Nimeshangaa usiku huu na habari za ITV

Ndugu wana JF salaam toka Brussels
Nimekuwa naangalia news usiku huu na nimeona matukio 3

1.Waziri Mkuu akiwa Serengeti leo , kwenye hadhara wameonyesha watu wakimsikiliza nimeona kuna mdada alikuwa ana cheza cheza wakati wa hotuba ya Pinda na open space kati kati nikawa najiuliza kama kulikuwa na muziki ukiendelea wakati hotuba ya Pinda inarindima .

2.Nimeona Mgombea wa Chadema Igunga na habari ya Utajiri wa kijiji alichokuwa anahutubia leo .

3.Nimeona Mukama akiongea , na Komba , na Mgombea wa CCM .Nimeshangaa sana sana kuona picha ya umati ulio kuwa kwa Pinda ndiyo wale wale ambao waneonyeshwa Igunga .Kwa kweli nimeshangaa mno na kama kuna yeyote kaona habari za usiku huu tafadhali anasaidie kuelewa .Je ITV wanataka kutueleza nini ? Wana chakachukua mkutano au hawakuwa na picha za matukio ya CCM za leo au Pinda kaonyeshwa kimakosa hakuwa na watu ? Nisaidieni kuelewa am confused .

Vyombo vya habari vina mifumo yake katika uwasilishaji wa habari. Na kila chombo kinatakiwa kifuate taratibu na mfumo wake ambao ni universal kwa dunia nzima.

Kwa mfano news za television lazima ziwe na yafuatayo, maneno na matendo, ili kukamilisha zoeli la maana ya TV, yaani:
tell vision, maana ya ongea na onyesha picha za vitendo au ongea na onyesha vitendo vinavyoendelea.

Na inapotokea kwamba TV haina picha ya tukio basi habari hiyo inatakiwa iwasilishwe katika vyombo vingine vya habari kama radio au magazeti kwa kuwa hayafungwi na utaratibu wa utangazaji wa sheria za TV.

Ni kosa kwa sheria za utangazaji wa TV kuchukua picha ya tukio lingine na kuiingiza kwenye tukio lingine, na katika mataifa yaliyoendelea ni kosa lenye kusababisha mhusika kuchukuliwa nidhamu. Kwa Tanzania hayo yamezoeleka sana kwa sababu idara na vyombo vingine vya serikali vinavyosimamia vyombo vya habari ndio wanaendekeza huu uchakachuaji. That is really shame to IPPMedia, they have to regret and apologize to the public mission.
 
Apo juu upo sahihi kwa mantiki..lakn kuweka kumbukumbu sawa hakuna "Tell Vision" ila kuna "Tele Vision"....Tele=Far,remote or a distance...e.g Tele Graph=a remote msg,Tele phone=a far calling(muito wa mbali)...Tele Commando=Remote Control(Kiitaliano)...usijenge hoja kwa kupangua maana halisi ya kitu flani...hoja "itapalanganyuka" ile maana "ikipalanganyuliwa"
 
Tunajitahidi sana kuweka dondoo ambazo mtu asiye na taaluma hiyo aweze kuelewa vizuri na ndivyo darasa letu la habari lilivyo. Lakini hii hapa chini ni kwa wale wanaoishia ya darasani bila kuelewa maana ya nadharia tutabaki kutoa vielelezo kama vifuatavyo hapo chini:
Television (TV) is a telecommunication medium for transmitting and receiving moving images that can be monochrome (black-and-white) or colored, with accompanying sound. "Television" may also refer specifically to a television set, television programming, television transmission.
The etymology of the word has a mixed Latin and Greek origin, meaning "far sight": Greektele (τῆλε), far, and Latin visio, sight (from video, vis- to see, or to view in the first person).

Tutanakiwa kutumia lugha rahisi ambayo kile anayesoma hata kama hana idea ye yote katika taaluma hiyo anaelewa. Hivyo hitimisho la TV ni Tell people and they have to see the vision (pic) thats all. Mwanahabari wa Televion lazima afuatane na professional photographer ili habari ikamilike na ndivyo nilivyojifunza na ndivyo nilivyofanya field. Lakini hii ya asili ya maneno na viambisho vyake ni mambo ya darasani kujua asili yake na historia yake, ila nilichoeleza ndicho kinachofanyika. Kwa mchanganuo huo ni sawa kusema Television inapaswa kutolewa kwa picha zinazoambatana na sauti, yaani maelezo na picha.

Television (TV) is a telecommunication medium for transmitting and receiving moving images
with accompanying sound.
 
