Fahamu Jinsi ya Kuchagua Jina la Biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,497
5,532
Kuchagua jina la biashara ni mchakato muhimu sana katika kuanzisha biashara yoyote. Jina la biashara lina uwezo wa kuwa nembo inayojulikana na kuitambulisha biashara yako kwa wateja na jamii kwa ujumla. Ni sehemu ya kwanza ambayo wateja wako wataiona na inaweza kuathiri jinsi wanavyoona biashara yako.

Katika kusaidia watu kusajili majina ya biashara nimekutana na watu ambao wanachagua majina bila kuzingatia masuala ya muhimu matokeo yake hujikuta wakitumia majina ya biashara ambayo hayabebi hisia na malengo yao ya kibiashara.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia unapotaka kuchagua jina la biashara
  1. Thamani na Malengo ya Biashara:Kabla ya kuanza kutafuta jina la biashara, ni muhimu kuelewa kwa kina thamani na malengo ya biashara yako. Thamani na malengo haya yatasaidia kuweka msingi wa jinsi unavyotaka biashara yako ionekane na ijulikane na wateja. Kwa mfano, unaweza kufikiria kama unataka kuwa biashara ya kifahari, ya bei nafuu, au yenye kutoa huduma ya kipekee.
  2. Utafiti wa Soko:Elewa soko lako na wateja wako walengwa. Tambua ni kundi gani la watu unataka kuwavutia na ni mahitaji gani ya soko unataka kujaza. Fanya utafiti wa kina kuhusu wateja wako, tabia zao, na matakwa yao ili uweze kutengeneza jina la biashara ambalo litawavutia.
  3. Ubunifu na Unyofu:Chagua jina la biashara ambalo ni rahisi kusikika, kusoma, na kukumbuka. Epuka majina marefu au magumu ambayo yanaweza kuchanganya au kuwa ngumu kwa watu kuelewa au kukumbuka. Jina la biashara linapaswa kuwa la kipekee na kuelezea kwa njia sahihi bidhaa au huduma unazotoa.
  4. Utafiti wa Kisheria:Hakikisha jina la biashara unalochagua halitumiwi na biashara nyingine na kwamba linapatikana kisheria. Fanya utafiti wa jina la biashara kwenye tovuti BRELA ama mamlaka ya usajili wa biashara katika eneo lako ili kuhakikisha kuwa jina hilo halitumiwi na biashara nyingine.
  5. Uchunguzi wa Mtandao:aSiku kila biashara huwa na mpango wa kuanzisha uwepo wa mtandaoni, hakikisha jina la biashara unalolichagua linapatikana kama kikoa cha tovuti. Kufanya hivyo mapema kunaweza kukuokoa kutokana na kuchelewa au kukosa jina la kikoa unalolitaka.Kikoa ni Domain name.
  6. Uthibitishaji:Baada ya kuchagua jina la biashara, hakikisha linalingana na kile unachotaka kuwakilisha na kwamba linatoa picha sahihi ya biashara yako. Fanya majaribio kwa watu wengine ili kupata maoni yao na kujua jinsi wanavyolielewa jina hilo.
  7. Usajili wa Jina:Hatimaye, mara tu unapokuwa umefanya uteuzi wa mwisho, lisajili jina la biashara yako ili kulinda haki zako za kibiashara. Hii inaweza kuhusisha usajili wa jina la biashara kwa mamlaka husika au kufanya mchakato wa usajili wa alama ya biashara au vyote kwa pamoja
Kwa kufuata hatua hizi, utakuwa umepata jina la biashara linalofaa na linalovutia wateja wanaostahili. Ni muhimu kuchukua muda wa kutosha na kufanya utafiti wa kina ili kuhakikisha kuwa jina la biashara linalochaguliwa linaambatana na mwelekeo na malengo ya biashara yako.

Je unahitaji kusajili Jina la Biashara,Kampuni,NGO au Taasisi yoyote?Je Ungependa kupata msaada wakufanyiwa utafiti wa JINA pamoja na Usajili?Kama Jibu ni Ndio basi wasiliana nasi kwa Email:masokotz@yahoo.com
 
Hakuna biashara inayouza kwa sababu ya jina never, tatua changamoto za watu jina ina asilimia ndogo sana kw aukuwaji wa biashara mpya
 
Jina vitu gani? Hela! Helaaaa! anza biashara! Hayo mengine mbwembwe
 
Mimi nina swali,

Nina mpango/lengo la biashara ambalo kupitia huo mpango wangu nlipata na idea ya jina la biashara ntakayoitumia.

Huo mpango wangu ni wa miaka mitatu ijayo,

Swali, Naweza kusajili jina la biashara litambulike mapema na kulilinda hilo jina ili lisije kutumiwa na mtu mwingine ?

Na je sheria inaruhusu hivyo ? Yani kusajili jina la biadhara pasipo kufanya biashara kwa muda nliotaja ?
 
Mkuu unaweza kusajili Jina.Sheria Haikukatazi kusajili JINA
 
Kama unafikiri vunja bei ndio inauza bidhaa zake unasafar ndefu zaidi yangu, mifumo ya biashara za USA unatuletea tandale never applied
Mkuu nafikiri wewe una safari ndefu bado.Kwani Tandale Sio Jina?Kama unafikiri Jina halina maana kwenye biashara Jiulize Ungewezaje kutambua kwamba kuna mambo ya USA na mambo ya Tandale.Kuwa na Jina zuri hakuna maanisha kwamba biashara itakuwa nzuri na ya kuvutia.Ila Imagine Uwe na Biashara ya Spare za Magari Halafu Uipe Jina ambalo linahusiana na Biashara ya Mama ntilie.Ina maana mteja itamchukua muda anaposikia au kuona Jina na kulinganisha a biashara husika
 
Kitu ninachopinga kwako hi hiki, jina sio big deal sana kwenye biashara zetu za nnchi maskini, fumula n ile ile tu tafuta location sahihi, kuwa na mzigo sahihi uza bei sahihi. Yan hata kama ujaweka jina wateja watakupa tuh, sasa mtu unauza nguo ambayo mtaani kwenu tuh kwa poputation na kipato n cha watu n vitu viwil tofaut unakomaa na jina ? Binafs nyie ambao hamfanyi biashara mnawapotosha sana watu wanao anza kufanya biashara
 
Actually vunja bei ni jina ndilo linabeba biashara kwasababu bila hivyo nani alivutika kwenda kwenye ile biashara kununua kwasababu gani?

Tazama walioibuka baada yake, wengine wakaita Bosi kalewa, Kama kariakoo, Bei chee, Jiokotee, etc.
 
Mkuu nafikiri wewe una safari ndefu bado.Kwani Tandale Sio Jina?Kama unafikiri Jina halina maana kwenye biashara Jiulize Ungewezaje kutambua kwamba kuna mambo ya USA na mambo ya Tandale.Kuwa na Jina zuri hakuna maanisha kwamba biashara itakuwa nzuri na ya kuvutia.Ila Imagine Uwe na Biashara ya Spare za Magari Halafu Uipe Jina ambalo linahusiana na Biashara ya Mama ntilie.Ina maana mteja itamchukua muda anaposikia au kuona Jina na kulinganisha a biashara husika
Mkuu shida ya Tanzania sasa ni kuwa na watu wajuaji hadi wanafika hatua kwa ujuaji wao wanaingilia hata taaluma za watu wengine.

Mimi kuna siku nilikuwa nabishana na mtu aliyesomea engineering ya umeme kuhusu maswala ya marketing ya vifaa vya umeme.

Yaani mimi ni mtaalamu wa masoko na ujaisiria mali na ni kitu nimesomea chuoni, yeye ananionesha kuwa yeye anajua umeme na vifaa vya umeme kunishinda, yaani kahama kwenye field ya umeme anakuja kubishana na mimi eneo la masoko na hapo tumepewa kazi ya kupanga mikakati ya kimasoko ya kuuza hizi tools za kazi kama drrills, misasa na randa za umeme, misumeno ya umeme, tool boxes, etc.

Sasa mtu anakukazia utadhani yeye anajua hicho kitu na unaona kabisa huyu anacholeta ni ujuaji hapa. Kwani ukimuacha mtu ataoe hoja yake na wewe ukajenga ya kwako bila kumshambulia na kuattack alichosema unapungukiwa nini?

Watu ni wajuaji sana mzee. Na ukitaka kutana na hizi sampuli nenda kwenye Taasisi za serikali aisee ndio utaelewa kwann kuna upumbavu mwingi.
 
Kitu ninachopinga kwako hi hiki, jina sio big deal sana kwenye biashara zetu za nnchi maskini, fumula n ile ile tu tafuta location sahihi, kuwa na mzigo sahihi uza bei sahihi. Yan hata kama ujaweka jina wateja watakupa tuh, sasa mtu unauza nguo ambayo mtaani kwenu tuh kwa poputation na kipato n cha watu n vitu viwil tofaut unakomaa na jina ? Binafs nyie ambao hamfanyi biashara mnawapotosha sana watu wanao anza kufanya biashara
Mkuu sidhani kma tunapingana,nafikiri tuseme tuna elimishana.Lazima uwe na Jina Uspokuwa nalo utapewa.Watasema Pale kwa MIRA01 anauza vitu vizuri kwa Bei nzuri n.k.Kwenye Biashara JINA ni muhimu mkuu elewa hilo Hayo mengine unayoelezea ni ya muhimu.So badala ya kusema JINA sio Muhimu,Sema Mambo mengine ya Kuzingatia ni Pamoja na..... kama hayo unayosisitiza.
 
Nyumba moja hatupaswi kugombania fito, mimi kwenye jina ni hatua ya mwisho kabisa tena huja baadaye baada ya kukamilisha hatua za kwanza , wajasiliamal wachanga nimepita maeneo mengi wamefanikiwa kuji brand lkn hawajafinikiwa kwenye sales
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom