Nifanyeje baba yangu mzazi ajue kwamba mimi ni mwanae?

rafiki yanu mpenzi thanks a lot.

kuhusu ishu ya yy kuwa mzito naenda kutafuta unafuu labda ajishuku tu manake ukweli sina shida kiviile ya maisha na si kwangu tu hata kwa wanangu najimudu kimtindo.
nafsi yanu sijui kwann inaniimbia sana juu ya kumtafuta huyu baba, mpaka nakosa amani kabisa lkn naogopa sana nisije nikamuudhi baba mlezi na mama yangu. Lkn nafikir kuna sababu za yy baba mzazi kujua kwamba mm ni mwanae ama unasemaje hapo??
Dear gfsonwin usijilaumu mydia, ni haki yako kumfahamu babako mzazi na believe me not hiyo nafsi yako haitonyamaza hata ujitahidi kiasi gani. I was there, have been there nikajikausha kwa kadri niwezavyo ...'nafsi, dhamira' haikutulia mpaka...
thanks a lot my friend!!
hili pepo na lishindwe kabisa linaninyima raha sana

Hata sio pepo mydia, ni kuwa maishani mwako kuna 'void' that need to be filled. Wengi hawaielewi na wengi wanahisi kuwa babako mlezi ameujaza moyo wako na hivyo anatosha, ninakwambia tu kuwa hatoshi, hata awe ni mwema kiasi gani, kile kitendo cha wewe kujua tu kuwa huyu sio babako mzazi tayari ni msukule utakaokuandama mpaka utakapoamua kuufanyia kazi.
 
Last edited by a moderator:
na mimi mentioning him kwa cheo nilitaka nipate the actual views manake hiding it bado ningekuwa na obstructions.

kimsingi Kaunga i wish ungeufungua moyo wangu, sitak cheo chake na ndio maana toka wakati akiwa mkurugenz wa wizara fulan nilijua na sikumtafuta hata kuja kwenye ndoa yangu na hapo ndipo wapambe waliponiambaia nimtafute lkn niligoma kabisa kwamba hastahili kupokea mahari yangu asilan.

mahari alipokea baba mlezi ambaye mpaka leo ananilea mimi. sitaki anione nikoje kwa leo lkn japo ajue tu kwamba hata yule alomzaa anaishi manake ni kama vile alikuwa nataman nife tu.

Baba mlezi anatambua kuwa wewe ni mtoto wa kando?
 
Last edited by a moderator:
Nimejua unataka nini? kama nilivyokuambia hapo juu hata my wife wangu nilichomsaidia baada ya kumkataza kwa mda mrefu nikumpigia simu huyo baba yake ya kibaiologia na cha ajabu aliongea naye na kumwambia kwa sasa ameolewa but hiyo ilikuwa siri yetu mimi na yeye, hatukumwambia mama. Alikuwa satsfied ajabu mpaka leo hawajawahi ongea tena na huyo baba yake lakini wala hata hamfikilii na maanisha hamuumizi kama alivyokuwa anamuumiza mala ya kwanza. Kuna haja ya kutimiza matakwa yako dada yangu ongea naye ajue unaishi basiii!

Aksante sana kaka Henge, this satisfaction ndio inayotafutwa hapa kwa gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
mfuate tu ongea nae, ni mtu poa sana, na anao wengine wengi tu kama wewe, kwahiyo usipate tabu sana...
 
Sijui kama mtanielewa ila nataka nieleweke hata kwa kutumia akili za mwisho mlizo zaliwa nazo.

Mimi ni mtu mzima of course najua mema na mabaya na kwa upeo wangu leo hii ninatamani kujiweka huru ili nafsi iwe huru asilani.

Najijua kwamba baba aliyenilea sio baba yangu mzazi, lkn pia sitokuwa na moyo wa shukurani nisipomshukuru kwa moyo wa upendo na wa kujali wa baba aliyenilea. ukweli sijawah kujuta kulelewa nae na wala sijawah kuona tofauti kati yangu na watoto aliowazaa yeye. kanisomesha toka std 1 hadi elimu ya juu, kaniozesha kwa heshima zote na bado kanipa zawadi za kuanzia maisha mimi na hubby wangu. Ukweli najivunia kuwa naye as baba na naitwa kwa jina lake.

Wapendwa wangu kama mjuavyo damu nzito kuliko maji katika kukua kwangu wapambe (of which hawakosekanagi ) walinipa ukweli juu ya baba yangu mzazi. sijawah kumwona kwa macho ingawa namwona kwenye tv na magazeti tu. Mbaya zaid huyu baba sina uhakika kama alishawah kunitolea hata sh kumi ya matumiz lkn nimejikuta nafsi yangu ikitaka tu huyu baba ajue kwamba mm ni mwanae. kumwambia mama naogopa as nitamuumiza ama pia naweza kumuumiza baba. lakin nafsi inanisukuma sana nimtafute nimwambie ukweli.

sasa ishu inakuja hivi kwanza nitawezaje kumwambia huyu baba aniamini kwamba ni kweli?? wengi husema nimefanana naye usoni lkn sijui sana as najiona kama nimefanana na mama. kwa status yake pia naogopa isije ikawa headlines kwenye news ikamchafulia hadhi yake manake ni waziri fulan kwenye hii serikali.

on the other hand hivi nitakuwa nimemuumiza vipi mama yangu kwa kumwambia huyu baba ukweli?? je baba mlezi atachukulia poa ama ndio nitakuwa nimemkwaza?? ikumbukwe kwamba kanilea toka niko kachanga hadi leo hii na sijawah kujuta kwa yy kunilea.

naomba ushauri wako wa busara na sio matusi ama kashfa.
kitu cha moral dilemma
google kohlnberg stages, then fanya uamuzi kwa kutumia stage ya tano na ya sita
 
Dhamira yako na undani wako utimize " GO AHEAD " dadangu wee ni mkubwa kuhimili yote bila kujali nenda umContact Bio-dad wako na ajue UKWELI na hili liwesomo/fundisho kwake na kwa jamii.!! Tija la kujitambulisha kwake ni ahueni kwenu. Kuliko kujiweka katika CAGE ya maisha. after all kama atakukana ipo DNA itaprove ! Ni bora ufunguke sasa kuliko baada
ya too leti.....
Wanyumbani (baba n mama) watakuona jasiri na shujaa. Good luck
 
Kuna pointi ya msingi sana watoa ushauri wanaisahu,kwamba damu ni nzito kulikomaji embu sisi tujiweke katika position ya mtoa mada hivi ni kweli tusingekuwa tayari walau kumwambia huyo biological father kwamba mimi ni mwanao,mimi naona cha msingi utafute best aproach ya kumwambia huyo uliyeambiwa ni baba yako bila ya kumuumiza yoyote baba aliyekulea,mama yako wala huyo unayemfuata usimpe shida kama hatakupokea basi umpe tu info then you are done,lakini ukweli ni kwamba huyu baba yako aliyekulea hata jisikia vizuri kusikia habari hizi,so in whatever you are doing make sure humuumizi huyu mtu!!! Cooz you are everything to him
 
nakushauri we ishi maisha yako dada......mimi kuna ndugu yangu mmoja alilelewa na wazazi wangu toka mdogo kama wewe. Baada ya kuolewa akajipendekeza kwa sababu huyo mshua wake alikua na mkwanja.....bahati mbaya yule mzee alifariki baada ya mwaka toka yule ndugu yangu ajitambulishe.......kilichotokea siku ya msiba ilikua ni aibu na fedheha kwake. Hakupewa hata ruhusa ya kuingia sebuleni....alijifanya anazimia sijui baba sijui nini...watu wanamwangalia tu kama kichaa....kwenye sijui kuweka udongo...na historia fupi watu wakampa kubwa......ni noma aisee wewe piga kimya tu dada.
usisahau kwmba damu nzito kuliko maji!!! Yeye ashasemahana shida na mali za huyo jamaa so anataka tu ampe info kwamba yeye ni mwanae though kitu cha msingi amabcho anapswa atuambie ni kwamba ana muda gani toka ajue hizo habari?
 
pole bestito kwa matatizo hayo, kwa kukushauri tu best anza maombi ya kufunga huku ukitafuta nafasi ya kukaa na mama yako kwa upendo na furaha kisha anza kumwambia dukuduku lako uenda atakusikiliza na kukwambia ukweli wote, halafu kama una ndugu wakubwa washirikishe hilo jambo uenda nao watatoa msaada huo wa kujua baba yako.
pole sana na Mungu atakusaidia kama ukimwomba yeye kwani kwake hakuna linaloshindikana soma yeremia 32:27
Sijui kama mtanielewa ila nataka nieleweke hata kwa kutumia akili za mwisho mlizo zaliwa nazo.

Mimi ni mtu mzima of course najua mema na mabaya na kwa upeo wangu leo hii ninatamani kujiweka huru ili nafsi iwe huru asilani.

Najijua kwamba baba aliyenilea sio baba yangu mzazi, lkn pia sitokuwa na moyo wa shukurani nisipomshukuru kwa moyo wa upendo na wa kujali wa baba aliyenilea. ukweli sijawah kujuta kulelewa nae na wala sijawah kuona tofauti kati yangu na watoto aliowazaa yeye. kanisomesha toka std 1 hadi elimu ya juu, kaniozesha kwa heshima zote na bado kanipa zawadi za kuanzia maisha mimi na hubby wangu. Ukweli najivunia kuwa naye as baba na naitwa kwa jina lake.

Wapendwa wangu kama mjuavyo damu nzito kuliko maji katika kukua kwangu wapambe (of which hawakosekanagi ) walinipa ukweli juu ya baba yangu mzazi. sijawah kumwona kwa macho ingawa namwona kwenye tv na magazeti tu. Mbaya zaid huyu baba sina uhakika kama alishawah kunitolea hata sh kumi ya matumiz lkn nimejikuta nafsi yangu ikitaka tu huyu baba ajue kwamba mm ni mwanae. kumwambia mama naogopa as nitamuumiza ama pia naweza kumuumiza baba. lakin nafsi inanisukuma sana nimtafute nimwambie ukweli.

sasa ishu inakuja hivi kwanza nitawezaje kumwambia huyu baba aniamini kwamba ni kweli?? wengi husema nimefanana naye usoni lkn sijui sana as najiona kama nimefanana na mama. kwa status yake pia naogopa isije ikawa headlines kwenye news ikamchafulia hadhi yake manake ni waziri fulan kwenye hii serikali.

on the other hand hivi nitakuwa nimemuumiza vipi mama yangu kwa kumwambia huyu baba ukweli?? je baba mlezi atachukulia poa ama ndio nitakuwa nimemkwaza?? ikumbukwe kwamba kanilea toka niko kachanga hadi leo hii na sijawah kujuta kwa yy kunilea.

naomba ushauri wako wa busara na sio matusi ama kashfa.
 
umeona eeh, shosti sijui anajidanganya nini. Ni bora afanye anayotaka kufanya and for sure she is going to hurt some people in theprocess lakini so what? Bora apate anacho kitaka (baba yake ajue kuwa gfsonwin anaishi) baasi.
roho inaniuma kuona huyu baba mlezi akijua hizi taarifa za yeye kumtafuta bio fathwer wake itakuwaje!! Ipi itakuwa espond yake,ushauri wangu uleule kwa mtoa mada ahakikishe in whatever she is doing huyu baba yake mlezi haumizwi na kama ataumizwa panapobudi basi ni kwa kiasi kidogo sana,
 
Ah! hapa unatakiwa kuwa makini sana.kama walivyosema wachangiaji wengine,anaejua ukweli wa nani ni baba yako ni mama yako pekee.Kama hajakueleza mpaka unafikia Umri huu ina maana kuna siri kubwa anayo moyoni ambayo huenda kama ikivuja inaweza kugharimu uhai wa ndoa yake ama maisha yake kabisa ,kumbuka majeraha ya mapenzi huwa ni magumu sana kuyaponya.Kumfahamu baba yako wa kibaiologia ni muhimu kulingana na baba mwenyewe anavyolichukilia umuhimu wake.Wasiwasi wangu unaweza kumpata baba yako wa kibailojia kwa gharama ya kumpoteza mama yako.Kuwa mwangalifu sana kwa hili ni mama yako pekee anaeweza kukufungulia ukweli wa jambo hili kwa njia muafaka kabisa.
 
na mimi mentioning him kwa cheo nilitaka nipate the actual views manake hiding it bado ningekuwa na obstructions.

kimsingi Kaunga i wish ungeufungua moyo wangu, sitak cheo chake na ndio maana toka wakati akiwa mkurugenz wa wizara fulan nilijua na sikumtafuta hata kuja kwenye ndoa yangu na hapo ndipo wapambe waliponiambaia nimtafute lkn niligoma kabisa kwamba hastahili kupokea mahari yangu asilan.

mahari alipokea baba mlezi ambaye mpaka leo ananilea mimi. sitaki anione nikoje kwa leo lkn japo ajue tu kwamba hata yule alomzaa anaishi manake ni kama vile alikuwa nataman nife tu.
KAMA ALIVYOSEMA KAUNGA KUNA KITU KIMEKUTRIGGER SASA HIVI,SO USHAURI WANGU MWINGINE NI ONGEZA MAPENZI KWA BABA YAKO MLEZI INCASE ANYTHING KIKIHAPPEN AJUE KWAMBA UNAENDELEA KUMPENDA AND YOU WILL ALWAYS DO NA KUMUAPRECIATE AS WELL,MPE VIZAWADI CARING IZIDI NA VITU KAMA HIVYO!!!,huku ukiendelea kufuatilia best aproach ya baba yako kukujua(bio one)
 
kiukweli mimi huwa sifikirii kufukunyua nani baba yangu mzazi as long as napata kila ninachohitaji......mengine unafunika kombe mwanaharamu apite mwishowe ufe kwa presha kwa majibu utakayopewa na waziri ooh sorry baba yako mzazi,muache baba mlezi aishi kwa amani na mama yako bhana kama ulimkojolea utotoni akakuvumilia kwanini wewe leo usimvumilie hata kama umeshajua ukweli.
 
usisahau kwmba damu nzito kuliko maji!!! Yeye ashasemahana shida na mali za huyo jamaa so anataka tu ampe info kwamba yeye ni mwanae though kitu cha msingi amabcho anapswa atuambie ni kwamba ana muda gani toka ajue hizo habari?
Sawa kabisa lakini ukiangalia thread za dada hapa inaelekea baba anajua ila hajali wala hana mpango naye......mimi naona cha muhimu ni furaha........ kama story ya yule mchezaji Mario baloteli, watu wengi walimuona kichaa alipompa kubwa baba yake....kumbe lazima upime pande zote. Kama mtu ananyanyasika na anapata mateso ni sawa kabisa kumtafuta mzazi aliempotea, lakini kama mzazi anajua anamtoto alafu hakutafuti wewe ukimtafuta haisaidii kitu...anayetakiwa aumie ni mzazi sio mtoto...maana mtoto tayari ana watu wamecover hiyo nafasi ya wazazi.
 
......sisi wanaadamu watu wa ajabu sana. Mahaba na mshikamano wote huu ni kwasababu Mama Mzazi na Baba "mlezi" wapo hai.....

......hata ukiwa na umri na uwezo gani, siku huyo "baba" mlezi akizimika (mwenyezi mungu apishilie mbali ....) gfsonwin watu wa mwanzo kukukana mbele ya watu watakuwa the so called mliozaliwa tumbo moja...

Am writing through a very troubling close experience, hasa linapokuja suala la mirathi, iwe Kimila, Kidini au kiserikali..... Hata kama unauwezo wako, 'kutengwa' itakuwa -kisu cha mwanzo!-

Anyway, Mungu atakuongoza.

