Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hongera ndugu.....sasa inabidi usijifiche,umekuwa mtu-umma(public figure)...wenzio Mnyika,Zitto,Dr Slaa wanatumia true IDs...kwa hiyo come out na useme jimbo TUSAIDIANE kulichukua

Nashukuru sana kwa wazo zuri lakini kwa sasa itwakuwa ngumu.Dr Slaa,Zitto na Mnyika wanatumia majina yao kwa kuwa tayari mnawafahamu.Mimi ni kapuku tu,nitakuja na jina langu huko mbele ya safari lakini pia GS itaendelea kama kawa..
 
Wakuu.Jana tulikuwa na mchakato wa kura za maoni jimboni kwetu.Tulikuwa wagombea wawili katika chama chetu.Nimefanikiwa kushinda kura za maoni kwa kishindo na kumuangausha mpinzani wangu,hivyo kuipeperusha bendera ya CHADEMA katika jimbo hili.Nimeandika historia kwa kuwa kijana wa kwanza kugombea kwenye jimbo hili tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi kwa vyama vyote vilivyowahi kusimamisha wagombea ubunge kwenye jimbo hili. Ni mtaji kwangu..

Tuko pamoja...Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Tafadhali naomba msiniulize nagombea jimbo gani.Ni jimbo moja la Mkoani,Wilaya yenye jimbo moja..Zaidi ya hapo usiniulize.

Alunta continua

Natumaini kampeni zenu zilikuwa za kimyakimya na hata hujazunguka ukajua ukubwa wa jimbo lako na wapiga kura wako wakakufahamu. CCM are very clever, kampeni zao wanazunguka jimbo zima hivyo kabla hata kampeni hazijaanza mgombea wao anafahamika jimboni na anafahamu kila uchochoro wa jimbo lake. Wewe wakati utakuwa unatumia muda mwingi ili watu wakufahamu, wenzio watakuwa kwenye hatua ya kueleza sera na kuomba kura. You need to work very hard to win
 
Hata nie nakutakia kheri na baraka katika safari hii ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli. Najaribu kutengeneza picha ya baadae sipati jibu.

Hapo tutakapokuwa na Rais aliye member wa JF, pia wabunge kama 50 hivi ambao ni member hapa JF, na hakika mawazo ya watu weledi ambao ni member humu (Sio wakina MS ) yatafika Bungeni na pengo la Slaa kutokuwepo halita onekana.
 
Hongera sana GenderSensitive tuko pamoja katika hili.
naamini utaendelea kufanya vizuri zaidi .
 
hongera; ila mimi nina safari ya mkoani itakuwaje kama naenda huko nikajaribu kukupigia ndogondogo; be free mkuu
 
ongela! halaf hakikisha yule invisible mysterious lover wako wa JF haathiri kampeni zako na utawala wako kama utachaguliwa. nitakutumia kiapo cha kuhakikisha utailinda katiba kupitia PM.

Ha ha ha,yule nimpendaye wasiri hawezi kuathiri kampeni zangu.Ni mtu mabaye ananisapoti sana tu,nimekubali kwamba haiwezekani kuwa naye,sina jinsi.Tumebaki kuwa marafiki wakubwa.Ananiunga mkono na mguu pia..Ha ha ha!
 
Natumaini kampeni zenu zilikuwa za kimyakimya na hata hujazunguka ukajua ukubwa wa jimbo lako na wapiga kura wako wakakufahamu. CCM are very clever, kampeni zao wanazunguka jimbo zima hivyo kabla hata kampeni hazijaanza mgombea wao anafahamika jimboni na anafahamu kila uchochoro wa jimbo lake. Wewe wakati utakuwa unatumia muda mwingi ili watu wakufahamu, wenzio watakuwa kwenye hatua ya kueleza sera na kuomba kura. You need to work very hard to win
kama kujulikana ni mpaka ukamatwe na takukuru, then CCM ni vinara wa ku-strategize, if that is what you people call strategies!
 
Hongera sana,kaza buti mpaka kieleweke.
Mwenyezi Mungu na akutangulie,Ubarikiwe mpaka ushangae.
 
Natumaini kampeni zenu zilikuwa za kimyakimya na hata hujazunguka ukajua ukubwa wa jimbo lako na wapiga kura wako wakakufahamu. CCM are very clever, kampeni zao wanazunguka jimbo zima hivyo kabla hata kampeni hazijaanza mgombea wao anafahamika jimboni na anafahamu kila uchochoro wa jimbo lake. Wewe wakati utakuwa unatumia muda mwingi ili watu wakufahamu, wenzio watakuwa kwenye hatua ya kueleza sera na kuomba kura. You need to work very hard to win

Nakubalina na wewe ingawa hazikuwa za kimya kimya kama unavyodhani.Nilikuwa huku about three weks ago na nilifanya kazi kwenye kata kadhaa.Nikarejea Dar nikarudi tena.Ni ukweli kwamba mfumo wa CCM wa kupigiwa kura za maoni na wanachama ni mfumo mzuri mabo unakufanya mgombea unajitambulisha mapema kwa wananchi.Sisi kwetu ni tofauti hivyo unakuwa nyuma kidogo,ukilinganisha na wao.I real needa to work hard na ndio mkakati ninaohangaika nao sasa.
 
Gender Sensitive,
Hongera sana na tunakutakia kila la kheri mpiganaji wetu. Lakini usije sijahau kwani kuchaguliwa kwenda vitani sio vita yenyewe. Huko uendako ndiko kwenye uzito zaidi..
 
Gender Sensitive,
Hongera sana na tunakutakia kila la kheri mpiganaji wetu. Lakini usije sijahau kwani kuchaguliwa kwenda vitani sio vita yenyewe. Huko uendako ndiko kwenye uzito zaidi..

Mkuu Mkandara,heshima mbele.

Ni kweli kabisa mchakato ndio kwanza umeanza,vita bado.Kijasho kimeanza kunitoka,nimeanza maisha mapya kabisa.Kila ninakopita lazima nisimame na kusalimia watu.Kazi kweli kweli..
 
Hongera sana...Mungu awe nawe, na akusaidie...
Vipi signature yako, neno mtarajiwalitoke au mpaka majina yapitishwe na kamati kuu?
 
Sasa campaign unafanya kwa kificho ? Hata kama watu wanataka kukupigia kura au kampeni watawezaje mtu mwenyewe hutaki kujitambulisha?

Hivi unaelewa sacrifices za uongozi wewe kweli ? Unaelewa essence ya campaign ? Unaelewa majukumu ?

Au tunataniana tu ?
 
Mkuu hata mimi nilijiuliza hilo lakini nimefikiria kwa undani na hakika hana sababu ya kujitambulisha hapa kwani kura hazipigwi JF. Pili kama hukujiandikisha jimbo lake huwezi kumsaidia kwa kura ila kama anahitaji msaada ataandikia watu barua pepe.
Tatu, kama wewe upo jimboni kwake sidhani kama utampigia kura kwa sababu yupo JF isipokuwa kutokana na kujiuza kwa chama na YEYE hata kama akiwa ni Malaria_Sugu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom