Nimeshindwa kumsoma!!!!!

Mh mwana mbona hujui kuconnect scenes za movie?? Mkoa wenyewe huo IRINGA(ful baridi)+Mesej zako kufutwa kwenye simu yake+kukuta mesej za midume 6+hatak uwende anapoish+kujiliza na kusema hafai kwako+penz la mbali= ???.Hebu fanyafanya editing hzo scenes mie natayarisha mabango tuirushe.Hyo itakuwa bonge 1 la muvi kaka 2takoka kimaisha.Kuwa editor mzur co lazma usomee ni kujaribu kuwa m2ndu na kujua kupangilia hzo scenes mwisho wa cku muvi itasomeka.kama bdo hujaelewa utakuwa una matatzo kwny brain yako na unastahili kwenda dodoma kwenye ukumbi mdogo wa bunge a.k.a milem**
 
Wewe umeelewa kabisa kinachoendedelea lakini kwa sababu unampenda huamini kuwa si wako tena.
 
Sijui hata niseme nini!Ah kumbe nimeshasema!Haya mambo ya wanawake bana aaaargghhhh!!
 
Iringa kumekucha siku hizi! Wadau watakuwa wameshaweka zygote tayari! Pole sana!
 
Jamani mi nimepita tu kuwasalimu na kuwatakia sikukuu njema.
 
Nashukuru kwa mchango wen japo wengine wamekejeli taaluma za wahusika sio mbaya sana, ni mawazo na mtazamo wao. Ahsanteni sana wadau! Sikukuu njema! Bwana awatie nguvu!!
 
kama amekuambia hafai hata kuwa mbwa wako,kwanini unataka kulzaimisha kuwa mfaga mbwa wake?tafuta mbwa mwingine,huyo hafai usikute anangoma.ohh
 
Wadau, wakati nipo chuo nilikutana na mrembo mmoja tukiwa mwaka mmoja lakini vitivo tofauti, tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi, tulipomaliza chuo mwaka jana tukawa tumepangwa vituo vya kazi ktk mikoa tofauti, lakini tukawa tunawasiliana huku kila mmoja wetu akimpa hope mwenziwe kuwa ndio wake wa maisha, lakini juzi nilimtaarifu kuwa naenda kwake(Iringa) ambako ndo kituo chake cha kazi kilipo, akanijibu kuwa ana safari hivyo nisije. Nikawa kichwa nazi nikaja jana, nikampigia simu akaja hapa hotelini nilipofikia, nikaanza kukagua simu yake ya mkononi ili nijiridhishe lakini nilikuta message za mapenzi kama za wanaume 6 tofauti huku message yangu hata moja hamna, zote kafuta. Nilipomuuliza kuhusu safari kajibu kuwa "pole sana kwa yote". Nimeshangaa zaidi jana alivyokuwa anarudi kwake jioni ile hakuthubutu hata kunikaribisha kwake, leo asubuhi kaja hapa chumbani(hotelini) asubuhi tangu saa 4 analia tu hadi muda huu huku hatoi hata neno moja kila nikimuuliza sababu ya kulia huku hata mimi akinitia woga, kajibu tu "sistahili kuwa hata mbwa wako, mi sikufai, pole kwa ukatili niliokufanyia". Je wadau huyu binti nimfanyeje? Na mimi nimependa?

Achana naye unauliza nini tena?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom