Pretty
JF-Expert Member
- Mar 19, 2009
- 2,575
- 552
jamani mi naona sifikiriwi hapa! nyani ngabu unanishauri ninyonye 'koni' ndiyo nini hiyo mzee?
swala kubwa mume huyu ni kutoka kwa makabila yale ya' amri amri' kule kuzunguka ziwa maarufu hapa kwetu Tz, kitu ambacho nafikiria kinachangia na kutonijali mimi kwamba nahitaji kuridhishwa pia.
Kufanya mambo ya chumbani ni kama chakula hakuna lingine analowaza, hajali nimechoka wala niko kwenye hedhi.. angekuwa basi ananirusha roho kwa kachumbari nisingenungunika. Kwa upande wangu hata hayo niliyofundishwa kwenye kichen-party nashindwa kupractise kwake, kwani inapofika muda narukiwa kama mzoga. Akisha mwagilia na siku ndiyo imetoka hiyo.
Wakati mwingine natamani nimuulize kama alipobarehe alifundishwa jinsi ya kumridhisha mwanamke, ila naogopa kufanya hivyo.
wala usiogope wewe muuulizie tu. Yaani wewe unaogopa kumuuliza mumeo swali kama hilo? Kwenye mapenzi kunatakiwa kila mtu awe muwazi kwa mwenzie, hapo ndio itakuwa rahisi kila mmoja kumfahamu mwenzio vizuri.