Intelligent businessman
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 26,109
- 52,835
AMEPOTEA KISIWANI KEY WEST - 1 Umewahi kujua kwamba taa za barabarani huwekwa pia Kamera? Si kwa Tanzania, lakini katika miji mingine mikubwa taa za barabarani huwekwa Kamera ili ziweze kunakiri matukio mbalimbali na kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama.
Fuatilia kisa hiki cha mwanaume mmoja aliyepotelewa na mke wake huko kisiwani Key West, nchini Marekani.
-------
Katika miji ambayo mitaa yake imefungwa kamera maalumu za kunasa matukio, karibu kila tendo linalofanyika mitaani hunaswa na kumbukumbu zake huhifadhiwa. Teknolojia ya leo inafanya matumizi ya simu hata kwa sekunde moja tu, kutosha kujua mahali mtumiaji wa simu alipo. Kila dakika, mfumo wa kutambua mahali alipo mtu au kilipo kitu, maarufu kama GPS (Global Position System) husaidia kuangalia mienendo ya vyombo vya usafiri vya ardhini na majini.
Kwa msaada wa teknolojia hiyo ya mawasiliano, katika miji miwili wapelelezi waligundua uhalifu uliotokana na usaliti, tamaa na uroho.
Ilikuwa siku ya mwezi wa Januari, 2003, Michael Garvin, wakala wa majengo na mmiliki wa kampuni ya Magnolia Properties aliondoka nyumani kwake mjini Jacksonville akiwa na mkewe Shirley kwenda kisiwa cha Key West kwa ajili ya mapumziko ya ‘weekend’. Asubuhi ya kwanza akiwa kisiwani huko, Michael alitembea hadi duka la dawa la karibu na kununua dawa kwa ajili ya mkewe. Aliporudi hotelini lisaa limoja baadaye, Shirley hakuwepo.
Michael alifikiri mkewe amekwenda mgahawani au pengine amekwenda kujinunulia mahitaji yake binafsi. Lakini alipogundua kuwa mkoba wa mkewe upo katika chumba kile cha hoteli, alianza kuhisi dalili ya jambo baya. Baada ya masaa mengi bila mkewe kurudi, Michael aliamua kupiga simu kituo cha polisi na kuripoti kuwa mkewe amepotea.
Maofisa wa polisi walipowahoji wahudumu wa hoteli, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amemuona Shirley asubuhi ile. Ndugu na jamaa walianza kupata mashaka, lakini habari za kustua ni kuwa Shirley si tu hakuwepo hotelini, bali hakuwepo katika kisiwa cha Key West. Tayari maofisa wa polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vilijiridhisha kuwa Shriley hayupo ndani ya kisiwa kile kidogo. Hakukuwa na mtu mwenye taarifa za mrembo huyo. Ndugu zake waliwaambia polisi kuwa wajaribu kufuatilia maduka ya vito vya thamani kwa sababu ndugu yao alipenda sana kuvaa pete na mikufu ya thamani kubwa. Lakini hata hilo halikusaidia.
Sasa maofisa wa polisi waliamua kuanza uchunguzi wa kimahakama mara moja kwa kutafuta alama za vidole za mtu tofauti na wawili wale yaani Michael na Shirley, ndani ya chumba chao cha hoteli. Hakukuwa na alama za vidole za mtu mgeni. Mbwa maalumu aliyefunzwa kunusa na kujua endapo kuna mgeni aliingia chumbani humo lakini hakupata taarifa yoyote.
Siku iliyofuata, habari ilitoka katika gazeti moja kisiwani humo ikiwa na kichwa cha habari kinachosema; ‘Nini kimetokea kwa Shirley Garvin’? Vyombo vya habari vilitangaza taarifa hiyo na kuwaomba wafuatiliaji kutoa taarifa zozote zitakazosaidia, lakini hakukuwa na taarifa.
Maofisa wa polisi na wapelelezi waliendelea kumtafuta Shirley katika maeneo yote ya kisiwa cha Key West ambacho kina ukubwa wa maili za mraba sita tu, bila mafanikio. Lakini walifanikiwa kupata jozi ya viatu vya wazi (sandals) vilivyofanana na viatu vya Shirley. Jambo hilo lilijenga hisia kuwa pengine Shirley alikuwa amezama baharini. Lakini pia kulikuwa na taarifa nyingine ya kutilia maanani.