Nia ya Dhati ya Wanaharakati Kumshtaki Livingstone Lusinde kwa Child Abuse

Hii kesi ilitakiwa tiyari kuwa lodged na si kutafuta maoni. Human respect and dignity should be preserved anywhere by anybody at any time. Read more on Convention on the Rights of the Child Here

Mimi nadhani wange concentrate ktk ile child law zaidi kwani ndio ratification ya Convention bongo!
 
Kweli Nchi hii inaonekana ukiwa mwanasiasa wa CCM uko juu ya Sheria.Wakati Lusinde anaporomosha matusi jukwaani, pembeni kuna wana Usalama .Labda IGP Mwema anaweza kutusaidia majibu sahihi kama ni sahihi mtu kuporomosha matusi mbele ya hadhara na huku walinda sheria wakiangalia tu.

Jambo jingine ni kuwa kuna haja ya kuwa na Kanuni inayosimamia hadhi na nidhamu ya Mbunge mbele ya jamii kama ilivyoawapo Bungeni na mara inapovunjwa na mbunge yeyote lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.
Hivyo basi heshima ya Bunge haiishie ndani ya ukumbi wa Bunge tu.Napendekeza kuwa kikao kijacho kifungu hii ya Kanuni ya Bunge 2007 ifanyiwe marekebisho ilikulinda heshima ya Bunge .
63.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba
yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika
Bunge , ni marufuku kabisa kusema uongo na kutoa lugha ya matusi Bungeni au nje na kwa sababu

hiyo, Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni au nje ya ukumbi wa Bunge ana wajibu wa

kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au
suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo
jambo la kubuni au la kubahatisha tu na kwamba lugha iliyotuka si ya matusi au kejeli kwa Mtu au jamii.


(9) Endapo Mbunge mwingine yeyote ataona kwamba uwongo
uliosemwa na Mbunge huyo Bungeni au nje ya Bunge ni mkubwa kiasi cha kuathiri

heshima ya Bunge, anaweza kutoa hoja kwamba, Mbunge huyo: -
(a) ikiwa ni kosa lake la kwanza, asihudhurie
vikao vya Bunge visivyozidi kumi;
(b) ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi, asihudhurie
vikao vya Bunge visivyozidi ishirini;
(c) achukuliwe hatua nyingine za kinidhamu
zitakazotajwa katika hoja yake

Naomba kuwasilisha:

hapo kwenye Kijani, hakuna adhabu inayomtosha Lusinde kwa matusi aliyoyaporomosha........................
Yanni mimi nilikuwa naangalia ile clip na watu, nilitoka kwa kuona aibu. sijui wale waliokuwa uwanjani mambo yalikuwaje!!!!!!!!!!!!!
 
Wazo zuri sana, nadhani inaweza kusaidia kurejesha viongozi wetu ktk njia sahihi. kabla hatujajemga jamii ya watukanaji.
 
Daaah, nimeangalia iyo video.......what a shame! Mtu kama huyo eti yuko mjengoni kwa ajili ya wa-tz......:tape2::tape2:
 
This insane Lusinde should be judged individually.He is not a representative of a tribe as you claim.Was this crazy voted by all wagogo?What if any individual mistake will be viewed with the "eyes of tribe" as you do?So please and please mr/madam lets talk about Lusinde.His tribe has nothing to do with the case at hand.

Don't get upset Mnyikati, Mundali alikuwa anafikisha ujumbe kwa waliompigia kura Lusinde kwani anawa-aibisha, haiwezekani watu wenye akili timamu wampigie kura za ndiyo mtu mwenye mdomo mchafu kama Lusinde. Yeye mwenyewe alisema kwake "matusi ndo kwao"! Hivyo kutukana ni tabia yake toka nyumbani, kama ni tabia yake ina maana jamii ya wagogo inayo mzunguka inamfahamu fika, kwanini wamchague mtukanaji?

Kwani watanzania tunapojiuliza "tumelogwa na nani" kwani ina maana wote-hapana, ni kwa vile tunaruhusu watawala wachache kuingia mikataba ya kinyonywaji na kuwa acha wanakwiba rasilimali za Taifa huku tukitazama bila kuchukua hatua, basi tunakuwa tumeingia kwenye mkumbo wa wote! Be patient but you have to educate your fellow "Gogonese" to select a decent person who will reflect your humble culture not Lusinde type-heri ya Vuvuzela la CDM toka Mkoa wa Simiyu!
 
...A child who give his mother a father sleepless night will he himself will never sleep.... Huyu Lusinde sio bure hii ni laana ya baba yake mdogo mzee J S Malecela kijana ali "mvua" nguo sana huyu mzee kule Mtera wakati wa kura za maoni, so mimi wala sishangai! Halfalu ndio bado nashangaa sijui kwanini Spika Makinda hakumkubalia lile wazo lake la kutaka wabunge wapimwe akili! mi nafikiri alikuwa anataka "justification" ya uchizi wake ili bunge limpeleke India kutibiwa! anahitaji maombezi huyu!
 
Wadau naomba tuziweke pembeni siasa katika kujadili mada hii, tuweke michango yetu kwa nia ya kulitimiza hili....maneno aliyoongea Mbunge Lusinde yametugusa sana sisi wanaharakati wa haki za watoto, ukizingatia kwamba kulikua na watoto wadogo pale ambao waliyasikia..technically, he did abuse those children..kwa hilo basi, tuna nia ya kulifikisha shauri hili katika vyombo vya sheria ili wanasiasa au watu wenye tabia ya kuongea offensive and abusive words mbele ya watoto wafahamu kwamba watawajibika kwa matamshi yao kisheria!

1. tunaomba weledi wa sheria za kitaifa na za kimataifa; hasa katika Child Rights' watoe mwongozo katika hili...

2. tunaomba wakazi wa Arumeru, waandishi wa habari, au yeyote aliyehudhuria mkutano ule awe tayari kutoa ushahidi, ikibidi mahakamani...

3. tutashirikishana katika kila hatua itakayoendelea katika hili..

3. ikibidi tuwe tayari kwa michango ya hali na mali ili kufanikisha jamobo hili....

Mwisho; tukumbuke kwamba mtoto wa mwenzio ni wako........nakaribisha michango na ushauri...

Mkuu jifanye mimi sikuwahi kusikia na uorodheshe aliyoyasema kaka.
 
Wazo zuri ili hatua sitahiki zichukuliwe na hatimaye tujenge jamii iliyositarabika yenye wanasiasa wenye kujenga hoja za msigi kwa mustakabali wa taifa.
 
mwenzetu mgeni hapa Yerusalemu?

Sixteen minutes of Shame, Lusinde utafikiri amemeza CD ya matusi! Aibu gani hii kwa Chama Tawala-Wasipo mpa adhabu kali ntakuwa nimejiridhisha kwamba "Hatuna serikali bali genge la wahuni"
 
Bila kuchelewa tuanze kuchukua hatua kuhusu ili jambo. Niko tayari kuchangia gharama za wakili, kama kuna mtu anajua tufanye nini na vipi kuhusu michango yetu atusaidie kwa hili.
 
Kuna mwenye Video clip ya tukio? Na tupate mashahidi wasiopungua watatu. Ni PM kama hizo evidence zipo.
 
Angekuwa CDM mngefanikiwa lakini kwa kuwa yuko CCM mtapoteza muda. Mie ushauri wangu msibishane na mwehu watu wa Arumeru wameshatupa zawadi nzuri kwa kutosikiliza maneno ya mwehu hiyo ni adhabu kubwa na inamtosha.

No, lazima ashitakiwe, wenye weledi wa kutengeneza hii kesi msisite kutoa ushauri wenu.
 
wadau naomba tuziweke pembeni siasa katika kujadili mada hii, tuweke michango yetu kwa nia ya kulitimiza hili....maneno aliyoongea mbunge lusinde yametugusa sana sisi wanaharakati wa haki za watoto, ukizingatia kwamba kulikua na watoto wadogo pale ambao waliyasikia..technically, he did abuse those children..kwa hilo basi, tuna nia ya kulifikisha shauri hili katika vyombo vya sheria ili wanasiasa au watu wenye tabia ya kuongea offensive and abusive words mbele ya watoto wafahamu kwamba watawajibika kwa matamshi yao kisheria!

1. Tunaomba weledi wa sheria za kitaifa na za kimataifa; hasa katika child rights' watoe mwongozo katika hili...

2. Tunaomba wakazi wa arumeru, waandishi wa habari, au yeyote aliyehudhuria mkutano ule awe tayari kutoa ushahidi, ikibidi mahakamani...

3. Tutashirikishana katika kila hatua itakayoendelea katika hili..

3. Ikibidi tuwe tayari kwa michango ya hali na mali ili kufanikisha jamobo hili....

Mwisho; tukumbuke kwamba mtoto wa mwenzio ni wako........nakaribisha michango na ushauri...

kabla ya kufanya chochote ni muhimu kujua kwanza kama kuna sheria yeyote alivunja kwa kusema matusi hadharani namna ile.
 
Siamini kama kimaadili na nafasi aliyonayo katika taifa anaweza kutamka maneno yenye matusi kama yale. Haikubaliki katika jamii ya kitanzania kuwa kiongozi asiyejua maadili hasa anapotumia vibaya majukwaa kutukana viongozi wenzake ambao wote lengo lao ni moja ila tofauti inakuja katika sera na jinsi ya kuzisimamia kutokana na tofauti ya itikadi za vyama vyao. Jiulize kwa kutumia matusi ndio wananchi watakuona una akili au ndo unaharibu taswira hata ya chama iliyokupa dhamana ya kuwakilisha watu katika jimbo lako. Kwa kuheshimu maadili yetu ya Kitanzania, napendekeza yafuatayo:
1: Chama husika(ccm), kupitia kamati ya maadili ichukue hatua stahiki katika kuliangalia hili, kusafisha taswira ya chama.
2:Chadema kisinyamazie matusi yaliyotolewa na mheshimiwa hata ikiwezekana wafungulie kesi suala hili ili kusaidia kuondoa viongozi wasio na maadili katika nchi
3: Wanaharakati chunguzeni kama kuna uwezekano wa kumshtaki Mh. hasa katika misingi ya haki za binaadam na sheria ya siasa hasa katika mambo ya kampeni inasemaje pale viongozi wanapokiuka maadili na misingi ya kampeni. Je watoto wanapata athari gani kutoka kwa viongozi kama hao.
Siasa sio matusi, siasa ni chombo cha kumkomboa mnyonge na kumpa faraja ya maisha. Inapotumiwa vibaya tunajenga tabaka la viongozi ambao siku moja watasababisha damu kumwagika.
Watanzania tujenge nchi yetu, tofauti ya siasa iwe chagizo la maendeleo.
 
mdau umenena vyema na pia jamvi la wanajamii liko active kiushirika na thread yako kwa manufaa ya wale tuliopitwa na hizo sentensi tata za mheshimiwa,tungependa udadavue ..1,2,3,4....etc ya hayo matamshi ili angalau tuweze kuchangia vema,nina tatizo lakutumia muda mrefu shambani.
 
Back
Top Bottom