Nimegundua wasanii wengi ni watoto wa single mothers; kama ni kweli why?

viongozi wa dini wanasemaje??

Na kipi kinakwepa kusemwa labda nitaelewa zaidi.
hii topic ni veru touchy
watu wameichukulia very personal i guess
na kama ukisikiliza viongozi wa dini wanavyosema
kuna kitu very deep hapa kinakwepa kuzungumziwa
 
ni familia ngapi ambazo baba anakuwa soft kuliko mama?

Hujawahi kutana na mtu anasema 'sijawahi chapwa na baba' na baba alikuwa rafiki kuliko mama?

Je usichoweza wewe inawakilisha wanawake wote au asilimia kubwa??

Bora The Boss umeiangalia kwa jicho la tatu.

Unajua mtu unaweza ukapitia kitu kama kulelewa na mama peke yake...kikakufanya uwe hivyo ulivyo lakini usijue sababu ilokufanya uwe hivyo ulivyo.

Mimi ndio maana napenda sana kusoma saikolojia ingawa si field yangu ili nijue mapungufu yangu niyafanyie kazi.

Na nimegundua kuwa as a woman nina ka usoftness fulani...japo watu unambia mi mkali.

Sasa pale napokuwa irrational (kwa sababu niko too emotional) mzee anakazia basi kijana anakuwa kwenye mstari.

Nafikiria ningeweza vipi kuwalea hawa kina nanii bila baba yao...japo kiuchumi I can take care of any size of extended family. As a head of a household. Lol
 
pinkmousse, umeongelea stigma kwa mtoto wa single parent, stigma gani hiyo uliyoipata kama utakuwa tayari kushare?
 
Last edited by a moderator:
The Boss, mtoto yeyote mzazi wake huwa ndio role model.

Sishangai mtoto wa porn star kuwa porn star ihusishwe na u-single mother? Au single father?

Mfano, mzazi wangu ni engineer wa umeme, nilianza penda kazi ya umeme tangu la kwanza, na nilipenda physics na maths simply bcoz na ndoto ya kuwa engineer kama mzazi.

Kwa nini iwe ajabu kwa porn star? Au kwa mtoto wa single parent kupenda kazi ya mzazi anayemlea?

Capital, hao akina baba wa ku-enforce law and order umewapimaje?? Hakuna mababa bushoke? Soft hata anaweza chomwa kidole jichoni na mtoto?

Ili nizunguze uelewe
kwanza tenganisha
Ulaya na Africa
kuna cultural differences nyiingi mno

Mfano in Eurpoe mtu anaweza amua tu kuwa
nitahitaji mtoto na akaenda kwenye sperm bank
kwetu haipo hiyo

kiafrica bado mfumo dume upo saana
Baba ndie kiongozi wa familia
asipokuwepo ni sawa na kusema familia haina kiongozi
 
viongozi wa dini wanasemaje??

Na kipi kinakwepa kusemwa labda nitaelewa zaidi.

Kuna somo moja alitoa Mwakasege
kuhusu mzaliwa wa kwanza
sijui unakumbuka?
na sisemi kila kinachozungumzwa na wachungaji au viongozi wa dini ni sahihi asilimia 100
ninachosema ni kuwa wanachangia mitazamo ya jamii sana
 
pinkmousse, umeongelea stigma kwa mtoto wa single parent, stigma gani hiyo uliyoipata kama utakuwa tayari kushare?

unaambiwa kabisa live live au saa nyingine unasikia kwa bahati mbaya kwamba unatoka nyumba iliyovunjika,nilikuwa nawashangaa sana najisemea kimoyomoyo kama ni hivyo mbona watoto wenu wa nyumba kamili siwaelewi pia kwa sababu kama shule na mambo mengine nafanya vizuri kuliko hao 'kamili',nilikuwa kama nakabeef nao kwa hiyo nahakikisha naexcel kwenye mambo yangu just to make my mama proud na kuwaprove wrong,yani hilo neno nyumba iliyovunjika lilikuwa linanikera kweli
 
kila kitu ni kwa mtizamo unaoamua kuchukulia.

Familia iwe ya single mom, single father au wazazi wote, kama ni goi goi lazima watoto wapinde.

Na sijaona kama kuwa msanii ni kwamba mtu amefeli kihivyo.

Na napima ukuaji wa mtu kulingana na alivyoweza kujikwamua kutoka zero to hero.

