Nimrod Mkono: Nitaisaidia serikali kupunguza au kufuta deni la DOWANS

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,515
20,005
DOWANS itaibua vioja vingi! Mtuhumiwa wa kashfa hiyo Nimrod Mkono ameibuka kwenye kikao cha CCM na kudai ataisaidia serikali kupunguza au kufuta deni la DOWANS,..alikuwa wapi??..naye huyu si mtuhumiwa katika malipo haya??

Source: Gazeti la Mwananchi
 
dowans itaibua vioja vingi,.mtuhumiwa wa kashfa hiyo nimrod mkono aibuka kwenye kikao cha ccm na kudai ataisaidia serikali kupunguza au kufuta deni la dowans,..alikuwa wapi??..naye huyu si mtuhumiwa katika malipo haya??
source;gazeti la mwananchi

hahaaa,bado sana,yataibuka mengi sana kwnye hii muvi.
 
Kivipi kama chama chake kimeashaamua kulipa? Au ataisamehe serikali isimlipe? (Maana anajulikana naye yumo)
 
huyu ni mwanasheria sasa ataisaidia kisheria tuondokane na hili deni au atatoa cash kupunguza deni
 
mkono angekuwa na moyo hou wa uzalendo? mbona hata madini tungeona faida yake? hawa watu bwana wanachojali ni matumbo yao tu he is talking rubbish
 
Kivipi kama chama chake kimeashaamua kulipa? Au ataisamehe serikali isimlipe? (Maana anajulikana naye yumo)

Wameshaona ishu ngumu wanajaribu kuzuga sasa waje waseme deni limefutwa! Kelele zimezidi sasa wanatafuta mbinu baada ya kuona wanaelekea kufeli waseme Dowans imesamehe baada ya Mkono kuisaidia serikali
 
mweee mwaka huu ni vituko tupu jamani
hivi hii nchi ina rais kweli
 
mkono angekuwa na moyo hou wa uzalendo? mbona hata madini tungeona faida yake? hawa watu bwana wanachojali ni matumbo yao tu he is talking rubbish

Yaani limetengeneza mikataba mibovu ya madini na Chenge wake, leo anakuja kuwa mwema kwa DOWANS ambayo kuna tetesi naye anahusika......nafikiri hatuhitaji msaada wake,bora Tundu Lissu atusaidie :playball:
 
Mbona ni rahisi kumwelewa; Huyu ndiye msemaji wa serikali kivuli chini uongozi wa RA na EL.

Kupunguza deni = watatoa discount labda ya 30% ili tulipe kitu kama 65 billion
Kufuta deni = tukiwa-convince vya kutosha basi watatusamehe deni lote.

Tunaomba wazee wa kanisa pale Magomeni Adventists wampembeleze mzee mwenzao watanzania tusamehewe deni hili!!!!!!!!!!!!
 
picha kama ya kihindi...starring anakufa unadhani picha linaisha...ha ha ha mbwa anenda kulipa kisasi...inabidi kutenngenezea documentary la saga hii ya dowans ikiisha...very interesting.....kila kiongozi anaongea lake...kweli ukitupa jiwe gizani linaweza lisimpate mmoja vilio vingi kweli..limewapata..wanahaha...:shut-mouth::nono:
 
Huyu mzee angekaa kimya kabisa akamalizia pesa alizotulamba BOT..
apunguze kama nani na alikuwa wapi siku zote?
kesi alizosimamia BoT walishinda ngapi na yeye alikuwa akilipwa $500 kwa saa!!
amakweli nyani haoni ........
 
mukono ni mnafiki fisadi tena ni mjasiriamali wa ikulu hana nia njema.si waku muamini.
 
Asiseme ATAISAIDIA SERIKALI...NI dharau kubwa hiyo..aseme ukweli kuwa mambo yamekuwa magumu, na kila mtu anatafuta mlango wa kutokea..
 
Kivipi kama chama chake kimeashaamua kulipa? Au ataisamehe serikali isimlipe? (Maana anajulikana naye yumo)

Ataondoa mgawo wake kwenye malipo yanayotarajiwa na hapo atakuwa amepunguza deni. Hapa kweli patamu
 
picha kama ya kihindi...starring anakufa unadhani picha linaisha...ha ha ha mbwa anenda kulipa kisasi...inabidi kutenngenezea documentary la saga hii ya dowans ikiisha...very interesting.....kila kiongozi anaongea lake...kweli ukitupa jiwe gizani linaweza lisimpate mmoja vilio vingi kweli..limewapata..wanahaha...:shut-mouth::nono:

Hii kweli kama tambara la kidosi, hahahaaa nimeipenda hii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom