Nimegundua wasanii wengi ni watoto wa single mothers; kama ni kweli why?

Jamani sijafanya research na hata ningefanya kwa kutumia methodology gani bado ingekuwa ni estimation tu...ndo maana nikasema wengi...by just observing.

ratio ya watu ambao hawaja-make it in life ikoje?

Wale wa single mom na both parent?
 
msanii anayeingiza kipato halali kaharibikiwa??

Drgba? Messi? Kaka? Desel? Jay Z?
For me nimesema kitambo kuwa USANII NI FANI,na ni positive in terms of life,AND NILISEMA KUWA USANII HAUNA RELATION NA U SINGLE MUM
 
Yawezekana ni kweli. katika mfumo ambao family ime-collapse na mama akawa mhimili, watoto huanza kukosa enforcement (toka kwa baba) na mwelekeo wao huwa ni katika mambo yaliyopinda, mambo ya kisanii na mwishowe huwa wasanii. mifano iko tele. wamarekani weusi walioko kwenye sanaa wengi wao hawana baba wa kueleweka.
Mambo ya kisanii ni mambo yaliyopinda? Unataka kusema ni mambo ya ovyo, au? Siamini kama sanaa ni mambo ya ovyo kiasi cha kuona kwamba wanaoifuata ni watu waliopotoka au wamepinda njia. Chukua sanaa katika uchanya wake kwani inaonya, inafundisha, inaburudisha, nk. Hayo yote ni mema.
 
Thanks. Nimekupata.

Haya ndio majibu hata kama si sahihi ni plausible.

Sasa wengine wanataka watengeneze maswali yao afu ndio wajibu...lakini ndo tulivo wabongo...swali lajibiwa kwa swali. Lol.

Kina mama kwa hulka yao ni watu wenye sentiments nyingi. Kwa sababu hiyo, nadhani sitakosea nikisema kwamba kina mama kwa hulka yao ni artists. Angalia walivo na uwezo wa juu sana katika kupamba, kuweka order ndani ya nyumba, kuongea, kubuni vitu (creativity), nk. Watoto waliolelewa na mama tu ni watoto wanaochukua mengi kutoka kwa mama ikiwa ni pamoja na hizo sentiments za ndani ya mtima, yaani uwezo wa kuona, kueleza kisanaa jambo au mambo.
 
Thanks kwa mchango wako.

Kweli wasanii wengi wana make it in life.

Ila kuna wengi wanao potelea njiani kuelekea kwenye usanii...wengine wanaishia kugawa uroda, wengine wanaishia kuwa wavuta bangi...lakini focus yao ilikuwa wawe wasanii.

Usanii ni fani lakini ni fani ngumu sana kwa kuwa chance ya kutoka ni ndogo ukilinganisha na kufuata mfumo mwingine wa maisha ndio maana labda wababa wengi hawataki kusikia mtoto analeta stori za 'nataka kuwa msanii.'
Kulelewa na mama tu hakumfanyi mtu kuwa mvuta bangi au malaya. Hizo ni tabia za mtu ambazo anaweza kujifunza si lazima awe nyumbani kwa mama bali hata shuleni, na makundi ya vijana. Kuna vijana wengi ninawafahamuu wenye kukaa na wazazi wao wote lakini ni wa wavuta bangi, watumia madawa ya kulevya, nk. Tafadhali tusiwe na prejudice na hawa vijana. Kwa mawazo yangu, na ninasisitiza, wanakuwa wasanii kwa sababu they want to be like their mothers who are naturally artists. Na unakuta baadhi yao wana elimu nzuri tu.
 
Wale wanaokuwa kwenye mchakato wa kuwa wasanii afu wakapotelea njiani...wanakuwa kina nani?

Wale wanaopanga foleni kwa Madam Ritha na hawakuchaguliwa wanaenda fanya kazi gani?

Ndio maana kama umenisoma nimesema ni risk route to take na wazazi wengi kama ni their wish wangependa watoto wao waende shule si kutegemea kutoka kupitia usanii.

Mfano mzuri ni wasanii wa Nigeria na Ghana majority ni graduates. Na ukiwauliza wanasema ni wazazi wao waliowaambia elimu ni security wasome kwanza usanii baadae...ili wasipotoka wawe na option.

Ulishawahi wauliza hao wavuta bangi wanataka kuwa nani maishani? Nina uhakika watakwambia tunataka kuwa kama Bob. marley...wasanii.