Kama watoto wa wazazi wote wana facilities zote na bado wanaishia kuwa watu wa kati, basi wasanii wamepiga hatua zaidi toka maisha duni hadi ku-run miji.

Suala la risk route, ni nini sio risk kufanya?? Na risk hii tunaiangalia kwa angle gani? Maana hata biashara tu ina risk ya kukata mtaji, shule ina risk ya kufeli.

Sijaona nini kinajaribu kuelezwa hapa.

Kimsingi hapa unaweza kukuta watu wanazungumzia vitu viwili tofauti
mfano success unayozungumzia wewe probably ni material zaidi
sasa kuna wengine wanazungumzia success kivingine zaidi
labda 'furaha zaidi'
 
pamoja na mfumo kutawala afrika, bado sikubaliani na dhana kuwa familia kukosa baba ni sawa haina kiongozi.

Inategemea na msimamo tu wa anashikilia familia hiyo baada ya baba kuondoka.

Ndio maana kuna baadhi ya familia zina baba na mama lakini bado watoto hawajafanikiwa hata kufikia rank ya usanii.
kiafrica bado mfumo dume upo saana
Baba ndie kiongozi wa familia
asipokuwepo ni sawa na kusema familia haina kiongozi
 
unahisi watoto wa single parent hawana furaha zaidi??

Kimsingi hapa unaweza kukuta watu wanazungumzia vitu viwili tofauti
mfano success unayozungumzia wewe probably ni material zaidi
sasa kuna wengine wanazungumzia success kivingine zaidi
labda 'furaha zaidi'
 
pamoja na mfumo kutawala afrika, bado sikubaliani na dhana kuwa familia kukosa baba ni sawa haina kiongozi.

Inategemea na msimamo tu wa anashikilia familia hiyo baada ya baba kuondoka.

Ndio maana kuna baadhi ya familia zina baba na mama lakini bado watoto hawajafanikiwa hata kufikia rank ya usanii.

Wewe unazungumzia familia ambazo mama ana MBA i guess
hebu tazama familia ambazo mama ni wa kijijini kabisa
hata darasa hakuliona
halafu uone watoto walikuwaje?
hasa kama hawakubahatika na elimu ya bure ya seerikali..
 
unahisi watoto wa single parent hawana furaha zaidi??

Labda nikujibu hivi

mtu kuwa msanii huwa na msukumo wa kiana fulani hivi
kutoka moyoni
kuna msemo unasema
all artists are insecure.....
sasa kutoka kwenye single parent kunaleta insecurities fulani
sio kwa wote,but mostly...
so baadhi ya hizo insecurities huweza ku zi channel kwenye creative works zao za kisanii
mfano utunzi.uimbaji wa hisia na kadhalika

watoto wa wazazi wawili,huwa hawana insecurities hizo
ndo maana sio high achievers sana

hizi insecurities hum push mtu ku achieve pia zaidi
mfano Obama na wengineo
 
kitu kimoja mie nimejifunza.

Kitu muhimu kwa mtoto ni kumfundisha kuwa proud ya yeye alivyo na mazingira anayoishi, period.

Hujawahi kutana na watoto enzi za shule wanasema uongo labda kwetu tuko hivi au vile kitu ambacho ni kinyume kabisa na hali halisi??

Inaonesha kuna familia zinalea watoto kwa kutowafundisha kujikubali na kufurahia wao walivyo.

Na je unadhani usingekuwa mtoto wa familia iliyovunjika kusingekuwa na kitu kingine cha kukukera??

Ngoja nikupe mfano: mie nilikuja gundua darasa la saba, wasichana wote wamejiunga na kwenda kujisomea shule bila mie kualikwa eti kisa wanitoe kwenye nafasi yangu. Nilijisikia vibaya maana sikujua kama ile nafasi ingeweza sababisha mie watu waunde syndicate ya kunisomea.

Nilijisikia kutengwa lakini sikutilia maanani hasa nilipoona na rafiki yangu kashiriki na kuja kuniambia baada ya kama wiki 2.

Haya ya kunyanyapaa, kutengwa yapo tu kama si lile ni hili.

unaambiwa kabisa live live au saa nyingine unasikia kwa bahati mbaya kwamba unatoka nyumba iliyovunjika,nilikuwa nawashangaa sana najisemea kimoyomoyo kama ni hivyo mbona watoto wenu wa nyumba kamili siwaelewi pia kwa sababu kama shule na mambo mengine nafanya vizuri kuliko hao 'kamili',nilikuwa kama nakabeef nao kwa hiyo nahakikisha naexcel kwenye mambo yangu just to make my mama proud na kuwaprove wrong,yani hilo neno nyumba iliyovunjika lilikuwa linanikera kweli
 
kwa nini uone ni insecurities??

Kwa nini usiseme wana inner drive 'achievement'?

Au kuna baadhi ya watu wanaamua kuwa creative sababu hawawezi kukaa kwenye formal institution zenye uongozi 'free spirit'?

Labda nikujibu hivi

mtu kuwa msanii huwa na msukumo wa kiana fulani hivi
kutoka moyoni
kuna msemo unasema
all artists are insecure.....
sasa kutoka kwenye single parent kunaleta insecurities fulani
sio kwa wote,but mostly...
so baadhi ya hizo insecurities huweza ku zi channel kwenye creative works zao za kisanii
mfano utunzi.uimbaji wa hisia na kadhalika

watoto wa wazazi wawili,huwa hawana insecurities hizo
ndo maana sio high achievers sana

hizi insecurities hum push mtu ku achieve pia zaidi
mfano Obama na wengineo
 
kwa nini uone ni insecurities??

Kwa nini usiseme wana inner drive 'achievement'?

Au kuna baadhi ya watu wanaamua kuwa creative sababu hawawezi kukaa kwenye formal institution zenye uongozi 'free spirit'?

Sio mimi ninaoita hizo ni insecurities
ni wataalam
so wewe unaweza kuita inner drive
but wataalam wanasema ndo inner securities zenyewe
nimekupa mfano wa Obama hapo
 
kitu kimoja mie nimejifunza.

Kitu muhimu kwa mtoto ni kumfundisha kuwa proud ya yeye alivyo na mazingira anayoishi, period.

Hujawahi kutana na watoto enzi za shule wanasema uongo labda kwetu tuko hivi au vile kitu ambacho ni kinyume kabisa na hali halisi??

Inaonesha kuna familia zinalea watoto kwa kutowafundisha kujikubali na kufurahia wao walivyo.

Na je unadhani usingekuwa mtoto wa familia iliyovunjika kusingekuwa na kitu kingine cha kukukera??

Ngoja nikupe mfano: mie nilikuja gundua darasa la saba, wasichana wote wamejiunga na kwenda kujisomea shule bila mie kualikwa eti kisa wanitoe kwenye nafasi yangu. Nilijisikia vibaya maana sikujua kama ile nafasi ingeweza sababisha mie watu waunde syndicate ya kunisomea.

Nilijisikia kutengwa lakini sikutilia maanani hasa nilipoona na rafiki yangu kashiriki na kuja kuniambia baada ya kama wiki 2.

Haya ya kunyanyapaa, kutengwa yapo tu kama si lile ni hili.

I agree, mimi nilijifunza kukubali maisha na kuyafurahia nikiwa mdogo sana,yani unyonge unyonge niliukataa kabisa na niliamini mpaka leo naamini kwamba in life not everything is perfect na kwamba kama kuna vitu vinamiss unakubali,unajifunza,na unaendelea,mpaka leo hii naweza kutwa na kitu nikawa mwepesi kucope mpaka mtu anashangaa mbona hushtuki, umenchekesha ulivyoenda kusomewa,mie nilikuwa naambiwa huyu naye kila mahali yumo tu hachoki maana michezo,kuimba,darasani kote kulihusu maana nilikuwa chautundu flani
 
Hizo stigma hizo ndio zinaweza mfanya mtoto ajue jamii ina expect less from them...sasa mpaka awe na akili kuwa anatakiwa kuwa prove wrong...wengi wanaishia ku prove right.

Lakini stigma is just part of it...single motherhood ni kazi na ukikubali hilo unaweza ku deal na challenge zake kuliko kuukana ukweli.
 
unadhani malezi ya wazazi wawili ni marahisi kivile?? Hakuna challenge??

Na ni nini kisicho na challenge hapa duniani??

Mi naona ni 'strength' ya akili ya mtu zaidi.

Hizo stigma hizo ndio zinaweza mfanya mtoto ajue jamii ina expect less from them...sasa mpaka awe na akili kuwa anatakiwa kuwa prove wrong...wengi wanaishia ku prove right.

Lakini stigma is just part of it...single motherhood ni kazi na ukikubali hilo unaweza ku deal na challenge zake kuliko kuukana ukweli.
 
Comment yako iko makini sana. Nadhani hapa kuna fundisho kwa single mothers na single mothers to be.

