Kwanini mimi si Mtanganyika bali Mtanzania

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
921
1,638
Tanganyika ilianzishwa chini ya wakoloni wa Kiingereza mnamo mwaka 1921 mara baada ya vita ya Kwanza ya dunia kuisha. Nchi hii ambayo toka ilipochukuliwa na Mjerumani mwaka 1885 iliitwa German East Africa Colony.
Hii ikimaanisha Kabla ya hapo hatukuwa na Tanganyika wala hakukuwepo nchi. Mjerumani alichofanya ni kukusanya tawala mbalimbali za kikoo na kichifu na hata makabila na kuifanya iwe nchi ambayo aliipa jina la German East Africa. Hii ilijumuisha maeneo yote ambayo leo ni nchi za Rwanda na Burundi.

Mjerumani alipopoteza makoloni yake mara tu baada ya vita ya kwanza ya dunia. Hii nchi wakati huo ikijulikana German East Africa ilikabidhiwa kwa mwingereza ili kuisaidia ipate kujiongoza na kuilinda. (Protectorate) Hapa ndipo Mwingereza akaja na majina ya kupendekeza hii nchi iitwe Tanganyika.

Hili jina lilitokea maeneo ya kusini huko nyasa, na si watu wanavyotafsiri kama ilitokea Tanga. Na maana yake ili neno kwa Nyasa au huko malawi inamaanisha asili ya mtu au itokanayo na mwanadamu. Na si Tanga kama tembea katika nyika. Hili ni jina moja tu. Ambalo asili yake ni huko Nyasa na Malawi.
Kumbuka Malawi ilikuwa koloni kongwe la mwingereza hivyo ilikuwa rahisi kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa kikanisa. Na inasemekana Padre ndiye alipendekeza jina hili la Tanganyika.

Baada ya Muungano iliitwa Tanzania. Vijana wengi wa leo na hata wanao elekea uzee wamezaliwa katika Tanzania. Sioni ubaya wa jina hili. Je ni wangapi tunaijua hiyo Tanganyika. Tunajua Tanganyika ilitokea wapi? Na kwanini iliitwa Tanganyika?

Najiona na kujisikia fahari napoitwa mtanzania kuliko hilo jina tulilopewa na wakoloni. Najua maana halisi ya Tanzania. Najua ushirikiano na umoja wa ndugu wa pande zote mbili za muungano.

Nchi kadhaa Africa zilizokuwa zimepewa majina na wageni au wakoloni zilifuta majina hayo. Mfano nchi ya Upper Volta mwaka 1984 Sankara alibadili jina na Kuiita hiyo nchi Burkinafaso.

Zaire ilibadilishwa na Rais Kabila na kuitwa DRC. Gold Coast ilibadilishwa na kuitwa Ghana. The Royal Niger Company Terretory iliitwa Nigeria. Mnakumbuka Rhodesia maeneo ya Zimbabwe ikabadilishwa pia. Na nchi nyingine nyingi tu ziliondoa majina zilizokuwa zimepewa na wakoloni.

Sasa tunapodai kuitwa watanganyika kwa hoja zipi zaidi? Ni wangapi wanauwezo kueleza jina asili la Tanganyika na si kama wanavyofikiria na kupotosha maana. Tukumbuke kabla ya ukoloni hakukuwa na nchi kulikuwa na utawala wa maeneo kutokana na kabila, machifu, na koo.

Tujivunie Utanzania, tuishi katika utanzania, tuukubali utanzania kuliko huo utanganyika hata hatuujui ulipotokea na kwanini walichagua hilo jina. Na kwanini lilitokea huko Nyasa, Malawi.

Tusijivunie jina tulilopewa na mkoloni. Mungu ibariki Tanzania. Bariki na watu wake. Amen!
 
Nitajivunia kuwa Mtanzania, siku Zanzibar itakapojitegemea yenyewe kama nchi, kwa 100%. Kinyume na hapo wacha tu niendelee kuipigania Tanganyika yangu inayonyonywa miaka nenda na kupe anayeitwa Zanzibar.
 
..lakini jina Tz asili yake ni Tgk na Znz majina ya kikoloni.

..Na wengine wanadai muungano wetu haikuwa wa hiyari wananchi tulilazimishwa na viongozi wa wakati huo.
 
