Nimempoteza kaka

nawashukuruni sana, kwa zenu nyingi salamu
ninamsifu maulana, kunivusha muda mgumu
simanzi ilinibana, litoweka tabasamu
asanteni wana jambo,nimefarijika sana.
 
Kinyau pokea salamu zangu za ramabirambi. Pole sana kwa msiba huo, lakini kama tulivyofundishwa, kazi ya Mungu haina makosa. Tuliza mawazo yanko, jisahahulishe na msiba huo uangalie yaliyoko mbele yako.

Mola aiweke pema peoponi roho ya marehemu.
 
Pokea Pole

Mpendwa Kinyau,

Pokea pole Kinyau, kaka'ko kuondokea
Muumba msisahau, mwenywe ameamua
kumbuka pia Kinyau, kaka'ko kumuombea
Kuondokewa Kaka'ko, Kinyau pokea pole

Nasema pokea pole, kwa sala nawaombea
Punguza pia kelele, mayowe kumlilia
kumbuka mengi ya kale, kaka'ko mlotendea
Kuondokewa Kaka'ko, Kinyau pokea pole

Mapenzi yake Muumba, kaka'ko kumchukua
Hakuna cha lambalamba, mganga wa kugangua
Avuta bila ya kamba, Muumba wetu wajua?
Kuondokewa Kaka'ko, Kinyau pokea pole

Ni kwake tulipotoka, na kwake tutarejea
Nimtajaye Rabuka, aliyeumba dunia
Na kila kiloumbika, mwenyewe kakiumbia
Kuondokewa Kaka'ko, Kinyau pokea pole

Nakuagia kwaheri, ya tano nina ishia
Kinyau uwe jasiri, mama'ko asubiria
Jikaze uwe ngangari, nduguzo wahitajia!
Kuondokewa Kaka'ko, Kinyau pokea pole

Wasalaam,

Nduguyo Choveki
 
Pole sana kinyau, kwa yote yalokufika,
yaliyotokea sahau, watu yanatufika,
ni ngumu kusahau, hayo yakitufika,
mola amurehemu, kaka alotutoka
 
Kinyau pole sana kwa masaibu yalokukuta. Mola akupe faraja na subira.
Najua huzuni uliyoyano hapo kwani nami nimempoteza mwanangu wiki hii na najua uzito wa kumpoteza wa karibu yako. Mungu akusaidie Kinyau na akupe nguvu kipindi hiki
 
Ndugu Msanii,

Nawe Pole sana kwa kuondokewa na mwanao. Tuko pamoja tunakuombea upate faraja ktk kipindi hiki kigumu kwako
 
Msanii na Kinyau...
Poleni kwa kuondokewa na wapendwa wenu....Tuko pamoja katika kipindi hiki.
 
Msanii na Kinyau...
Poleni kwa kuondokewa na wapendwa wenu....Tuko pamoja katika kipindi hiki.

Ninapata faraja sana kwa kuwa nanyi ktk forums hii.
Sante sana na Mungu akubarikini ila mjue kuna kibarua kigumu ktk hospitali zetu za kulipia bongo.... kuna walakini kule na wizara ya afya wamekaa kimya ili wafe wengi
 
Pole sana kwa msiba,mungu akupe matumaini na faraja katika kipindi hiki kigumu.
 
oh Msanii pole sana ndugu yangu, Mungu amlaze mwanao peponi. Salamu za pole ziifikie familia yako.
Hakika bwana alimpenda zaidi mwanao amemwita kwake mbinguni.Pole sana.
 
poleni sana kazi ya mungu haina makosa.

ila tuamkeni na tuanza kuwashughulikia wazembe, tena tuwashughulikie kwa nguvu zote mpaka waamke
 
Lol,
msiba ni jambo kubwa. Poleni sana hatuna cha kusema manake uchungu wa msiba anaeujua mfiwa.
poleni sana tunawakumbuka katika sala ili mpate nguvu za kuendelea bila wapendwa wenu.
 
Back
Top Bottom