JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
Kumekuwepo maswali ya watu wengi wakitaka kujua ASILI ya JINA la TANGANYIKA.
Ili kuweza kuhakikisha mjadala unakuwa endelevu na msomaji anapata majibu sahihi, tumeonelea ni vema kuweka mjadala huu kwa pamoja:
ILIANZA HIVI:
=============
Baadhi ya maoni:
Ili kuweza kuhakikisha mjadala unakuwa endelevu na msomaji anapata majibu sahihi, tumeonelea ni vema kuweka mjadala huu kwa pamoja:
ILIANZA HIVI:
Jamani nimekuwa nikijiuliza sana jina la Tanganyika lilitokeatokea vipi, kama lilitungwa ni nani aliyelitunga na maana yake ni nini. Naomba wataalamu wa historia wanijuze tafadhali.
=============
Baadhi ya maoni:
Neno Tanga ni la Kiarabu limetokana na neno Tanja na Waarabu walipofika pwani ya Afrika mashariki ijulikanayo kwa sasa kama Tanga, waliufananisha na mji uitwao Tangier (Morocco) na kwa kuwa Tanga kulikuwa na msitu unaoingilika (Nyika) na ili kutofautisha kati ya Tanja ya mjini na Tanja ya nyikani, ikaitwa Tanganyika ikimaanisha kutofautisha baina ya Tanga (mji) na kuingia (Ushenzini) Tanga-nyikani.
Huwezi kuuondoa Uarabu uliopo Afrika, hata ufanye nini, kwani Uarabu mwingi upo Afrika kuliko huko kunakojulikana kwa sasa kama Uarabuni. Huo ndio ukweli. Amini usiamini.
Bora wewe umetoa maelezo yenye mashiko!!!
Ningependa kuongezea kidogo:
Wajerumani walivyokuja waliipenda sana milima ya Usambara hususani Usambara Mashariki (Amani). Walikuta wenyeji Wasambaa, Wabondei na Wadigo maeneo yale.
Wabondei walikuwa wakiyaita maeneo ya tambarare yanayoelekea bahari ya Hindi NTANGA(au TANGA kwa kiswahili chepesi) wakimaanisha Shambani.
Hiyo ndio source ya jina Tanga. Kazi ikawa kwenye maeneo ya interior ya Tanzania. Wasambaa na Wabondei waliyaita maeneo ya mbali na kwao kwa jina la NYIKA (sawasawa na jina KYASAKA kwa kichagga). Wajerumani walivyowauliza wenyeji jina la maeneo yaliyoko mbali na kwao ukiachilia mbali eneo la pwani ya bahari ya Hindi walisema ni NYIKA. Ndipo wajerumani walipoamua kulipa koloni lao la DUTCH OSTA AFRIKA jina la TANGANYIKA meaning TANGA na NYIKA ZAKE au TANGA INCLUDING ITS INTERIOR LANDS
Katika muendelezo wangu wa kutafuta kiini cha la Matatizo yetu, leo hii najikita ktk kuelezea kuhusu Jina la Tanganyika yaani asili yake na ni nini mana yake, kwa wale ambao bado hawafahamu...
Tanganyika ni Muunganiko wa maneno mawili yaani Tanga na Nyika. Maneno haya yaliunganishwa pamoja na kuunda neno Moja Tanganyika, na hili lilifanywa na Wajerumani waliokuwa wakitawala Nchi yetu kipindi hicho!
Wajerumani walikuja na jina hilo baada ya kuanza kutawala Nchi yetu ambayo Mpaka wake kwa Upande wa Kusini ni Mto Ruvuma na Magharibi ni Ziwa kubwa lilokuja kupewa Jina la Tanganyika (na Wajerumani).
Kumbuka Wajerumani walivyofika walikaa kwanza Pwani ambapo walijenga Bandari ya Dar na pamoja na Tanga, sasa Eneo la nchi yao au yetu lilikuwa linatoka Tanga mpaka kwenye Ziwa (baadae Tangayika), na mji wa Tanga peke yake ndio uliokuwa umepimwa yaani Mipango Miji lkn kutoka Tanga mpaka kwenye Ziwa kulikuwa na Misitu mizito yaani Nyika au kwa kifupi kulikuwa hakujapimwa hivyo wakaamua kuliita lile Ziwa Tanga-nyika yaani kati ya Tanga na Nyika au misitu minene.
Baada ya Waingereza kuja walitaka kubadilisha jina la Nchi iliyokuwa inaitwa Ujerumani ya Afrika Mashariki, kulikuwa na majina manne ambayo waliyapendekeza nayo ni New Maryland, Windsorland na Victoria, lakini pia Majina ya Kilimanjaro na Tabora yalipendekezwa na mwishowe Gavana aliyekuwa anajulikana kwa jina la Alfred Milner akaamua kuchukua jina Ziwa ambalo lilibatizwa Tanganyika na Wajerumani kama jina la Nchi yao!
Nafikiri ndio moja ya sababu ya Mlm.Nyerere kulikataa jina la Tanganyika baada ya Uhuru kwani kwake yeye bado lilikuwa ni jina la Mkoloni kama vile ilivyokuwa Ghana- Gold coast, au Zimbabwe na Zambia- Rhodesia, Malawi -Nyasa land na Hata Afrika Kusini au South Africa kuna kipindi ANC walikuwa hawalitaki kwamba ni jina la Kizungu na walitaka kutumia Azania badala yake!