Tanganyika ilianzishwa chini ya wakoloni wa Kiingereza mnamo mwaka 1921 mara baada ya vita ya Kwanza ya dunia kuisha. Nchi hii ambayo toka ilipochukuliwa na Mjerumani mwaka 1885 iliitwa German East Africa Colony.
Hii ikimaanisha Kabla ya hapo hatukuwa na Tanganyika wala hakukuwepo nchi. Mjerumani alichofanya ni kukusanya tawala mbalimbali za kikoo na kichifu na hata makabila na kuifanya iwe nchi ambayo aliipa jina la German East Africa. Hii ilijumuisha maeneo yote ambayo leo ni nchi za Rwanda na Burundi.

Mjerumani alipopoteza makoloni yake mara tu baada ya vita ya kwanza ya dunia. Hii nchi wakati huo ikijulikana German East Africa ilikabidhiwa kwa mwingereza ili kuisaidia ipate kujiongoza na kuilinda. (Protectorate) Hapa ndipo Mwingereza akaja na majina ya kupendekeza hii nchi iitwe Tanganyika.

Hili jina lilitokea maeneo ya kusini huko nyasa, na si watu wanavyotafsiri kama ilitokea Tanga. Na maana yake ili neno kwa Nyasa au huko malawi inamaanisha asili ya mtu au itokanayo na mwanadamu. Na si Tanga kama tembea katika nyika. Hili ni jina moja tu. Ambalo asili yake ni huko Nyasa na Malawi.
Kumbuka Malawi ilikuwa koloni kongwe la mwingereza hivyo ilikuwa rahisi kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa kikanisa. Na inasemekana Padre ndiye alipendekeza jina hili la Tanganyika.

Baada ya Muungano iliitwa Tanzania. Vijana wengi wa leo na hata wanao elekea uzee wamezaliwa katika Tanzania. Sioni ubaya wa jina hili. Je ni wangapi tunaijua hiyo Tanganyika. Tunajua Tanganyika ilitokea wapi? Na kwanini iliitwa Tanganyika?

Najiona na kujisikia fahari napoitwa mtanzania kuliko hilo jina tulilopewa na wakoloni. Najua maana halisi ya Tanzania. Najua ushirikiano na umoja wa ndugu wa pande zote mbili za muungano.

Nchi kadhaa Africa zilizokuwa zimepewa majina na wageni au wakoloni zilifuta majina hayo. Mfano nchi ya Upper Volta mwaka 1984 Sankara alibadili jina na Kuiita hiyo nchi Burkinafaso.

Zaire ilibadilishwa na Rais Kabila na kuitwa DRC. Gold Coast ilibadilishwa na kuitwa Ghana. The Royal Niger Company Terretory iliitwa Nigeria. Mnakumbuka Rhodesia maeneo ya Zimbabwe ikabadilishwa pia. Na nchi nyingine nyingi tu ziliondoa majina zilizokuwa zimepewa na wakoloni.

Sasa tunapodai kuitwa watanganyika kwa hoja zipi zaidi? Ni wangapi wanauwezo kueleza jina asili la Tanganyika na si kama wanavyofikiria na kupotosha maana. Tukumbuke kabla ya ukoloni hakukuwa na nchi kulikuwa na utawala wa maeneo kutokana na kabila, machifu, na koo.

Tujivunie Utanzania, tuishi katika utanzania, tuukubali utanzania kuliko huo utanganyika hata hatuujui ulipotokea na kwanini walichagua hilo jina. Na kwanini lilitokea huko Nyasa, Malawi.

Tusijivunie jina tulilopewa na mkoloni. Mungu ibariki Tanzania. Bariki na watu wake. Amen!
Tanganyika tanganyika inakuja...
 
Suala la Muungano ni pasua kichwa ktk nchi hii.
 
Ulichoandika wala hakina mantiki kwasababu kinachopigiwa kilele kimantiki sio jina kama utambulisho bali nchi kama mamlaka. Tanganyika ata kama hapo awali ingeitwa kondoo bado ilipoungana na nchi yenye mamlaka nyingine nchi zote zinatakiwa ziwepo, kwasababu muungano ni makubaliano ya pande mbili. Kilichofanyika nikuwapumbaza wazanzibar ili waone hawajamezwa lakini kimsingi wao ndio wanufaika wakubwa na kwenye hili wako smart kuliko watanganyika wanaokana nchi yao. Kwahiyo wewe ni mojawapo ya wanaoikana nchi yako.
 