Kwa kuongezea tu atueleze wengi wa ngapi? Ukilinganisha na walolelewa na wazazi wote wawili kuna tofauti ya "wengi" kiasi gani

Ooooh yeah, hii ni soga si utafiti kwa hiyo wengi jazia wewe idadi unayotaka :]
Kwa kumsaidia mleta mada (kwa sababu naamini conclusion yake) labda ungepitia study hii Statistics « The Fatherless Generation.

Sports na music bado sijaona sababu ya kurelate na fatherlessness ila kuna article hii inayoonyesha watoto waliolelewa na single mothers wana uwezekano mkubwa wa kuwa successful kwenye "self-paced" activities kama sports, arts na music. more than academics (which is more instructional)
Comparison of Black and White Boys' Performance in Self-paced and Reactive Sports Activities - Dunn - 2006 - Journal of Applied Social Psychology - Wiley Online Library
 
Wale wanaokuwa kwenye mchakato wa kuwa wasanii afu wakapotelea njiani...wanakuwa kina nani?

Wale wanaopanga foleni kwa Madam Ritha na hawakuchaguliwa wanaenda fanya kazi gani?

Ndio maana kama umenisoma nimesema ni risk route to take na wazazi wengi kama ni their wish wangependa watoto wao waende shule si kutegemea kutoka kupitia usanii.

Mfano mzuri ni wasanii wa Nigeria na Ghana majority ni graduates. Na ukiwauliza wanasema ni wazazi wao waliowaambia elimu ni security wasome kwanza usanii baadae...ili wasipotoka wawe na option.

Ulishawahi wauliza hao wavuta bangi wanataka kuwa nani maishani? Nina uhakika watakwambia tunataka kuwa kama Bob. marley...wasanii.
Kupotelea njiani hakutokani na wao kuwa watoto wa mama tu, bali ni vishawishi vya kawaida vinavyowakumba vijana wawe na mama tu au wa mama na baba. Wote hao wanaweza kujikuta hawafikii malengo yao kwa sababu ya ujana.
Bluu: Ni wazi lazima tukubali pia kwamba wale wanaolelewa na mama mmoja wanaweza pengine wakawa na shida ya kiuchumi zaidi kuliko wale wanaolelewa na wazazi wawili. Wanakosa sapoti ya kiuchumi kuweza kuendelea na masomo ya juu na kulazimika kukatiza masomo. Kwenda kwenye sanaa inakuwa kama alternative. Ninachokataa mimi ni kuona kwenda sanaa ni matokeo ya kukosa malezi bora, au kuwa na uhuru wa kupindukia wa vijana kwa vile tu wako na mama pekee.
 
Thanks kwa kuleta hii study.

Ila mimi nilivyoandika kilichoni motivate ni mziki huo nilioweka link...baada ya kuusikiliza nikawakumbuka wasanii wetu.
Hivyo hizo study za kisayansi sijazipitia zaidi ya ku google baada ya kuona watu wamegoma kutoa mapoint. Kwenye google sikuona study ya usanii na single mother ila zipo study za school drop outs na u single mother which relates to what you have brought here.

Hivo basi hii niloweka humu bado inahitaji researcher kama kuna mwenye interest.

Kwa kumsaidia mleta mada (kwa sababu naamini conclusion yake) labda ungepitia study hii Statistics « The Fatherless Generation.

Sports na music bado sijaona sababu ya kurelate na fatherlessness ila kuna article hii inayoonyesha watoto waliolelewa na single mothers wana uwezekano mkubwa wa kuwa successful kwenye "self-paced" activities kama sports, arts na music. more than academics (which is more instructional)
Comparison of Black and White Boys' Performance in Self-paced and Reactive Sports Activities - Dunn - 2006 - Journal of Applied Social Psychology - Wiley Online Library
 
Sanaa ina uhusiano na uhuru. Mimi nakumbuka baba yangu alimpiga marufuku kaka yangu kucheza mpira kwa ku relate na perfomance yake mbaya darasani. Kama angekuwa huru sasa hivi labda angekuwa Chelsea Lol.

