Nimekoma jamani! Hiki chumba ni balaa tupu

Kwa mfano kama huyo rafiki yako aliyekukirimu ni member humu na anasoma huu udhalilishaji unaomfanyia hapa?

Kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo.

**** na Ovyooo!
Mkuu usitumie lugha kali sababu hii hali haijakukuta. Kwangu imekuwa jambo la ajabu maishani maana sijawahi kukesha kutokana na hali mbaya ya chumba. Kiafya tunashauliwa walau tulale saa sita kwa siku, je hii ya kukesha kwako unaona poa tu!
 
Hiko chumba kina pepo wabaya sana aka majini...muombe sana Mungu wako.
 
Bure ghali Mkuu...Pole sana...Sasa utunge story ya kumridhisha mwenyeji wako kwanini unataka kuhamia hotel....au kama huoni noma mwambie tu kwamba panya na mbu wa humu ndani siwawezi kabisa...sikulala usiku kucha.
Hapa nilisha peki vitu vyangu. Nasubiri aamke nikamuage.
 
Mkuu acha mazarau hio mifugo ktk familia za kwetu ni kawaida sana au umezaliwa peponi mwezetu?
 
KWa waafrika na Tanzania nadhani kukaribishana ni jadi. Na mtu hujiona umeheshimiwa endapo mtu anakubari kukaa kwako. Nyakati nyingine huwa tunasahau vyeo, ukwasi tuliokuwa nao kwa kuwa huwa tunatanguliza kuheshimu ukarimu uliooneshwa kwetu.Ukisema umchane live....nahisi wewe si muungwana. Pengine alitamani mkae pamoja mpige stori pamoja. Kumchana live sio sahihi, na ukisema unaenda hoteli kwa sasa itabidi uwe na sababu kubwa otherwise aga kuwa unarudi/unasafiri ndo uende hoteli.
Mkuu wala sijamdhalilisha na bado nasema huo ndiyo uwezo wake lakini kumbuka hapo awali nilimwambia anitafutie hotel nzuri. Neno hotel nzuri linatosha yeye kujua ni aina gani ya chumba nilikimaanisha. Na isitoshe alikuwa na nafasi ya kunionyesha chumba mapema kabisa na kuniuliza kama kingenifaa kuliko kusubiri mpaka muda wa kulala.
 
ungeamua 1 ukimbizane na hao panya mcheze KOMBOLELA haki kukuche, kuliko kukesha na mwawazo hadi asubuh
 
Nimekuja zangu kikazi katika mji huu jina kapuni. Baada ya kufika nikapokelewa na rafiki yangu. Tukiwa standi, nilimwambia anisaidie kutafuta hotel nzuri ya kulala na yeye akajibu nisiwe na shaka nitaenda kulala nyumbani kwake. Basi tukaenda hadi nyumbani kwake na baada ya mazungumzo akanipeleka kwenye chumba nitakacholala. Tukatakiana usiku mwema na yeye kwenda kulala chumbani kwake. Mimi baada tu ya kuzima taa ndipo balaa lilipoanza. Chumba kimejaa panya sijawahi ona! Panya vurugu mtindo mmoja hadi wanataka kunitafuna miguu. Zaidi ya hapo, chumba kimejaa mbu japo kuna neti lakini kelele za mbu huwezi kulala hata uwe umelewa vipi. Sasa najiuliza hivi huyu rafiki yangu amenifanyia makusudi au ni ukarimu tu maana hapa natamani niende nikalale ndani ya gari.
Niukarimu wake na kukuthamini kama mtu wake wakaribu kaona haina haja ya wewe kulala hotel wakati nyumba iko,
lakini wewe umezowea kufikia 5star hotel sio? sasa basi nadhani utakua unaujua uwezo wa mwenzio kama hakai uzunguni
ungemwambia umesha fanya Reservation yeye akupeleke tuu kuliko kujishau hapa mbu eeee mbu kama vile hujawahi kuwaona tangu uzaliwe,Panya eeeeee panya ebu jikaze mtoto wakiume wewe wacha ubishoo.....
 
Mkuu naturally tuna culture moja, we dont observe trends

ikitokea umehamia nyumba ikaanza kuwa na mende mara nyingi huwa hatuoni hadi wanapoanza kupita sebuleni wakati mnakula au kusali, na wakati mwingine pia hiyo hamuoni mwisho wanahamia panya, mwisho inakua a house of rodents, ndivyo hali ilivyo

cha maana ni kutoa ushauri wa usafi au hata kusema madhara in a friendly way

wenye nyumba wana tabia ya kudharau hoja za wapangaji, lakini ni jukumu la mpangaji kuishi sehemu safi

Oh yeah na ikabidi rafiki yangu ahame na kumuachia kodi yote ya mwaka mzima .akatafuta nyumba na kulipa upyaaa na kumuachia kodi ya mwaka mfuga panya na mende.
 
Je, Mkuu mambo hayo yangekutokea kijijini kwenu kwenye nyumba ya wazazi wako au jamaa zako ungesema nini!
 
kama mna urafiki wa kweli, basi mweleze rafiki yako wazi nini kimekusibu na kisha mshauri namna ya kuondoka na viumbe hao. Unajua mara nyingine huwa hatufahamiani vizuri na wale tunawaita marafiki zetu mpaka pale tunapokaa jirani sana. Si ajabu hicho chumba huwa haingii na wala hajui kina vurugu na hekaheka za usiku, na pengine pia anafahamu lakini kwake as long kuna net anajua upo salama. Vunja ukimya...sema nae! utamsaidia hata yeye.

Na ili uwe na amani tafuta hotel mwenyewe maana kesho hukawiii kutueleza tena ...jamaa kanipeleka kwenye hotel hiyo! Bafu lipo nje kwa foleni na ndoo chafu ile mbaya. Uzuri ni relative term.
 
Nimekuja zangu kikazi katika mji huu jina kapuni. Baada ya kufika nikapokelewa na rafiki yangu. Tukiwa standi, nilimwambia anisaidie kutafuta hotel nzuri ya kulala na yeye akajibu nisiwe na shaka nitaenda kulala nyumbani kwake. Basi tukaenda hadi nyumbani kwake na baada ya mazungumzo akanipeleka kwenye chumba nitakacholala. Tukatakiana usiku mwema na yeye kwenda kulala chumbani kwake. Mimi baada tu ya kuzima taa ndipo balaa lilipoanza. Chumba kimejaa panya sijawahi ona! Panya vurugu mtindo mmoja hadi wanataka kunitafuna miguu. Zaidi ya hapo, chumba kimejaa mbu japo kuna neti lakini kelele za mbu huwezi kulala hata uwe umelewa vipi. Sasa najiuliza hivi huyu rafiki yangu amenifanyia makusudi au ni ukarimu tu maana hapa natamani niende nikalale ndani ya gari.

Bure ghali mkuu
 
Pole sana, ila amkufanyia hivyo kwa nia njema ya kusave vijisenti
 
Je, Mkuu mambo hayo yangekutokea kijijini kwenu kwenye nyumba ya wazazi wako au jamaa zako ungesema nini!
Malazi, Chakula na Mavazi ni vitu ambavyo jumuhiya ya kimataifa inatambua kuwa ni basic needs kwa binadamu. Ni sawa na kuniuliza nikimuona mtu anatembea utupu wa mnyama nitasemaje. Jibu ni kwamba nitashangaa.
 
ungeamua 1 ukimbizane na hao panya mcheze KOMBOLELA haki kukuche, kuliko kukesha na mwawazo hadi asubuh
Chumba kilivyojaa maboksi na makoro koro mengine, ukiinuka tu kitandani panya na wenyewe wanapotea.
 
Nimekuja zangu kikazi katika mji huu jina kapuni. Baada ya kufika nikapokelewa na rafiki yangu. Tukiwa standi, nilimwambia anisaidie kutafuta hotel nzuri ya kulala na yeye akajibu nisiwe na shaka nitaenda kulala nyumbani kwake. Basi tukaenda hadi nyumbani kwake na baada ya mazungumzo akanipeleka kwenye chumba nitakacholala. Tukatakiana usiku mwema na yeye kwenda kulala chumbani kwake. Mimi baada tu ya kuzima taa ndipo balaa lilipoanza. Chumba kimejaa panya sijawahi ona! Panya vurugu mtindo mmoja hadi wanataka kunitafuna miguu. Zaidi ya hapo, chumba kimejaa mbu japo kuna neti lakini kelele za mbu huwezi kulala hata uwe umelewa vipi. Sasa najiuliza hivi huyu rafiki yangu amenifanyia makusudi au ni ukarimu tu maana hapa natamani niende nikalale ndani ya gari.

pole sana.
 
Kuna dada mmoja yuko maliasili na utalii anatafuta mchumba. Siku alimpata yule mume mtarajiwa akomba waende wote likizo kujitambulisha. Kufika ukweni yule dada mila na desturi zilimshinda akatoroka. Sasa anatafuta tena mchumba. VUMILIA NDG YANGU WEMA WAKE USIMPONZE KWA WEWE KUMUUMBUA ETI NYUMBA YAKO INAPANYA
 
Back
Top Bottom