Nimweleze au?

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Kama mnakumbuka kuna kijana aliniomba mtoko juma lileee lililopita, nikaja hapa kuomba ushauri wa kivazi cha kutupia. Nawashukuru saaana, maana kila aloniona alinisifu kuwa nimependeza, maana hata barabarani wanaume walinivunjia shingo. Tuyaache hayo.

Wiki iliyopita nilimtembelea shoga yangu ambaye alikuwa anasoma huko mikoani, sasa akaniletea photo album yake ili niangalie picha wakati yeye anapika. Lahaula lakwata, si nikaona picha zake nyingi alizopiga na yule kijana wa mtoko, tena wakiwa katika mikao ya hasara hasara. Yaani huhitaji kuuliza kama ni mtu na mpenziwe kwani kila kitu kilikuwa kinajionyesha.Mara shoga akaja, nami kwa shauku nikamuuliza kama yule ni mpenziwe? Naye akanijibu kuwa alikuwa mpenzi wake wakati walipokuwa wakisoma wote huko kanda ya ziwa, lakini waliachana siku nyingi tangu akiwa kidato cha tatu, baada ya kumfumania na shangingi moja huko mitaani. Kwa kuwa walikuwa wamepishana vidato, yule kijana aliwahi kumaliza, na hawajaonana zaidi ya miaka mitatu sasa na wala hajui yuko wapi.

Nilijaribu kudadisi tabia zake kwa ujumla, akaniambia kwamba ni kijana mtulivu ila ana wivu sana na pia ana mkono mwepesi kupiga pale kunapotokea kutofautiana, aliendelea kusema kuwa ni mtu mwenye hasira za haraka asiye na subira, ila anajua kupenda na ni mnyenyekevu kweli. Mwenzenu limenishuka shuu, Je nimweleze kuwa huyo kijana anataka niwe na uhusiano naye au nijikaushe, na niachane na huyu kijana kimya kimya, maana hata kumkubalia sijamkubalia ila tunachat sana FB na SMS kila siku……………..
 
mhm...hapo naona itbidi kwanza uhakikishe hayo aliyoyasema shoga yako.....na kwa sababu hujatoka nae officially...wewe taratibu endelea kumdadisi na kutafuta njia za kumfanya true colours zake zijionyeshe.
 
Ndiyo mueleze! If the girl is your friend why wouldn't you?Kama watu wenyewe they dated back in highschool What's there to hide? Infact waeleze wote.!
 
Abusers huwa hawaachi rafiki! Think seriously abt that. Ongea na rafikiyo manake asipojua sasa atajua baadae. Ongea nae kwanza kama unahisi umemfananisha huyo kaka ili muongee uzuri.
 
Anajua kupenda kweli ndio maana "akalimfumania na shangingi".

Ukiingia kwenye hayo mahusiano ingia ukijua kwamba kama anayosema rafiki yako ni kweli uwezekano wa yaliyotokea kwake kukutokea wewe upo ikiwa huyo kijana hajabadilika. Kwahiyo uingie ukiwa umejiandaa na ukijua anaweza akakupiga. . . kucheat ili usije ukarudi ukilia umepigwa ama umetoka kufumania.
Ila pia kwa kumkatalia kwa vigezo hivyo tu kunaweza kukufanya upoteze mtu ambae angekua mzuri kwako kimahusiano kwasababu inawezekana rafiki yako aliongeza chumvi ili story inoge. . . inawezeka kakueleza tu kukwepa ukweli kama upo zaidi ya huu au kama ni kweli inawezekana jamaa alishabadilika..yani akili imekomaa sasa.

So spend time na mshkaji. . . onyesha nia ya kutaka kumjua kiundani zaidi na kumpa fursa ya kufunguka kwako.Pia unaweza kumwambia rafiki yako kwamba unamjua mshkaji na pia uko interested nae usikie atasemaje.Unaweza kushangaa story inabadilika ghafla.
 
ni vizuri kuwaeleza wote wawili wakajua ukweli.lkn ninashaka kidogo na huyo shoga yako anaweza akarudi kwa huyo jamaa...
 
Hapo mi naona suala ni wewe tu, Je unampenda kijana huyo?
Pia rafiki yako anahitaji kujua ukweli, unaamini watu wanabadilika tabia?
 
Abusers huwa hawaachi rafiki! Think seriously abt that. Ongea na rafikiyo manake asipojua sasa atajua baadae. Ongea nae kwanza kama unahisi umemfananisha huyo kaka ili muongee uzuri.

Lakini wala hajawahi kuonesha dalili za kuwa abuser, tena kuna wakati tuki chat, nampa majibu yenye kukera, lakini huwa haoneshi kukasirika. shoga alijaribu kunidadisi iwapo namfahamu huyo kijana nikakanusha, kwani maswali yangu yalimfanya adhani kuwa namfahamu.
 
Anajua kupenda kweli ndio maana "akalimfumania na shangingi".

Ukiingia kwenye hayo mahusiano ingia ukijua kwamba kama anayosema rafiki yako ni kweli uwezekano wa yaliyotokea kwake kukutokea wewe upo ikiwa huyo kijana hajabadilika. Kwahiyo uingie ukiwa umejiandaa na ukijua anaweza akakupiga. . . kucheat ili usije ukarudi ukilia umepigwa ama umetoka kufumania.
Ila pia kwa kumkatalia kwa vigezo hivyo tu kunaweza kukufanya upoteze mtu ambae angekua mzuri kwako kimahusiano kwasababu inawezekana rafiki yako aliongeza chumvi ili story inoge. . . inawezeka kakueleza tu kukwepa ukweli kama upo zaidi ya huu au kama ni kweli inawezekana jamaa alishabadilika..yani akili imekomaa sasa.

So spend time na mshkaji. . . onyesha nia ya kutaka kumjua kiundani zaidi na kumpa fursa ya kufunguka kwako.Pia unaweza kumwambia rafiki yako kwamba unamjua mshkaji na pia uko interested nae usikie atasemaje.Unaweza kushangaa story inabadilika ghafla.

kutokana na kuwa na mawasiliano naye mara kwa mara, nimejikuta nikizidi kumpenda, ila maelezo ya shoga angu, yanazidi kunichanganya, mie sijazoea kupigwa achlia mbali kufinywa, sasa kuingia kwene uhusian wa kutiana ngeu, mh! mwenzenu naogopa
 
jarib kuwa makin coz inawezekana huyo shoga ako alikuwa hajatulia ndo msela akapiga chin, ila ss hv anajisafisha kwako.
 
kuna kila dalili ya kitabu kuzaliwa kutokana na muendelezo wa hii stori. Kitabu kikiwa tayari naomba unijulishe kama mambo ya Zawadi!
 
Nimem-Text huyo kijana kumuuliza kama anamfahamu huyo shoga yangu, hebu ngojeni niwape summary ya jinsi tulivyo chat muda mfupi uliopita:

Mimi: mambo dear
yeye: safi my sweetheart, vipi kesho weekend can we meet and chat?
mimi: Nope, will be busy with chores here home
Yeye: ok, but we can chat via FB, wht do u think?
mimi: yeah........may I ask u something?
yeye: sure, ask!
mimi: eti unamfahamu xxxx
yeye: dont remember, kwani vipi?
Mimi: am just asking, hujawahi kusoma mkoa xxxxxx
Yeye: Yeah, nimewahi kusoma katika mkoa huo sometimes back...
Mimi: and you dont remember her!
Yeye: Sorry you said xxxx who?
mimi: her family name is xxxxx
yeye: Yeah, I remember her.........., do you know her?
mimi: I met her somewhere with friends and she mentioned your name...... now tell me how do you know this lady?

Ulipita ukimya fulani, nadhani alikuwa akitafakari, baadaye akajibu

yeye: Sorry, can we meet and talk about that, it is long story my sweetheart
mimi: ok, thank you...........
 
inafurahisha! Mshkaji alitaka kukanusha kidizaini. Ukishameet nae tupe feedback.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom