mama firstborn
Member
- May 30, 2023
- 43
- 130
Habari za Jumatatu,
Naomba ushauri kuhusu rafiki yangu huyu.
Huyu rafiki yangu alizaa na mpenzi wake miaka ya tisini mwishoni, lakini hawakufanikiwa kuwa pamoja, Baba alioa mwanamke mwingine, akabaki kuhudumia mtoto wake tu japo alikuwa anaishi na mama yake. Ila huyu mzazi mwenzie ambaye ni rafiki yangu naye baada ya miaka kadhaa alipata mume ambaye anamtoto wa kike, aliyezaa na mwanamke mwingine ambaye alishafariki.
Rafiki yangu akaona ni vyema hapa, coz na yeye anamtoto wa kike, hasa umri walipishana mwaka mmoja tu, aliona watakuwa marafiki baada ya kuingia kwenye ndoa. Ila baada ya kuolewa mzazi mwenzie alimfuata na kumwambia kuwa anamtaka mtoto wake ili amlee yeye mwenyewe na sio na mwanaume mwingine.
Rafiki yangu akaona hapana mtoto anataka akaenae yeye mwenye. Kwa kifupi uliibuka ugomvi mkubwa tu. Sijajua walifikia hatua gani maana namuona kama kuna vitu anaficha huyu my friend, ila naamini alimlisha maneno mtoto kuhusu baba yake, ila baadae mtoto akabaki nae na mwanaume wake aliyeolewa nae.
Mtoto alivyokuwa mkubwa akahitaji kuwa karibu na baba yake, alijaribu kuwasiliana na baba yake lakini alikuwa haonyeshi ushirikiano wowote. Alijaribu hivyo mara kadhaa lakini alishidwa kabisa, pia alijaribu hata kufika nyumbani kwake alishidwa kabisa.
Mwaka jana alihitaji kwenda kwa baba yake laini still baba hakumtaka kabisa, rafiki yangu alijaribu kuongea na baba yake, naye hakutaka hata kusikia kabisa.
Mtoto akataka kujua shida ni nini, amekuja kugundua kuwa kumbe kipindi yupo mdogo baba yake alikuwa anamtaka kumchukua ila mama aligoma kabisa na ugomvi juu.
Pia binti anamuuliza maswali mama yake anashidwa hata kumjibu mengine. Kwa sasa mtoto mwenyewe hataki kwenda hata kwa mama yake, yupo tuu mwenyewe.
Ila mimi nimeona baba yake mzazi ni mtu mwenye uwezo sana tena sana. Hata kuliko alipolelewa yeye, nafikiri mtoto kinamuumiza sana. Rafiki yangu ameshidwa nini cha kufanya.
Ila mimi naamini huenda mtoto akiwa mdogo alimlisha maneno ya kumjibu vibaya baba mtoto ili abaki nae. Yeye alisema kuwa aliona ni vyema kwa sababu mwanaume aliyemuoa nae alikuwa na mtoto wa kike, alitaka akae nae kwa sababu aliona itakiwa vyema apate mtu wa kucheza nae, na kujenga mahusiano mazuri yeye na mume wake.