Nimrod Mkono: Nitaisaidia serikali kupunguza au kufuta deni la DOWANS

Amesema ataisaidia serikali kupunguza au isilipe......atalipa yeye! Fedha hizo anazo! Tunamshukuru sana!
Msando kwa nini ailipie serikali hizo pesa si angefanya jimbo lake kuwe pepo ya eden yaani watu wajimwamwaye kwenye bustani nzuri yenye maji tele elimu bure afya bure mitaji kwa vijana bwelele usafiri huo,uvuvi,ufugaji,kilimo kwa sanaa,asitubabaishe hapa mwizi mkubwa sana hana lolote atungikwe tuu
 
Njia rahisi ya kupunguza hili deni la DOWANS ni kwa baadhi ya wahisika kijitoa katika mgao na hivyo kupunguza jumla ya fedha zinazohitajika kulipwa. Nadhani ndio jinsi Mh Mkono anavyotaka kutusaidia kwa kujitoa au kuwatoa wenzake kwenye mgawo.
 
Ni rahisi sana kumkamata mwizi kwa kutumia mwizi. Tumpe hilo jukumu ili tusilipe hizo pesa. Ila asije kutudai ujira kwa kutufanyia kazi hiyo
 
Ni rahisi sana kumkamata mwizi kwa kutumia mwizi. Tumpe hilo jukumu ili tusilipe hizo pesa. Ila asije kutudai ujira kwa kutufanyia kazi hiyo
I like that! kuna msemo unasema" mwizi mpe mzigo akuchungie"
 
DOWANS itaibua vioja vingi! Mtuhumiwa wa kashfa hiyo Nimrod Mkono ameibuka kwenye kikao cha CCM na kudai ataisaidia serikali kupunguza au kufuta deni la DOWANS,..alikuwa wapi??..naye huyu si mtuhumiwa katika malipo haya??

Source: Gazeti la Mwananchi


Siasa za tanzania ni kama Comedy vile!

Onyesha mambo yako tuone.
 
MBINU MPYA CCM KUJILIPA MARA 3 SHEA WANAYOISUBIRIA DOWANS KWA KUWAUZIA WANANCHI JOTO JINGI NA GIZA NENE KWA MAVUNO MANONO ZAIDI KARIAKOO:

Jamani zaidi ya mara tatu ya hilo deni geresha CCM wameshaikusanya kwa kuleta mbinu chafu hiyo hapo ya kukata umeme. Kama huamini hili hebu waulize wanamahesabu watakuambia.

Wanachokifanya CCM kwa kuzima umeme masaa mengi ni kwamba wanaenda kwa wahindi Kariakoo kila jioni kukusanya kitenesi chao kwa kutoa mwanya wa kuuza zaidi mi-jenereta feki za kichina kwa bei za juu ajabu.

Katika hii mbinu mpya ni kwamba CCM inaokoa garama ya kuendesha mitambo kibao ya umeme inayotumia mafuta / diesel lakini bado wanapata faida mara tatu zaidi kwa mkondo mwingine wa biashara haramu kwa kuwauzia tu wananchi giza na joto jingi.

Sie huku wana-Mafinga, aaka ni giza tu jeto tunalisikia tu redioni. Wananchi tukomeshe hii biashara haramu ya CCM kutuchuuzia giza na joto kali kwa mavuno manono kuliko ya Dowans kule Kariakoo.

Hivi wana jamii kwa nini tusiijibishe CCM na serikali yake iliyoko madarakani kwa kutuletea madudu haya.Tuwawajibishe kwa kuwakataa hadharani na kuandamana kwamba Serikali iliyopo madarakani imesababisha hali ya maisha imekuwa ngumu na sasa mzigo wa Dowans haubebeki kabisa.

Tuandamane mpaka serikali nzima ianguke na kuunda serikali mpya itakayowaadhibu wote waliohusika kutufikisha hapa tuhakikishe tunawafilisi na kuwashitaki wote.
 
Huu ni wizi na hakuna namna tunaweza kukubali Nimrod Mkono atusaidie kwa kuwa na yeye ni mtuhumiwa,labda cha kufanya atoke hadharani na kuwaomba watanzania msamaha kwa kuhusika kwake kwenye kashfa hii ya ufisadi na kashfa nyinginezo zinazohusiana na utafunaji wa fedha za watanzania.
 
kama anazo si ajenge barabara, badala ya kulipa deni..deni ni priority kweli..huko musoma?
 
Haka kababu baada ya kusomeshwa na JKN kame asi falsafa za mwalimu na kuwa kafisadi kakubwa...................
Eti juzi kanaongea kanataka kujenga kiwanja cha mpira na kama hela haitatosha katauza ndege yake... hivi kana ndege yake?

Haka kazee kanataka kasamehe mgao wake ili waseme tumepunguziwa deni.
Mimi nasema kabla hawajatusamehe ni lazima tuujuwe ukweli wa DOWANS kwanza ndo watusamehe tusiwe wajinga.

HATA KAMA WATASAMEHE ISSUE HAIISHII KWENYE KUFUTA DENI BALI LAZIMA WATU WAWAJIBIKE KWA KUTAKA KUTUIBIA. LAZIMA TUWE NA ZERO TOROLENZI KWA MTU ANAYETAKA KUIIBIA NCHI.
 
Yaani hadi nywele zinataka kunitoka atasaidia vp wakati yeye ndio mpangaji mkuu wa mipango? Au watanzania wanatuona mazuzu? The master minder wa plan ni yeye na RA sasa atatusaidia vp katika hiyo kesi? Atusaidie kulipa maana hatuna pesa!!!!!
 
Du kwanza atutajie ni kina nani hao Dowans ndio tutaamini anaisaidia Nchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom