Mwanamke wangu mbaya wa sura na muonekano ila ndie anaeniweka mjini

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
884
Nina demu mmoja anasoma chuo, ananipenda sana lakini mimi namchukulia kawaida tu kwasababu ananiweka mjini, naishi kwake ananilisha na bills zote analipia yeye, mimi mchango wangu kweke ni kidogo sana nkipata pesa kidogo kidogo ndipo nachangia.

Kwanza kabisa demu tulikutana mtandaoni tukabadilishana namba tukawa tunawasliana, alinikaribisha getto kwake room amepanga kuna kila kitu ndani, na anaonyesha kunipenda sana lakini mimi simpendi kama yeye anavyonipenda, inshort namuigizia tu kwasababu bado najitafuta.

Sababu kuu inayonifanya nisimpende ni kwasababu ana sura mbaya na muonekano mbaya, lakini ana rafiki yake mmoja mzuri sana alishawahi kunikutanisha nae akanitambulisha kwake, yule rafiki yake nilimuelewa sana mpaka sasa huwa natamani kumuona kila mara, dem wangu akiwa ananisimlia story za rafiki yake huwa natamani aendelee kunisimlia details nyingi zaidi kumuhusu huyo rafiki yake ili nimjue kiundani zaidi ili nikija kumtokea iwe virahisi kumnasa.

Huyu dem wangu kwanza hata kutembea nae barabarani huwa naona aibu kwasababu mimi ni bishoo na ni handsome kiaina lakini demu wangu ana muonekano mbaya amevimba kama baunsa wa club.

Sasa nilikua nafikiria kuanza kumcheat huyu demu wangu ambae mpaka sasa bado naishi kwake na ananiamini sana na huwa ananitishia kuwa siku akijua kuwa namcheat anaweza kunifanyia kitu kibaya ambacho kitanifanya nijutie maisha yangu yote hapa duniani, na kwa muonekano wake ana hasira za karibu sana (short temper) mpaka kuna muda huwa nataman nimweleze ukweli kuwa nahtaji tuachane lakn naogopa anaweza kunifanyia kitu kibaya maana nimetumia vitu vyake vingi sana na nimekula pesa zake nyingi sana.

Rafiki yake nmekutana nae leo tukawa tunapiga story nyingi sana nkawa natamani kumuomba namba ya simu but naogopa,

Kitu kinachonifanya mpaka natamani kuwa na rafiki yake ni kwasababu rafiki yake ni mrembo sana na ana muonekano mzuri hata nikitoka nae out balabalani siwezi kuona aibu maana binti ni mrembo sana, kingine kinachonifanya natamani kuwa na huyo binti ni kuwa yeye hasomi yupo anaishi kwake na ana hakiri za maisha ya kujitaftia, mimi pia nina mtaji kidogo nafikiria kumtongoza akinikubaria tuanze maisha yetu mapya na huyu bint wa ndoto zangu, then huu mtani nilionao tufanye biashara ili tuweze kutafta maisha kwa pamoja.

JE NIACHANE NA HUYU DEMU MBAYA WA SURA NA MUONEKANO ILI NIAZE MAISHA MAPYA NA RAFIKI AKE AMBAE NI MREMBO NA ANANIVUTIA ZAIDI..?
 
Jitafute kwanza achana na mapenzi.

Inamaana mpaka umediriki ku date na demu usiyempenda(mbovu kwa maoni yako) kisa pesa zake ni dhahiri kuwa unapenda kulelewa hiyo haifai kwa mwanaume mkuu.

Mwanaume unatakiwa ujifunze kusimama na kujitegemea wewe kama wewe.

NB: mbona hii ni kama chai lakini 🤔
 
Kwamba wewe ni mrembo kuliko demu wako, unaona aibu kutembea naye barabarani kisa ni mbaya na wewe ni mzuri....nikarudi tena kuangalia avatar yako nikaona kweli wewe ni mrembo, chakufanya achana na huyo dada mzuri katafute huyo mrembo mwenzio, naye ukimshindwa unatakiwa kutafuta basha la kukugongelea misumali.
 
Uzi uishie hapa nadhani majibu yapo hapa.😂😂
Kwamba wewe ni mrembo kuliko demu wako, unaona aibu kutembea naye barabarani kisa ni mbaya na wewe ni mzuri....nikarudi tena kuangalia avatar yako nikaona kweli wewe ni mrembo, chakufanya achana na huyo dada mzuri katafute huyo mrembo mwenzio, naye ukimshindwa unatakiwa kutafuta basha la kukugongelea misumali
 
Sijasoma huo utopolo wako ila ushauri wangu baada ya kusoma headline tu ni hivi kama ni mke oa kama ni goma tu la mda piga sepa... Usiume kichwa
 
Kwa hilo joto la dar unaamka saa 2 asubuhi, unakuta dem wako kakuandalia chai tayari.
Unawasha tv kucheki movie huku unachapa chai(wakati huo kaenda chuo).

Mchana unapika chakula cha fasta au unanunua kwa pesa aliyokupa ya matumizi. Utakula ili ujaze tumbo kidogo ili mida ya saa 9 hivi upate bia zako hata 3 hivi wakati unasubiri arudi chuo akupikie.

Saa 12 miguu juu unacheki movie au mechi kama ipo hiyo siku, huku bibie akikuandalia msosi wa nguvu .
Saa 2 unakula na unamla na yeye.

Na hii ndio inakua ratiba yako kila siku mpaka ufikie miaka kama 45 hivi utabadili kwa ule muda wa jioni utakua unaenda kucheza bao na wazee wazembe kama wewe.

What a life, mkuu unaishi vyema sana. Hongera.
 
Back
Top Bottom