala hakuwa target ya serikali kulingana na vita ile isipokuwa wale walioficha mali na kuzua uhaba wa mali.. sasa mimi nimekwenda one step further kuelezea kwa nini mali zetu zilifichwa na nini sababu ya uhaba wa mali nchini.

Labda mada hii umeichukulia katikati na swala kubwa kwako limekuwa walanguzi.. nadhani ni mimi niliyesema kuhusiana na walanguzi na nimewataja kwa nafasi yao kama middlemen na walihusika vipi ktk hujuma za Uchumi wetu, sikuwa na maana ya kuzungumzia Ulanguzi kwa ujumla wake.

Sasa wapi mimi nimeelezea tofauti na hoja hiyo..Nilichoandika mimi sio tu principal ya demand na supply isipokuwa factors ambazo zinaweza kuathiri demand na supply..maadam inategemea tu the point of intersection between demand na supply..
Je, unafahamu kwamba price control inapokuwa chini ya market equilibrium, demand ya kitu hicho kupanda kuliko suppply na kuzua shortage..Je, unakubali kwamba meaning it's not necessary kulaumu viwanda kama Jokakuu alivyozungumza kuwa uzalishaji ndio ulisababisha supply kuto tosheleza.

Mkandara, Umenena hapo.

Suala la msingi tuangalie dhumuni la sheria hiyo lilikuwa ni nini? Mimi nahisi tunahitaji sheria karli kama watu wanahujumu uchumi wa nchi lazima wafagiliwe na fagio la chuma. tunaongela suala kama la EPA lile ni kuhujumu uchumi kwa sababu lingeweza au liliweza kusababisha artificial inflation na kudumaza uchumi. Mimi nafikiri tunahitaji kuifufua hiyo sheria kwa sababu sasa hivi mashtaka yaliyo chini ya hiyo sheria lazima yabalikiwe na DPP ndo yaende Mahakamani. Sheria inatakiwa iendane na jamii iliyopo. Hiyo sheria inatakiwa ibadilike. Tena nahisi kama ingweza kuboreshwa ifanane fanane na Patriotic Act ya U.S. itasaidia kuwabana wabaka uchumi wa taifa.

Hakuna sheria kali ndo maana hata PM anapata kigugumizi cha namna gani ya kukabiliana na makundi kama ya EPA.

Tuna aja ya kuwa na chombo huru na makini cha kushughulikia masuala ya jinai. Kuna sophiscated crimes ambayo ni aibu kuunda tume ili kukabiliana nayo. Kama tutakuwa na chombo kama hicho hapa Tanzania, Itasaidia kupambana na wahalifu especially white collar crimes. Au watanzania tumeridhika kuwa na vitume kila ikitokea issue kama ya EPA?

Naomba kuwakilisha.
 
Mkandara et al

Mimi wakati huo nilikuwa mwanafunzi; ila nina mawili matatu ambayo yananichanganya kwenye "miaka" ambayo vipindi hivi muhimu katika historia nchi yetu ilipitia. Baada ya kusoma hoja zetu, naona wote mpo sahihi ila mnapishana sehemu ndogo ya miaka.

Mkandara unasema bidhaa zilikuwepo Tanzania ila walanguzi walivificha ili wazipeleke Kenya na kwingineko, kitu ambacho kilipelekea Demand kuwa kubwa kuliko Supply: Hapa nakubaliana wewe 100%, nina wanafamilia waliokuwa kama wewe. Wa kwanza ni Mjomba wangu ambaye alikamatwa na lori limejaa makatoni ya Konyagi akiwa anavusha mpakani kuingiza Kenya kupitia Rombo; aliwekwa Rumande miaka 7 na hata alipotoka akili haikuwa sawa sawa. Wa pili ni Baba Mdogo aliyekamatwa na shehena ya Mabati mapya nyumbani kwake; kwa lengo la kuyauza kwa magendo Tanzania. Aliponea chupu chupu kwa kukimbilia Kenya alikojificha kwa miaka 4 (na huko ndiko alikojifunzia kiingereza..!!).

Kwa mifani hiyo ambayo ni "facts" nakubaliana na Mkandara kuwa Tanzania ilikuwa inazalisha bidhaa zilizokuwa na soko zuri Kenya.

JoKaKuu, Kichuguu et al wanasema viwanda vyetu vilikuwa havizalishi bidhaa za kutosha. Na hivyo kulikuwa demand kubwa ya bidhaa muhimu. Hili naamini lilitokea, lakini katika kipindi cha mbele zaidi miaka ya mwishoni mwa 80, mwanzoni mwa 90. Sababu hasa ni kuwa nina wanafamilia wengine huko Arusha waliokuwa wanaaingiza vitu kuoka Kenya hasa Bia kwa wingi kwa sababu Tanzania bia zilikuwa zimeadimika. Katika kumbukumbu zangu pia nakumbuka kutumwa Bia bar na mzee wangu lakini kwa sababu kulikuwa na uhaba wa bia wenye bar walikuwa wanaringa kuuza mpaka ununue na nyama ya mbuzi.!!

Je, sio sahihi kwamba nyie wakuu mnapisha kwenye miaka na sio matukio?
 
Shadow,
Mkuu shukran sana kwani umenipa somo zuri sana ulipotaja Patriotic Act. Hawa wenzetu wanakwenda na wakati na kama navyosisitiza siku zote kwamba ni muhimu kutambua uliposimama yaani Watu na Mazingira ni muhimu sana ktk utunzi wa kitu chochote ikiwa ni pamoja na sheria...Kila hatua ya maendeleo inahitaji kutazama vitu hivyo laa sivyo tutakuwa tunajikanyaga tu kila siku.
Kwa umaskini wetu sisi waafrika ni sawa na mafisi wenye njaa. sasa kama utawafuga fisi karibu na machinjioni inabidi uweke sheria ama vikwazo ambavyo unafahamu watu(fisi) hawa hawawezi kuvizia mifugo yako ktk mazingira yale (machinjioni). Na hata kama ukisema wale watu sio mafisi ila ni mbwa tu, basi malezi ya kuwapa nyama mbichi ya mifugio yako kila siku inaweza kuwafanya wakaanza kula hata mifugo yako pindi ukichelewa tu kuwalisha.
Tanzania leo hii tunapata matatizo yote haya sio kwa sababu ya demand and supply bali imekuwa ni mila na desturi ya Mdanganyika kutafuta utajiri kiujanja ujanja. Umaskini fedheha jamani!
Ukitazama mafisadi wote hawa ni matajiri wa kutupa, hao viongozi wetu wanapewa mishahara kuliko hata viongozi wa nchi za Ulaya lakini bado kila siku wanatafuta mbinu za kutuibia zaidi nje ya mishahara na marupurupu wanayopewa..
Ni lazima fagio la chuma lirudishwe!. Ni lazima Azimio la Zanzibar life haraka sana, laa sivyo hakuna kinachoendelea Tanzania. Tusidanganywe na siasa wala vyeti vikubwa ukutani kutuambia uchumi unatakiwa kuendeshwa hivi ama vile..
Binafsi nampongeza Kikwete kwa hatua zote alizokwisha chukua hadi sasa hivi na muhimu zaidi kauli yake aliposema viongozi wote wanaotaka kufanya biashara inabidi waachie madaraka... kauli hiyo naomba iwe ktk Kanuni na maadili ya viongozi Kitaifa.
 
Zakumi,
Mkuu tunazungumzia vita ya Uhujumu Uchumi na sio walanguzi.. Na mlanguzi ambaye aliuza vitu ndani ya nchi hakuweza kuhujumu uchumi kulingana na hoja iliyotangulia, wala hakuwa target ya serikali kulingana na vita ile isipokuwa wale walioficha mali na kuzua uhaba wa mali.. sasa mimi nimekwenda one step further kuelezea kwa nini mali zetu zilifichwa na nini sababu ya uhaba wa mali nchini.

Labda mada hii umeichukulia katikati na swala kubwa kwako limekuwa walanguzi.. nadhani ni mimi niliyesema kuhusiana na walanguzi na nimewataja kwa nafasi yao kama middlemen na walihusika vipi ktk hujuma za Uchumi wetu, sikuwa na maana ya kuzungumzia Ulanguzi kwa ujumla wake.

Sasa wapi mimi nimeelezea tofauti na hoja hiyo..Nilichoandika mimi sio tu principal ya demand na supply isipokuwa factors ambazo zinaweza kuathiri demand na supply..maadam inategemea tu the point of intersection between demand na supply..
Je, unafahamu kwamba price control inapokuwa chini ya market equilibrium, demand ya kitu hicho kupanda kuliko suppply na kuzua shortage..Je, unakubali kwamba meaning it's not necessary kulaumu viwanda kama Jokakuu alivyozungumza kuwa uzalishaji ndio ulisababisha supply kuto tosheleza.

Mkandara:

Nakubaliana na wewe kuw price control inapokuwa chini ya market equilibrium demand inapanda.

Lakini ni lazima ukubali kuwa viwanda vya Tanzania pamoja na kuzalisha bidhaa zilizokuwa na market nje bado uzalishaji wa viwanda hivyo ulikuwa ni wa kiwango cha chini kukidhi mahitaji ya ndani pekee yake. Hapa nazungumzia volume ya vitu vilivyozalishwa na sio quality ya vitu hivyo.

Mtu anaposema Watu walikuwa wanachukua Konyagi na kupeleka Kenya; haina maana kuwa Konyagi zile zingebakia Tanzania zingeweza kutosheleza soko la ndani.

Unachukua instances ya vitu vichache vya Tanzania vilivyouzwa nje na ku-justify points zako.

Lakini unashindwa kuelezea kwani chumvi na vibiriti vilikosekana madukani.
 
yebo yebo,
Umesema kweli kabisa muda wanaozungumzia kina Jokakuu sio wakati wa vita ya Uhujumu Uchumi..

Zakumi,
Duh mzee umesharudi mara!..
Haya tuendelee... maadam umekubali kwamba price inaweza ku affect demand na supply..Kitu kingine niongezee Je, kuficha mali kunaweza kupandisha demand na kuonyesha shortage ya supply?..
Ikiwa utakubali hili basi ni vigumu kusema viwanda vilikuwa havizalishi vya kutosha ikiwa mali imefichwa ili kutafuta soko nje lenye kulipa mara mbili ama tatu zaidi ya T shilingi.
Mkuu nitarudia tena kwamba ikiwa wakulima 100 wa Tanzania watahitaji majembe 100 na yakatengenezwa majembe 100 kwa wakati yanapohitajika huwezi kusema kiwanda kimeshindwa kutengeneza majembe 100 kwa sababu tu majembe hayo hayakumfikia mkulima. Kuna sababu nyingi sana na ktk mada hii mimi nimezungumzia sababu ya majembe hayo kupelekwa Kenya kuwa ndio sababu ya upungufu wa majembe kwa wakulima 100...

Kama unakumbuka scandal ya Idd Simba, yeye alitaka ku floor market na sukari ili bei ishuke kwani kungekuwa na surplus lakini wahindi (wale wale) aliwaamini kama mawakala wa sukari waliichukua na kuificha.. Sukari ikiwa taabu kupatikana pamoja na kwamba Idd Simba alipeleka supply kuzidi demand. matokeo yake Idd Simba ndiye akaonekana mbaya na kiongozi asiyefaa kwa sababu tu macho yetu yalitazama demand na supply. Kama vitu havimfikii mwananchi lazima shina la supply lilikuwa na matatizo.. Sio kweli mkuu wangu ni muhimu sana tutazame kwa undani..
Kisha unapozungumzia Chunvi na Vibiriti uliambiwa uhujumu uchumi wali target vyombo ama watu wanaofanya viwanda vishendwe kuzalisha vitu hivyo!.. Mkuu kuna vitu viwili hapa. Kuna vitu vilivyokuwa adimu kutokana na production hivi havikuwa sababu ya vita ya uhujumu Uchumi isipokuwa ni vile ambavyo vilichukuliwa nje kimagendo hivyo kuongeza shida nchini..
 
Mkandara et al

Mimi wakati huo nilikuwa mwanafunzi; ila nina mawili matatu ambayo yananichanganya kwenye "miaka" ambayo vipindi hivi muhimu katika historia nchi yetu ilipitia. Baada ya kusoma hoja zetu, naona wote mpo sahihi ila mnapishana sehemu ndogo ya miaka.

Mkandara unasema bidhaa zilikuwepo Tanzania ila walanguzi walivificha ili wazipeleke Kenya na kwingineko, kitu ambacho kilipelekea Demand kuwa kubwa kuliko Supply: Hapa nakubaliana wewe 100%, nina wanafamilia waliokuwa kama wewe. Wa kwanza ni Mjomba wangu ambaye alikamatwa na lori limejaa makatoni ya Konyagi akiwa anavusha mpakani kuingiza Kenya kupitia Rombo; aliwekwa Rumande miaka 7 na hata alipotoka akili haikuwa sawa sawa. Wa pili ni Baba Mdogo aliyekamatwa na shehena ya Mabati mapya nyumbani kwake; kwa lengo la kuyauza kwa magendo Tanzania. Aliponea chupu chupu kwa kukimbilia Kenya alikojificha kwa miaka 4 (na huko ndiko alikojifunzia kiingereza..!!).

Kwa mifani hiyo ambayo ni "facts" nakubaliana na Mkandara kuwa Tanzania ilikuwa inazalisha bidhaa zilizokuwa na soko zuri Kenya.

JoKaKuu, Kichuguu et al wanasema viwanda vyetu vilikuwa havizalishi bidhaa za kutosha. Na hivyo kulikuwa demand kubwa ya bidhaa muhimu. Hili naamini lilitokea, lakini katika kipindi cha mbele zaidi miaka ya mwishoni mwa 80, mwanzoni mwa 90. Sababu hasa ni kuwa nina wanafamilia wengine huko Arusha waliokuwa wanaaingiza vitu kuoka Kenya hasa Bia kwa wingi kwa sababu Tanzania bia zilikuwa zimeadimika. Katika kumbukumbu zangu pia nakumbuka kutumwa Bia bar na mzee wangu lakini kwa sababu kulikuwa na uhaba wa bia wenye bar walikuwa wanaringa kuuza mpaka ununue na nyama ya mbuzi.!!

Je, sio sahihi kwamba nyie wakuu mnapisha kwenye miaka na sio matukio?

Yebo Yebo:

Umeeleza phenomena mbili ambazo zote zilitokea katika kipindi kimoja. Na phenomena hizi zilikuwa zote zinasababishwa na uhaba wa vitu Tanzania na sio kitu kingine.

Na kuna kitu hapa ambacho Mkandara anakisahau kabisa. Kitu hiki kinaitwa Exchange Mechanism ambayo inaweza kutokea bila kuwepo kwa muundo rasmi wa kifedha.

Ukitaka kuingiza bidhaa Tanzania kutoka nchi jirani ni lazima uwe na pesa za nchi hizo.

Na njia moja ya kupata rate nzuri ni kuchukua bidhaa zinazotengenezwa Tanzania na ambazo unaweza kuziuza katika nchi hizo jirani.

Hivyo mtanzania aliyetaka kununua mitumba ya nguo kutoka Burundi au Rwanda alitakiwa apeleke Radio za 277 na batteries. akifika katika nchi hizo aliuza kwa faranga na baadaye kununua mitumba.

Hivyo kuna ukweli kuwa bidhaa ziliuzwa nje kutoka Tanzania. Lakini sehemu kubwa ilitumika kama Exchange Mechanism.

Hakuna data zinazoonyesha kuwa bidhaa hizo zingebaki Tanzania, basi nchi isingekuwa na uhaba wa vitu.

Anachozungumza Mkandara ni Myth na Voodoo, kwa sababu hakuna data zozote zinazonyeesha kuwa bidhaa hizo zingebaki ndani zingetosheleza mahitaji yetu.

Lakini kile anachoeleza Kichuguu kuwa aliuza ngozi Kenya na kurudi na sabuni Tanzania kinaeleza kabisa kuwa kulikuwepo na Exchange Mechanism ambayo ilifanyika bila watu kuijua.
 
yebo yebo,
Umesema kweli kabisa muda wanaozungumzia kina Jokakuu sio wakati wa vita ya Uhujumu Uchumi..

Zakumi,
Duh mzee umesharudi mara!..
Haya tuendelee... maadam umekubali kwamba price inaweza ku affect demand na supply..Kitu kingine niongezee Je, kuficha mali kunaweza kupandisha demand na kuonyesha shortage ya supply?..
Ikiwa utakubali hili basi ni vigumu kusema viwanda vilikuwa havizalishi vya kutosha ikiwa mali imefichwa ili kutafuta soko nje lenye kulipa mara mbili ama tatu zaidi ya T shilingi.
Mkuu nitarudia tena kwamba ikiwa wakulima 100 wa Tanzania watahitaji majembe 100 na yakatengenezwa majembe 100 kwa wakati yanapohitajika huwezi kusema kiwanda kimeshindwa kutengeneza majembe 100 kwa sababu tu majembe hayo hayakumfikia mkulima. Kuna sababu nyingi sana na ktk mada hii mimi nimezungumzia sababu ya majembe hayo kupelekwa Kenya kuwa ndio sababu ya upungufu wa majembe kwa wakulima 100...

Kama unakumbuka scandal ya Idd Simba, yeye alitaka ku floor market na sukari ili bei ishuke kwani kungekuwa na surplus lakini wahindi (wale wale) aliwaamini kama mawakala wa sukari waliichukua na kuificha.. Sukari ikiwa taabu kupatikana pamoja na kwamba Idd Simba alipeleka supply kuzidi demand. matokeo yake Idd Simba ndiye akaonekana mbaya na kiongozi asiyefaa kwa sababu tu macho yetu yalitazama demand na supply. Kama vitu havimfikii mwananchi lazima shina la supply lilikuwa na matatizo.. Sio kweli mkuu wangu ni muhimu sana tutazame kwa undani..
Kisha unapozungumzia Chunvi na Vibiriti uliambiwa uhujumu uchumi wali target vyombo ama watu wanaofanya viwanda vishendwe kuzalisha vitu hivyo!.. Mkuu kuna vitu viwili hapa. Kuna vitu vilivyokuwa adimu kutokana na production hivi havikuwa sababu ya vita ya uhujumu Uchumi isipokuwa ni vile ambavyo vilichukuliwa nje kimagendo hivyo kuongeza shida nchini..

Baadhi ya masuala yako hapa nimeyajibu katika posti ya YEBO YEBO. Ambayo nimeezea kitu kinachoitwa Exchange Mechanism.
 
Zakumi,
Unachozungumza ni Biashara halali mahala nchi mbili zina trade kibiashara. haikuwa hivyo mwaka 1983 wala 1984.
Pili, Mwaka 1983/84 hapakuwa na uhaba wa vitu ambavyo vilisababisha vita ya Uhjumu Uchumi. Huwezi kuanzisha vita ya Uhujumu uchumi ikiwa wewe mwenyewe huna kitu kilichoibiwa. It doen't make sense na zaidi ya hapo kuwatukana viongozi wetu kwa kutumia kitabu ni kujaribu kuondoa maana ya mjadala.
Na mwisho, kama unaelewa jikiwe cha Salamander mwaka 1983-84 aidha uliwahi kukisikia ama kuwepo basi utaelewa unazungumza na mtu gani zaidi hapo mkuu wangu tutakuwa tunapoteza wakati bila kumsaidia msomaji yoyote..
Kwa maana yako wewe unafikiria kwamba vita ya Uuhujumu uchumi ni kupoteza muda tu, na ujinga ikiwa supply haiwezi kukidhi demand, wakati huo huo unashindwa kuelewa kwamba kuna factors nyingi sana zinazoweza kusababisha uhaba wa bidhaa..equilibrium point inaweza kushift kulingana na sababu kibao wala sio moja hivyo demand na supply pekee sio solution hata kidogo.
Nimekupa hadi mfano wa mafuta hapa nilipo kwamba jana siku nzima hatukuwa na mafuta wakidai kwamba gas station zote zimekauka!..
Well sababu kubwa inaweza kuwa imetokana na kushuka kwa bei ya mafuta kiasi kwamba demand ikaongezeka kuliko supply, pia kuna possibility ya mafuta hayo kuwa yamefichwa na wenye gas station kwa sababu wameyanunua ghali na sasa bei kushuka imeondoa fungu kubwa la faidi yao hivyo wanasubiri kesho bei itakapo ongezeka..hizi zote ni sababu za Uhaba, moja halali na nyingine ni crime hivyo inawezekana itatokea crackdown kisheria.

Sasa hapa tunazungumzia swala moja la mafuta na itakuwa ujinga kama nikianza kuingiza habari ya demand na Supply inayohusu Christmas kujaribu kujibu Ukame wa mafuta haya...Swala la Christmas shopping tutalizungumzia kama sababu ya biudhaa zinazoweza kuathirika na mfumo mzima wa biashara kwa siku hiyo nje kabisa ya ukosefu wa mafuta mjini kwani hapakuwepo na discount sale hizo za asilimia 50 hadi 75..
Ukielewa hapo basi nadhani tutakuwa mstari mmoja..
 
