Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,838
18,250
Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.

Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.

Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.

Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
1703090514594.png

Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
1703090382854.png

Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!

Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?

Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
 
View attachment 2848392

Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390

Wenye A karibu wote wa PHILADELPHIA PRIMARY SCHOOL iliyopo Kongowe ya Mbagala Dar, wamepelekwa Mwandege kutwa..!!
 
Kina kitu kinaitwa uwiano. Uwiano si ushindani. Hata hao wawili ni bahati yao
 
Kwa hiyo kumbe selection haifuati ufaulu bali inafuata uwiano kama vile Tanganyika inavyowiana na Zanzibar? Hii kali aisee!

Hebu tufafanulie kidogo mkuu huenda unakuwemo kwenye selection board. Huwa mnachagua kwa kutumia muongozo kutoka juu bila kuzingatia ufaulu?
 
Mazingira sawa ? How? Yaana aliesoma private na government wawe na mazingira sawa? Walimu sawa? Miundombinu sawa? Kisa tu wako eneo moja? Serikali iko sawa kabisa, mim mwanangu yuko private akifaulu ntapambana aende shule teule za private..
 
Mambo usiyoyajua mkuu usikimbilie kuja kuilaumu serikali, kilichofanyika hapo ni hesabu ya hali ya juu! Wewe umeshindwa kungamua tu!! Kwa hili naipongeza serikali! Kilichofanyikq hapo mm nakijua ni utaratibu na hesabu ndizo zinazofanya hivyo mkuu wala sio ubaguzi!!
Hivi unajua unachokiongea kweli mkuu? Hesabu gani hizo ambazo hazifuati ufaulu? Ina maana hizi nafasi zinagawiwa kama njugu kwa matakwa ya watu kutoka juu? Ili iweje?
 
Kama wazazi wao walikua na uwezo wa kuwasomesha private basi bado wana uwezo wa kutoa takrima kuwahamishia shule nzuri za serikali. Mkuu awamu hii tumia akili ya kuzaliwa badala ya kulalamika
 
Mazingira sawa ? How? Yaana aliesoma private na government wawe na mazingira sawa? Walimu sawa? Miundombinu sawa? Kisa tu wako eneo moja? Serikali iko sawa kabisa, mim mwanangu yuko private akifaulu ntapambana aende shule teule za private..
Kwanini sasa wasitungiwe mitihani tofauti? Kama unasapoti ujinga huu, basi kuna haja ya kuwa na mabaraza mawili ya mitihani.....private na public. Au basi wawe wanatunga mitihani aina mbili...for private and government candidates.

Huwezi kusema hakuna usawa wakati wote wanasoma mtaala mmoja na vitabu vimoja. Bado hjanishawishi. Tangu lini nchi hii kila kitu kikawa sawa?
 
Back
Top Bottom