Nilitaka kumpiga makofi Afisa wa uhamiaji

Restless Hustler

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
4,744
18,002
Kwa muda mrefu Nilikuwa nasikia kwamba Maafisa Uhamiaji wengi ni wababaishaji, Leo nimeshuhudia kwa macho.

Nilijaza fomu la maombi ya passport online Nikalipia kisha nika download na kuwasilisha Ofisi za uhamiaji mkoa.

Afisa Aliyenipokea akaniuliza wewe ni kabila gani? Nikamuambia Maasai. Akaniuliza, Sasa Maasai utatoboa kweli? Nikamkazia uso🤨

Akaanza kukagua majina na attachments akaniuliza cheti cha kuzaliwa baba nikamuambia alifariki. Akaniambia cheti chake cha kifo Kiko wapi nikamchomolea.

Akaniuliza namba yake ya NIDA Iko wapi? Nikamuambia mtu aliyefariki mwaka 1996 namba ya NIDA inapatikanaje? Akaniambia ndiyo utaratibu uliopo. Nikashindwa kumuelewa🙄

Akaniambia anataka kitambulisho Cha mama, nikamuambia nimeambatanisha barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa mtendaji na kuna namba yake ya ya NIDA kwenye hiyo barua.

Akasema anataka cheti cha kuzaliwa, nikamuambia Kuna Affidavit hapo akasema affidavit siyo cheti.

Hapo ndipo nikajua jamaa ni mpumbavu, nikamuambia kwahiyo mlipoweka kwenye tovuti yenu kuwa affidavit ni mbadala wa cheti cha kuzaliwa, mlikuwa mnatania?

Tukaanza kurushiana maneno nikataka kumpiga makofi akatokea dada mmoja(Afisa mwenzake) Akaniambia samahani kaka naomba nikusikilize. Nikamueleza scenario yote, akakagua fomu na attachments zangu na kuniambia viko sawa niondoke, nitapigiwa simu.

Nikaondoka hatua chache, nikawaza kuwa hawa jamaa wameshaonesha negative attitude, Kuna uwezekano hawatatuma fomu langu makao makuu. Nikarudi nikawaambia wanipe fomu langu nikapokea na kuondoka nalo. Nitaenda likizo hivi Karibuni nitafanyia hili zoezi mkoani kwetu. Ila kumbe Maafisa Uhamiaji wengi ni wapumbavu.
 
Thubutuuu ungejaribu kunipiga uone karateka zangu, unadhani me mnyonge. Tangu umekuja ofisini nakuhudumia nikaona kama una madhereu hivi nikasema huyu mtu hatoboi leo kwangu, hata yule dada aliyechukua fomu zako ni mke wangu bahati yako machale yalikucheza. Fomu zako tungeenda kuwapa watoto wetu nyumbani wajifunze kutengeneza tiara.
 
''Sasa maasai utatoboa kweli?''

Hii kauli ni ya kibaguzi sana Prejudice, Kwani Maasai sio wananchi? Hawastahili Passport?

Mkuu huyo jamaa muweke wazi ili wahusika wadeal nae, siku nyingine uwe unarekodi kwa siri au japo urekodi sauti tu,kwa ushahidi wa tukio husika,

Pole sana Mkuu.
 
Kwa muda mrefu Nilikuwa nasikia kwamba Maafisa Uhamiaja wengi ni wababaishaji, Leo nimeshuhudia kwa macho.

Nilijaza fomu la maombi ya passport online Nikalipia kisha nika download na kuwasilisha Ofisi za uhamiaji mkoa.

Afisa Aliyenipokea akanuliza wewe ni kabila gani? Nikamuambia Maasai. Akaniuliza, Sasa Maasai utatoboa kweli? Nikamkazia uso

Akaanza kukagua majina na attachments akaniuliza cheti cha kuzaliwa baba nikamuambia alifariki. Akaniambia cheti chake cha kifo Kiko wapi nikamchomolea.

Akaniuliza namba yake ya NIDA Iko wapi? Nikamuambia mtu aliyefariki mwaka 1996 namba ya NIDA inapatikanaje? Akaniambia ndiyo utaratibu uliopo. Nikashindwa kumuelewa

Akaniambia anataka kitambulisho Cha mama, nikamuambia nimeambatanisha barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa mtendaji na kuna namba yake ya ya NIDA kwenye hiyo barua.

Akasema anataka cheti cha kuzaliwa, nikamuambia Kuna Affidavit hapo akasema affidavit siyo cheti.

Hapo ndipo nikajua jamaa ni mpumbavu, nikamuambia kwahiyo mlipoweka kwenye tovuti yenu kuwa affidavit ni mbadala wa cheti cha kuzaliwa, mlikuwa mnatania?

Tukaanza kurushiana maneno nikataka kumpiga makofi akatokea dada mmoja(Afisa mwenzake) Akaniambia samahani kaka naomba nikusikilize. Nikamueleza scenario yote, akakagua fomu na attachments zangu na kuniambia viko sawa niondoke, nitapigiwa simu.

Nikaondoka hatua chache, nikawaza kuwa hawa jamaa wameshaonyesha negative attitude, Kuna uwezekano hawatatuma fomu langu makao makuu. Nikarudi nikawaambia wanipe fomu langu nikapokea na kuondoka nalo. Nitaenda likizo hivi Karibuni nitafanyia hili zoezi mkoani kwetu. Ila kumbe Maafisa Uhamiaja wengi ni wapumbavu
Hao jamaa nawachukia Sana bila rushwa utoboi
 
Back
Top Bottom