Nini asili ya jina Tanganyika na Nani alilitunga jina hili?

Kweli kabisa, ni combination ya majina mawili ya samaki was Ziwa Tanganyika: intanga n'inyika,
You are wrong! Kwanza Wajerumani hawakuwa na shida na samaki. target yao ilikuwa malighafi yamadini, pembe za ndovu na ardhi ya kilimo. Tanga ndiko ilikokuwa ikulu yao na walifungua mashmba makubwa ya katani huko. Ikulu waiihamisha Dar baada ya kuteka kwa nguvu maili nane iliyokuwa himaya ya Sultani wa Zanzibar. Asili yakeni Tanga yaani nyika ya kuelekea Tanga, baada ikitwa Tanganyika.
 
wengi wenu mnakurupuka hapa hatubishani juu ya Tanzania na Tanganyika ila tunataka asili ya tanganyika na c Tanganyika pekee unaweza kufikiria nnchi nyingine za Africa asili ya majina yao........na huyo mpuunzi nani kamwambia wanaoitaka Tanzania ni ccm kama huna cha kukoment soma kama wezako
 
Tanganyika asili yake ni huko tanga na nyika ni vichaka vidogo vilivyo na nyasi fupi watu wa tanga baada ya kuvua Samaki wanaenda nyikani kubadilishana na mazao ya kilimo .....hata wajurumani walifika kwanza tanga ndo wakaenda nyikani inavyo semekana wale wajurumani wakwanza kufika nyikani kuwaelekeza walipo ndio asili ya Tanganyika source makumbusho Tanga
 
Asili ya jina Tanganyika limetokana na lugha ya kabila la Wabondei. Kwa Kibondei tanga maaa yake ni shamba. Siku za zamani sana kabla ya ujio wa Wajerumani, wakulima wa Kibondei walikuwa na mashamba mbali na vijiji vyao na huko kulikuwa na mapori. Wakulima hao walipokua wanakwenda shamba walikuwa wanaaga asubuhi kwa kusema, "Naita tanga" maana yake naenda shamba. Mkulima akiulizwa, "tanga kuhi?" yaani shamba ni wapi? alijibu, "Kuda kwe nyika" yaani kule porini. Wajerumani walipoanzisha mashamba makubwa ya mkonge, walichukuwa yale mashamba, "tanga" yaliyokuwa ni mapori,"nyika" Maeneo haya yakawa Tanganyika, " Mashamba ya porini au mashamba ya mbali.
 
Tanga ndiyo ilikuwa sehemu waliyoipenda sana wajerumani hivyo waliwabeba vibarua kutoka sehemu mbalimbali kuelekea tanga ule umbali wa kutoka mikoa mbalimbali kwenda tanga tena nyikani ikawa wanaita nyika za kwenda tanga au tanganyika. Kwa ufupi ni msitu wa tanga au mwitu wa tanga hilo tanganyika walilijenga wenyewe wabantu wakimaanisha msitu wa kuelekea tanga hivyo basi wajeruma walitumia hilo kama jinsi ya kuitambua

Asili au chimbuko la jina Tanga ni nini?
 
Haswaaa! tunaitaka ili nasi tuwe katika nchi ya kweli, si kama ilivyo ivi sasa ni nchi ya KUFIKIRIKA TU.
 
Hilo Ni suala gumu kwani hata Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kusema hajui jina Hilo lilitoka wapi
 
Neno Tanga ni la Kiarabu limetokana na neno Tanja na Waarabu walipofika pwani ya Afrika mashariki ijulikanayo kwa sasa kama Tanga, waliufananisha na mji uitwao Tangier (Morocco) na kwa kuwa Tanga kulikuwa na msitu unaoingilika (Nyika) na ili kutofautisha kati ya Tanja ya mjini na Tanja ya nyikani, ikaitwa Tanganyika ikimaanisha kutofautisha baina ya Tanga (mji) na kuingia (Ushenzini) Tanga-nyikani.

Huwezi kuuondoa Uarabu uliopo Afrika, hata ufanye nini, kwani Uarabu mwingi upo Afrika kuliko huko kunakojulikana kwa sasa kama Uarabuni. Huo ndio ukweli. Amini usiamini.
Hizi ni kamba tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom