Nifanyeje baba yangu mzazi ajue kwamba mimi ni mwanae?

Kaunga kama angelijua kwamba ninaish basi kama baba walau angetake trouble kujua where about zangu. najua kwa mama yangu mzazi kumpata mtu ambaye alimpenda na kukubali kunilea hiyo kwake ni faraja ambayo asingependa kuipoteza. na ndio mana hata mimi hajawah kuniambia wazi baba yako ni yupi ingawa anajua kwamba najua huyu mlezi sio baba yangu.

mpaka nakuja hapa nimekuwa nimelilibebea hili moyoni for yrs,nimejiuliza maswali mengi ambayo najiuliza na kujijibu. napata ucungu sana pale nionapo wanangu wana umri unaolingana na watoto wa baba, nashindwa kuelewa hivi watakuja kuwa na maisha gani mbeleni manake wasije wakaoana ( ingawa proba ni ndogo) lkn ni mawazo tu.

sina ninachotaka kutoka kwake ila tu ajue kwamba ninaishi kama alisha wah kuassume kwamba nimekufa

hivi sijasoma sehemu ambapo alijua juu ya ujio wako duniani, ila kutokana na system ya jeshi hakuweza kuwa responsible?
Unless uniambie hakujua kabisa kama alimpa mama yako mimba ndipo nitaelewa, lakini kama hivyo sivyo ina maana anajua kuna mtu duniani lakini HAJALI. Sad lakini ndio ukweli wenyewe.
Umelibeba kwa miaka mingapi mpaka sasa?
 
Umesema mwenyewe, bio-baba wako ni public figure hivyo watoto wake ni rahisi kuwajua so sidhani kama itakuwa ni shida kiasi hicho.
Mimi nafikiri gfsonwin, unajua unachotaka kukifanya; kwanini usifanye tu na u-get over with. Haijalishi nani ataumia on the way, lakini itii hiyo curiosity yako.
By the way, ni lini uliambiwa na hao jirani juu ya uwepo wa huyo baba yako?

Very Good Kaunga sasa umemuelewa vizuri sana gfsonwin. Mimi nimeshasema huyu kumshauri aachane na haya mawazo haisaidii sana maana inaonekana ameshapambana nayo sana. Kilichobaki ni kumsaidia jinsi ya kukabiliana na matokeo ya anachotaka kukifanya.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama mtanielewa ila nataka nieleweke hata kwa kutumia akili za mwisho mlizo zaliwa nazo.

Mimi ni mtu mzima of course najua mema na mabaya na kwa upeo wangu leo hii ninatamani kujiweka huru ili nafsi iwe huru asilani.

Najijua kwamba baba aliyenilea sio baba yangu mzazi, lkn pia sitokuwa na moyo wa shukurani nisipomshukuru kwa moyo wa upendo na wa kujali wa baba aliyenilea. ukweli sijawah kujuta kulelewa nae na wala sijawah kuona tofauti kati yangu na watoto aliowazaa yeye. kanisomesha toka std 1 hadi elimu ya juu, kaniozesha kwa heshima zote na bado kanipa zawadi za kuanzia maisha mimi na hubby wangu. Ukweli najivunia kuwa naye as baba na naitwa kwa jina lake.

Wapendwa wangu kama mjuavyo damu nzito kuliko maji katika kukua kwangu wapambe (of which hawakosekanagi ) walinipa ukweli juu ya baba yangu mzazi. sijawah kumwona kwa macho ingawa namwona kwenye tv na magazeti tu. Mbaya zaid huyu baba sina uhakika kama alishawah kunitolea hata sh kumi ya matumiz lkn nimejikuta nafsi yangu ikitaka tu huyu baba ajue kwamba mm ni mwanae. kumwambia mama naogopa as nitamuumiza ama pia naweza kumuumiza baba. lakin nafsi inanisukuma sana nimtafute nimwambie ukweli.

