Nilichokiona na Kukisikia Kijijini Nyololo, Siku 4 Baada ya Mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi...

Nadhani mleta uzi ulitaka utujulishe kuwa nawe ulienda 'hijja Nyololo', kama si hivyo tafadhali nenepesha simulizi zako!
 
Kumlaumu Maggid ni kupoteza muda wetu bure, yeye alishatowa msimamo wake kushirikiana na Jeshi la Polisi na hii ni sehemu ya kazi yake katika makubaliano yao.

Kwa wale amabao hawaelewi kitu ukweli ni huu kutoka kwa aliyeuwawa, hapa ni LIVE bila chenga mimi huwa siogopi ban.


Imeandikwa na: Mlyafinono | 2nd September 2012 12:00


icon1.png
Polisi Iringa wajiandaa kuua mkutano wa Chadema Mufindi


Jeshi la polisi mkoani Irinaga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wameshindwa kufikia maafikiano kuhusu makubaliano ya awali ya kuanza kwa mikutano yao baada ya kumalizika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi.

Wakati jeshi la polisi wakitaka chadema kusubiri hadi tarehe 8 mwezi huu baada ya muda wa sensa kungezwa chadema wanasema mkutano wao ambao umepangwa kufanyika Mafinga wilayani Mufindi upo palepale.

Kauli za Viongozi

RPC iringa, Michael Kamuhanda.

-nina digrii ya maswala ya kipolisi, CHADEMA hawawezi kutushinda.
-wasipotii agizo letu nakufanya mkutano wao mafinga tutumia uwezo wetu wote kuhakikisha tunawadhibiti.

Benson Kigaila.........

Wamezuia mkutano wetu kwa kisingizio cha sensa, wakati bububu zanziba leo kuta uzinduzi wa kampeni za uchaguzi,je huko hakuna sensa?

-Liwalo na liwe mkutano leo lazima ufanyike mafinga.

Dk. slaa........

Kauli ya Benson ndo msimamo wa CHADEMA.

-Nilionge na IGP jana kumweleza kuwa tulikubaliana kistaarabu kwahiyo aheshimu makubaliano.
-Mkutano wetu leo Mafinga lazima ufanyike tumechoshwa na ukandamizaji wa Jeshi la poisi.

My take.........
Kama kweli mkutano utafanyika mafinga maafa huenda yakawa makubwa kuliko ilivyokuwa morogoro kwani tayari magari 8 ya polisi yameshakwenda mafinga kupambana na lolote litakalotokea
 
Majid ana njaa, anatafuta cheo. Umeishachelewa - it is too late brother
Ndugu yangu hapo katafutaje cheo vipi?Leo tunamsulubu ili atueleze aliyoyabana lakini sioni kama makala hii imelalia upande gani na ndo maana tunalumbana hapa ili tujue alikuwa anasimamia upande.gani.
Tuijadili hoja ya leo kwa kumuninginiza kikamilifu kwa hoja na si matusi wala kejeli.
 
Labda walioko Iringa na Njombe wataisoma vizuri story hii kupitia gazeti la kina Maggid la Kwanza Jamii.
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo
Rejao wewe ni binadamu hata kama unatumia ID fake, damu ya Mwangosi inakulilia, chunga sana kebehi zinazohusu damu ya mtu
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

Hivi wenye uchu wa madaraka ni CDM AU ccm? Zumbukuku bana!
 
maggid sioni cha maana ulichokiona zaidi tu ya kutaka watu waamini kwamba wananchi wa nyololo wana hofu.
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

Pole sana ndugu yangu ambaye hata kisu huwezi kukiita kisu kwa sababu tu ya matakwa ya mtu mwingine. Ni jambo la aibu sana kwa mtu mzima kutumiwa na watu wengine na yeye anatumika kama ling'ombe tu wala hatumii akili yake kutafakari. Aibu kubwa sana.
 
Haya nenda kwa nepi mwambie akupe buku moja yako
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo
 
Ndugu zangu,

IJUMAA alfajiri ya Septemba 7 niliondoka nyumbani Iringa kuelekea Njombe kikazi. Jana yake, alhamisi usiku, Mwandishi Gershom Malegesi wa Redio Ebony FM alinipigia simu kuniomba nishiriki kwa simu kwenye kipindi chake maarufu cha ' Morning Talk'.

Nikamjibu, kuwa kwa vile nina safari ya Njombe, basi, nikifika kijijini Nyololo, Mufindi, nitasimama na kuongea na wakazi wawili watatu waniambie wanachofikiri juu ya kilichotokea. Kisha Maregesi aniunganishe kwa simu nikiwa hapo Nyololo tuongee redioni. Tukakubaliana.

