Barua ya wazi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mkurugenzi na Afisa Elimu

Mpendwa

Member
Jun 9, 2011
56
11
Barua ya wazi Kwa mkuu wa wilaya ya Ubungo, Mkurugenzi na afisa elimu.

Sisi ni wazazi wa watoto wanaosoma shule ya msingi Msumi.

Ndugu wakuu wetu tunahitaji Sana msaada wetu kuhusu upotevu wa pesa zetu ambazo tulichangishwa na Kamati ya makande inayosimamiwa na Kamati kuu ya shule chini ya uongozi wa mwenyekiti ndugu Noel Maphie

Tuna michango mingi ambayo Hadi sasa hatujui mustakabali wake maana hatujapewa hesabu, zake za mapato na matumizi, kwamba walikusanya kiasi gani na wametumia kiasi gani kwenye matumizi yapi.

Tulichangishwa michango ifuatayo

1. Pesa ya ukarabati wa kisima cha maji, sh 1000 kila mzazi

2. Pesa ya makande Kwa watoto ambapo walikusanya viwango tofauti tofauti kwenye madarasa

3. Michango ya masufuria ya kupikia chakula michango tofauti Kwa madarasa.

Jumamosi ya tarehe 10/02/2024 tuliitwa na Kamati ya shule kupokea taarifa mbalimbali.

Kama wazazi tulitarajia kupata taarifa zenye maelezo ya kutosha juu ya makusanyo na matumizi yote.

Cha kushangaza, badala ya kamati kuu, alikuwepo mwenyekiti peke yake, wajumbe wengine hawakuwepo Kwa maelezo kuwa mmoja alifiwa na mwingine alikuwa anaumwa macho ingawa tunamfahamu na tulimkuta kwenye biashara zake akiendelea nazo wakati wa kikao na hata baada ya kikao.

Mwenyekiti amekuja kutupa taarifa ya kupatikana Kwa mzabuni wa kuwauzia watoto wetu chakula, Sisi kama wazazi tuna wasiwasi na usalama wa pesa zetu kwani hatuna uhakika na utendaji wake maana hakuna taarifa ya pesa za nyuma.

Mwenyekiti alipoulizwa juu ya pesa hizo, alidai kuwa wamefanikiwa kukusanya sh 800,000. Ila hajasema jumla pesa ya makande, masufuria na maji walikusanya sh ngapi. Hili pelee linazua maswali mengi Sana kwetu.

Pamoja na haya yote, taarifa zilizopo ni Kwa mwenyekiti wetu huyu anaishi Dodoma na kufanya kazi huko. Sasa kama anaishi huko atawajibikaje kwenye majukumu yake kama mwenyekiti?

Pamoja na hayo, yeye mwenyekiti z makamu wake na wajumbe wengine wawili hawana watoto wanaosoma shule yetu Kwa sasa. Tunajiuliza, ni Kwa sababu hiyo ndo maana hawajali pesa zetu?

Na kama hawana watoto wanaosoma hapa kwetu, wanakuwaje wajumbe hai wa bodi ya shule? Au kuna mlango wanautumia kujinufaisha?

Pia tunaamini miongoni mwa wazazi, wapo wenye uwezo wa kuingia kwenye Kamati, Kamati hii (bodi) ipo madarakani tangu mwaka 2016 na watoto wao walishamaliza Hadi shule za secondary na hawana watoto tena hapa. Kwa nini?

Nulipouliza uhalali wa kikao cha juzi Kwani kilikuwa na mjumbe mmoja Tu Kati ya wanne, mwenyekiti alinijibu Kwa dharau na kusema Mimi sijui lolote kuhusu idadi Yao na pia yeye ni muwakilishi wao. Sasa nauliza, suala la akidi likoje? Sisi tunajuaje kama aliyoyaleta mkutanoni ni mawazo yake au ya kamati yake?

Tunaomba msaada toka kwenu viongozi wetu.

Asanteni
Mzazi
 
Back
Top Bottom