sasa ishu inakuja hivi kwanza nitawezaje kumwambia huyu baba aniamini kwamba ni kweli?? wengi husema nimefanana naye usoni lkn sijui sana as najiona kama nimefanana na mama. kwa status yake pia naogopa isije ikawa headlines kwenye news ikamchafulia hadhi yake manake ni waziri fulan kwenye hii serikali.

on the other hand hivi nitakuwa nimemuumiza vipi mama yangu kwa kumwambia huyu baba ukweli?? je baba mlezi atachukulia poa ama ndio nitakuwa nimemkwaza?? ikumbukwe kwamba kanilea toka niko kachanga hadi leo hii na sijawah kujuta kwa yy kunilea.

naomba ushauri wako wa busara na sio matusi ama kashfa.

Nakushauri we ishi maisha yako dada......mimi kuna ndugu yangu mmoja alilelewa na wazazi wangu toka mdogo kama wewe. Baada ya kuolewa akajipendekeza kwa sababu huyo mshua wake alikua na mkwanja.....bahati mbaya yule mzee alifariki baada ya mwaka toka yule ndugu yangu ajitambulishe.......Kilichotokea siku ya msiba ilikua ni aibu na fedheha kwake. Hakupewa hata ruhusa ya kuingia sebuleni....alijifanya anazimia sijui baba sijui nini...watu wanamwangalia tu kama kichaa....kwenye sijui kuweka udongo...na historia fupi watu wakampa kubwa......ni noma aisee wewe piga kimya tu dada.
 
Ni upepo tu, labda you are going thru kipindi kigumu kwenye maisha yako kwa sasa, so unahitaji kitu kingine cha kukupa furaha ama a kind of distraction kusahau unachopitia.

Hujawahi kaa siku moja ukamkumbuka hata mtu ambaye huwa humkumbuki kabisa? Kwa ajili tu umeboreka na a certain situation?

Nadhani jipe muda, mwezi labda au miwili hadi mitatu. Ukiona haipungui then unweza kuanza mchakato wa kuongea naye. Ila itakuwa vizuri ukimshirikisha kwanza mama yako.

At the end of the day, we are human, we have our weaknesses and desires. Kama itakupa furaha na more meaning to life, mtafute while you can. We live once!

thanks a lot my dearest.
sasa nifanyeje haya mawazo yanitoke?? yaani ni a second wk sasa naish kwa mawazo sana na moyo uko mzito sana sana
 
sihitaj mafao yake hata senti manake ya kwangu tu kwa miaka niliyofanya kazi yananitosha. wala sitak hata kuitwa kwa jina lake manake halitonisaidia kitu.

Vipi akisema
"samahani mwanangu, ninajua sikuwa baba ambaye nilipaswa kuwa; you are my girl sio lazima ubadilishe jina lakini naomba nimake it up to you; chukua shamba hili la heka 500 na mradi huu simamia" ma machozi juu; kweli utakataa na kusema sina shida na senti yako?

lengo la kumtafuta ni nini kama sio kumake up?
Usijidanganye bwana, (maana kwa kuirudia hiyo sentensi mara 101 ina maanisha unajishawishi hivyo) nimekuuliza for how long ulijua kuhusu huyo baba yako (years) and why now? Maana hilo swali ndio mzazi wako atakuwa anajiuliza na honestly itamuumiza sana.
Dont be selfish.

Umeshauriwa mconsult kwanza mama yako, sijui unaona ugumu gani.
 
Kwenye bold yes, just a sense of belonging and love, typical human behavior (Maslow's hierarchy of needs)

She is just being human! Ndio maana nimemwambia, kama itampta more meaning to her life akamtafute tu.

......hujanisoma ukanielewa.

Nimezungumzia experience yangu, ambayo nimeona ndugu wa tumbo moja walivyopasua udugu wao baada ya kifo cha mzazi wao!