Baada ya kutoka Mafinga na kuumaliza msitu wa Sao Hill, nilianza kuiona Nyololo kutoka mlimani. Nilipaki gari yangu takribani nusu kilomita kabla ya kuingia kijijini Nyololo. Nikaanza kutembea kwa miguu kuelekea kijijini bila kushika kamera wala mkoba.

Sweta nililovaa siku hiyo ra rangi ya zambarau huenda lilinifanya nionekane kama ' wapasua mbao' wengine! Ilinisaidia, maana, kwenye meza ya kwanza ya biashara pale kijijini, niliwakuta akina mama watatu wakisikiliza kwa makini ' Morning Talk' ya Ebony FM. Kulikuwa na watu waliokuwa Nyololo siku ya tukio wakitoa ushuhuda wao studioni.

Nilimwandikia meseji mtangazaji Malegesi kuwa angeweza kuniunganisha hewani kwa wakati huo. " Kaka, nimeshafika Nyololo!" Nilimwandikia. Naye akanijibu; " Kuna jamaa wanatoa ushuhuda wao studioni, nitakuunganisha baada ya dakika 15".

Taratibu nami nikajivuta karibu zaidi kwenye meza ile ya biashara ya mboga mboga iliyozungukwa na akina mama waliokuwa wakifuatilia kinachosemwa kuhusu kilichotokea mahali ambapo wao ndipo walipo kwa wakati huo.

" Kamwene!"- Niliwasalimia kwa Kihehe. Kisha nikajiunga kwenye kusikiliza ' Morning Talk'.

Niliwasikiliza akina mama wale wakijadiliana pia katika baadhi ya waliyokuwa wakiyasikia. Niliwaona wakitingisha vichwa kukubali baadhi ya yaliyokuwa yakisemwa na mashuhuda. Niliwaona pia wakitingisha vichwa kuyakataa baadhi ya yaliyokuwa yakisemwa na mashuhuda.

Nikavuta pumzi, kisha nikawauliza; " Mwenzenu napita njia tu, hivi siku ile ya Jumapili ilikuwaje na mlijisikiaje?"

Nikawaona walivyo na hamu ya kumsimulia ambaye hakuwepo. Nikawasikiliza. Mmoja anasema; hakuwahi hata siku moja kusikia mlio wa bomu. Ilkuwa ni mara yake ya kwanza. Mwingine akaniambia; " Yaani , mimi , niloposikia mabomu tu, nikajifungia ndani na kulala!". Naam, huyu aliugeuza mchana kuwa usiku.

Akina mama wale wanasema, kuwa usiku ule wa Jumapili walikosa hata hamu ya kula chakula. Hawakula chakula. Walilala kwa mashaka pia.

Kando ya meza ile nikawaona watoto wakisogelea na kusikiliza mazungumzo. Nilizioona sura za watoto wenye hofu. Msichana wa miaka 13 akasimulia jinsi alivyokimbilia porini kuhofia maisha yake.

Ndio, kuna watoto wengi wa Nyololo leo ambao wangehitaji msaada wa kisaikolojia kuelewa kilichotokea na kuwapunguzia hofu yao.

Nikiwa nimesimama pale kwenye meza ya biashara nikaisikia simu yangu ikiita. Ni Mtangazaji Gershom Malegesi wa Ebony FM aliyekuwa tayari kuniunganisha na studio. Lakini, kwa nilichokuwa nikikiona na kukisikia pale kutoka kwa wakazi wenyewe wa Nyololo, nikashindwa kuijibu simu ya Malegesi. Sikutaka tena kuunganishwa hewani. Nilihitaji muda wa kutafakari.

Hakika, niliyoyaona kutoka kwa wakazi wa Kijijini Nyololo ni pamoja na hofu, mashaka, hasira na zaidi maswali ya ' Kwa nini?". Kuna wanaojisikia vibaya sana kuona tukio lile baya limetokea kijijini kwao. Kuna wanaojisikia kukatishwa tamaa na mambo ya siasa na hawaipendi siasa kwa sasa. Kuna wanaojisikia aibu kuwa Kijiji chao kimejulikana sasa kwa sifa mbaya ya mauaji. Kuna wanajisikia kuwa watu wa kutoka nje wamekuja na kufanya mambo mabaya kijijini kwao.

Nilizunguka kwa miguu kwenye mitaa ya kijiji cha Nyololo. Niliziona teksi mbili tatu kuu kuu ambazo hufanya safari za kutoka barabara kuu hadi vijiji vya ndani. Kuna ambao siku ya tukio gari zao zilikodishwa kuwakimbiza majeruhi au waliotaka kuikimbia Nyololo kwa haraka.

