Nifanyaje! ili huyu mwanaume anielewe?

Hebu tueleze wewe una kazi gani? pia mumeo/mchumba ana kazi gani? Vipi kwa ujumla kuhusiana na kipato chenu kikoje.Ukijibu hapo tutaanza kupata jinsi ya kulifanyia kazi suala lako.
 
Haya mambo ya wazazi wanataka mjukuu yameshapitwa na wakati, kabla ya kuamua kuzaa ni lazima kujipanga kwanza kwani maisha ya sasa si ya kukurupuka.

Unaweza ukaamua kuzaa ili kuwafurahisha wazazi lakini baadae ukakosa amani katika mahusiano yako, hivyo ni vema mkakaa na kujadili kwa kina.
 
unapenda mwanao au wanao waje walelewe na babu na bibi na wakati kwa muda huu hamtaki wazazi wenu wawalee wanenu?
Baba ako na mama ako wapo tayari kulea watoto na nyi mnasema mnataka kujipanga mtajipanga lin wkt kwa miaka 7 mmeshindwa au mnataka mzeeke ndo mzae watoto wenu waje kuwaita babu na bibi badala ya baba na mama!
Acha ujinga tega zaa ka anashindwa ni pm mim nikupe mtoto.
 
Sasa kwa hali hii miaka 7 uchumba?Duuh hyo kali!NAPENDEKEZA HATA HONEY MOON IFUTWE TU haina value tena!vjana twaruka xana kizaz hki ni hatari!2naoa b4 uchumba?hamna thaman ya uchumba tena!
 
Huyo mchumba anajipanga mzae au mfunge ndoa? Mbona huongelei ndoa unaongelea mtoto tu umeshakata tamaa ya ndoa?
 
kama humwelewi tafuta anayeeleweka bana................mwanaume mwenye uzazi si yeye tu

Kwanza anaweza akupotezee muda na baadae hata asikuoe huyo maana wanaume bana we acha tu!
 
habarini. nina mchumba wa mda mrefu zaidi ya miaka saba ,wazazi wangu wanapenda wajukuu, na mimi nimezaliwa mwenyewe, na ndio ninatakiwa niwaletee wazazi wangu mjukuu nifanyeje? wakati mchumba wangu nikimwambia tuzae anasema mpaka tujipange? nifanyaje na mimi nataka mtoto na wazazi wamezeeka nao wanawish kuwa na mjukuu . msaada wa mawazo wakuu nifanyaje ili huyu mwanaume anielewe na sitaki kuzaa na mtu mwingine?:yawn:

Yafaa ukubaliane na maamuzi yake kwani huwezi lazimisha mambo ambayo hayapo kwenye mipangilio yake pia hata ktk imani zenu sidhani kama mnaruhusiwa kuzaa ama kufanya tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa
 
kama amekua mpenzi wako kwa miaka yote hio basi jua anajipanga kutafta wa kumfaa zaaidi na wewe hakupendi. Uchumba gani miaka 7?
 
Wewe ndio tatizo,kwani mki-do unampa mabwepande??? Kama sio kwanin usitegeshe siku za hatari zen upate ujauzito? Au jamaa yako dushelele halina risasi? Au wewe Ngorongoro craters pana matatizo!

aisee king kong umechekesha sana, toka february ianze sijacheka kama leo
 
Nina mama yangu mkubwa mwanae ana takribani 36 yrs hajaoa...yuko sawa kiumri na kaka yangu mwingne ambae ashaoa kitambo na mtoto wake yupo darasa la 5 sasa...huyu mamangu mkubwa akimuona mtot wa kakangu analia...anapata uchungu kwann mwanae haoi.....
Kuna hasara gani wazazi wako wakifariki kabla hawajamuona mjukuu? Wao ndio watakao mlea huyo mtoto mpaka wakulazimishe kubeba mimba? Halafu huyo mwanaume anajipanga miaka saba yote ya nini mnataka kuoana huku mkiwa mamilionea au?
 
Wewe ndio tatizo,kwani mki-do unampa mabwepande??? Kama sio kwanin usitegeshe siku za hatari zen upate ujauzito? Au jamaa yako dushelele halina risasi? Au wewe Ngorongoro craters pana matatizo!

mabwepande... Ngorongoro crater...nimecheka mkuu
 
Hakuna hata sikumoja mwanaume huwa anakua tayari kuzaa. Kwa sababu sisi wanae tuna fear for unknowns kiasi kwamba daily utaona hauko tayari. Sidhani kama kuna mwanampe yeyote alizaa mtoto wa kwanza kwa kupanga. Dawa shika tu mimba, atakasirika at first, later atazoea na mambo yataenda tu
 
kutegesha inaweza isimsaidie kama alikuwa anatumia njia za uzazi wa mpango aache coz inachukua muda kupata ujauzito kwa wale waliokuwa wanatumia hizo njia
 
Hakuna uchumba wa miaka saba bwana! Ka hujui tu wewe sio chaguo la huyo jamaa! Anashindwa kukwambia tu kuwa MAMA NENDA ZAKO NSHAKULA VYA KUTOSHA! Siku akikupatia kosa ndo utajua. tafuta mtu ambaye yuko serious na kuanzisha familia! huyo ni play boy tu mama. Sorry ka nimekukwaza!
 
Achana na mambo ya wazaz kuna raha yake kujipanga kama alivyosema mchumba wako hayo mambo ya zaman eti "nataka nimuone mjukuu kabla sijafa."HAYO Ndo mambo yanazidi kutuzamisha wabongo kwenye dimbwi la umaskin kila siku.
 
Achana na mambo ya wazaz kuna raha yake kujipanga kama alivyosema mchumba wako hayo mambo ya zaman eti "nataka nimuone mjukuu kabla sijafa."HAYO Ndo mambo yanazidi kutuzamisha wabongo kwenye dimbwi la umaskin kila siku.
Punguza uoga mangi wazazi wako wangejipanga hivyo labda saa hii usingekuwa hapa jukwaani
 
Back
Top Bottom