Tanganyika ilianzishwa chini ya wakoloni wa Kiingereza mnamo mwaka 1921 mara baada ya vita ya Kwanza ya dunia kuisha. Nchi hii ambayo toka ilipochukuliwa na Mjerumani mwaka 1885 iliitwa German East Africa Colony.
Hii ikimaanisha Kabla ya hapo hatukuwa na Tanganyika wala hakukuwepo nchi. Mjerumani alichofanya ni kukusanya tawala mbalimbali za kikoo na kichifu na hata makabila na kuifanya iwe nchi ambayo aliipa jina la German East Africa. Hii ilijumuisha maeneo yote ambayo leo ni nchi za Rwanda na Burundi.

Mjerumani alipopoteza makoloni yake mara tu baada ya vita ya kwanza ya dunia. Hii nchi wakati huo ikijulikana German East Africa ilikabidhiwa kwa mwingereza ili kuisaidia ipate kujiongoza na kuilinda. (Protectorate) Hapa ndipo Mwingereza akaja na majina ya kupendekeza hii nchi iitwe Tanganyika.

Hili jina lilitokea maeneo ya kusini huko nyasa, na si watu wanavyotafsiri kama ilitokea Tanga. Na maana yake ili neno kwa Nyasa au huko malawi inamaanisha asili ya mtu au itokanayo na mwanadamu. Na si Tanga kama tembea katika nyika. Hili ni jina moja tu. Ambalo asili yake ni huko Nyasa na Malawi.
Kumbuka Malawi ilikuwa koloni kongwe la mwingereza hivyo ilikuwa rahisi kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa kikanisa. Na inasemekana Padre ndiye alipendekeza jina hili la Tanganyika.

Baada ya Muungano iliitwa Tanzania. Vijana wengi wa leo na hata wanao elekea uzee wamezaliwa katika Tanzania. Sioni ubaya wa jina hili. Je ni wangapi tunaijua hiyo Tanganyika. Tunajua Tanganyika ilitokea wapi? Na kwanini iliitwa Tanganyika?

Najiona na kujisikia fahari napoitwa mtanzania kuliko hilo jina tulilopewa na wakoloni. Najua maana halisi ya Tanzania. Najua ushirikiano na umoja wa ndugu wa pande zote mbili za muungano.

Nchi kadhaa Africa zilizokuwa zimepewa majina na wageni au wakoloni zilifuta majina hayo. Mfano nchi ya Upper Volta mwaka 1984 Sankara alibadili jina na Kuiita hiyo nchi Burkinafaso.

Zaire ilibadilishwa na Rais Kabila na kuitwa DRC. Gold Coast ilibadilishwa na kuitwa Ghana. The Royal Niger Company Terretory iliitwa Nigeria. Mnakumbuka Rhodesia maeneo ya Zimbabwe ikabadilishwa pia. Na nchi nyingine nyingi tu ziliondoa majina zilizokuwa zimepewa na wakoloni.

Sasa tunapodai kuitwa watanganyika kwa hoja zipi zaidi? Ni wangapi wanauwezo kueleza jina asili la Tanganyika na si kama wanavyofikiria na kupotosha maana. Tukumbuke kabla ya ukoloni hakukuwa na nchi kulikuwa na utawala wa maeneo kutokana na kabila, machifu, na koo.

Tujivunie Utanzania, tuishi katika utanzania, tuukubali utanzania kuliko huo utanganyika hata hatuujui ulipotokea na kwanini walichagua hilo jina. Na kwanini lilitokea huko Nyasa, Malawi.

Tusijivunie jina tulilopewa na mkoloni. Mungu ibariki Tanzania. Bariki na watu wake. Amen!
Mzanzibari anajivunia Utanzania au Uzanzibari?
 
Acha porojo na mauwongo yako rudi darasani
 
Kujivunia utazania na kuutweza utanganyika haina mantiki. Ni sawa na kumdharau babu yako na kujivunia babaako bila kujali huyo babaako alitokana na babu yako. Vilevile Tanganyika haijabadilisha jina na kuitwa Tanzania, Tanganyika iko hai ndani ya muungano unaoitwa Tanzania, mwisho thibitisha kwa source au logic kwamba jina Tanganyika asili yake ni Malawi.
 
Tanganyika ilianzishwa chini ya wakoloni wa Kiingereza mnamo mwaka 1921 mara baada ya vita ya Kwanza ya dunia kuisha. Nchi hii ambayo toka ilipochukuliwa na Mjerumani mwaka 1885 iliitwa German East Africa Colony.
Hii ikimaanisha Kabla ya hapo hatukuwa na Tanganyika wala hakukuwepo nchi. Mjerumani alichofanya ni kukusanya tawala mbalimbali za kikoo na kichifu na hata makabila na kuifanya iwe nchi ambayo aliipa jina la German East Africa. Hii ilijumuisha maeneo yote ambayo leo ni nchi za Rwanda na Burundi.

Mjerumani alipopoteza makoloni yake mara tu baada ya vita ya kwanza ya dunia. Hii nchi wakati huo ikijulikana German East Africa ilikabidhiwa kwa mwingereza ili kuisaidia ipate kujiongoza na kuilinda. (Protectorate) Hapa ndipo Mwingereza akaja na majina ya kupendekeza hii nchi iitwe Tanganyika.

Hili jina lilitokea maeneo ya kusini huko nyasa, na si watu wanavyotafsiri kama ilitokea Tanga. Na maana yake ili neno kwa Nyasa au huko malawi inamaanisha asili ya mtu au itokanayo na mwanadamu. Na si Tanga kama tembea katika nyika. Hili ni jina moja tu. Ambalo asili yake ni huko Nyasa na Malawi.
Kumbuka Malawi ilikuwa koloni kongwe la mwingereza hivyo ilikuwa rahisi kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa kikanisa. Na inasemekana Padre ndiye alipendekeza jina hili la Tanganyika.

Baada ya Muungano iliitwa Tanzania. Vijana wengi wa leo na hata wanao elekea uzee wamezaliwa katika Tanzania. Sioni ubaya wa jina hili. Je ni wangapi tunaijua hiyo Tanganyika. Tunajua Tanganyika ilitokea wapi? Na kwanini iliitwa Tanganyika?

Najiona na kujisikia fahari napoitwa mtanzania kuliko hilo jina tulilopewa na wakoloni. Najua maana halisi ya Tanzania. Najua ushirikiano na umoja wa ndugu wa pande zote mbili za muungano.

Nchi kadhaa Africa zilizokuwa zimepewa majina na wageni au wakoloni zilifuta majina hayo. Mfano nchi ya Upper Volta mwaka 1984 Sankara alibadili jina na Kuiita hiyo nchi Burkinafaso.

Zaire ilibadilishwa na Rais Kabila na kuitwa DRC. Gold Coast ilibadilishwa na kuitwa Ghana. The Royal Niger Company Terretory iliitwa Nigeria. Mnakumbuka Rhodesia maeneo ya Zimbabwe ikabadilishwa pia. Na nchi nyingine nyingi tu ziliondoa majina zilizokuwa zimepewa na wakoloni.

Sasa tunapodai kuitwa watanganyika kwa hoja zipi zaidi? Ni wangapi wanauwezo kueleza jina asili la Tanganyika na si kama wanavyofikiria na kupotosha maana. Tukumbuke kabla ya ukoloni hakukuwa na nchi kulikuwa na utawala wa maeneo kutokana na kabila, machifu, na koo.

Tujivunie Utanzania, tuishi katika utanzania, tuukubali utanzania kuliko huo utanganyika hata hatuujui ulipotokea na kwanini walichagua hilo jina. Na kwanini lilitokea huko Nyasa, Malawi.

Tusijivunie jina tulilopewa na mkoloni. Mungu ibariki Tanzania. Bariki na watu wake. Amen!

Wewe naye una matatizo. Kwani jina Tanzania lilipatikanaje?. JIBU kwanza.
 
Asante kwa Bandiko lenye historia na rejea Mkuu.

NAAMINI WAKUU WAMESHAELEWA KWANINI WEWE SIO MTANGANYIKA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Utanganyika wako uliporwa na wazanzibari wanaoitawala Tanganyika kwa sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom