Nilichokiona na Kukisikia Kijijini Nyololo, Siku 4 Baada ya Mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi...

Hii riwaya ya mjengwa naona inahitaji unazi kuielewa, mimi binafsi nilitarajia kusikia ushuhuda wa wanakijiji wa nyololo jinsi walivyoshuhudia tukio zima, maoni yao kiukweli nani kafanya fujo, ni wao wanakijiji ama ni polisi.

Nilitarajia kusikia kutoka kwa hao wanakijiji kuwa nini kiliwasababisha wafanye fujo hadi kusababisha polisi watumie mabomu kuwaua.

Nyololo walikuwa na wageni wa aina mbili, CHADEMA na POLISI, kama si wao wanakijiji ni nani alianzisha fujo bin vurugu

Mjengwa unauliza vimaswali kama mwalimu wa watoto wenye mtindio wa ubongo!!!!

Nakupa DISLIKE
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

**** kichwa kilichojaa maji....pointless,umeangalia video iliyopostiwa humu au umekunywa maji ya chooni??

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo
- Fikra Dhaifu
- Mawazo Dhaifu
- Akili Dhaifu
- Mipango Dhaifu
- Matokeo Dhaifu
- Matarajio Dhaifu

Habari za BUBUBU
 
Maggid, no offense lakini mbona sioni habari katika ulichoandika?

Kwamba watu wana hofu ni kitu kinachofahamika na sidhani kama kinastahili kuanzishiwa thread.

Kwamba ukweli utafutwe, ndio lilikuwa linazungumziwa toka siku ya kwanza.

Kwamba watu wana majonzi sidhani kama linahitaji kulifungia safari mpaka Nyololo.

What exactly is the output of your visit to Nyololo?
Mkuu ZeMarcopolo, read him in between the lines utamuelewa, mbona mimi nimemsoma mara moja tuu, nimemuelewa!.
 
Hapana, watawachukia sana polisi, maana ndio walioua mwandishi asiye na hatia hata kidogo. Mwandishi hakuwa na kosa lolote, hakuwa mwana Chadema, hakuwa anaadamana, wala pale kijijini hapakuwa na maandamano wala mkutano wa hadhara.
Picha zote zipo zinaonyesha polisi wakipiga mabomu ya machozi kwenye ofisi ya Chadema ambayo ilikuwa imefungwa !!
Polisi wakabomoa mlango na kupiga mabomu ya machozi ndani ya ofisi ambayo ilikuwa imefungwa !!!
Rai kwa wana-JF wote wataotetea na kusherehekea mauaji haya kwa kushirikiana na CCM:-
Kumbukeni kuwa damu ya watanzania wasio na hatia inawalilia kwa uchungu mkubwa sana, na hakika, itawafuata ninyi wote akina Rejao na vizazi vyenu vyote mpaka mwisho wa maisha yenu.
Atawalaye kwa upanga, hakika, atakufa kwa upanga.
Mkuu, cha muhimu cha kuangalia ni source ya hayo mauaji na siyo end result. Tukumbuke kuwa CDM wamekuwa wakisababisha vurugu sehemu nyingi ambazo end result yake ni mauaji kwa raia wasio na hatia.
Hatuwezi kuwalaumu polisi kwa asilimia zote. Kumbuka nao ni binadamu. Wanakuwa provoked, na wewe nadhani unafahamu impact ya kuwa provoked. Unaweza kufanya kitu ambacho hukutarajia kukifanya.

Chamuhimu CDM wajifunze njia nyingine za kuwawin wananchi kama kweli wana dhamira ya kuongoza nchi. Vurugu na maandamano haziwajengi, bali zinazidi kuwaharibia. Imagine kwa sasa, CDM wakiitisha mkutano kijijini Nyololo, kuna mwananchi yoyote atakayetokeza?? Hawa ndugu zangu wachaga wajipange tena, mbinu wanazotumia hazifai kabisa.
 
maggid,

Porojo zako ni nzuri kama ingekuwa ni tafrija fulani, lakini Nyololo kumetokea msiba ambao umesababishwa na Serikali (polisi wake), na kama ulivyosimulia hiyo hadithi yako, message unayotaka kutwambia ni kuwa; has it been not Siasa watu wa Nyololo hawangeona huo msiba, na wala hawangeona hayo mabomu.

You are happy that Nyololo now have learned a lesson, politics belong to 'you and CCM'.

Tumekuwa ni Nchi ya wahuni sasa, maana ukiona mtu anatabasamu na kupiga porojo kwenye msiba na kucheka sana lazima ujue huyo mtu ana walakini. Sasa sijui hiyo habari uliyoandika inatafsiri vipi kwa kifo cha mwandishi wa habari??
 
hujaandika cha maana hapa, umezungukazunguka kama hadithi za pwagu na pwaguzi.
Nakushauri uendelee kureport habari za kipolisi kama ulivyosisitiza hapo awali.
 
Wana-JF wenzangu, hiki ni kichwa!!!!!!!!!!!

For the sake of curiosity,kwa nini ulikataa kuwekwa hewani wakati tayari ulukuwa na watu ambao wangetoa first hand information?.Je walizungumza jamboambalo lilikuwa kinyume na ulivyoa mini kiasi ambacho ulijisikia vibaya?
Hapa ni lazima utufafanulie kwani niliamini ungeingia hewani na ukawaweka mashuhuda hewani pia,kipi kilikuogopesha,tuambie.
 
Mkuu, cha muhimu cha kuangalia ni source ya hayo mauaji na siyo end result. Tukumbuke kuwa CDM wamekuwa wakisababisha vurugu sehemu nyingi ambazo end result yake ni mauaji kwa raia wasio na hatia.
Hatuwezi kuwalaumu polisi kwa asilimia zote. Kumbuka nao ni binadamu. Wanakuwa provoked, na wewe nadhani unafahamu impact ya kuwa provoked. Unaweza kufanya kitu ambacho hukutarajia kukifanya.

Chamuhimu CDM wajifunze njia nyingine za kuwawin wananchi kama kweli wana dhamira ya kuongoza nchi. Vurugu na maandamano haziwajengi, bali zinazidi kuwaharibia. Imagine kwa sasa, CDM wakiitisha mkutano kijijini Nyololo, kuna mwananchi yoyote atakayetokeza?? Hawa ndugu zangu wachaga wajipange tena, mbinu wanazotumia hazifai kabisa.

Kwa kuwasafisha wauaji, moja kwa moja unashiriki dhambi ya uuaji.
Unakumbuka mauaji ya Arusha ?? watu walikuwa wanaandamana kwa amani barabarani (kama walivyoandamana waislamu wiki hii DSM).
Polisi wakafyatua risasi hovyo wakaua watu. Unataka kushiriki kwenye dhambi hii pia ??
Unakumbuka baada ya hapo, Chadema walifanya maandamano na mikutano bila ulinzi wa polisi (unakumbuka) ??
Niambie, katika maandamano hayo huko Arusha ambayo hayakuwa na ulinzi wa polisi, watu wangapi waliuawa ?? (unakumbuka) ??
Sasa sema bila unafiki wala ushabiki, Nani anayeua watanzania wasio na hatia ??
Atawalaye kwa upanga, hakika atakufa kwa upanga.
 
Hapokwenye red colour,
Unadhani mbinu yenu ya mauaji ya watu ili kuwatisha watu wasiende kwenye mikutani ya Chadema itafanikiwa ??
Angalia historia. Mauaji mliyoyafanya Arusha, yalifanikiwa kuwatisha watu wasiende kwenye mikutano ya Chadema??
Mtaua sana, wala hamtafanikiwa kuwatisha watu, bali mtaendela kuchukiwa sana kwa mauaji yenu.
Atawalaye kwa upanga, hakika atakufa kwa upanga.
 
Bado sioni mantiki ya thread yako, mbona umeishia kuzunguka zunguka na mwisho wa siku hakuna cha maana ulichotuambia?
 
Mkuu, cha muhimu cha kuangalia ni source ya hayo mauaji na siyo end result. Tukumbuke kuwa CDM wamekuwa wakisababisha vurugu sehemu nyingi ambazo end result yake ni mauaji kwa raia wasio na hatia.
Hatuwezi kuwalaumu polisi kwa asilimia zote. Kumbuka nao ni binadamu. Wanakuwa provoked, na wewe nadhani unafahamu impact ya kuwa provoked. Unaweza kufanya kitu ambacho hukutarajia kukifanya.

