MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,090
- 22,373
Leo nimeamua kuwapongeza CHADEMA kwa kuonyesha weledi wa kisiasa kwa kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria ya uchaguzi. Safari hii ufipa wamejitahidi tofauti na wakati mwingine.
Hata kama sikubaliani na maoni yao yote ila nakubaliana na namna walivyojitahidi kupanga hoja zao.
Nawapongeza pia kutoruhusu kila kada wa Ufipa na kupost maoni kwenye social media hali inayofanya CHADEMA ionekane kama familia ya kambale kila mwanafamilia ana ndevu.
Imezoeleka huko UFIPA kila mtu ni msemaji wa chama. Pia nakipongeza ACT kwa kuwafundisha CHADEMA siasa za kisomi. ACT wao hutoa matamko yao kisomi na sio kila mwanachama kuropoka mitandaoni.
Maoni mengi sio mabaya kwa kutolewa na chama cha siasa kinachotaka kushika dola ingawa maoni mengi ni copy & paste toka kwenye rasimu ya Warioba. Mimi nimeshangazwa sana na hoja namba 5 inayosomeka hivi:
"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".
Hii ni hoja ambayo haikutakiwa kutolewa na chama kinachojinadi kuguswa na mzigo wa kodi walio nao wananchi kugharamia uendeshaji wa serikali. Yaani kwenye hizi zama tunazotaka wabunge wapungue kutoka 393 hadi labda 100 wao CHADEMA ndo wanataka waongezeke wengine? inashangaza na kutia hasira mno.
Wabunge wa kuchaguliwa mwaka 2020 walikuwa 264 kwahiyo kwa hesabu za hovyo za Ufipa wanataka waongezeke wengine 264. Hoja yao hii ikipita tutakuwa na wabunge zaidi ya 528 kwenye bunge lijalo. INAKERA SANA kuwa na upinzani unaowaza jinsi gani waingie madarakani na kutafuna kodi za wananchi.
Ninashauri hoja za CHADEMA zisomwe kwa utulivu mkubwa kwasababu kuna hoja zina nia ovu kwa mwananchi mlipa kodi. Hoja zao zimejikita kushika dola zaidi bila kujali maumivu atakayopata mtanzania.
Pia wanaCCM na wazalendo tusichoke kukiadhibu hiki chama cha Mbowe kila fursa ya sanduku la kura inapojitokeza. Kuanzia ngazi ya kitongoji lazima tukiadhibu CHADEMA.