nimekua pasipo kumjua bab yangu, ila baade tulifahimshwa kuwa amefariki wakati huo nipo fm 3, haikuniuma kwa sababu sikuwahi hata kumjua nafananaje, kumbe yeye miaka yote anajua kabisa ana watoto sehemu, ila humwambia mke wake, basi kwenye mirathi akatuandika na sisi, alitugawia ardhi yake, nipo chuo mwaka wa nne ndipo ndugu wa baba wakatutafuta na kutufahamisha kuhusu huo urithi alioacha baba, hakuna kati yetu mwenye hamu ya kuona ile ardhi, watumie walioitunza miaka yote, yaani mtu alime shamba urithi apewe mwingine eti kisa baba alimwaga shahawa sehemu flani, big no, ndugu wa baba wanatushangaa mpaka leo, mapenzi ya baba ni zaidi ya mali jamani, baba yangu angenithamini angenilea, ndo tulichotaka kwake tu, umuhimu wa baba sio mirathi, akitaka apeleke hata kanisani, na wanaogombana sababu ya mali ni njaa na uvivu wa kufanya kazi,
 
Hii scenario yako ni ya kweli lakini nikupe msimamo wangu kama babu

1. 1975 dada akiwa amepata mchumba aliniletea katoto ka miezi mitatu ili awe huru kuolewa. Nilikachukua nakukalea kama kangu. Miaka mitatu iliyopita huyu mtoto akaja analia "kumbe uncle umenilea nilipokuwa Mtoto?" Nikamwambia mbona tulikokulia sisi ulezi ulikuwa baraka. Akaniambia nimemjua baba yangu nifanyeje? Nikamwambia ni jambo jema ila umshirikiswhe mama yako ili akupe baraka zake (unajua maana yake). Akamshirikisha mama yake akathibitisha; na kweli baba (biological) ana nafasi nzuri kijamii na kiuchumi. Akapokelewa kwa furaha na mama aliyeko kama mtoto wa kwanza wa mumewe. Kifupi aliamua kuwa hana sababu ya kujiunganisha na biological family na kubakia kwetu. Sababu anazijua yeye.

2. Miaka mitatu sasa imepita mwanangu wa kiume alinijia nakuniambia kuna msichana wa Chuo Kikuu amemwambia atjifungua mwezi mmoja ujao, na yeye ndiye mshirika wa mimba hiyo. Akaniambia wanataka kwenda kupima DNA ili ikiwa kweli amhudumie mtoto wake. Akaniuliza aoni yangu ni yepi? Nikamwambia na kumshukuru kwa taarifa na kumuomba aachane na masula ya DNA. Awe wake au wa mtu mwingine tuhakikishe binti anajifungua salama na kichanga chake tukilee ili akamilishe masomo yake. Nikamuapiza iwapo mama mtu atasema si mtoto wake akubali mtoto aende kwa baba yake. Mtoto akiamua kubakia kwetu atakuwa na haki zote pamoja na ukweli huo. Sababu ni ndogo MTOTO HAKUTUMA MAOMBI YA KUZALIWA KWENYE MAZINGIRA HAYO. Ni kweli kiimani sisi wengine tunaona ni mtihani mbele ya Mungu ambao unatulazimisha kiimani ya kumtendea mema kiumbe wa Mungu.

3. Kuna mtoto alizaliwa wakati wa vita ya pili (before 1950). Baba akatoa taarifa kwa wahusika wote kuwa ana mtoto na angependa wajue hilo. Na alipooa tena akamwambia mkewe kuwa ana mtoto kwa hiyo kwenye matumizi awe anamgawia na huyo mtoto. Mkewe alifanya vyema kupeleka matumizi ya mtoto ambaye alikuwa analelewa na watu fukara sana. Kwa bahati nzuri walimlea kwa upendo kuzidi hata wa watoto wao. Bahati mbaya yule baba alifariki kwa ajali.

Kama ulivyo wewe yule mtoto akiwa miaka 8 naye akapata hamu kwenda kwa baba yake wa damu ambaye kwa bahati mbaya alikuwa amefariki. Alipokelewa na babu yake na mama mdogo vizuri na kupewa nafasi yake kama mtoto wa familia. Ni hadithi ndefu lakini inaonyesha mazingira ya kuzaliwa na malezi.

4. Wapo wababa waliofurahia sana watoto wao walipojulikana. Wapo pia waliojuta.

Mantiki

1. Mtoto anapozaliwa ni "vulnerable" na akipata a "home" ni kitu kikubwa kwa sababu atatayarishiwa mafanikio au kushindwa kwa maisha yake.

2. Malezi yanakufanya uwe wewe ulivyo. Nina maana ungelelewa kidhaifu ungekuwa dhaifu tu. Kwa hiyo kama waswahili wasemavyo Kuzaa hata panya wanazaa lakini malezi ni mambo yote. Mtu anayechukua jukumu la kulea ni mtu wakumheshimu sana kuliko kitu kingine, na anafanya hivyo kwa majaliwa ya Mungu si uwezo.

3. Kuzaa au kuzaliwa ni matakwa ya Mungu. Kulea ni majaliwa na si uwezo. Fikiria umri huu unavyohangaika kumlea mtoto wako kwenye ugonjwa, furaha hadi mnaongea naye anakuchekesha unamchapa akikosea, ni tunu zinazotokana na malezi si uzazi.

4. Wanadamu ni "social animals". Wazazi wana fursa ya ulezi kwa dhamira yao. Walezi wana fursa ya ulezi kwa "default" yaani kimazingira. Kufanikiwa kumlea mtoto hata ajitambue, kwangu mimi ni baraka; sitarajii zawadi kwa kulea INATOSHA mtoto akijitambua na yeye alee watoto wake.

5. Tendo za kuzaa lina mahusiano na mahitaji ya kimwili ("biological"). Tendo la kulea lina mahusiano na matakwa ya kijamii (social obligation). Haya mawili yana uzito tofauti. Ni imani yangu sasa hivi suala ulilo nalo ni la kijamii zaidi kuliko uzazi. Kwa hiyo suluhisho lake ni la kijamii zaidi kuliko la uzazi.

Inawezekana ukamtonesha mama yako kwa kumfanya ajihisi msaliti. Inawezekana ukamtonesha mama yako kwa kujiona si mwaminifu kwa baba aliyekulea. Inawezekana baba aliyekuelea asikuelewe kwa kudhani kuna kitu kakifanya wewe hujaridhika nacho. Inawezekana unachotarajia kwa kumtambua baba yako kikakupa faraja au majuto. Nafasi aliyonayo baba yako wa damu na mke wake wa sasa inaweza kutatizwa au kunufaika. Inawezekana ndugu zako (wadogo zako) pande zote wasikuelewe au wakufarahie sana au mchanganyiko.

USHAURI

Si suala la ukweli ni upi, ni suala la jinsi gani utafanikisha kupata matokeo gani. Anzia kumshirikisha mama yako. Atakachosema umtii, maana anaujua ukweli kuliko mtu ye yote. Na kama maumivu ndiye ataumia kuliko mtu ye yote.

Chukua ushauri unaokufaa achana na mengine. Wa kwanza kufanya maamuzi ni wewe sisi tunashauri tu.
 
Sawa kabisa lakini ukiangalia thread za dada hapa inaelekea baba anajua ila hajali wala hana mpango naye......mimi naona cha muhimu ni furaha........ kama story ya yule mchezaji Mario baloteli, watu wengi walimuona kichaa alipompa kubwa baba yake....kumbe lazima upime pande zote. Kama mtu ananyanyasika na anapata mateso ni sawa kabisa kumtafuta mzazi aliempotea, lakini kama mzazi anajua anamtoto alafu hakutafuti wewe ukimtafuta haisaidii kitu...anayetakiwa aumie ni mzazi sio mtoto...maana mtoto tayari ana watu wamecover hiyo nafasi ya wazazi.
lakini huyu hajawahi kusikia kauli ya baba yake hata mara moja juu yake nahisi ana haki ya kujiridhisha kwa hilo.then hapo atakuwa free milele
 
Sijui kama mtanielewa ila nataka nieleweke hata kwa kutumia akili za mwisho mlizo zaliwa nazo.

Mimi ni mtu mzima of course najua mema na mabaya na kwa upeo wangu leo hii ninatamani kujiweka huru ili nafsi iwe huru asilani.

