Nimeamini Lowassa ndiye rais ajaye

Ufalme wako umepimwa umeonekana umepungua siku zako zinahesabika......
 
Kweli ni ndoto...tusubili mchakato halali wa chama chetu kitukufu najua kitatupa mgombea atakaye tuvusha tulipo....
 
Ndg wana jamvi usiku wa kuamkia leo nimejikuta nikikubwa na ndoto ambayo nimeshuhudia Mh. Lowassa akipita kwa kishindo ktk kura za maoni Dodoma na kuamsha shamrashamra kila kona ya nchi. {Si kawaida yangu kuota wana siasa zaidi ya pilikapilika zangu}. Je ndoto hii ina ukweli? NB: Sitarajii matusi na kejeli.

ndoto ni elimunafsi.....nadhani ni vigumu kumuota donot usiyemjua au kumsikia....kwanini umuote unayemjua au kumsikia?.....ingekuwa ndoto kama ungetuuambia umemwota mtawala wa visiwa vya malta amekuwa rais wa tz au ungeuliza lowasa ni nani ili tuone kwamba kweli umemwota usiyomjua au kumsikia plz next time post thread ndoto ni nini hapo tutapata watu wa elimunafsi(psychology) watusaidie.
 
Ndg wana jamvi usiku wa kuamkia leo nimejikuta nikikubwa na ndoto ambayo nimeshuhudia Mh. Lowassa akipita kwa kishindo ktk kura za maoni Dodoma na kuamsha shamrashamra kila kona ya nchi. {Si kawaida yangu kuota wana siasa zaidi ya pilikapilika zangu}. Je ndoto hii ina ukweli? NB: Sitarajii matusi na kejeli.

Ndoto siku zote ni kumbukumbu ya kitu ulichokiwaza sana mchana ama kukifanya/kukiona.sasa kama mchana kutwa ulishinda unamuwaza huyu fisadi,ulitarajia kwenye ndoto umuote Wema Sepetu?.endelea kujidanganya!ni bora hata ungemshauri akachuane na kina Malinzi Tff aitwe "rais" ili kiu ya hilo jina aikate.otherwise atakufa kwa presha hiyo 2015 atakaposhuhudia Dr wa Dr anatinga ikulu kiulaainiiiiiiiii.
 
Sasa mbona unajihami wakati umewasilisha mawazo yako! Au umekuwa paid,maana hiyo ni saikolojia ya mkosaji.
 
Nimeona umakini mkubwa sana kwa Lowassa na kambi yake. Hawakurupuki, hawaropoki ovyo hawajibu tuhuma hovyo, wamejipanga vya kutosha na wako makini sana.

Sijawahi ona Lowassa akikurupuka kujibu tuhuma.
Sijaona Lowassa akisema sema ovyo.
Sijaona Tuhuma iliyothibitisha wazi kama Lowassa ni mwizi

LOWASSA
Amekuwa mtu makini sana
Mwenye msaada mkubwa kwa jamii
Mwenye kusikiliza
Anayesaidia vijana
Aliyewatoa watu wengi tofauti na hawa wabinafsi wetu
Mwenye mwelekeo maalumu
Asiyependa utani na mtu
LOWASSA
Hataowaonea huruma wazembe (Alifanya hivi pale alipokuwa waziri mkuu)
Hataacha mambo yaende kiholela
Hata kuwa na ubia kwenye urais wake
Atafanya maamuzi magumu
Atawaangalia wazee
Atawaangalia vijana
Hatawaacha wakinamama
Atawatetea wanyonge.
Atafufufua matumaini yalioachwa na Nyerere

Lowassa aweza ,Lowassa atosha.
 
Lowassa,Lowassa,hatuna haja na sifa zisizokuwa na mashiko,tunataka kwanza hela za Escrow zirudi toka mikononi mwa mafisadi kwa Serikali.
 
Nimeona umakini mkubwa sana kwa Lowassa na kambi yake. Hawakurupuki, hawaropoki ovyo hawajibu tuhuma hovyo, wamejipanga vya kutosha na wako makini sana.

Sijawahi ona Lowassa akikurupuka kujibu tuhuma.
Sijaona Lowassa akisema sema hovyo.
Sijaona Tuhuma iliyothibitisha wazi kama Lowassa ni mwizi

LOWASSA
Amekuwa mtu makini sana
Mwenye msaada mkubwa kwa jamii
Mwenye kusikiliza
Anayesaidia vijana
 
Back
Top Bottom