Chamuhimu CDM wajifunze njia nyingine za kuwawin wananchi kama kweli wana dhamira ya kuongoza nchi. Vurugu na maandamano haziwajengi, bali zinazidi kuwaharibia. Imagine kwa sasa, CDM wakiitisha mkutano kijijini Nyololo, kuna mwananchi yoyote atakayetokeza?? Hawa ndugu zangu wachaga wajipange tena, mbinu wanazotumia hazifai kabisa.

Source ya mauaji ni Polisi, wanaeua ni polisi, wewe unaamini kweli Chadema wana-provoke polisi?? Yule aliyeuawa (muuza magazeti) Morogoro ali-provoke polisi, Mwangosi ali-provoke polisi. Si kweli kabisa. Mabosi wa polisi washaelekezwa ku-contain CDM, na kutimiza wajibu huo basi lazima watumie nguvu, na hizo nguvu ndiyo zinafikia kuua watu. It is pressure from the ruling party and its government to contain Cadema, open your mind!!
 
Hii makala inaongelea nini? Inaongeza kitu gani kati ya yale tunayoyajua hadi sasa?
 
Mkuu, cha muhimu cha kuangalia ni source ya hayo mauaji na siyo end result. Tukumbuke kuwa CDM wamekuwa wakisababisha vurugu sehemu nyingi ambazo end result yake ni mauaji kwa raia wasio na hatia.
Hatuwezi kuwalaumu polisi kwa asilimia zote. Kumbuka nao ni binadamu. Wanakuwa provoked, na wewe nadhani unafahamu impact ya kuwa provoked. Unaweza kufanya kitu ambacho hukutarajia kukifanya.

Chamuhimu CDM wajifunze njia nyingine za kuwawin wananchi kama kweli wana dhamira ya kuongoza nchi. Vurugu na maandamano haziwajengi, bali zinazidi kuwaharibia. Imagine kwa sasa, CDM wakiitisha mkutano kijijini Nyololo, kuna mwananchi yoyote atakayetokeza?? Hawa ndugu zangu wachaga wajipange tena, mbinu wanazotumia hazifai kabisa.

Hapo kwenye red inadhihirisha mkuki kwa nguruwe, Pia unapaswa kufahamu hapo Nyalolo ilikua ni ufunguzi wa tawi na haikua mkutano wala maandamano, inadhihirisha kuwa mmeshindwa kasi ya mabadiliko mpaka mnaamua kuingilia shuhuli za CDM kwa kutumia mtutu.
Hapo kwenye blue, nilikuwepo mlivyouwa raiya kwenye maandamano ya arusha na hatujasita kuhunduria mikutano ya chadema.
Hichi unachokifanya hapa ni ule muendelezo wa CCM kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe.

Read this ...

Polisi Wakorogana

• Anayetuhumiwa kuua mwandishi akwama kufikishwa mahakamani

na Abdallah Khamis​

WINGU jeusi limeendelea kutanda ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Iringa baada ya baadhi ya askari mkoani humo kunyoosheana vidole kuhusu tukio la polisi kuua mwandishi, huku baadhi yao wakimlaumu Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Michael Kamuhanda.

Askari kadhaa waliozungumza na gazeti hili kwa siri jana, walisema kama RPC angesikiliza ushauri wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) kuhusu namna ya kukabiliana na wanachama wa CHADEMA, maafa yasingetokea.

Walisema Kamuhanda ndiye aliwaamuru askari wake kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutano wa ndani wa ufunguzi wa tawi katika Kijiji cha Nyololo, kwa maelezo kuwa hakuwaruhusu kufanya hivyo.

“Kama mnakumbuka, RCO mwanzo alizielewa hoja za CHADEMA juu ya vikao vyao vya ndani, lakini alipokuja RPC hali ikabadilika kutokana na kupewa maelezo na mkuu wetu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa,” alidokeza mmoja wao.

Walisema kwamba hata katika tawi la kwanza walilofungua viongozi wa CHADEMA, RCO alifika lakini hakuwashambulia. Wakati wakifungua tawi la pili, ndipo RPC akafika, na amri zikatolewa kuwashughulikia viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Kwa maelezo ya polisi hao, viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakuwa wameleta fujo yoyote, na kwamba kama polisi wangelinda tu mikutano yao yaliyotokea yangeweza kuepukwa.