Anyway, ni ngumu kuelewa Uzito wa jambo hili mpaka litakapokupata. Ama kwa hakika siku likimpata mtu ndipo atapoujua uzito wa jambo hili.

It's only a sense of belonging Kongosho, pesa na mali sio kila kitu hapa duniani!
 
Wanajamvi wenzangu, niawashukuru sana kwa ushauri wenu uliojaa busara na hekima san. kwa mara ya kwanza kwa experience yangu ya kuweka nyuzi hapa huu uzi haujachakachuliwa na kila mtu ametoa michango iliyojaa hekima sana. Ukweli katika hili nawashukuru sana snaa.

ingawa sijamwona dada yangu AshaDii na Fixed Point na kipenzi changu cacico na mtani wangu The Boss lkn nyie wote mliotoa mawazo yenu nimeyapokea kwa moyo mkunjufu sana.

huu hapa ndio msimamo wangu.

nitamwomba sana Mungu anipe uwezo wa kusahau uwepo wake na nitajifunza kuona kwamba ni aina ya maisha ambayo yanaweza kumtokea mtu yyte so siko peke yangu. Pia nitajifunza kwamba kuwa na baba mzazi ama baba mlezi sio big deal iwapo tu aliyepo anakutosheleza kimalezi.......

i will leave the matter as it is na sitataka hata kumuwaza tena,,,,,,,,,,,,ni ngumu sana sana hata Nguruvi3 anajua hilo lkn nitajitahd ili nisije nikajikuta mwishomwe namuumiza mama yangu kipenzi, baba yangu kipenzi na ndugu zangu wapendwa. Pia sitaki kumuudhi chubby na wanangu kwa jambo ambalo kama mlivyosema halitonisaidia maishani mwangu.

MBARIKIWE SANA SANA RAFIKI ZANGU. NA MUNGU AWAZIDISHIE HEKIMA NA BUSARA KATIKA KUSHAURI WENGINE.

Lots of love
gfsonwin
 
hivi sijasoma sehemu ambapo alijua juu ya ujio wako duniani, ila kutokana na system ya jeshi hakuweza kuwa responsible?
Unless uniambie hakujua kabisa kama alimpa mama yako mimba ndipo nitaelewa, lakini kama hivyo sivyo ina maana anajua kuna mtu duniani lakini HAJALI. Sad lakini ndio ukweli wenyewe.
Umelibeba kwa miaka mingapi mpaka sasa?
Kaunga mimi nilijua kamba huyu baba mlezi sio baba yangu nikiwa chuoni mwaka wa kwanza na hapo ni miaka 10+ toka sasa
 
Last edited by a moderator:
Vipi akisema
"samahani mwanangu, ninajua sikuwa baba ambaye nilipaswa kuwa; you are my girl sio lazima ubadilishe jina lakini naomba nimake it up to you; chukua shamba hili la heka 500 na mradi huu simamia" ma machozi juu; kweli utakataa na kusema sina shida na senti yako?

lengo la kumtafuta ni nini kama sio kumake up?
Usijidanganye bwana, (maana kwa kuirudia hiyo sentensi mara 101 ina maanisha unajishawishi hivyo) nimekuuliza for how long ulijua kuhusu huyo baba yako (years) and why now? Maana hilo swali ndio mzazi wako atakuwa anajiuliza na honestly itamuumiza sana.
Dont be selfish.

Umeshauriwa mconsult kwanza mama yako, sijui unaona ugumu gani.

hicho ni kitu ambacho siwez kukubali na sababu kubwa ni kwamba hata hubby aliwah kuniambia ukileta chochote toka kwa huyu bio dad basi utarudi nacho ulikokitoa. sitoweza kumwabia sitak ila sitoweza kupokea chochote zaid ya kumwambia tu aendelee kuvitunza kwanza.
swala la kum-consult mama hilo linategemea zaid akili inaamkaje manake namjua mama yangu na maisha aliyoish na mumewe ya ndoa. najua ataumia sana sana na sitak kumuumiza kwa lolote huyu mama ama baba
 
swali zuri sana hili.
bada ya kuambiwa na watu nikachunguza kwa mama nikakuta ni kweli ingawa mama hakuniambia yy.
niliambiwa na mdogo wake na mama (ma'mdogo) ukweli na alinionyesha hadi picha ya baba ambazo walipiga na mama wakati wako na uhusiano. kutoka hapo nikaanza kuangalia nilivyosadifu na ndugu zangu nikagundua kuna utofauti mkubwa sana.

lkn pia nilipochukulia tarehe ya mama kufunga ndoa na niliyozaliwa iliacha gap kubwa sana na niliwah kuisoma kadi ya mama ya kliniki akiwa na mimba yangu iliandika jina la huyu baba mzazi. sijawah kumwambia mama hili manake niliiona kwa bahati mbaya tu kabatini mwake.

istoshe niliambiwa kwamba nilipozaliwa aliambiwa ila kwasabau ya system ya jeshi ya wakati huo hakuweza kusema juu ya hatma yangu, so alimwacha mama kwenye wakati mgumu sana na hapo ndipo walipopotezana kimawasiliano.

Bandugu,

BAK et al, ni waziri yupi mwenye chembe chembe za kijeshi katika hili baraza?
 
hata sijui nianzie wapi kushauri hili....
unalijua fika unalolitaka my dear friend gfsonwin na kweli nimekusoma na kuona umeshakata shauri la kuonana na huyu waziri.
Watu wengi wamekushauri na kujaribu kukufikirisha in a negative way, ngoja mimi nijaribu in a positive way tuone pia utajisikiaje.
Imagine unatoroka kwa mama + babako (hawa kweeli mimi ndo naamini ni wazazi wako), unapanga miadi na baba (yako peke yako, maana hata Mungu sidhani kama anamkubali kuwa ni babako). unafika, baba anakupokea vizuri, unaongea naye naye anakumbuka kila kitu, anaamua "sababu umejileta" anakupokea. anaongea na mamsap, mama naye kama yupo kama mimi anakupokea (afterall umeshaolewa na una maisha yako, so siyo big deal, pia alikuzaa kabla yeye hajaolewa). wanaamua kukukaribisha rasmi home, kukutambulisha kwa ndugu zako, jamaa na marafiki..... sherehe kama ile ya "mwana mpotevu"......
utakataa kukaribishwa? kwa grounds gani? kwa nini ulienda in a first place? hainiingii akilini sababu yako kuwa "just ajue naishi....." so what?
nina uhakika unataka kuungana na familia ya waziri, kwa hiyo utakubali ukaribisho maana huna sababu ya kukataa, usingeenda kama hukutaka kuungana na hiyo familia. wewe unamjua babako, inatosha, siyo lazima yeye ajue.... na kwa uhakika kabisa anajua kuwa upo na unaishi, HATAKI KUKUTAFUTA. kama unavyosema ulizaliwa wazazi wakiwa wadogo sana kwa hiyo lazima huyo waziri anakujua myumbani kwa wazazi wa mamako.....
sasa kama utapokea mwaliko wa waziri....... hapo sasa, unadhani babako na ndugu zako watajisikiaje? hasa babako ambaye alitumia kila alichonacho kukufikisha hapo ulipo? naweza nikawa sikufahamu saaanaaaa, lakini kwa uchache wa ninavyokufahamu sidhani kama ulilelewa kirahisi sana na babako.... babako alivumilia yoooteeee kukufikisha hapo ulipo..... mtoto wa kike ambaye si wake.
Kama nilivyosema mwanzo, tunajitahidi tu kukuwazisha, solution unayo mwenyewe.... wewe ndo unajua haswa unachokitaka.... follow your heart.
 
Last edited by a moderator:
Bandugu,

BAK et al, ni waziri yupi mwenye chembe chembe za kijeshi katika hili baraza?

umesahau kwamba mawaziri karibu wote walipita jeshini miaka hiyo?? ama unafikiri ni mjeda kama mjeda??
 
umesahau kwamba mawaziri karibu wote walipita jeshini miaka hiyo?? ama unafikiri ni mjeda kama mjeda??

gfsonwin, nikijaribu kunukuu maelezo yako hapo juu kwamba ' kulingana na system(sema: mfumo) wa jeshi wa wakati huo .... National Service nachelea kusema haiingiaa hapo...kumbuka jeshi (JWTZ) ndo lenye mfumo mgumu linapokuja suala la kuoa /kuolewa. gotcha u!
 
hata sijui nianzie wapi kushauri hili....
unalijua fika unalolitaka my dear friend gfsonwin na kweli nimekusoma na kuona umeshakata shauri la kuonana na huyu waziri.
Watu wengi wamekushauri na kujaribu kukufikirisha in a negative way, ngoja mimi nijaribu in a positive way tuone pia utajisikiaje.
Imagine unatoroka kwa mama + babako (hawa kweeli mimi ndo naamini ni wazazi wako), unapanga miadi na baba (yako peke yako, maana hata Mungu sidhani kama anamkubali kuwa ni babako). unafika, baba anakupokea vizuri, unaongea naye naye anakumbuka kila kitu, anaamua "sababu umejileta" anakupokea. anaongea na mamsap, mama naye kama yupo kama mimi anakupokea (afterall umeshaolewa na una maisha yako, so siyo big deal, pia alikuzaa kabla yeye hajaolewa). wanaamua kukukaribisha rasmi home, kukutambulisha kwa ndugu zako, jamaa na marafiki..... sherehe kama ile ya "mwana mpotevu"......
utakataa kukaribishwa? kwa grounds gani? kwa nini ulienda in a first place? hainiingii akilini sababu yako kuwa "just ajue naishi....." so what?
nina uhakika unataka kuungana na familia ya waziri, kwa hiyo utakubali ukaribisho maana huna sababu ya kukataa, usingeenda kama hukutaka kuungana na hiyo familia. wewe unamjua babako, inatosha, siyo lazima yeye ajue.... na kwa uhakika kabisa anajua kuwa upo na unaishi, HATAKI KUKUTAFUTA. kama unavyosema ulizaliwa wazazi wakiwa wadogo sana kwa hiyo lazima huyo waziri anakujua myumbani kwa wazazi wa mamako.....
sasa kama utapokea mwaliko wa waziri....... hapo sasa, unadhani babako na ndugu zako watajisikiaje? hasa babako ambaye alitumia kila alichonacho kukufikisha hapo ulipo? naweza nikawa sikufahamu saaanaaaa, lakini kwa uchache wa ninavyokufahamu sidhani kama ulilelewa kirahisi sana na babako.... babako alivumilia yoooteeee kukufikisha hapo ulipo..... mtoto wa kike ambaye si wake.
Kama nilivyosema mwanzo, tunajitahidi tu kukuwazisha, solution unayo mwenyewe.... wewe ndo unajua haswa unachokitaka.... follow your heart.

nimekuelewa my dearest...............lkn ukweli sitaki hata jina kwa huyu baba mzazi ila nilitaka tu ajue kwamba ninaish manake kweli umzae mtoto umwache pasi hata salam ya mdomo??
 
Kaunga mimi nilijua kamba huyu baba mlezi sio baba yangu nikiwa chuoni mwaka wa kwanza na hapo ni miaka 10+ toka sasa

So why now?
And dont give the ...past two weeks thing...
lazima kuna kitu kimekutrigger, just be honest to yourself.

