Nimekutana na changamoto hii nikifuatilia passport, naombeni ushauri

Habari magreat thinkers, Last week nilienda immigration kufatilia passport nikiwa na kila kitu wanachotaka kama cheti cha kuzaliwa, affidavit ya mzazi na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa, nimefanya process zote vizuri tuu ile nimeenda kwa afisa wa mwisho akawa anakagua form zangu akaona kwenye cheti changu cha kuzaliwa sehemu ya mama mzazi jina la baba yake halipo lipo jina la mama tuu tatizo likaanzia hapo nikaambiwa cheti ni fake inabidi niende RITA niombe cheti kingine cha kuzaliwa, nikasema fine nimefika RITA nikaambiwa inabidi niapply online na niambatanishe leaving certificate ya form 4 au 6 na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa. Tatizo ni kwamba leaving certificate zinaonesha nimezaliwa 1994 na nida yangu inaonesha nimezaliwa 1993 na cheti nilichoambatanisha mwanzo cha kuzaliwa immigration kinaonesha nimezaliwa 93, issue ni kwamba hata nikitafuta cheti cha kuzaliwa kingine bado kitatoka cha 94 kwasababu ya zile leaving certificate nikienda immigration wataona miaka inatofautiana na kwenye NIDA so nipo njia panda naombeni ushauri wakuu nifanyeje? mtanisamehe kwa uandishi m'bovu.
Kabadili Nida. Cha muhimu cheti cha kuzaliwa kifanane na Nida. Leaving certificates achana nazo.Sema uliishia la saba.
 
Ok, nenda mahakama ya ardhi ukaape kisha wakupe deed poll certificate.
Au nenda kwa msajili wa vizazi na vifo ukaombe cheti cha kuzaliwa 1993, kisha utalipia 10 after 7 days unaenda kukichukua.

Shukran mkuu kwa ushauri.
 
Kabadili Nida. Cha muhimu cheti cha kuzaliwa kifanane na Nida. Leaving certificates achana nazo.Sema uliishia la saba.

Cheti cha kuzaliwa ninacho mkuu ndio hicho hicho nilikitumia kupata namba za nida bila usumbufu issue ni kwenye hicho cheti cha kuzaliwa jina la baba mzaa mama(babu yangu mimi) halipo ndio maana immigration wakakikataa wanataka nikatafute cheti kingine.
 
Cheti cha kuzaliwa ninacho mkuu ndio hicho hicho nilikitumia kupata namba za nida bila usumbufu issue ni kwenye hicho cheti cha kuzaliwa jina la baba mzaa mama(babu yangu mimi) halipo ndio maana immigration wakakikataa wanataka nikatafute cheti kingine.
Kwa hiyo mama yako hana Baba?Kwa nini cheti hakina jina la Baba wa mama yako?
 
Halafu si utengeneze affidavity ya Baba.Maana uhamiaji tunapeleka affidavity ya mzazi mmoja tu.
 
Sasa kwenye cheti cha kuzaliwa Mama yako hana Baba,then kwenye affidavity yake ana Baba.Hapo haikubaliki. Ila kama Baba yako yeye ana Baba kwenye cheti cha kuzaliwa.Si upeleke Affidavity ya Baba.Maana Jina la Mzazi kwenye cheti cha kuzaliwa linatakiwa liendane na affidavity yake.
 
Affidavit ya mama niliambatanisha pia kwenye fomu mkuu ila bado wanasumbua.
Ndo kosa kubwa.Maana kwenye affidavity ana jina la Baba,kwenye cheti chako cha kuzaliwa hana Baba.Hapo Passport hutatengenezewa hata aje Yesu. Halafu uzuri Uhamiaji wanataka affidavity ya mzazi mmoja tu.Si upeleke ya Baba? AU Peleka ya Mama ila usiweke jina la Baba yake kama ilivyo kwenye cheti chako.
 
Mkuu hapo usihangaike Sana tafuta Mtu wa Rita akusaidie swala lako,

Achana na habar za leaving certificate. Swala la msingi hapo ni cheti cha kuzaliwa kitoke kikiwa na taarifa zote muhimu ,ikiwemo Hilo Jina la Babu yako (Baba ake mama ako)

Mimi pia wakati nashughulikia passport yangu cheti cha kuzaliwa cha mwanzo kilinikwamisha ,kutokana na Jina la Baba Angu kukosewa herufi moja na tarehe ya kuzaliwa kutofautiana na ya nida na driving licence

Nlichofanya kuna Mtu nlipewa no yake Kule Rita ,nkampa kiasi Fulani cha pesa akanisaidia kurekebisha cheti changu cha kuzaliwa within a week kikatoka kikiwa sawa kabisa nkaenda ku attach kwenye form za passport ,wakazipokea na passport ilishatoka

Kwa lugha rahisi ni kwamba ukipenda kufuata utaratibu kwenye kila Jambo kwa nchi yetu hii kuna sehemu either utakwama au kama sio kukwama basi utacheleweshewa mambo yako
Nchi ya kitu kidogo, nchi ya watu wadogo
 
Hiyo ni nje ya kulipia passport mkuu nilianzia stationary nikafanya application online nikapewa control no. nikaenda kulipia elfu 20 then nikaingia immigration nikapewa tena control no. nikaenda kulipia laki na 30 jumla 150k hiyo ndio gharama ya passport ya halali, hiyo laki na 30 nilimpa ofisa ili anifanyie mchongo.

😂😂
Ulimpa Rushwa sio??

Ni muhimu documents zako zifanane hata kama hufuatilii Jambo lolote lile.
 
Nchi hii bila Rushwa Mambo hayaendi. "RUSHWA NI ADUI WA HAKI" Wakati wewe unahangaika kwenda RITA etc Kuna mtu hapo katoa elfu 50 tu haulizwi hata swali ..fomu inapitishwa fasta anasubiria kupigwa picha ....
 
Back
Top Bottom