Najijua kwamba baba aliyenilea sio baba yangu mzazi, lkn pia sitokuwa na moyo wa shukurani nisipomshukuru kwa moyo wa upendo na wa kujali wa baba aliyenilea. ukweli sijawah kujuta kulelewa nae na wala sijawah kuona tofauti kati yangu na watoto aliowazaa yeye. kanisomesha toka std 1 hadi elimu ya juu, kaniozesha kwa heshima zote na bado kanipa zawadi za kuanzia maisha mimi na hubby wangu. Ukweli najivunia kuwa naye as baba na naitwa kwa jina lake.

Wapendwa wangu kama mjuavyo damu nzito kuliko maji katika kukua kwangu wapambe (of which hawakosekanagi ) walinipa ukweli juu ya baba yangu mzazi. sijawah kumwona kwa macho ingawa namwona kwenye tv na magazeti tu. Mbaya zaid huyu baba sina uhakika kama alishawah kunitolea hata sh kumi ya matumiz lkn nimejikuta nafsi yangu ikitaka tu huyu baba ajue kwamba mm ni mwanae. kumwambia mama naogopa as nitamuumiza ama pia naweza kumuumiza baba. lakin nafsi inanisukuma sana nimtafute nimwambie ukweli.

sasa ishu inakuja hivi kwanza nitawezaje kumwambia huyu baba aniamini kwamba ni kweli?? wengi husema nimefanana naye usoni lkn sijui sana as najiona kama nimefanana na mama. kwa status yake pia naogopa isije ikawa headlines kwenye news ikamchafulia hadhi yake manake ni waziri fulan kwenye hii serikali.

on the other hand hivi nitakuwa nimemuumiza vipi mama yangu kwa kumwambia huyu baba ukweli?? je baba mlezi atachukulia poa ama ndio nitakuwa nimemkwaza?? ikumbukwe kwamba kanilea toka niko kachanga hadi leo hii na sijawah kujuta kwa yy kunilea.

naomba ushauri wako wa busara na sio matusi ama kashfa.

This is very complicated. Du. and I know it may not be fiction. Neno linalonijia haraka haraka ni "truth and reconcilition." Linatumika katika siasa, lakini linao uhusiano na hisia za chuki katika moyo wa binadamu. Kwamba mara nyingi ukweli una desturi ya kusababisha msamaha.

Ukweli katika hili jambo ni kwamba baba yako wa damu alipishana kitu na mama yako mzazi. Hatuwezi kujua ni kipi, na pengine si vizuri kukifuatilia sana kwa sababu inaweza kufanana na kufukua choo. Lakini je, kufukua choo husaidiaje katika mazingira ya truth and reconciliation? Mimi naona watu watatu katika inner circle ya mgogoro, na mtu mmoja kwenye circle ya pili ya mgogoro.

Mimi ningefanya hivi: Ningempigia simu huyu baba wa kibaolojia au ningemfuata mahali nimweke katika mazingira ambayo tupo wawili tu. Nikiwa katika mazingira hayo ningemwambia kwamba nina habari za kuaminika kwamba yeye ndiye baba mzazi wa kibiolojia, na kwamba natamani kujua ukweli kutoka kwake mwenyewe kwa lengo la kutua mzigo nilio nao moyoni. Hapa ingekuwa vizuri kutanguliza maelezo kuhusu malengo yako; kwamba malengo hayo hayana uhusiano na mahitaji ya misaada ya mali kwa kuwa hauna mahitaji hayo; kwamba unayo mahitaji ya kisaikolojia ambayo yanaweza kumalizwa na ukweli.

Atakubali, atafunguka, ataomba msamaha. Ana sababu za kisiasa na kijamii kushuka. Katika mila za makabila mengi ya kibantu, msamaha utaombwa kwa faini kulipwa ikiwa ishara ya kutubu. Na faini hii analipwa baba mlezi pamoja na mama yako mzazi. Hii inaweza kutosha kubadili jina. Lakini wewe unahitaji kuwa na roho ngumu sana ya msamaha. Utahitaji kumsamehe huyu baba yako wa kibaolojia kwa sababu kosa kubwa zaidi kuliko mengine kakufanyia wewe, ambapo kosa la pili ingawa linaweza liwe na unafuu fulani kamkosea mama yako.

angalizo hapo ni maneno haya matatu: truth, reconciliation, na neno linaitwa Msamaha.
 
Back
Top Bottom