Do you want your popular dad to know of your achievement and maybe be proud of you?
Is the feeling of my dad is a minister (you know the power thing, sio lazima pesa) is so good that you want people around you to know of course na watoto zako (wajukuu wa waziri)

Nisamehe kwa kuwa mkavu hivi, lakini as a friend l think l should.
huu uzi huenda ungepata mchango tofauti kama usingemention cheo na umaarufu wa baba biological; na huenda hata mama, baba, na mumeo wasinge react the way tunavyotilia mashaka kama ungemtafuta 10+ years ago wakati hajawa waziri (au alikuwa tayari?) Ndio maana nimeshauri nyuma, kama umeweza kaa na hicho kitu kwa kipindi chote hicho kwanini usivumilie miaka 2 ijayo in case hatarudi kwenye baraza la mawaziri.
 
sredi closed. Dada mkubwa gfsonwin hebu utendee haki huu uzi kwa kuufungilia mbali, maana ushakata shauri hakuna haja ya kuendelea kujadili.

Nimependa kuwa japokuwa ulikuja na msimamo thabiti wa kutaka kumuona baba lakini umeweza kusikiliza ushauri na kubadilika, japokuwa ni mzigo mzito kwako. FP amegonga ikulu hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, nikijaribu kunukuu maelezo yako hapo juu kwamba ' kulingana na system(sema: mfumo) wa jeshi wa wakati huo .... National Service nachelea kusema haiingiaa hapo...kumbuka jeshi (JWTZ) ndo lenye mfumo mgumu linapokuja suala la kuoa /kuolewa. gotcha u!

basi go and look for him manake yaelekea wewe una info zaid yangu
 
Mimi binafsi nahisi nisengelimtafuta kwa sababu sipendi kuwa a nuisance kwa mtu yoyote na hapo kwa uchache lazima utakuwa udhia kwa watoto wake na mkewe hata kama watakuja ku-accept baadae

Una uhakika alikuwa na habari ya wewe kuzaliwa kwako na Ana resources zote za kukutafuta lakini hajafanya hilo, ikimaanisha hataki

Labda hataki kwa sababu anathamini familia yake aliyonayo zaidi ya uhusiano wa kukutambua tu kuwa wewe una vinasaba vyake, au labda hataki kwa sababu nyenginezo

Si api, lakini nisingemtafuta mtu aliyejua uwepo wangu na kunidharau

Baba uliyenae si baba mlezi kama unavyomwita bali baba mzazi maana kafanya yote kwako kama mzazi, tena mzazi bora, anatakiwa afanye kwa mwanawe

Vinasaba kitu gani?
 
wewe jilipue tu ...maisha ni haya haya
halafu uchagani bwana l kumjua baba yako origino ni issue mi dada yangu kaolewa na mtu ambae dada yake ni mtoto wa baba yetu
yaani wifi yake ni dada yake ...chezeiya!
 
Vipi akisema
"samahani mwanangu, ninajua sikuwa baba ambaye nilipaswa kuwa; you are my girl sio lazima ubadilishe jina lakini naomba nimake it up to you; chukua shamba hili la heka 500 na mradi huu simamia" ma machozi juu; kweli utakataa na kusema sina shida na senti yako?

lengo la kumtafuta ni nini kama sio kumake up?
Usijidanganye bwana, (maana kwa kuirudia hiyo sentensi mara 101 ina maanisha unajishawishi hivyo) nimekuuliza for how long ulijua kuhusu huyo baba yako (years) and why now? Maana hilo swali ndio mzazi wako atakuwa anajiuliza na honestly itamuumiza sana.
Dont be selfish.

Umeshauriwa mconsult kwanza mama yako, sijui unaona ugumu gani.
ha haaa, niliandika comment yangu kabla sijaisoma hii yako......
hebu nisome hapo yaani nimejitahidi sana kumfikirisha kama ulivyoandika hapa, lol! unawaza ninachowaza mimi wakati mimi nawaza..... mbona hukuyaandika haya before?
 
Back
Top Bottom