Dodoma: Yaliyojiri Ufungaji wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali (NGO's) - Oktoba 5, 2023

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
543
3,575
Link hii hapa, karibuni



==========

DKT. DOROTHY GWAJIMA, WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM

Jukwaa hili kitaifa ni la tatu, ambapo la kwanza lilikuwa ni mwaka 2021 na Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Na la pili lilikuwa mwaka 2022 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa. Na la tatu ndiyo hili ambalo Mh. Makamu wa Rais ndiyo Mgeni Rasmi.

- Utekelezaji wa miradi umechangia kuboresha utoaji wa huduma
NGO’s zimekuwa zikiunga mkono jitihada za serikali kupitia utekelezaji wa miradi na afua mbalimbali – ikiwemo miradi ya afya, mazingira, kilimo, elimu, maji, utawala bora, nishati na uhifadhi wa jamii, na uwezeshaji wa jamii nikiyataja haya kwa uchache.

Utekelezaji wa miradi hiyo umechangia kuboresha utoaji wa huduma, kuzalisha ajira, kuongeza mapato ya serikali na hatimaye kuongeza ukuaji wa uchumi kupitia ongezko la kipato cha mtu mmoja mmoja, kaya na taifa kwa ujumla. Kwa msingi huo, wizara itaendelea kuboresha mazingira wezeshi kwa NGO’s ili ziweze kuisaidia jamii kwa kuzingatia mipango, mikakati na vipaumbele vya taifa.

Kwenye jukwaa la 2022, kama nilivyosema, alizindua Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unaokwenda hadi mwaka 2027, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mgeni Rasmi kwenye Jukwaa la mwaka 2021…

- CCBRT imepunguza utegemezi
Mojawapo ya mafanikio makubwa ya mlkakati huu ni Taasisi ya CCBRT… imeweza kufanikiwa kupunguza utegemezi kwa asilimia kubwa sana. Na imeweza kujisimamia kutafuta fursa nyingi sana. Hii ni moja ya kati ya nyingi ambazo zimefanya, hivyo taarifa yake tutaendelea kuitoa hata kwenye taarifa itakayotolewa leoya mchango wa NGO’s kwenye taifa letu. Hivyo, tuna Imani na mkakati huu utaendelea kutusaidia ili NGO’s zetu hizi ziweze kusimama vizuri zaidi hata pale changamoto za kidunia zinapojitokeza.

- Fursa za ndani na za nje
Kutokana na maelekezo hayo, jana tarehe 4 Oktoba, 2023, kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa hili yameendesha majadiliano ya fursa za ndani na za nje ambapo sekta binafsi ilipata fursa ya kuelezea fursa za ufadhili zilizopo katika maeneo yao, vigezo na njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa na NGO ili kuzipata fursa hizo. Na hii imekuja wakati ambapo tayari majadiliano ya kuwa na mfuko wa pamoja wa wadau yapo kwenye utaratibu.

- Uzinduzi mfumo wa kidigitali
Mfumo wa kidigitali utakaotuzindulia leo, utakaotuambia NGO gani ipo sehemu gani, inafanya nini, inamsaidia nani – sasa tutaweza kuongea lugha moja, kuja kuandaa kwa pamoja wale wanaofanana wanasemaje kuwa na mfuko wa pamoja ili kusiwe na mtu anatoka kule anakwenda kufanya kazi ile ile, sehemu ile ile bila kuwa na coordination. Huu mfumo utatusaidia kwenye ajenda hii ambayo tumeanza kuiratibu ya namna gani tunaweza tuka-mobilize resources za wadau wote zije kwenye mfuko wa pamoja.

- Utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara kwa kushirikiana na wadau imeendesha majadiliano kuhusu sera na sharia za kodi ili kujenga uelewa wa pamoja kati ya serikali na NGO’s… Vile vile kwa kwa mwaka huu tumepanua wigo wa majadiliano na kujadili utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na majukwaa mengine ya kimataifa. Na kama unavyoona leo kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kuwa na msajili wa mashirika kama haya kutoka nchini Uganda. Naomba tumpongeze mgeni wetu huyu ambaye amekuja kuungana nasi. Na lengo ni kubadilishana uzoefu wa uratibu ndani ya Afrika Mashariki.

Pia jukwaa hili limejadili kuhusu teknolojia na ubunifu pamoja na mikakati dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Kupitia majadiliano haya, NGO’s, Serikali na sekta binafsi kwa pamoja tumebaini kuwa pande zote zinahitaji ushirikiano na ubunifu ili kufikia malengo ya ukuaji wa NGO’s, kuongeza fursa zaidi, kuleta tija na usanisi sambamba na kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza shughuli zao.

Wizara itaendelea kusimamia uzingatiaji wa misingi ya uwazi na uwajibikaji wa mashirika haya na kushirikiana kwa karibu na Baraza la Taifa la NGO’s ili kuhakikisha mchango wa mashirika haya unaendelea kutambuliwa na kuthaminiwa.

DKT. PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS - JMT

- NGO's zinachagiza maendeleo
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yamekuwa yakichagiza jitihada za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali na hasa katika sekta za afya, kilimo, elimu, maji, mazingira, utawala bor, uwezeshaji wa jamii, miundombinu, mifugo na uvuvi, na sekta nyingine mtambuka. Hakika miradi hiyo imewanufaisha wananchi wengi kijamii na imechangia katika kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana wetu, wanawake na watu wenye ulemavu.

Nimepata fursa ya kujionea shughuli zinazotekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia mabanda machache ya maonesho ambayo nimeyatembelea. Na ningependa niseme nilichokiona kimenithibitishia kwamba mashirika haya yanatoa mchango mkubwa sana katika kuleta maendeleo endelevu kwa taifa letu.

Tunapoadhimisha kilele cha jukwaa hili, yapo mambo ambayo ningependa kuyawekea msisitizo. Na hususan mambo manne.

- Uwazi na Uwajibikaji katika NGO's
Jambo la kwanza ni kuhusu uwazi na uwajibikaji katika mashirika yasiyo ya kiserikali. Bado hakuna uwazi wa kutosha kuhusu rasilimali zinazopatikana na namna zinavyotumika katika kutekeleza miradi iliyokusudiwa na wakati mwingine kuna matumizi ya rasilimali hizo ambayo hayawiani na malengo. Kwahiyo, ninawasisitiza mzingatie uwazi kwakuwa ni sehemu muhimu katika kuwezesha serikali kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu uratibu na shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali na ikiwemo misamaha ya kodi, michango ya mashirika hayo katika maendeleo ya nchi, n.k.

Nafurahi pia kuwa kwenye ratiba kuna mashirika ambayo yatapewa tuzo nav yeti. Na ninawapongeza sana wote kwa ubunifu huo. Lakini pia, nilikuwa nateta na Mh. Waziri (Dkt. Dorothy Gwajima) pale nikamwambia kwamba pia itafaa pawepo tuzo hasi kwa kwa taasisi ambazo hazitimizi wajibu wake.

- Uzingatiaji wa maadili ya Kitanzania
Lakini la pili ambalo ningependa kuliwekea msisitizo, ni kuzingatia maadili ya Kitanzania. Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawajibika kutunza na kulindamaadili kwa kuheshimu mila, desturi, na tamaduni za Kitanzania katika utekelezaji wa afua na programu mbalimbali. Aidha ninawakumbusha kuzingatia sharia za nchi na kufuata miongozo mbalimbali ambayo inaratibu shughuli za mashirika yenu.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, naiomba ishirikiane na wadau wengine katika kusimamia hili. Ninawaomba sana msikubali kutumiwa. Maadili yetu mazuri ya Kitanzania lazima tuyatunze, lazima tuyalinde. Msikubali kuwa tarumbeta za watu wasiotutakia mema. Hili ni muhimu sana. Tanzania ni ya kwetu na watu wasitumie mlango wa NGO’s kupenyeza ajenda zao ambazo haziendani na maadili yetu mazuri ya Ktanzania.

- Mabadiliko ya tabianchi
Jambo lingine ni la mabadiliko ya tabianchi. Hili ni eneo muhimu sana na linapaswa liangaliwe kwa jicho la kipekee na mashirika ya kiserikali. Nchi yetu ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi na hali hii tunaiona kupitia mvua zisizotabirika, ongezeko la joto; kuna ukame, mafuriko na magonjwa. Na kwa upande wa mifugo kuna ukosefu wa malisho, vyanzo vya maji vinatoweka. Na athari hizi zimeathiri sekta mbalimbali – kilimo, utalii, nishati, afya, mifumo ya ekolojia ya bahari nan chi kavu. Na maana yake pia pato la taifa linaathirika.

Nimefurahi pia kusikia kwamba kwa sehemu kubwa mashirika yasiyo ya kiserikali, kwa kiasi kikubwa, fedha zake nyingi zinaelekezwa kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hongereni sana! Hata hivyo, serikali ingependa kuona ushiriki zaidi wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu na hamasa kuhusu uhifadhi wa mazingira, udhibiti wa majanga, lakini pia Maisha endelevu (Disaster management and sustainable livelihood) na kuchangia katika utengenezaji na uboreshaji wa wa sera mbalimbali.

- Mamlaka zifanye kazi kwa karibu na NGO's
Jambo la nne, ninaridhia ombi la la Mwenyekiti wa Bodi, Mama Mwantum. Na ninapenda nitumie nafasi hii kuelekeza mamlaka za mikoa na wilaya katika nchi yetu zifanye kazi kwa karibu na mashirika yasiyo ya kiserikali na zifuatilie kazi zao. Wameanza vizuri; tumesikia hapa kila mkoa wamefanya mikutano lakini hiyo haitoshi – uwe ni mwanzo tu wa mashirikiano kati ya serikali katika ngazi za mikoa.

Tumekuwa na ushiriki wa wasajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali, najua walialikwa kadhaa lakini amefika ndugu yetu kutoka Uganda. Naamini hii ni fursa ya wao kujifunza na kuchota maarifa kutoka kwetu namna ambavyo mashirika yanavyoratibiwa na yanavyotekeleza majukumu yake.
 
Back
Top Bottom