Nimefarijika kwa matokeo ya Kidato cha Sita kwa kuona Shule ya Serikali Kibaha imeongoza kitaifa

Sio rahisi kuamini, kuna kitu kimechezwa lakini hongera zenu!
 
Napongeza sana kwa ufaulu huu,

Ila yasije kuwa kama ya kikwete yale ya MATOKEO MAKUBWA SASA (BIG RESULT NOW)...

Bdo natafakari, nawaza nawazua.
 
Ilboru ni ya 13, Msalato ya 17
Masikini!
Pamoja na hali ilivyo ngumu bado wanapambana tu.
Ina maanisha hawa wakipata walimu wazuri na maabara za kisasa watatisha.
Lakini ifike mahali tukubali kwamba Ubora wa Elimu haupimwi kwa kiwango cha ufaulu peke yake.
Itatubidi tuangalie hawa wasomi wanatufanyia nini wakitoka hapo na huo ufaulu wao................
 
je siyo mpango wa wizara na wa ndalichako kuitumia Kibaha kama pilot kwa jinsi wanavyojua wao ili ionekane ktk miaka hii mi 3 ya Jiwe shule za serikali zimerudi kileleni na kupoteza za private
Hili swala nimeliwaza pia..kwa miaka hii miwili feza boys wamefichwa kabisa
 
ukiangalia utitiri wa shule kwa sasa ilboru, Tabora school (The Head of Tanzania), mzumbe,kilakara IMO bado wanafanya vizuri
Nimeona,
Matokeo yao yanatia moyo kiasi.
Japo bado watoto wetu hawa wanasoma katika mazingira magumu sana.
Niliwahi kutembea baadhi ya shule na kukuta kuna walimu wa kuhesabika hivyo wanatoroka wanaenda kusoma Tuition. Sasa ukiona Practical watoto wanaenda kusoma kwa walimu binafsi au wanasubiri zivuje, viwango vyetu haviridhishi kabisa.
 
Mwanzo mwanzoni, napenda kuweka mambo yafuatayo wazi ili nisieleweke vibaya. Mosi, napenda sana kuimarika kwa elimu na kuongezeka kwa ufaulu. Kuimarika kwa elimu na kuongezeka kwa ufaulu kunatupa matumani ya kupata wataalamu wa kada mbalimbali za kisayansi na kijamii katika kusongesha mbele gurudumu la Taifa letu pendwa la Tanzania. Wanafunzi wanapaswa kusoma, kuelimika na kufaulu.

Pili, napenda Shule zote bila kujali ni za Serikali au za watu binafsi. Elimu bora yaweza kupatikana popote. Naomba nitanie kidogo. Katika miaka ya tisini na elfu mbili mwanzoni, 'wenye akili' walikuwa wakisoma katika shule za Serikali. Kusoma shule binafsi kulikuwa ni kujianika kuwa una walakini katika ufaulu wako. Ni kama waliofeli ndio waliokuwa wakisoma Shule binafsi. Mambo yakabadilika hivi karibuni.

Katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne na sita, Shule za Serikali hazikuwa zikifua dafu. Zilitupwa nje hata kwenye Shule kumi bora za kitaifa na hata hazikutoa wanafunzi bora wa kitaifa. Hata zile 'Shule za Vipaji Maalum' za Kibaha, Mzumbe, Ilboru, Msalato na Kilakala hazikufua dafu. Suala hili si tu lilikuwa likisumbua vichwa vya viongozi wetu, bali hata wadau wa elimu kama mimi.

Hivi punde, Baraza la Taifa la Mitihani nchini limetangaza matokeo ya kidato cha sita. Niweke wazi kuwa nimefarijika sana. Ni kwakuwa Shule za Serikali 'zimerejesha heshima yake' kupitia kwa Shule ya Sekondari ya Kibaha iliyoongoza katika matokeo hayo. Kwa kupitia kwangu kwa haraka kwa matokeo hayo, nimeiona pia Shule ya Sekondari ya Mzumbe katika nafasi ya nne kitaifa. Ilboru, Tabora Wavulana na Tabora Wasichana hazikufanikiwa kuingia kumi bora.

Sikufurahia kwakuwa nazichukia Shule binafsi, la hasha. Nimefurahi kwakuwa wadogo zetu wanaojiunga na Shule za Serikali tulikopitia kuanzia Msingi hadi Sekondari watatiwa moyo na matokeo haya na kuziamini Shule za Serikali. Wataamini kuwa hata katika shule za kiserikali kuna ufaulu endapo kutakuwa na nidhamu,juhudi na kujitoa. Kibaha wameonyesha njia, wamekuwa 'Chilongola' baada ya miaka mingi kupita.

Hongera Shule ya Sekondari ya Kibaha na hongera kwa Shule ya Mzumbe kwa kutoa mshindi wa kwanza kitaifa!


Wakili msomi Kismiri ni shule ya umma pia. Na miaka yote imekuwa ikifanya vizuri sana. Lakini matokeo haya yana jambo gumu kifikra imekuwaje PCB wadominate top 10 wakati miaka yote haikuwahi kuwezekana?
 
Back
Top Bottom