Naona mama yako alitambua challenge ya kulea watoto peke yake, na akaamua kuwa inabidi a play double role; ya umama na ubaba. Alikuwa anaweza toa amri mkafuata ...labda alikuwa mkali au alikuwa na watoto wasikivu...wanasema ana bahati.

Mimi mwenyewe wazazi walitngana lakini nilikuwa mkubwa kidogo; form one, na nilikuwa last but one; hivyo nilikuwa na wakubwa zangu kibao wanaojitegemea except mimi na mdogo wangu.

Ila hatukueda kuishi kwa mama...tulilelewa na baba; na mpaka leo anajisifu kwa kuweza kutulea vema akiwa peke yake. Hakuwa mkali na hajawahi hata kunipiga kofi ila ana speak with authority...na alikuwa hachoki kutukanya kuhusu maisha yetu mpaka ikawa wimbo. Na kwa kuwa tulikuwa tunampenda sana...he was the last person we wanted to dissapoint.

Sikuwahi feel stigmatized. Wala sijawahi kuwazia. Labda kwa kuwa nilikuwa naishi na baba si mama.

Ila cha hajabu mama toka aachane na baba alianza kuwa mpole hajabu. Alikuwaga mkali sana alipokuwa home. Nadhani tungekaa nae tusingekuwa hapa tulipo; maybe yes maybe not.

Sina uhakika ila inawezekana. Kuwa mtoto wa single mother unadeal na mengi,kukosa emotional attachment ya mzazi mwingine,stigma, na mengineyo. Sisi tulikuwa tunaambiwa shule kwanza hivyo vipaji vingine baadae,sana sana alichofanya alikuwa anahimiza tushiriki michezo,maigizo,kwaya shuleni au kanisani ili tuenjoy vile vipaji vyetu vingine. Pia kuhakikisha tulikuwa na routine ambazo tunazifuata kila siku. Vile vile tulimwona yeye kama role model kwa sababu alikuwa anafanya kazi kwa bidii na active kwenye community. Mpaka leo hii nashangaa aliwezaje peke yake mpaka wote wanne tukawa poa kwa sababu baada ya kupata watoto naona jinsi malezi yalivyo ni kazi sana. Nilikuwa naona anavyochoka pia kulea peke yake,sio kazi rahisi hata kidogo na asingekazia msuli sijui... Malezi ni kusaidiana,ingawa ikitokea bahati mbaya inabidi usichoke hata robo. Ngoja niishie hapa maana haka katopic kanagusa kweli
 
Nakubaliana na wewe asilimia 150.

Tunakuwa na descipline mara nyingi sababu ya fear. Iwe ni kumuogopa Mungu au mzazi. Sasa kama huna wa kumuogopa unategemea nini...ndio yale wazaramo wanasema namwaga radhi...ananjua nani.

Imagine unakuwa na mama ambaye kila baada ya miaka kadhaa anawa introduce new 'uncle'. Ukiwa mdogo marafiki wanakuuliza huyu nani? Inakuwa rahisi kuwajibu 'uncle'. Ukikua unagundua kuwa mama anabadili partners...unaanza kuona noma, unaanza kuonea aibu kuwa kwenye familia ulonayo.

Wengine wanaamua kutumia madawa kuua soo au ku replace feelings za rejection; wengine wana take advantage ya situation wakijua chochote ntakachofanya mama hana authority ya kunikemea. Ushaona binti anatukanana na mama yake? Wengi ni mabinti wa single mothers.

Wamama, kama walivyo wababa, kila upande una kasoro linapokuja suala la malezi ya watoto. mama akiwa sole parent, na baba likewise, kuna tatizo. kwa vile watoto wengi hujikuta wakiishi na mama endapo, kwa sababu yoyote baba hayupo. kama nilivyosema awali, kazi ya baba ni ku-enforce 'law and order', kitu ambacho kina mama wengi hawana au wanatake for granted. ndo maana 'watoto wa mama' kwanza hawana discipline, haijalishi kwao ni maskini au tajiri. hapa sitaki kusema kuwa wasanii ni watu wasio na discipline, ila wengi wao ni careless, hawana values. hii ni kutokana na backgrounds zao. wasanii wengi wanafanana katika jambo moja au jingine, mfano ngono na ulevi.

hitimisho: uwezekano wa watoto kukosa discipline au values na hatimaye kuwa wasanii ni mkubwa kwa waliolelewa na mama pekee kuliko kwa waliolelewa na baba na mama.

tujadili.
 
Back
Top Bottom