Askari hao walisema inasikitisha kwamba uamuzi wa mtu mmoja umelifanya jeshi zima lionekane baya mbele ya umma; na kwamba hata wao wanatii amri kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kuhoji amri za wakubwa wao.

Baadhi yao walisema hata maneno na vitisho vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, kwamba CHADEMA kina vurugu, ni uonevu na propaganda za kisiasa, kwani vurugu zilitokea pale CHADEMA walipoanza kutawanywa.

Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka mkoani humo zinadai kuwa baadhi ya askari waliohusika kwenye vurugu hizo si polisi halali wa jeshi hilo, bali ni vijana wa mtaani ambao walivishwa sare kwa lengo la kuwadhibiti CHADEMA, ndiyo maana walikuwa wakibabaika katika matumizi ya silaha.

Wakati huo huo, jeshi hilo jana lilishindwa kumfikisha mahakamani askari polisi anayetuhumiwa kufyatulia bomu lililomchanachana na kumuua mwandishi wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Awali, taarifa za mtuhumiwa huyo kupandishwa kizimbani zilizagaa kila kona; gazeti hili likapiga kambi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, lakini mtuhumiwa hakuletwa mahakamani.

Jana gazeti hili liliripoti taarifa za kukamatwa kwa siri na kuhojiwa kwa askari watano kati ya saba akiwamo yule anayetuhumiwa kumuua marehemu Mwangosi.

Tanzania Daima lilidokezwa kuwa askari wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi ni wale walioonekana kwenye picha mbalimbali za magazeti na mitandao wakimpiga marehemu huyo kabla ya kumsababishia kifo.

Habari za ndani zilieleza kuwa mtuhumiwa huyo wa mauaji hakuweza kufikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa kutokana na kuendelea kutoa maelezo mbele ya mlinzi wa amani.

Chanzo cha taarifa kilidai kuwa utaratibu huo wa kutoa maelezo ulianza juzi na huenda mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Jumatatu.

“Suala la mauaji ni kubwa, si kama mashitaka ya mwizi wa kuku au karanga. Hivyo, juzi na jana yule bwana alikuwa anaendelea kutoa maelezo yake kwa mlinzi wa amani. Sasa suala la kukiri kuua au kutokuua litabaki katika moyo wake,” kilisema chanzo hicho.

Source. Polisi wakorogana
 
Kwa kuwasafisha wauaji, moja kwa moja unashiriki dhambi ya uuaji.
Unakumbuka mauaji ya Arusha ?? watu walikuwa wanaandamana kwa amani barabarani (kama walivyoandamana waislamu wiki hii DSM).
Polisi wakafyatua risasi hovyo wakaua watu. Unataka kushiriki kwenye dhambi hii pia ??
Unakumbuka baada ya hapo, Chadema walifanya maandamano na mikutano bila ulinzi wa polisi (unakumbuka) ??
Niambie, katika maandamano hayo huko Arusha ambayo hayakuwa na ulinzi wa polisi, watu wangapi waliuawa ?? (unakumbuka) ??
Sasa sema bila unafiki wala ushabiki, Nani anayeua watanzania wasio na hatia ??
Atawalaye kwa upanga, hakika atakufa kwa upanga.
Kumbuka kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao. Wanapohisi kuwa mkutano/maandamano fulani yatasababisha uvunjifu wa amani, lazima wayasambaratishe, huu ni wajibu wao. Na hiki ndicho kimekuwa kikitokea Arusha. Mikutano iliyofanyika bila polisi ni kwamba polisi walifanya uchunguzi na kuona hapatakuwa na negative impact yoyote, ndio maana wakaacha iendelee bila uwepo wao.

Kuhusu waislam, kumbuka waislam waliandamana kwa amani na habari hii polisi walikuwa nayo mapema na waliona kutakuwa hamna uvunjifu wa amani. Maandamano ya waislam yalikuwa na common goal ambalo ni achievable. Tofaut na hawa CDM wanaojiamkia tu kuingia barabarani bila kujua wanahitaji nini. Kumbuka pia masuala ya siasa na masuala ya iman ni vitu viwili tofauti kabisa. Treatment ya watu wanaondamana kwa masuala ya kiimani na kisiasa ni tofauti kabisa.
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

Wrong strategy,crazy and mad thinking of CCM, huwezi kuuwa innocent civilian kwenye mikutano yao na CDM ukiamini kuwa watu wataichukia CDM
 
Back
Top Bottom