Yebo Yebo:

Umeeleza phenomena mbili ambazo zote zilitokea katika kipindi kimoja. Na phenomena hizi zilikuwa zote zinasababishwa na uhaba wa vitu Tanzania na sio kitu kingine.

Na kuna kitu hapa ambacho Mkandara anakisahau kabisa. Kitu hiki kinaitwa Exchange Mechanism ambayo inaweza kutokea bila kuwepo kwa muundo rasmi wa kifedha.

Ukitaka kuingiza bidhaa Tanzania kutoka nchi jirani ni lazima uwe na pesa za nchi hizo.

Na njia moja ya kupata rate nzuri ni kuchukua bidhaa zinazotengenezwa Tanzania na ambazo unaweza kuziuza katika nchi hizo jirani.

Hivyo mtanzania aliyetaka kununua mitumba ya nguo kutoka Burundi au Rwanda alitakiwa apeleke Radio za 277 na batteries. akifika katika nchi hizo aliuza kwa faranga na baadaye kununua mitumba.

Hivyo kuna ukweli kuwa bidhaa ziliuzwa nje kutoka Tanzania. Lakini sehemu kubwa ilitumika kama Exchange Mechanism.

Hakuna data zinazoonyesha kuwa bidhaa hizo zingebaki Tanzania, basi nchi isingekuwa na uhaba wa vitu.

Anachozungumza Mkandara ni Myth na Voodoo, kwa sababu hakuna data zozote zinazonyeesha kuwa bidhaa hizo zingebaki ndani zingetosheleza mahitaji yetu.

Lakini kile anachoeleza Kichuguu kuwa aliuza ngozi Kenya na kurudi na sabuni Tanzania kinaeleza kabisa kuwa kulikuwepo na Exchange Mechanism ambayo ilifanyika bila watu kuijua.

Naona umeaona tuegemee kwenye facts...sasa kuna taarifa hii ambayo ilisomwa bungeni na P Marmo...pengine itasaidia.

Watu 4,000 walikamatwa uhujumu uchumi 1983

Gloria Tesha, Dodoma
Daily News; Wednesday,July 09, 2008 @20:08

Serikali imesema kampeni ya kuwanasa wahujumu uchumi ya mwaka 1983 ilikuwa ni operesheni ya serikali katika kukabiliana na wafanyabiashara za magendo nchini na watu 4,000 walikamatwa. Pia ilifanyika kukabiliana na wafanyabiashara waolikuwa wanajilimbikizia bidhaa na kusababisha upungufu mkubwa wa mahitaji muhimu hususani vyakula, dawa na vifaa vya hospitali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo alisema jana kuwa kampeni hiyo pia kuwadhibiti watu waliokuwa wakitorosha bidhaa nje ya nchi huku ndani kukiwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa hizo.

Marmo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM), aliyetaka kujua kampeni hizo zimewezesha watu wangapi kufungwa kwa kuhujumu uchumi na wangapi waliachiwa na mahakama kwa kutokuwa na kesi na kurudishiwa mali zao.

Shelukindo katika swali lake hilo la msingi alitaka kujua pia kama ufisadi uliozuka katika miaka ya 2000 hauwezi kushughulikiwa kama kampeni za mwaka 1983.
Marmo alisema zoezi la mwaka 1983 lilitekelezwa kwa amri ya utendaji na kwa uharaka ili kuwashtukia wahusika wote na wadau wao na kwamba idadi ya waliokamatwa mwaka huo ni zaidi ya watu 4,000.

"Idadi hiyo ni kwa mujibu wa Tume ya Jaji Mwita iliyotembelea mikoa yote Tanzania Bara mwaka 1990 na waliachiwa kwa maamuzi ya mahakama na kulipwa fidia serikali ilitekeleza ambapo mwishoni mwa zoezi hilo watu 148 kifuta machozi kilichofikia Sh milioni 849," alisema.

Waziri huyo alisema ulipwaji huo ulikumbwa na kasoro nyingi kutokana na uhaba wa vielelezo na kumbukumbu sahihi kutoka kwa wahusika. Akifafanua kuhusu utekelezwaji wa masuala ya ufisadi hivi sasa, Marmo alisema matukio ya kupotea fedha za serikali katika miaka ya 2000 na kuhusishwa na ufisadi yanatekelezwa tofauti na operesheni ya 1983.

Source: HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Watu 4,000 walikamatwa uhujumu uchumi 1983
 
Back
Top Bottom