Kupotelea njiani hakutokani na wao kuwa watoto wa mama tu, bali ni vishawishi vya kawaida vinavyowakumba vijana wawe na mama tu au wa mama na baba. Wote hao wanaweza kujikuta hawafikii malengo yao kwa sababu ya ujana.
Bluu: Ni wazi lazima tukubali pia kwamba wale wanaolelewa na mama mmoja wanaweza pengine wakawa na shida ya kiuchumi zaidi kuliko wale wanaolelewa na wazazi wawili. Wanakosa sapoti ya kiuchumi kuweza kuendelea na masomo ya juu na kulazimika kukatiza masomo. Kwenda kwenye sanaa inakuwa kama alternative. Ninachokataa mimi ni kuona kwenda sanaa ni matokeo ya kukosa malezi bora, au kuwa na uhuru wa kupindukia wa vijana kwa vile tu wako na mama pekee.
 
Unajua woga pia unachangia watoto kufuata wazazi wanachotaka wafanye. Mfano utasikia nikifeli baba ataniua...Ushasikia mtu anasema nikifeli mama ataniua...mimi sijawahi.
 
Sanaa ina uhusiano na uhuru. Mimi nakumbuka baba yangu alimpiga marufuku kaka yangu kucheza mpira kwa ku relate na perfomance yake mbaya darasani. Kama angekuwa huru sasa hivi labda angekuwa Chelsea Lol.
Ni kweli sanaa ina uhusiano na uhuru. Kama nilivyosema kwenye posts zangu za juu ni kwamba wengi wa hao vijana wanachukua mengi kwa mama zao ikiwa ni pamoja na mwelekeo wa sanaa. Hawa wanakuwa wamechagua sana kwa uhuru wao; huo ndo mwelekeo wao kutoka ndani ya moyo wao.

Lakini lazima tukubali pia kwamba wapo wanaoweza kwenda kwenye sanaa kama chaguo la pili baada ya kukosa kile walichokitaka katika maisha yao. Na hili si jambo geni, ni jambo la kawaida popte duniani. Mtu unapanga maishani kufanya hiki, lakini unajikuta huna uwezo: wa kifedha, qualification, nk unaamua kuingia kwenye fani nyingine. Hapo hakuna cha ajabu wala cha kushangaa. Kwa hiyo using'ang'anie sana kusema sanaa ni uhuru ukaishia hapo. Wakati mwingine mtu anaweza akaingia huko kutokana na kukosa njia nyingine ya kusonga mbele.
 
Unajua woga pia unachangia watoto kufuata wazazi wanachotaka wafanye. Mfano utasikia nikifeli baba ataniua...Ushasikia mtu anasema nikifeli mama ataniua...mimi sijawahi.
Mama yangu nilikuwa namuogopa sana. Halafu nikimuona yuko sad nilikuwa namind sana. Kwa hiyo hapo bado sijakubaliana na wewe.
 
Kutokubaliana na mimi sikushangai kwani kila kitu kina exception. Ila nijuavyo wamama wengi hata kama ni wakali vipi uwezekano wa watoto kuwageuza bibi ni mkubwa. Ndio maana mi naweza kumkalipia mtoto lakini badala ya kunikimbia ananikimbilia kujificha kwenye nguo yangu. Lol. Haniogopi..am his mother. Lol.

Mama yangu nilikuwa namuogopa sana. Halafu nikimuona yuko sad nilikuwa namind sana. Kwa hiyo hapo bado sijakubaliana na wewe.
 
Unajua woga pia unachangia watoto kufuata wazazi wanachotaka wafanye. Mfano utasikia nikifeli baba ataniua...Ushasikia mtu anasema nikifeli mama ataniua...mimi sijawahi.
Nakumbuka mama yetu tulimpa jina la MREMA,refer Mrema alivyokuwa waziri wa mambo ya ndani,tulisema sana tu kuwa tukishindwa kitu tutakoma kwa mama.
 
This goes to any entertainment career, ngumu kuielezea kwa maandishi I mean ni vizuri tukiwaiwa tunaongea sababu inahitaji elaboration nyingi. Tena ieleweke kuwa wanaofanikiwa kwenye hii tasnia wengi wanatoka kwenye familia duni sababu inahitaji moyo kujishusha angalau kwa nchi za wenzetu kidogo wengi wanaikalia darasani
 
"Wengi"? Kati ya wangapi? Ukisema wengi hata wakiwa watatu tu tayari ni wengi na hivyo tayari wanatosha kusupport hoja yako.

Halafu, katika hiyo observation yako ulikuwa unalinganisha na wasanii waliolelewa na "single father", "grand parent(s)", "ndugu wengine", "adopted" au "baba na mama"?

Anyway, weekend hii...lets take it easy!!!!
 
Back
Top Bottom