Apo juu upo sahihi kwa mantiki..lakn kuweka kumbukumbu sawa hakuna "Tell Vision" ila kuna "Tele Vision"....Tele=Far,remote or a distance...e.g Tele Graph=a remote msg,Tele phone=a far calling(muito wa mbali)...Tele Commando=Remote Control(Kiitaliano)...usijenge hoja kwa kupangua maana halisi ya kitu flani...hoja "itapalanganyuka" ile maana "ikipalanganyuliwa"

Tatizo hilo wanalipata wengi wanaingia darasani iwe shule za awali vyuo na wanachofanya ni kukariri nadharia ya asili ya maneno na historia yake. Lakini hawapambanui kuwa lugha hiyo inapotoholewa na kuingizwa ndani ya lugha nyingine, maana ya asili huanza kupotea kutokana na mabadiliko ya teknologia na maana ya maneno ya lugha nyingine. Kwa maana hiyo maneno mengi ya kiingereza yametokana na lugha za zamani za kigiriki na kilatini ambazo ukichukulia uambishaji wa maneno hayo kwa sasa si sahihi kwa vile neno hilo sasa linaelezeka kwa lugha ya kiingereza, kijerumani, kiarabu, kichina nk. Ingawa kitaaluma tunatakiwa kujifunza historia yake ilivyoanza.
 
Jamani, hivi vyombo vya habari vinapotoa habari za UONGO kama hizo hakuna chombo chochote cha kusimamia maadili kinachoweza kuvichukulia hatua?
 
Hawa tushawazoea hawana jipya zaidi ya kufanya CCM mtaji ili kutimiza na kupunguza njaa zao.Niaibu sana kwa kituo cha ITV kuikumbatia CCM wakati kipindi cha nyuma Mengi alikuwa anawashutumu makada wakubwa wa CCM (Manji) ,na baadhi ya Mawaziri kuwa wanamuhujumu.Kweli mapinduzi yana gharama kubwa ila kitaeleweka tu.
 
Al Jazeera ifanye hima kufungua ofisi huku EA.

Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa biashara za mzee mengi zinayumba kwa sana. Akifanya mchezo anapotea kabisa. Uchaguzi wa 2010 umemmaliza kabisa so lazima aipigie magoti magamba
 
duh...hatari sana....hayo ni baadhi tu ya mambo yanayofanyika hadharan...je ya chumban...kwel ccm ni chama cha majambazi
 
Huu ni ujinga kama uliofanywa na tume ya uchaguzi...walipoona wakisoma matokea kwa kufuata utaratibu Chadema wanaongoza...wakabadilisha utaratibu wakaanza kusoma maeneo ya vijijini ambapo ccm walishinda huku wakitumia muda huo kuchakachua maeneo ya upinzani....wanataka wananchi waamini kuwa wanapendwa kumbe sio....
 
huyu machache wa ITV ndiye aliyesema kina Rost utamu ni mafisadi papa na sasa anawasaidia kwa ki TV chake..manake nini kama sio unafiki mkubwa? freedom is coming today! CCM wako hoi sana na hizi ni dalili njema kwa wazaleno wa kweli
 
du..... mimi sikuelewa kinacho endelea kwani picha zilzooneshwa itv na tbc ni zilezle lakini habari tofauti .yule mdada aliesuka vizuru tshirt nyekundu na yulle mbibi alietoboa masikio ndio ushahidi inakuwaje wawepo igunga na mara wakati mmoja?hii ni muendelezo wa mipango mibovu ya ccm hata maendeleo ndio hivyo hawapo sahihi kujuwa nini waanze
 
Mliokuwepo 1995 mtakumbuka nini walikifanya hawa ITV.........Kuelekea uchaguzi mkuu.........mapicha ya mauaji ya Rwanda na kuyahusisha na kuchagua upinzani
 
ITV ni kama waislamu wa bakwata tu , kwao kutumiwa kama toilet paper ni kitu cha kawaida na hawaoni aibu nacho,kweli safari ni ndefu!!!!!
 
Kitu kama hiki nilishawahi kuona kilitumika katika mkutano wa CHADEMA wakati huo huo nikaziona katika mkutano wa CUF, wajirekebishe!!
 
Ndugu wana JF salaam toka Brussels
Nimekuwa naangalia news usiku huu na nimeona matukio 3

1.Waziri Mkuu akiwa Serengeti leo , kwenye hadhara wameonyesha watu wakimsikiliza nimeona kuna mdada alikuwa ana cheza cheza wakati wa hotuba ya Pinda na open space kati kati nikawa najiuliza kama kulikuwa na muziki ukiendelea wakati hotuba ya Pinda inarindima .

2.Nimeona Mgombea wa Chadema Igunga na habari ya Utajiri wa kijiji alichokuwa anahutubia leo .

3.Nimeona Mukama akiongea , na Komba , na Mgombea wa CCM .Nimeshangaa sana sana kuona picha ya umati ulio kuwa kwa Pinda ndiyo wale wale ambao waneonyeshwa Igunga .Kwa kweli nimeshangaa mno na kama kuna yeyote kaona habari za usiku huu tafadhali anasaidie kuelewa .Je ITV wanataka kutueleza nini ? Wana chakachukua mkutano au hawakuwa na picha za matukio ya CCM za leo au Pinda kaonyeshwa kimakosa hakuwa na watu ? Nisaidieni kuelewa am confused .

ITV ni moja ya television zilizohongwa na akina Nape kuhakikisha wanaitangaza ccm kwa mazuri
 
Mie nilidhani sijaangalia vizuri labda nilipitiwa na kausingizi, kumbe nilichokiona ni hicho hasaa!
 
Back
Top Bottom