Ndio, niliwaona vijana wale wa Nyololo, wa kike na wa kiume, ambao kwa kawaida ukipita Nyololo huonekana kuchangamka sana, lakini, Ijumaa ile niliyopita Nyololo niliwaona wakiwa kama ' Kuku waliomwagiwa' maji. Wengi hawakuchangamka. Hata kwenye sura z baadhi yao unaweza kuona, kuwa kuna jambo kubwa limewatokea na wako kwenye kutafakari na labda hofu pia. Maana, redio, runinga na magazeti bado yanazungumzia kilichowatokea.

Na kikubwa nilichokiona ni kuwa; wakazi wa kijijini Nyololo wana ukweli ambao huenda wengine hawaufahamu. Ni wajibu wa wote wenye jukumu la kuusaka ukweli mzima wa kilichotokea kuwasikiliza wakazi wa Nyololo pia.

Na bila shaka, kama Taifa, Nyololo inaweza kutusaidia kufungua ukurasa mpya wa namna iliyo bora na salama ya kwenda mbele kama ndugu wa Taifa moja. Kwamba kilichotokea Nyololo kisitokee tena.

Maggid,
Iringa.

Heshima yako MKUU Maggid!

Kumbuka hayo maneno niliyo kazia na rangi nyekundu, MKULU aliihakikishia dunia kwamba mauaji ya namna hii hayatatokea tena baada ya yale MAUAJI YANAYO FANANA NA YA NYOLOLO KULE ARUSHA!!!!!!!!!
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

Wamekuambia hawakipendi chadema? Mmnh! If wishes were horses ........................
 
Ndugu yangu hapo katafutaje cheo vipi?Leo tunamsulubu ili atueleze aliyoyabana lakini sioni kama makala hii imelalia upande gani na ndo maana tunalumbana hapa ili tujue alikuwa anasimamia upande.gani.
Tuijadili hoja ya leo kwa kumuninginiza kikamilifu kwa hoja na si matusi wala kejeli.
Ndugu yangu usijifanye wewe ni mgeni hapa JF ni tangu lini Maggid amewahi kujibu maswali magumu hapa JF? yeye amezowea kuitwa mwenyekiti na misukule wenzake kule kwenye blogu yake ya kishirikina hapa anapwaya na wala si sehemu yake.
 
CCM ile imeshakufa wamebaki waporaji kwa kutumia nembo ya CCM. Cha msingi ni vyema wahakikishe kuwa wako mbali na maovu ili weweze aminiwa.
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

kama ndio mlienda (polisi) kufanya mauaji (ya mwangosi) kwa makusudi ili ionekane CDM ndio wamesababisha basi sasa kila mtu anajua kuwa ni polisi ndio iliyoua na ilifanya makusudi kwa ushahidi wa picha na video, na mbinu hiyo imeshindwa kama zilivyoshindwa mbinu zenu nyingine nyingi, poleni jipangeni upya, ccm aka chama cha magwepande bye bye wauaji wakubwa msio na ubinadamu wala utu kila mtu amewajua :A S 465: :flypig:
 
Maggid, no offense lakini mbona sioni habari katika ulichoandika?

Kwamba watu wana hofu ni kitu kinachofahamika na sidhani kama kinastahili kuanzishiwa thread.

Kwamba ukweli utafutwe, ndio lilikuwa linazungumziwa toka siku ya kwanza.

Kwamba watu wana majonzi sidhani kama linahitaji kulifungia safari mpaka Nyololo.

What exactly is the output of your visit to Nyololo?
exactly, maggid unatakiwa utuambie haswa kilichokupeleka nyololo hivi vyote ulivyosimulia hakika kila mtu anajua
 
umeona ehh?
Nilidhani ni mimi peke yangu nileyeona hichi kilichoandikwa ni habari ya kufikirika.
Nadhani Maggid alitaka tujue kuwa alifika Nyololo.


mkuu nimegundua maggid ukweli anaujua ila hapendi kuuweka wazi maana ni kama utamgharimu,haiwezekani mwandishi anaejiita mbobezi wa habari za uchunguzi akaja na taarifa nyepesi kama hii,wakati huo anatwambia ameingia hapo kijijini kininja. Inasikitisha kuona pamoja na mwenzao kuuwawa lakini bado baadhi ya waandishi hawataki kuamuka dhidi ya serikali kandamizi, kitendo cha Maggid kushindwa kulaani mauaji kwa kukiri wazi kuwa atareport bila kizuizi habari za polisi inatia shaka ukongwe wake kwenye tasnia ya habari.!!!! Kuna mstari kaandika "watu kutoka nje wameharibu sifa ya kijiji chetu" ni vema angewataja hao watu kutoka nje ya wapi.!
 
Back
Top Bottom