Niseme wazi mimi huwa ni mlalamikaji pindi nikihudumiwa sivyo. Lakini Kwa hili napenda niipongeze wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu chini ya mwanamama mhe. Dkt Dorothy Gwajima.
Nimehudumiwa vizuri pasipo urasimu wowote mpaka kufanikisha usajili wa shirika lisilo la kiserikali (NGO) kwa njia ya mtandao.
Naweza kusema nilicheleweshwa na ngazi ya wilaya, kata na mtaa,lakini ilipofika ngazi ya taifa huduma zilienda kisayansi zaidi.
Unatuma document zinasomwa na baadae wanakupa marekebisho ya kufanya, ukikamilisha unahamia hatua nyingine.
Mwisho wanakwambia njoo uchukue cheti chako cha usajoli. Hakika mama huyu kumbe siyo umahili wa kuongea tu hata vitendo ni mchapakazi mzuri katika kusimamaia watendaji wa wizara yake. Hongereni sana wizara hususani ofisi ya msajili wa NGO kwa kazi nzuri.
Kule kwenye kata na mtaa ndipo Kuna shida. Kukuandikia barua tU ya utambulisho wanakwambia kamati ikae, maana yake uwalipe posho wajumbe qa kamati ya mtaa. Ikifika ngazi ya kata unaambiwa hivyo hivyo. Wizara iangalie namna bora ya kuondoa dosari hii.
Kule nhazi ya wilaya haina shida kwani wizara tayari imeweka mratibu wao kusimamia mchakato wa usajili.